Thursday, May 15, 2025

BEELZEBURI (Mkuu wa mapepo)

 

BEELZEBURI (Mkuu wa mapepo)

Beel maana yake ni mkuu/bwana

Zeburi maana yake ni mapepo wachafu

Beelizeburi ni shetani anayesimamia mapepo yote kwa kuyapa amri Marko 3:20-30,Mathayo 12:22-24,Luka11:24.Mapepo tabia zao ni anataka kuishi sehemu ambapo hapana maji (makavu/pakavu) pasipo na maji maana yake ni moyo mkavu-Roho Mtakatifu hayupo,na mapepo hayana makao maalumu yanasubilia kualikwa/kuitwa Marko 16:9,nchi ya Wagerasi Marko 5

AMEFUNGWA KWENYE MTI

Mti ulitumika kwenye Biblia kama sehemu ya mwisho ya hukumu kwa mtu.Mtu akifungwa kwenye mti baada ya hapo ni kifo.wachawi wanaweza kuutumia mti kama gereza kuyafunga maisha ya mtu au mafanikio ya mtu Yoshua 8:28-29,Esta 7:8-10,2:23,Danieli 4:13-14,Mathayo 27:38-40

Maombi

-kuwapiga waliokufunga kwenye mti

-kushuka kwenye mtu

KUONDOA VIZUIZI VYA KISHETANI

Vizuizi ni vikwazo

Adui wa maisha ya kila mtu ni shetani,shetani ni roho hutenda kazi kupitia mawakala wake ambao ni wachawi,wasoma nyota,waganga wa kienyeji n.k wanauwezo wa kukaa kwenye masomo,elimu,ndoa,kazi,biashara,fedha,maendeleo 1Wathesalonike 2:18,Mathayo 8:23-28,Danieli 10:11-14

Maombi

-kuwapiga wanaokuzuia

-kuondoa vizuizi

SAA INAYORUDI NYUMA

Saa ni kifaa kinachoonesha mudauliopo.Kuna saa za analogia na kuna saa za kidigitali.Kuna saa za asubuhi,kuna saa za mchana,kuwa saa za jioni,kuna saa za usiku.Zamani hata sasa walikuwa wanatumia jua,mwezi,sauti Marko 14:32-42,Mathayo 27:45-50,Mathayo 10:19-20,Mathayo 24:36,25:13.Shetani anaweza kuiona saa yako badala ya kwenda mbele yeye anairudisha nyuma au anaisimamisha mfano biashara,kazi,familia,elimu.Anakuwekea saa feki,

BADILI LUGHA YAKO

Maana ya lugha.Kuna lugha ya mazungumzo,maandishi,vitendo,picha.Kila nchi ina lugha yake ya taifa,lugha ndiyo chombo cha mawasiliano mfano mke na mume.Lugha ndiyo nguvu ya mahusiano 1Wakorintho 13:1

Lugha za wanadamu,za malaika,mashetani

Kunena kwa lugha ndiyo lugha ya ufalme wa Mungu lakini unaponena kwa lugha inapaswa moyo wako uwe safi unaweza ukawa unaongea vitu vingine kwa Mungu au shetani akatumia kinywa chako,hapa unapaswa kuwa makina sana.Matendo 2:1-4,Warumi 8:26,1Wakorintho 14:2.Sema nabadilisha lugha ya magonjwa,umasikini,shida,balaa,laana,mikosi,kushindwa n.k juu ya maisha yangu kwa jina la Yesu Kristo

No comments:

Post a Comment