Monday, October 20, 2025

SABABU ZINAZOWEZA SIMU YAKO KURIPUKA


 1️⃣ Kutumia Charger Isiyo Halisi 

➡ Charger fake au isiyo ya kampuni ya simu yako haina voltage sahihi.

➡ Inaweza ku-overcharge betri na kusababisha joto kupita kiasi.

2️⃣ Overcharging (Kuchaji Kupita Kiasi)

➡ Kuweka simu chaji muda mrefu (hasa usiku kucha) hujaza voltage nyingi.

➡ Joto likizidi, betri inaweza kuharibika au kulipuka.

3️⃣ Kutumia Simu Wakati Inachaji 

➡ Unapopiga au kucheza game ukiwa kwenye chaji, simu inapata pressure kubwa (charging + usage).

➡ Processor na betri hupata joto kupita kiasi.

 4️⃣ Kuweka Simu Kwenye Joto Kali

➡ Mfano: ndani ya gari lenye joto, karibu na cooker, au chini ya jua.

➡ Hii huongeza pressure ndani ya betri (lithium-ion).

5️⃣ Betri Iliyoharibika au Iliyovimba 

➡ Ukiona betri imevimba, toa mara moja na usitumie tena.

➡ Ni hatari kubwa ya mlipuko. 

 Charger Kuwa Na Tatizo la Wiring

➡ Wayar zilizochomeka au soketi za ajabu hupeleka voltage isiyo thabiti.

➡ Inaweza kusababisha short circuit kwenye simu. Kufunika Simu Wakati Inachaji 

➡ Kuweka simu chini ya mto, blanketi, au mfuko wakati inachaji ni kosa kubwa.

➡ Joto hukwama ndani, na betri inapata hatari ya kulipuka.

 Kumbuka:

➡ Tumia charger original pekee

➡ Usichaji simu ukiilalia

➡ Zima Wi-Fi, data na game wakati wa kuchaji

➡ Usipuuzie betri ikianza kuvimba au kutoa harufu ya moto

No comments:

Post a Comment