AINA ZA WASHIRIKA WAKOROFI KWENYE MAKANISA YENYE WACHUNGAJI VIONGOZI VIJANA
01. WASHIRIKA WASIOTAKA MAOMBI WALA KUJIFUNZA NENO LAKINI WANATAKA UWAPE NAFASI YA KUFUNDISHA NA KUHUBIRI KILA MARA.
Washirika Hawa Hupenda sana kuonekana na Kujionyesha kuwa wanajua hata kama hawajui.
Washirika wa jinsi hutawakuta kwenye maombi , Madarasa ya neno au mikusanyiko ya vikundi kanisani ila wakija wanataka Uwapishe uwaachie madhabahu.
NB: Ukiwapa Nafasi washirika kama hawa kanisani Unatengeneza washirika wasiojali sauti ya Mchungaji wao, Na Wengi huangukia Mafunuo Batili Na Ujanja ujanja wa kidali katika Huduma.
02. WASHIRIKA WAPINGA UONGOZI , LOLOTE KIONGOZI ANALOSEMA WAO WAPO KINYUME NAO.
Aina hii ya washirika ni Hatari sana mfano wake ni Kora , Dathani na Abiramu , unaweza kusoma habari zao kutoka katika biblia kitabu cha Hesabu, Washirika wa jinsi HUTENGENEZA MIKUSANYIKO KINYUME NA MCHUNGAJI
Hesabu 16:1-3.
1. Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni;
2. nao, pamoja na watu kadha wa kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa;
3.nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, BWANA naye yu kati yao; n’nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa BWANA?
NB: Mchungaji wa kanisa la mahali pamoja Ukiona watu kama Kora usiwape hata nafasi ya kusimama mbele au Kuongea na washirika , Watu hawa lolote wanalofanya lengo lao mwishoni ni Kuiba na kuigeuza mioyo ya washirika kinyume cha mchungaji wao.
03. WASHIRIKA WANAOMCHUKULIA MCHUNGAJI KIONGOZI KAMA KIJANA WAO , HIVYO AKILETA MAONO WANAMWITA PEMBENI KUMKEMEA NA KUMWAMBIA UWE TARATIBU HAYO MAONO NI MAKUBWA.
Mara nyingi washirika wa jinsi Hii huwa wanahisi kwa sababu ni wakubwa kiumri basi wanatakiwa kumuongoza mchungaji na kumuamuru nini cha Kufanya , washirika kama hawa hupenda kuita makanisa yenye viongozi vijana kama makanisa ya watoto.
Kuna wakati Petro aliona kama Yesu anakosea mafundisho yake kwa kueleza kuwa kuna siku atakufa na kufufuka akamwita pembeni akamkemea kiongozi wake ,
Matthew 16:21-23
21.Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.
22.Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.
23.Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu. Msalaba na Kujikana
NB: Washirika Wa Jinsi Hii Wape nafasi ya kuwasikiliza na Kuyapima mashauri yao kama yatakupigisha hatua katika Huduma au La.
04. WASHIRIKA WANAOJUA KUTOA AHADI ZA MICHANGO TENA MIKUBWA WANAONGEZA MATUMAINI KWENYE MALENGO YA KIFEDHA KATIKA MIRADI YA KANISA LAKINI HAWATOI , LENGO LA HUWA NI KUPATA SIFA TU.
Ogopa sana ikiwa watu hawa wakatoa ahadi na wasizitimize wanakatisha tamaa wengine kutoa hata kama walikuwa wanatoa kidogo.
MITHALI 20:25
“Ni mtego kwa mtu kutamka kwa haraka neno la nadhiri, kisha baadaye kufikiri juu yake.”
NB: Ukiwajua washirika wa Jinsi Hii Usiwape nafasi ya Kuahidi Tena kama hawaondoi nadhiri zao hii ni njia Ya Kuwalinda na Kuwapa nafasi ya Kujitathimini.
05. WASHIRIKA WANAOTONGOZA WAPENZI WAPYA KILA SIKU NA WANALETA KUTAMBULISHA KWA MCHUNGAJI LAKINI HAWAOI.
Washirika wa jinsi Hii huwa na mioyo myepesi katika kuanzisha mahusiano na kutoka mwishowe hutengeneza makovu kwa washirika yasiyopona.
Katika kizazi cha sasa jambo hili si kwa vijana tu bali hata mabinti anaanza mahusiano na kijana akiona hana pesa anampiga chini anaanza mahusiano mengine mapya, Hakuna Uaminifu , KANISA LINAJAA WASHIRIKA WENYE MAGONJWA NA VIDONDA VYA MAHUSIANO.
06. WASHIRIKA WANAOJUA TAARIFA ZA WASHIRIKA WOTE KANISANI NA KAZI YAO KUBWA NI KUTOA MAELEKEZO KWA WASHIRIKA WAPYA KWA KUSEMA HABARI ZA NDUGU ZAKE.
Mithali 20:19
19. Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.
“Mchongezi Hueneza Siri, basi usishirikiane naye azidishaye midomo yake.”
07. WASHIRIKA WAKOPAJI , KILA MTU KANISANI ANAKUWA ASHAKOPWA NA HALIPI.
Psalms 37:21
“21.Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.”
Hawa utawasikia wanasema Una Laki Hapo nitumie mara moja jioni kuna mchongo nausikilizia nakurudishia , Kwa sababu ni mpendwa Unampa Baada ya Hapo Harudishi, Hapokei simu , Hajibu sms , Akija kanisani anakuwa wa kwanza kuondoka asikutane na mtu.
Watu wa jinsi wakikutana na mshirika tajiri kanisani wanampiga kitu kizito mpaka mshirika anahama mpaka umegundua hilo tatizo ushapoteza washirika wapya wa maana.
NB: Usizoee kukopesha wapendwa ni Bora utoe kama sadaka ili kudumisha umoja
08. WASHIRIKA WASIOJALI WANAVYO VAA WAKIDAI MUNGU ANAANGALIA ROHO TU :
Washirika hawa hupenda mavazi yanayowaonesha maungo yao , Na ukiwasema tu unaonekana mchungaji una changamoto , Washirika Hawa Huwa na nguvu sana ya kuwavuta vijana wajinga kwa tamaa,
1 Timothy 2:9
“9.Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi.”
NB: Unaweza Usijali Kuhusu mavazi kama mchungaji lakini Watu ambao tumeitwa kuwa nuru kwao Wanajali na wanalitambua kanisa kwa namna mnavyo vaa Pia.
09. WASHIRIKA WANAOLIGAWA KANISA , ENDAPO KUNA WAHUDUMU ZAIDI YA MMOJA.
Washirika kama Hawa hutengeneza makundi ndani ya kanisa , Utakuta wako wanaosema mimi simuelewi mchungaji namuelewa mzee fulani , Wengine wanasema mimi simuelewi Mtu fulani akiongoza sifa , [ WASHIRIKA HAWA HULIGAWA KANISA NA KUFANYA KANISA LISITAWALIKE]
1 Corinthians 1:12-13
“12.Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.
13.Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?”
Washirka hawa hutumia Fedha na mali katika kuimarisha makundi yao ndani ya kanisa, Mchungaji asipokuwa makini washirika hawa huweza kulipasua kanisa au kufanya kanisa lisitawalike kabisa na Huduma kuwa ngumu.
10. WASHIRIKA WANAOPENDA KUFUATILIWA SANA NA KUPEWA AHADI NYINGI ILI WAJE KANISANI.
Washirika wa jinsi wanapenda mchungaji uwapigie simu kila wakati , uwatumie message na uwape Ahadi nono kabla hawajaja kanisani na usipofanya hivyo Unakuta hawaji kabisa kanisani , Kabla ya siku ya ibada wanataka usiku uwapigie simu , wanachosha sana hawa.
Aina hii ya washirika wanapenda wakija kanisa uwape ahadi za chakula , Juice au nyama choma ili waje kwenye ibada au mikesha ,
NB: Mchungaji mzembe Huwazoesha washirika wa jinsi Hii Na Kutengeneza kanisa na washirika dhaifu wasioweza Kujisimamia .