Friday, October 10, 2025

WATUMISHI WA MUNGU TUJIFUNZE KITU HAPA

 MUDA WANGU MFUPI KATIKA HUDUMA YA KICHUNGAJI, NIMEJIFUNZA JAMBO HILI MUHIMU KWA USTAWI WA KANISA.

Katika muda wangu mfupi wa huduma ya kichungaji, MUNGU amenifundisha jambo hili

"KILE UNACHOWAFUNDISHA WATU WAKO NDICHO WATAKACHO KIAMINI NA KUKIFANYA"

Dag Heward Mills anasema "Washirika watatii na kufuata kile mchungaji anawafundisha"

KWA KAULI HIZO NIKAELEWA KUWA;

1:- Chochote ambacho nataka washirika wa kanisani wafanye, sharti niwafundishe kwanza. Ni mara chache kuona mshirika akifanya kile ambacho hajasikia mchungaji wake akifundisha au kukazia.

2:- Chochote/lolote ambalo sijawafundisha watu nilioletewa na Mungu, sipaswi kulaumu ikiwa hawajalitenda vile napenda litendeke.

KATIKA MAZINGIRA HAYO NIKAELEWA KUWA

1:- Mchungaji anapaswa kuwa mpanda mbegu katika mioyo ya watu kwa jinsi ya fundisho la Kristo. Kadri fundisho la Kristo linavyopata nafasi ya kutosha katika mioyo ya watu, ndivyo Kristo huzidi kuumbika ndani yao(Rum 10:17)

2:-Mchungaji hapaswi kuogopa katika kuwafundisha watu wake,kufanya hivyo ni kuwanyima watu fursa ya kujitoa, kujituma na kujidhabihu kwa ajili ya kazi ya MUNGU.

•Mchungaji usisubirie mpaka mgeni aje kanisani ndio awafundushe watu uliopewa na MUNGU. Endelea kuwafundisha kwa kadri uwezavyo, umeaminiwa na MUNGU kwa ajili ya kuilisha hiyo familia uliyokabidhiwa!

•Unataka watu waombe, hakikisha unawafundisha kuhusu maombi...Kisha omba nao Mara kwa Mara, baada ya muda mfupi utaona matokeo.

•Chochote unachotaka washirika wafanye, wekeza maarifa ndani yao

No comments:

Post a Comment