Friday, November 14, 2025

LIQUIDITY LOCKED NI NINI?


1. Liquidity Locked ni nini?

Liquidity Locked ni hatua ambayo Dev anafunga liquidity (LP tokens) kwenye lockers kama:

-Unicrypt

-PinkSale Lock

-Team Finance

Hii inazuia Dev kuchukua fedha za liquidity kwa muda fulani, mfano mwezi 1, miezi 6, mwaka 1 au zaidi.

 Kwa nini Liquidity inafungwa?

-Kulinda wawekezaji wasiporwe

-Kuzuia rug pull

-Kuonyesha project ni serious

Bila liquidity lock:

Dev anaweza kutoa liquidity yote mara moja → token inaporomoka → watu wanapoteza hela.

2. Rug Pull ni nini?

Rug pull ni utapeli ambapo Dev anachukua liquidity kisha kutoweka.

Aina mbili za rug pull:

1. Liquidity Rug

Dev anatoa liquidity yote → token haiwezi kuuzwa → bei inakuwa 0.

2. Mint / Supply Rug

Dev ana uwezo wa kuchapisha token mpya nyingi → anaziuza kwa wingi → bei inaporomoka.

3. Jinsi ya Kujua Token ya Scam

Hizi ndizo dalili za haraka:

 1. Liquidity haijafungwa

– Angalia kama LP tokens zipo locked.

– Ikiwa zimefungwa kwa muda mfupi sana (saa 24, siku 7), sio salama.

2. Contract haina audit

– Hakuna audit kutoka Certik, SolidProof, Hacken.

3. Dev ana wallet yenye supply kubwa

– Dev akimiliki 20%+, token ni hatari sana.

4. Buy/Sell Tax kubwa (kama 15–25%)

– Mara nyingi hutumika kutapeli liquidity.

 5. Dev anaweza:

Kuzuia watu kuuza (blacklist function)

Kubadilisha tax wakati wowote

Kumiliki contract yenye authority kubwa sana

6. Liquidity ndogo sana (chini ya $10k)

– Inaleta risk kubwa ya price manipulation.

  Jinsi ya Kujilinda

✔ Angalia liquidity lock

✔ Soma contract kwenye BscScan / Etherscan

✔ Angalia community — kama ina hype tu bila facts, kuwa makini

✔ Tumia tools kama:


-Token Sniffer

-DexTools

-GoPlus Security


No comments:

Post a Comment