Saturday, May 10, 2025

NAWAPENDA WALE WANIPENDAO

 *🌲KAMA NINGALIWAZA MAOVU MOYONI MWANGU,BWANA ASINGESIKIA, HAKIKA MUNGU AMESIKIA; AMEISIKILIZA SAUTI YA MAOMBI YANGU. Zaburi 66:18-19🌲.Ee  Yehova Mungu Muumba wetu, Kwa mkono wako hodari, Umeiamuru tena ipambazuke asubuhi nyingine mpya siku  ya Ijumaa ya kwanza  ya  mwezi, tarehe mbili May 2025. Hii ikiwa ni weekend  ya kwanza ya mwezi May🌲🌲.Ee Baba yetu, tunazo sababu zote za kukurudishia wewe, shukurani, sifa na utukufu  kwa ulinzi ulio tupatia usiku kucha, hata asubuhi hii ya pili ya mwezi. Baba, kwa Roho wako Mtakatifu, utuongoze tena katika ibada zetu za maombi na maombezi ya ijumaa ya kwanza mbele yetu zikisalia siku 243 kabla  ya kuumaliza  mwaka huu wa 2025💫.Baba tupe kulitunza neno lako mioyoni mwetu ili tusipate kuwaza maovu ambayo huzuia usitusikie tukuombapo. Baba yetu, endelea kutuepusha na majanga mbali mbali nchini mwetu, zikiwemo ajali mbaya na nyingi zinazo tokea kila uchao. Pia uendelee  kutupatia  mvua za utulivu zenye neema ya chakula🌽🌾🌻🥔 . Mwisho kwa wale wote wanao safiri leo kwa njia mbalimbali, uwaongoze kwa Mkono wako hodari ili wafike salama kule waendako. Kwa machache haya na yale yote ambayo sijayatamka  twakuomba ututendee yote kwa  jina la Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu Aamin

*🌲NAWAPENDA WALE WANIPENDAO, NA WALE WANITAFUTAO KWA BIDII WATANIONA. Mithali 8:17🌲.Ee Yehova El-Shadai, Mungu wetu Muumba wa Mbingu na nchi uishiye milele. Umetupatia tena  siku mpya ya jumamosi ya pili  ya mwezi, tarehe kumi May 2025 🌲🌲.Ee Baba yetu , pokea shukurani zetu za dhati na adhama, Sifa na Utukufu wewe peke yako, kwa ulinzi uliotufanyia usiku kucha hata  tumeiona siku ya kumi ya mwezi . Ee Baba twakuomba kwa Roho wako Mtakatifu, utuongoze  tena weekend hii ya pili ya May tunapokabili majukumu yetu, pamoja na maandalio ya mioyo yetu kwa ajili ya ibada  za kesho siku ya jumapili ya  pili ya May, tutakapoingia ibadani ili kulihimidi jina  lako na kukuabudu kwa furaha, na kukutafuta uso wako kwa bidii ili ujifunue kwetu wewe pekee uliye kimbilio na nguvu na msaada uonekanao tele wakati wa mateso, mbele yetu zikiwa zimesalia siku 235 ili kuufikia mwisho wa mwaka huu wa 2025 💫. Baba yetu, endelea kutuepusha na majanga mbali mbali, kama ajali zinazo tokea mara kwa mara na kuchukua uhai wa ndugu zetu. Baba yetu, tunakushukuru sana pia kwa ajili ya mvua ambazo  zimenyesha vizuri sana, na sasa huku kwetu tayari tumeanza kuvuna 🌽🥔🌾🌻. Ee Baba yetu, tunawaleta kwako wale wote wanao safiri leo kwa njia mbalimbali, uwaongoze kwa Mkono wako hodari ili wafike salama kule waendako. Kwa machache haya, na yale yote ambayo sijayatamka,  twakuomba ututendee yote kwa  jina la Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu Aamin* 

No comments:

Post a Comment