Friday, October 10, 2025

MAMBO YANAYOKUFANYA WADHALAULIKE WATUMISHI WA MUNGU

 MAMBO YATAKAYO FANYA HUDUMA YAKO KAMA KIJANA KUDHARAULIKA NA WATU AU WATUMISHI WENZAKO

01. KUMKOSA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO.

Ukimkosa Mungu , Umekosa Heshima , Ukimshika Mungu umebeba Heshima.

Katika Umri ambao Mungu hutengeneza watu wenye Heshima ni Ujana , Na Katika Umri ambao shetani huwaandaa Vijana wanao onekana watumishi lakini ni wa Hovyo na watazaa aibu Ni Ujanani.

Ikiwa kijana Mungu amekupa nafasi Ya Utumishi mwandame Katika kila siku mpya ili akuheshimishe , Imani yako na Upendo wako kwa Mungu uwe kielelezo kwa watu wote.

02. KUKOSA MAONO YALIYO WAZI KUHUSU NINI MUNGU ANATAKA KWENYE HUDUMA YAKO NA WAPI UNAELEKEA.

Maono ya Kijana Katika Huduma na namna anavyo yaishi maono yake Huleta Heshima , Bali kijana mtumishi asiye na maono kila kitu atataka kufanya , Kila mahali atataka kwenda , Na Kila mtu atataka kumuiga , Na Kila style ya maisha atataka kuishi kwa sababu Hana maono :

NB: Maono Kwa Kijana yanampa Nguvu ya Kufocus na Nguvu ya Kuzaa matokeo yenye Tija Yanayoshikika.

03. KUMFANYA KILA MTU MZAZI WAKO WA KIROHO NA MENTORS KILA MAHALI.

Moja ya Baa kubwa linaloleta dharau kwa vijana wengi ni Kutaka kila mtu maarufu awe baba yake wa kiroho , Kila mchungaji maarufu mtandaoni ni mentor wake na mlezi wake , 

Katika maisha ya kawaida tu mtoto anayekula kula kwa watu anaitwa mlafi na mwenye tamaa , Watumishi wengi vijana wanaonesha tabia ya tamaa kwa kufikiri kuwaita wachungaji maarufu ni mababa zake , Unatoka baba X kwenda Y , Kesho uko kwa Baba A , Tena unahama unaenda kwa baba H

NB: UTULIVU HULETA HESHIMA KUTANGA TANGA HULETA DHARAU 

04. KUDEKA DEKA KWA WATU ILI WAKUONEE HURUMA KAMA WEWE NI MTUMISHI WA MUNGU.

Watu watakuheshimu kwa kadiri unavyo onesha kumtegemea Mungu kupo kwa Namna Gani.

Tupo katika kizazi ambacho vijana wengi wapo kwenye Huduma na hawajui mipaka yao kwa washirika au watu , Unakuta mtumishi wa Mungu kijana amejaza inbox za watu akiomba omba fedha au anatembelea watu kueleza shida zake ili aonewe huruma , Huo ni Utoto wa kiroho acha haitakujenga.

05. KUOMBA OMBA WATU PESA INBOX, HASA PESA ZA MATUMIZI YAKO BINAFSI KAMA CHAKULA , KODI YA NYUMBA AU MAVAZI.

Ni fedheha mtumishi wa Mungu Kuomba Omba kwa watu chakula , Mavazi au kodi Ya Nyumba , NI BORA SANA KUMUOMBA MUNGU. Ni Mbaya sana kwa mtumishi wa Mungu kuwalemea watu katika kupata mahitaji yako Bonafsi.

2 Corinthians 11:9

“9.Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda.

06. KUKOSA UTARATIBU NDANI YA KANISA, IBADA  ISIYO NA UTARATIBU INALETA DHARAU KWA KIONGOZI WA KANISA.

1 Corinthians 14:40

Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.

07. KUWA NA WASAIDIZI WALIOKOSA AKILI AU MAARIFA YA HUDUMA [ WATU HAWA WANAWEZA KUKURUDISHA NYUMA KILA SIKU].

Kila msaidizi unayemuweka kwenye Huduma yako ni sura yako na maonyesho ya tabia zako, 

Msaidizi mwema kwenye Huduma atakuletea heshima bali msaidizi mbaya atakuletea Mavuno ya dharau kwenye Huduma yako, Chagua kwa hekima na Uongozi wa Roho Mtakatifu mtu anayeweza kukukaimu majukumu Yako au anayeweza kusimama na wewe Vema .

08. KUMDHARAU MUME AU MKE WAKO KUTAFANYA HUDUMA YAKO IDONDOKE KABISA.

Waebrania  13:4

4.Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

09. KUVAA VIBAYA NI NYAVU YA KUVUA DHARAU .

Moja ya mtego mdogo ila wenye kuvuna dharau nyingi ni Mavazi, Kuna watu walikuwa wanaheshimika vema kabisa ila mpaka walipovaa mavazi fulani, 

Mavazi yanaweza kuleta aibu au heshima, Mpangilio wa Uvaaji wako unaweza kuleta heshima au dharau ,

NB: Mavazi ni Jambo la Kiroho sana Usipuuze.

10. KUPOST MAMBO YASIYO FAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII NA KUENDANA NA UADILIFU WA HUDUMA HUONGEZA DHARAU.

Kila jambo ambalo unalifanya kupitia mitandao ya kijamii linaweza kukuweka kwenye kundi la watu watakao pokea heshima au wale watakao pokea dharau, 

Mitandao ya kijamii inaweza kuvuta watu heshima wakuheshimu au watu wenye dharau wakudharau.

11. KUAMBATANA NA WATUMISHI WASIO NA MAADILI NA WASIOTAKA KUBADILIKA HATA WAKIONYWA.

Mithali 13:20

“20.Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.”

12. KUKOPA WASHIRIKA WAKO FEDHA AU KUWALAZIMISHA WAKUPE FEDHA  , 

Mtumishi kijana anayekopa kopa washirika fedha Huishia kwenye fedheha na dharau kabosa ,

Fikiri kidogo , Mchungaji madhabahuni unahuburi halafu mshirika anakudai yuko kanisani anakusikiliza ukisema pokea fedha , Mshirika anawaza nikitoka hapa namdai , Na Mchungaji unachukua sadaka kila siku kulipa madeni ambayo ulipata kwa sababu ya matumizi binafsi. NI AIBU.

NB: EPUKA KUKOPA WASHIRIKA AU KUWALAZIMISHA WAKOPE ILI WAKUPE WEWE FEDHA 

WEWE NI KIJANA, UNA NDOTO ZA KUWA MTUMISHI WA MUNGU, HII NI FURSA YAKO.

No comments:

Post a Comment