Friday, February 4, 2022

UPENDO WA MUNGU

 UPENDO WA MUNGU

Upendo: Ni hisia kali alizonazo mtu kwa mtu, kitu na namna mbalimbali zinazomuhasiri mtu.

Aina za upendo.

                                 i.            Upendo wa mzazi na mtoto

                               ii.            Upendo wa mume na mke

                            iii.            Upendo wa kitu

                            iv.            Upendo wa Mungu(Agape love)

                               v.            Upendo wa ndugu

Upendo wa Mungu (Agape love) kimsingi hakuna jambo la muhimu na la maana sana zaidi ya upendo, maana Mungu mwenyewe ni pendo.

“Nasi tumefahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi na kuliamini. Mungu ni pendo naye akaye katika pendo , hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake”.1Yohana 4:16

Mungu mwenyewe aliupenda ulimwengu alijua ndani ya ulimwengu amewaweka watu na watu hao lazima waokolewe ndiyo maana akamtuma mwana wake wa pekee ili kila amwaminie asipotee bali wote wawe na uzima wa milele, huo ni upendo wa Mungu kwetu sisi.

“kwa maana jinsi Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele” Yohana 3:16

 

Ukifuatilia huduma nyingi au makanisa mengi upendo wa Mungu haupo, kwa nini? Watu wanajifikilia wenyewe tu na hawana habari na watu wengine lakini. Biblia inasema kama sina upendo      ( kwa watu) nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao( shaba isiyo na kitu ndani yake)

 


“Nijaposema kwa lugha za wanadamu na malaika kama sina upendo nimekuwa kama shaba iliyo na upatu uvumao” 1wakoritho 13;1

 

Hata kama nitakuwa nimefahamu mambo mengi ya kiroho na kimwili kama sina upendo si kitu mimi. Hata kama wewe si kitu.

a.     Nijapokuwa na unabii .

b.     Kujua siri zote na maarifa yote

c.      Nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima. Kama sina upendo si kitu mimi.

d.     Hata nikitoa mali zangu zote kuwapa maskini.

e.      Hata nikijitoa mwili wangu niunguwe moto, kama sina upendo haisaidii kitu.

“Tena nijapokuwa na unabii na kujua siri zote na maarifa yote . nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo si kitu mimi. Tena nikijitoa mwili wangu niunguwe moto, kama sina upendo hainifani kitu” 1wakoritho 13:2-3

                   NGUVU YA UPENDO:

Upendo huvumilia:panapokuwa na upendo ndani ya kanisa, kwenye biashara, kazini, nyumbani kwenye jamii na sehemu zingine upendo huvumilia yote hata kama mtu amekutendea mabaya au akakusemea vibaya utavumilia kwa sababu ya upendo.

 

Upendo hufadhili: Kwa sababu ya upendo unaweza ukapata msaada kutoka kwa watu, mtu anaweza akakuonea huruma, akakusaidia kukulipia ada, kukupa chakula n.k.

 


Upendo hauhusudu: Kwenye upendo wivu usiokuwa na maana utaondoka, bali kutakuwa na wivu wa maendeleo.

 

Upendo hautakabari: Upendo unapokuwepo basi ujeuri utaondoka, kwa kila mmoja hamtafanyiana kiburi.

 

Upendo haujivuni: Panapo kuwa na upendo hakuna majivuno kujiona wewe ni bora kuliko mwingine jambo hilo linakuwa halina nafasi yake.

 

Upendo haukosi kuwa na adabu: Penye upendo lazima adabu itakuwepo, kuheshimiana.

 

Upendo hautafuti mambo yake:Upendo ukiwepo hauwezi kuanza kutafuta madhaifu ya mtu jinsi alivyo muumba Mungu ataendelea kupenda tu.

 

Upendo hauoni uchungu: upendo ukiwepo uchungu ya kuanza  kumjutia mtu na kuya weka ndani / kuyatunza ndani ya moyo wako kwa kuanza kumuachukia, kumsema vibaya utamuachilia na kuendelea  kumpenda (kupenda)

 

 

Upendo hauhesabu mabaya: upendo hauhesabu mabaya uliyotendewa.

 

Upendo haufurahii udhalimu: kama unampenda ndugu yako, au ameharibikiwa anatenda mabaya ni mrevi, kama unaupendo utamwombea  kwa Mungu amrehemu na atokane na hayo. Vile vile utamuonya kwa njia anayoenenda nayo kwamba sio nzuri.

 

 

Upendo hufurahi pamoja na kweli: mahali penye upendo panatakiwa kuwa na ukweli na uwazi ili zile taarifa  anazozipata mtu au alizo pata mtu ni vyema ukweli ukawepo ili mfurahi kwa pamoja.

 

Upendo huamini yote: kwenye upendo lazima tumaini liwepo, ili yule uliye au sehemu uliyopo uaminike.

 

 Upendo hutumaini yote: kwenye upendo lazima tumaini liwepo la kuona matumaini ya mbele au yatalajiwayo.

 

Upendo hustahimili yote :kwenye upendo kuna uimara, kusimama imara bila kusurubishwa.

 

Upendo haupungui neno wakati wowote:  Upendo ukiwepo utapewa kuyafuata maneno au neno zuri ili kuboresha mahusiano yaliyopo.  “Upendo huvumilia, hufadhili, upendo huwahusudu, upendo hautakabiri, haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake,haoni uchungu, hauhesabu mabaya, haufurahi udhalimu balihufurahi pamoja na kweli, huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote, upendo haupungui neno wakati wowote, bali ukiwepo unabii utabatilika, zikiwepo lugha zitakoma, yakiwepo maarifa yatabatilika “. 1wakolitho13:4-8

Upendo haunahofu: kwenye upendo hofu itakuwa haina nguvu bali mtu atakuwa jasiri, asiyeogopa chochote, na ambaye mwenye hofu hajakamilishwa na upemdo bado.

 

“Katika pendo hamna hofu, lakini  pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo”.1Yohana 4:18

 


Kanisa linapokuwa na upendo hapo Mungu anafurahi sana kwasababu  linamuakilisha yeye hapa duniani.

 

Alama za upendo:

                                           i.            Upendo umetoka kwa Mungu

                                         ii.            Kila apendaye amezaliwa na Mungu

                                      iii.            Anamjua Mungu

                                      iv.            Mungu amemtuma mwanawe wa pekee ulimwenguni(Yesu Kristo) ili tupate uzima wa milele.

 

“Wapenzi na mpendane kwa kuwa pendo latokea kwa Mungu na kila apendaye amezaliwa na Mungu. Yeye asiye penda hakumjua Mungu kwa maana Mungu ni upendo  katika hili pendo Mungu lilionekana kwetu kwamba Mungu amemtuma mwanae pekee ulimwenguni ili tupate uzima kwa yeye”1Yohana 4:7-9

v. Tumepatanishwa na Mungu baba

vi. Mungu hukaa ndani yetu

vii. Upendo wake umekamilika ndani yetu

viii. Ametushirikisha roho wake

 

“Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo,haya matatu na katika haya lililo kuu ni upendo” 1wakoritho13:13.

 

Kwahiyo tunaona hapo lililo  kuu ni upendo. Watu wengi kwenye jamii upendo umepoa , akienda kazini upendo haupo, mtaani upendo haupo, nyumbani upendo haupo, sasa basi kanisa ndilo linatakiwa kuwa tibia watu waliokosa upendo  ndani yao kwa jina la Yesu Kristo.Ameni

Kama tukisema kanisa tunampenda Mungu huku tunawachukia ndugu zetu ni waongo.

“Mtu akisema nampenda Mungu naye anamchukia ndugu yake ni mwongo kwa maana asiempenda ndugu yake ambaye amemuona hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumuona” 1Yohana 4:;20

“Upendano wa ndugu na udumu msisahau kuwafundisha wageni, maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua” Waebrania 13:1-2

 

Vitu vinavyo haribu upendo:

Moja ya vifungo kinacho sumbua watu ni kifungo cha tabia iwe ni kwenye:

Þ   Urafiki au mahusiano

Þ   Kwenye kazi au ofisini

Þ   Kwenye biashara na taasisi

Ili uweze kuendelea unatakiwa uwe na tabia nzuri.

“Hekima hiyo siyo ile ishikayo kutoka juu bali ni  ya dunia ya tabia ya kibinadamu na shetani. Yakobo 3;15.

 

Tabia;  ni hali au sifa za nafsi alizonazo mtu. Kwahiyo hapa utaona matendo, miitikio au mienendo itakayoweza kuonekana  wazi. Mfano; kunatabia za miti, wanyama, binadamu n.k, wapo wanaosema mazoea ujenga tabia.

 

Aina za tabia

Kunatabia ambazo mtu anakuwa

i)Amezaliwa nazo (kiasili)

ii).  Ameiga tabia kutokana na mazingira aliyokulia au kulelewa.

 

-Kuna wapo waliolelewa na mama peke yake

      -Kunawapo walio lelewa na baba peke yake

      -Kunawapo waliolelewa na mama na baba

      -Kuna wapo waliolelewa na ndugu

  -Kunawapo waliojilea wenyewe

Kwahiyo kwa namna zote hizo lazima mtu huyo hawezi kufanana na mtu mwingine kwasababu ya namna na mazingira aliyokulia au kulelewa lazima yatakuwa tofauti.

 

Tabia za kibinadamu

A.   Kuna msondani (introvert)

Mtu huyu ni Yule ambaye yeye sio mwongeaji sana, ni mkimya.

   Aina zake

                             I.            melancholy(melancolim)

-wapole na wasio na maneno mengi
-wanahisia kali za upendo( upendo wa dhati)

-wanajali wenzao

-wanamaombi mazuri kiimani

-wanahuruma

-wanabusara na hekima

 

                         II.            phlegmatic (pragmatic)

-ni mabingwa wa kuhairisha mambo

-wanapenda kupuuzia mambo

-watafiti na kufuatilia mambo

 

B.   Kuna msonje (extrovert)

Mtu huyu ni Yule ambaye ni muongeaji sana na anayeweza kujielezea kwa namna mbalimbali.

Aina zake

i). Sanguine

-ni wacheshi sana

-watu wenye maneno mengi wasio pumzika kuongea

-wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wanaongea.

-wana karama ya kuhubiri

-wanapenda kujaribu kila kitu..mfano petro.

 


ii). Choleric

-ni wakali

-wasiopenda kudharauliwa au kuonewa

-ni viongozi wa asili ya kuzaliwa

-wanajiamini

-hawaongei wala kucheka hovyo.

 

TABIA MBAYA AMBAZO MUNGU HAZIPENDI

i). Uzushi

ii). Umbea

iii). Usingiziaji

iv). Uongo

v).Uzinzi

vi).Ufitini

vii). Uasherati

viii).Ugomvi

ix). Kiburi

x). Jeuri

xi). Husuda

xii). Kijicho

xiii). Na mambo yote yanayofanana na hayo.

 

KUNAVITU ILI MTU AWEZE KUFANIKIWA

Ili mtu afanikiwe kunahitaji mambo mawili,

a)Kipawa / Karama.

Kipawa kinaweza kumfikisha mtu mbele za watu wakubwa na kujulikana.

“Zawadi ya mtu humpatia nafasi, humleta mbele ya watu wakuu” Mithali. 18;16

Mtu anaweza kuwa na kipawa  Fulani lakini tabia yako mbaya hakuna atakaye tamani kuwa karibu nawe.

 

b) Tabia ya mtu

Ili Mungu akutumie kwa kiwango cha juu ni muhimu kuanza kwa kubadili tabia yako mbaya na kuwa na tabia nzuri mbele ya Mungu na wandamu.

“kwa maana ndugu mnapendwa  na Mungu twajua uteule wenu ya kwamba injili yetu haikuwafililia katika maneno tu bali na katika nguvu na katika Roho Mtakatifu na zilivyokuwa tabia zetu kwenu kwa ajili yenu” 1wathesolenike 1;4-5.

“Lakini ndugu zangu mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo, 1wakorintho 3;1.

 

 

 

 

 

 

 

 

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

  

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

Karama : Ni zawadi anazotoa Mungu kwa watu au kipaji cha pekee kutoka kwa Mungu.

Lakini kazi hizi zote huzitenda roho huyo mmoja yeye Yule, akimgaia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye” 1wakorotho12:11

Katika karama hizi kuna tofauti ya:

v Kuna tofauti ya huduma

v Kuna tofauti ya kutenda kazi

Bali Mungu ni yeye Yule azitendae kazi zote katika wote

“Bali pana tofauti za karama bali roho ni yeye Yule, tena pana tofauti za huduma na bwana ni yeye Yule, pana tofauti za kutendwa kazi pana tofauti za kutenda kazi bila Mungu ni yeye Yule azitendae kazi katika wote.”1Wakorithio 12:4-6

.kwenye huduma na kutenda kazi kila mtu anakuwa anapewa ufunuo ili kusaidiana.

“Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa  roho kwa kufaidiana” 1Wakoritho 12:7

Kwa hiyo sasa baada ya kuokoka unatakiwa kumuomba Mungu akupe karama za rohoni ili mwili wa Yesu Kristo ujengwe kwa pamoja kwa umoja ndani ya kanisa 

 

“Takeni sana karama zilizo kuu, hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora”.1wakoritho12:31

Kabla ya kuoka tulikuwa tunazifuata sanamu zisizo nena, yaani kuabudu miungu ya kishetani “Basi ndugu zangu kwa habari ya karama za roho, staki mkose kufahamu, mwajua  ya kuwa mlipokuwa watu wa mataifa mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena kama mlivyoongozwa”1Wakolotho 12:1-2

 

AINA ZA KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

Kuna aina mbalimbali za karama za roho. Mwingine anaweza kupewa na Mungu karama zaidi ya moja:

“Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali kwa kadri ya nema mliopewa   ikiwa ni unabii, ikiwa huduma katika huduma yetu, mwenye kuonya katika kuonya kwake, mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu kwa furaha” Warumi 12:6-8

 

1.     Hekima: Ni hali bora ya mtu katika kutambua ukweli wa binadamu, vitu,matukio na mazingira mbalimbali hata kuchagua vizuri la kufanya au unaweza kusema ni maadili ya kitu na maadili ya ki mungu “Lakini hekima itakayo juu, kwanza ni safi tena ni ya amani, ya upole, tayari  kusikiliza maneno ya wato, imajua rehema na matunda mema haina fitina, haina unafiki” Yakobo 3:17

“Basi sasa nipe hekima na maarifa mjue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa kwa kuwa na nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi “2Nyakati 1:10

“Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako na kupambanua mema na mabaya maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako waliowengi” 1Wafalme 3:9.

 

“Maana mtu mmoja kwa roho apewa neno la hekima …. “1wakoritho 12:8

 

        2. Maarifa:  Ni ufahamu wa kuelewa kitu Fulani.

“--------- Mwingine neno la maarifa apewavyo roho yeye Yule “.1wakolitho 12:8(b)

“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa ----------“ Hosea 4:6 Kumbe ukikosa maarifa unaangamia na nguvu ya mtu siku zote ni kuwa na maarifa mengi(knowledge is power)

 

“Bali ajisifiyena ajisifu kwa sababu hii ya kwamba ananifahamu mimi na kunijua ya kuwa mimi ni bwana, nitendee wema na hukumu na haki katika nchi maana mimi napendezwa na mambo hayo asemaBwana,”.Yeremia 9:24.

   Ee mwanadamu yeye amekuonyesha yaliyo mema na     Bwana anataka nini kwako ila kutenda haki na kupewa rehema na kwenda kwa unyenyekevu na mungu wako”. Mika 6:8.

Na uzima wa milele ndio huu wanijua wewe mungu wa pekee wa kweli na yesu kristo aliyemtuma” Yohana 17:3

 

3.Imani:    Ni kuwa na hakika ya  mabo yatarajiwayo , ni       bayana ya mabo yaliyo onekana

Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo ya mambo yatarajiwayo  ni bayana ya mambo yasiyo onekana” Waebrania 11:1

“mwingine imani katika roho yeye Yule …………1Wakoritho 12:9(a)

“maana twenenende kwa imani si kwa kuona” 2wakoritho 5:7

 

“Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani naye akisitasita roho yangu haina furaha naye lakini sisi hatumo miongoni mwao hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu. Waebrania 10:38-39.kwahiyo ukisoma katika hiki cha Waebrania sura ya 11yote utaona inazungumziwa imani kwa asilimia kubwa.

 

4)Kuponya: Ni kumfanya mtu ambaye amekuwa mgonjwa kimwili, kiakili au kiroho apate afya njema.

“----------- Mwenye karama za kuponya katika roho Yule mmoja” 1wakoritho 12:9(b)

“Pozeni wagonjwa, fufufeni watu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo, mmepata bure, toeni bure”.Mathayo 10:8.

“Akampeleka mfalme wa Israeli waraka ule kusema waraka huu utakapo kuwasilia tazama nimemtuma mtumishi wangu naamini kwako ili upate kuuponya ukoma wake” 2Wafalme 5:6

Naamini alikuwa jemedari wa jeshi la mfalme wa shamu lakini alikuwa na ukoma ambao ni ugonjwa hatari sana. Mfanya kazi wa ndani akitoa habari za mtumishi wa Mungu Elia kwamba anaweza kumponya.

“Lakini Petro akasema mimi sina fedha wala dhahabu lakini nilicho nacho ndicho nikipendacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa nazareti simama uende. A kamshika mkono wa kiume akamwinua mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu” Matendo 3:6-7

“Hata ikiwa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa na kuwaweka juu majamvi na magodoro ili petro akijagawa kimli chake kimwangukie mmoja wapo wao.Nayo makuja watu wa miji ilioko kandokando ya yerusalemu wakakutanika wakileta wagonjwa .


Nao walioingiliwa na pepo wachafu nao wote wakaponywa” matendo 5:15-16

“kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi walio pagawa nao, wakalia kwa sauti kuu na watu wengi walio pooza na viwete wakaponywa”matendo 8:7.

 

“Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea mtu huyo amelala kitandani miaka minane, maana alikuwa amepooza. Petro akamwambia Ainea Yesu Kristo akuponya, ondoka ujitandikie, mara akaondoka na watu wale waliokaa Lida na Sharoni wakamwona wakamgeukia bwana” matendo 9:33-35.

 

5)Matendo ya miujiza:  Ni kutenda jambo kubwa lililo zaidi ya uwezo wako. Au ni jambo la ajabu ambalo hukutegemea kulipata au kutokea au umeweza kusema bila kuweza kulielezea.

 

“Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya,Yesu wa Nazareti mtu aliedhihirisha kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara ambazo  Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojuana” matendo 2:22.

“Na Stefano akijaa na neema na uwezo alikuwa akifanya maajabu na ashara kubwa katika watu. Matendo 6:8.


 

“Lakini walipomwamini Filipo akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu na jina lake Yesu Kristo wakabatizwa wanaume na wanawake na yeye Simon mwenyewe aliamini akabatizwa akashikamana na Filipo akashangaa alipo ziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka” Matendo 8:12-13

 

6) Unabii: Ni kitendo cha kutabili yaliyopo, yaliyopita na yanayokuja, Nabii ni mteuliwa wa Mungu aliyeitwa kupeleka ujumbe kwa watumwa.

 

“Mkijua neno hili kwanza ya kwamba hakuna unabii katika maadiko upatao kufasiliwa kama apendavyo mtu flani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu bali wanadamu walinena yaliyo toka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu”. 2Petro1:20-21

 

“Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi, naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake yohane alie lishuhudia neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani mambo yote aliyoyaona. Heri asomae na wao wajasikiapo maneno ya unabii huu na kuyashika yaliyo andikwa humo kwa maana wakati ukaribu”. Ufunuo1:1-3

 

“Basi uyaandike mambo hayo ulioyaona nayo yaliyopo na yale yatakayokuwa baada ya haya” Ufunuo1:19

 

Unabii utakao tolewa lazima utoke kwa Mungu ambao umebeba pumzi ya Mungu maneno au neno utakalo litoa linatakiwa liwe na mambo haya.

a.     Lafaa kwa mafundisho

b.     Lafaa kwa kuonya watu makosa yao

c.      Lafaa kwa kuwaadilisha watu katika haki

d.     Lafaa kwa kuwaongoza

“Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho na kwa kuwaonya watu makosa yao na kwa kuwaongoza na kwa kuwaadilisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda  kila tendo jema” 2Timotheo 3:16-17

Lakini ifahamike kwamba kuna manabii wa kweli (Mungu) na kuna manabii wa uongo (shetani). Yesu kristo aliwatahadhalisha wanafunzi wake kuhusu manabii wa uongo. Akasema mtawatambua kwa matendo yao.

 

“Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajua wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali mtawatanbua kwa matendo yao. Je watu huchuma zabibu katika miiba au tini katika mibaruti  vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwe motoni ndiposa kwa matunda yao nitawatambua” Mathayo 7:15-20

Yesu kristo anaposema mti hapa anamanisha mtu, tunapaswa kuzijaribu kila roho je, zinatokana na Mungu au lah.

 

“Wapenzi msiamini kila roho basi zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na mungu kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.katika hili  Mwanijua  roho kwa mungu kila ikiliyo kwamba yesu kristo amekuja katika mwili yatokana na mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga kristo ambayo mmesikia kwamba yaja na sasa imekwisha kwako duniani 1Yohana 4:1-3

 

7)Kupambanua roho: Ni kitendo cha kutambua kinachoendelea  katika ulimwengu wa roho.

“Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku usiogope, bila nena wala usinyamaze. Kwa kuwa mimi ni pamoja nawe wala hapana mtu atakae kusababishia ili kukudhuru kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu. Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu”  Matendo 18:9-11.

“Akamjibu usiogope mana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha akomba akasema ee bwana nakuishi mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yake mfumishi naye akaona na tazama kile kilima kilichokuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyo mzunguka Elisha pande zote” 2Wafalme 6:16-17.

 

8). Aina za lugha

Kikawaida kuna aina mbalimbali za lugha hapa duniani lakini pia kuna lugha ya mbinguni ambayo watu wake wanatumia (lugha za malaika)

“Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika kama sina upendo nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao”1wakoritho 13:1

 

 

“----------Mwingine aina za lugha “ 1wakoritho 12:10

Kwahiyo Mungu anawapa watu wake  karama hii kwa kuelewa lugha mbalimbali kwa usemi.

 

9)  Kutafsiri lugha

Mungu anapompa mtu karama hii lengo lake ni kufikisha ujumbe kwa wale watu ambao hawaifahamu lugha hiyo, kwa njia ya maombi au kwa njia ya kuhubiri.

“Kwasababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri”1wakoritho 14:13

“Yamkini ziko sauti za namna nyigi duniani wala hakuna moja isiyo na maana . Basi nisipo ijua maana ya  ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye, naye anenaye atakuwa mjinga kwangu”1wakoritho 14:10-11

“Lakini katika napewa kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha” 1wakoritho 14:19.

 

1o)Kuhutubu (kuhubiri)

Ni kitendo cha kutoa ujumbe toka kwa Mungu kwa maneno ya kawaida yanayoeleweka kwa lugha.

“Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja ili wote wapate kujifunza na wote wafarijiwe” 1wakoritho 14:31

“Kwa ajili ya hiyo ndugu takeni sana kuhutubu wala msizuie kunena kwa lugha. Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu” 1wakoritho 14:39-40

 

“Ufuateni upendo na kutaka sana  karama za rohoni lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu”1wakoritho14:1

“Bali yeye ahutubiye asema na watu maneno ya kuwajenga na kuwafariji na kuvuta moyo”1wakoritho14:3

Pamoja na karama hizo zipo za aina nyingi, Kulingana na neema ya Mungu alio mpa mwanadamu kama yeye atakayo roho..

 

Aina za Huduma ndani ya kanisa :

Huduma: Ni taasisi inayo simamia jambofulani kwa watu. Huduma ndani ya kanisa ni taasisi inayosimamia shughuli zote za kiroho kwa watu kimwili na kiroho lakini huduma hizi zinautofauti wa:

                   i.            Kutenda kazi

                 ii.            Kila mtu ufunuo wake

Ndani ya kanisa kuna huduma tofauti tofauti ambazo lengo lake ni kujenga mwili wa Yesu Kristo (kuukamilisha mwili wa Yesu Kristo)

 

HUDUMA TANO ZA MUNGU ( KANISA)

a.     Mitume: Ni mtumwa wa dini anae unganisha watu na Mungu. Ni watu waliotumwa na Mungu na kupewa uwezo katika kufanya umisheni.

b.    Manabii: ni wateuliwa Mungu aliewaita kupeleka ujumbe kwa watumwa.

c.      Wainjilisti: Ni mkristo mwenye utume wa kuhubiri na kutoa elimu ya habari njema za Mungu

d.    Wachungaji:Ni wahudumu ndani ya kanisa au mlezi wa wahumini mpaka amalize safari yake hapa duniani  kwa kuwafikisha salama kuingia mbinguni .


 

e.      Waalimu:Ni watu wanaotoa elimu au ufahamu na ujuzi kuhusu neno la Mungu (kufundisha )

“Naye alitoa wengine kuwa mitume na wengine kuwa manabii kuwa wachungaji na waalimu kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa kristo ujengwe” waefeso 14:11-12.

“Ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu, mwenye kufundisha katika  kufundisha kwake:. Warumi 12:7.


 

 

 

 

 

 

 

 

NDANI YA WOKOVU YAKUPASA KUELEWA HAYA.

 NDANI YA WOKOVU YAKUPASA KUELEWA HAYA.

-Ujue umesamehewa dhambi zako

-Dhambi zako hazikimbiwi tena

-Kuwa na imani kwa Yesu Kristo

-Una haki ya kumili

 

 

KUBADILISHWA JINA.

Kimsingi mtu anatambulika kutokana na jina lake. Lakini kabla ya kuokoka tulikuwa tunaitwa majina ya namna tofauti tofauti kulingana na ukoo au familia uliyozaliwa wapo walioitwa majina bila kujua maana zao au wengine wakijua maana zao, yamkini ni mazuri au mabaya. Mfano 1.Yabesi kwenye Biblia aliitwa jina hilo Yabesi yaani huzuni kwanini ni kwasababu alimzaa kwa huzuni (Alizaliwa kwa huzuni)

Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima  kuliko ndugu zake na mamaye akamuita jina lake Yabesi akisema ni kwasababu nalimzaa kwa huzuni. Huyo Yebesi

 

akamlingana Mungu wa Israel,akisema, Lau kwamba ungenibarikia kwelikweli na kunizidishia  hozi yangu na mkono wake ungekuwa pamoja nami nawe ungelishinda na uovu ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba 1Nyakati 4;9-10

         Kwahiyo tunajifunza mambo yafuatayo hapa

 

 

 

     a)Akamlingana Mungu

 

·        Akaanza kumtafuta Mungu

·        Akaanza kusoma neno la Mungu

·        Akaanza kufunga

·        Akaanza kwenda kanisani

·        Akaanza kuomba

·        Akaanza kwenda mikesha

·        Akaanza kumuabudu Mungu kwa nyimbo na tenzi za Rohoni

Lengo lake huyu Yabesi alishafahamu jina alilopewa siyo zuri bali ni baya hivyo akataka ajikomboe kutokana na nguvu ya jina alilopewa la huzuni (Yabesi)

 

b)Lau kwanza ungenibarikia kwelikweli hapa akawa anamuomba Mungu ambarikie kwelikweli alishaelewa ndani ya jina lake la Yabesi (huzuni) halina Baraka bali ni matatizo matupu tu kwake.

 

c)Kunizidishia kozi yangu

Alikuwa anamtaka Mungu amuongezee umiliki maana alishafahamu umiliki alionao ni mdogo kutokana na jina lake alitakaMungu

-Apanue mipaka yake kama ni kwenye kazi,mashamba, mifugo, fedha, biashara n.k.

 

-Apanue hema yake, maana yake nyumba ziongezeke, kama anayo moja ziongezeke zaidi kwa Jina Yesu. Amen.

 

d)Mkono wako ungekuwa pamoja nami

Alitaka mkono wa Mungu uwe pamoja naye kila mahali, alijua mkono wa Mungu.

 

·        Unanguvu ya kuokoa

·        Ni ulinzi

·        Ni afya njema

·        Ni wa huruma

·        Ni wa kuponya.

Alijua pasipo mkono wa Mungu kumuhatamia hakuna kitakachofanyika.

 

e)Nawe ungenilinda na uovu ili usiwe kwa huzuni yangu.

Alikuwa anatamka Mungu amlinde, ili ile laana ya jina isiwepo ndani yake, alielewa ndani ya jina hilo kuna;

 

·        Kuwaza mambo mabaya

·        Kukata tama.

·        Kuvunjika moyo.

·        Masikitiko.

·        Taabu

·        Laana.

·        Mikosi

·        Umasikini

·        Magonjwa  n.k

 

f)Naye Mungu akamjalia hayo aliyo yaomba.

Alijua maombi yanatufanya tumtafute Mungu “Nanyi mtanitafuta na kuniona mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” Yeremia 29:13

Alijua maombi yanainua mtu, Akawajibu yeyealiyemfanya mzima kuwa mzima ndiye aliyeniambia  jitwike godoro lako uende Yohana 5:11

Alijua maombi yankupa utajiri

“Maana nimejua Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa masikini kwaajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajirikwa umaskini wake 2Wakorintho 8;9

 

“Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya kristo Yesu. “Wafilipi 4;19”

 

Mfano 2. Ibrahimu (Baba yetu wa imani) na mke wake Sara.

Mungu alimuomba kwamba hawezi kumfanya baba wa mataifa mengi kama jina lake litabaki vile vile Abramu na hata mkewe ili awe mama wa uzao mwingi lazima jina libadilike asiitwe tena Sarai bali Sara.

 

“Mimi agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, wala jina lako hutoitwa tena Ibrahimu kwani ni mekuweka uwe baba wa mataifa mengi. Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana nami nitakufanya kuwa mataifa na wafalme watatoka kwako “ Mwanzo 17;4-6.

“Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo hutamwita jina lake Sarai kwakuwa jina lake litakuwa Sara. Nami nitambariki naye atakuwa mama wa mataifa na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake” Mwanzo 17;16.

 

Mfano 3. Yakobo

Yakobo alishindana na malaika wa Mungu, aking’ang’ania  Baraka. Lakini malaika alimuona Yakobo Baraka anazo ila kwasababu ya jina malaika akawa anaona ugumu kutoa Baraka mapaka akamuuliza jina lake naye akasema Yakobo hutaitwa tena Yakobo bali Israel.

“Yakobo akakaa peke yake na mtu mmoja akashindana naye mweleka hataalfajiri. Naye alipoona ya kuwa hamshindi alimgusa panapo uvungu  wa paja lake,

 

 ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. Akasema niache niende maana kunapambazuka. Akasema sikuachi usiponibariki, Akamuuliza jina lako nani, Akasema Yakobo. Akamwambia jinalako halitakuwa tena Yakobo bali Israel maana umeshindana na Mungu na watu nawe umeshinda. Yakobo akamuuliza akasema niambie tafadhali jina lako, Akasema kwanini waniuliza jina langu? Akambariki huko Yakobo akapata mahali pale Peneli maana alisema , nimeonana na Mungu uso kwa uso na nafsi yangu imeokoka” Mwanzo 32;24-30, Kwahiyo sasa baada ya kuokoka tumepewa majina mapya ,Majina yetu yamebadilishwa tunaitwa

 

a)Sisi sasa ni wana wa Mungu/watoto wa Mungu na baada tu ya kutubu dhambi zako (kuokoka) moja kwa moja ulimwengu war oho jina lina badilika.”Tazameni ni pendo la namna gani aliotupa Baba kwamba tuitwe wana wa Mungu na ndivyo tulivyo. Kwasbabu hii ulimwengu haututambui kwakuwa haukumtambua yeye 1Yohana 3;1” “Kwakuwa ninyi nyote  mmekuwa wana wa Mungu  kwa njia ya Imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo  mmemvaa Kristo” Wagalatia 3;26-27.

 

i)Majina yetu yameandikwa katika kitabu cha uzima.

Kwahiyo tunapookoka tunatakiwa kwendelea na wokovu ilimajina yetu yasifutwe.

“Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima name nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu na mbele ya malaika zake” Ufunuo 3;5

“Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandika katika kitabu cha uzima alitupwa katika lile ziwa la moto” Ufunuo 20;15

 

 

ii)Utaanza kuzijua siri za ufalme wa Mbinguni unapokuwa umeokoka unakuwa umejiunganisha na ufalme wa mbinguni yaani Mungu Baba anakujua , Mungu Mwana anakujua, Mungu Roho Mtakatifu anakujua na Malaika zake nao wanakujua. Hivyo utaanza kuzijua siri za ufalme wa Mungu, jinsi ya kuenenda na haki zako.

“Akajibu akawaambia ,Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakukaliwa” Mathayo 13;11.

 

iii)Tunapokea nguvu

Wakristo sisi nguvu yetu ni Roho mtakatifu aliye ndani yetu, hivyo baada ya kuokoka Roho mtakatifu aliye ndani yetu, hivyo baada ya kuokoka anakuwepo ndani sasa ni wewe kwa kumchochea ndani yake kwa kusoma neno la Mungu, kufunga na kuomba, kumsifu Mungu na kumuabudu n.k.

Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yelusalemu na uyahudi na somaria na hata mwisho wan chi” Matendo 1;8

 

Roho mtakatifu akianza kufanya kazi ndani yako mambo kadhaa yatabadilika;

i). Utakuwa jasiri

ii).Hutaogopa vitisho vya watu

iii)Hutaona aibu kushuhudia Neno la Mungu(utalisema neno la Mungu kwa ujasiri

iv)Utakuwa mtii kwa Mungu.

v)Atakubadilisha matendo yako mabaya

vi)Atakupa maarifa, kukuonya, kukwelekeza n.k

 

b)Unakuwa silaha ya bwana ya vita siku zote Mungu ni roho ili atende kazi katika mapambano atakutumia wewe kwenye maombi, Roho mtakatifu atatumia kinywa chako, mikono yako katika kupambana.

 

“Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi nay eye ampendaye na kwa wewe,nilivunja-vunja gari la vita nay eye achukuliwaye ndani yake, na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto na kwa wewe nitawavunja-vunja kijani mwanamume na kijana mwanamke na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake na kwa wewe nitavunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe na kwa wewe nitavunja-vunja maliwali na maakida. Nami nitamlipa babeli na wote wakaao ndani ya ukaldayo, mabaya yao yote waliyoyatenda katika sayuni mbele  ya macho yenu, asema BWANA” Yeremia 15;20-24.

c) Sisi si wa ulimwengu huu.

Kikawaida Yesu kristo yupo siku zote nasi haja ukamilifu wa dahali, Yeye yupo Rohoni lakini anatenda kazi kiroho na kimwili, kimwili tunaonekana jinsi tulivyo lakini kristo si waulimwengu huu. Yesu anasema katika maombi na Mungu Baba.

Mimi nimewapa neno lako na ulimwengu umewachukia kwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu, mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu.Uwatakase kwa ile kweli yako, neno lako ndiyo kweli.” Yohana 17;14-17

 

 

iv)Tunapewa uwezo na mamlaka na amri

Tunaposamehewa dhambi zetu, Yesu kristo anatupa mamlaka juu ya viumbe wote “Akawaita wale thenashara akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhiMathayo 9;1-2.

Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu wawatoe nakupooza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina”  Mathayo 10;1.

 

d)Wewe sasa ni mwali wa moto

Mungu anawapenda wana wake siku zote, katika maisha ya wokovu Mungu anatuwekea moto(miali ya moto) inakuwa ikitunzunguka pande zote. “Na kwa habari ya malaika asema, afanyaje malaika wake kuwa upepo na watumishi wake kuwa miali ya moto “Waebrania 1:7. Wewe ni mtumishi wa Mungu upo katika himaya yake (ndani ya ufalme wake).

Unapata ulinzi.

Unapo okoka unapata ulinzi toka kwa mungu kwa kuwatuma malaika zake wakulinde.  “Malaika wa bwana hufanya k…….akiwazungukia wamchao na kuwaokoa “. Zaburi 34:7

 

Sisi ni Nuru ya ulimwengu

Tunapo okoka tunafanyika kuwa kielelezo kwa wengine, kwa matendo yetu yanatakiwa kuwa mema ili wamtukuze baba yetu wa mbinguni.

Ninyi ni nuru ya ulimwengu mji hauwezi kusitirika ukwa juu yam lima –wala watu hawa washi taa na kiuweka chini ya pishi bali juu ya kiango nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu wapate kuyaona matendo yenu mema wamtukuze baba yenu aliye mbinguni

 

 

Mathayo 5:14-15

Sisi ni chumvi ya dunia

Unapompa Yesu Kristo maisha yako/ Mungu anakufananisha na chumvi, kwamba sisi ni msaada kwa wengine ambao hawamjui Mungu tunapokuwa sehemu hiyo lazima tuwabadilishe.

Ninyi ni chumvi ya dunia lakini chumvi ikiwa imeharibika itakuwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa ila kutupwa nje kukanyagwa na watu” Mathayo 5:13