Tuesday, May 6, 2025

BARAKA ZA MWEZI WA TANO

 BARAKA ZA  MWEZI TANO

1. Mbingu zako ziwe wazi mwezi huu, Ufurahie baraka toka kwa Bwana kila Eneo la Maisha yako.

2. Malango ya kubarikiwa kwako mwezi huu yawe Wazi daima usiku na mchana.

3. Mwezi Mei na Uwe wa habari njema kwako, kwa Uwekezaji wako na Familia.

4. Na uwe mwezi wa hatua mpya na za utukufu kwenye projects zako na biashara .

5. Mwezi Mei ni mwezi wa Shuhuda Mpya na za Utukufu kwako. Naamuru Shuhuda Mpya zichipuke .

6. Mungu na akupe Amani mwezi huu, kwenye Ndoa na Ajira na Biashara

7. Kama kuna kitu chema kilikufa kwa hatima yako Mwezi kifufuke.

8. Na huu uwe mwezi wako wa Mipenyo na fursa mpya kwako, kwenye hatima yako kitaifa na kimataifa, MACHO YAKO YATIWE NURU UONE FURSA ZAKO MWEZI HUU.

9. Na huu uwe mwezi wa Amani, Furaha na kicheko kila Eneo. 

10. Mungu na AKUEPUSHE na hasara na kuharibiwa mwezi huu.  Na ulindwe na kuepushwa na maovu yote. 

11. Ninakuunganisha na masaa yako ya Mpenyo mwezi huu.

12. Ninakutuma Ukafanikiwe na Kustawi kila Eneo mwezi huu, Ninakutuma Ukamiliki na Kuongezeka mwezi huu kwa ajili ya Kristo Yesu .

NA HAKIKA HUU NI MWEZI WAKO WA VIWANGO VIPYA NA MIPENYO MIPYA,

KTK JINA LA YESU

No comments:

Post a Comment