MASHIMO YA KICHAWI (Kiroho)
Agano la
kale mtu alipokuwa anafanya kosa au makosa alikuwa anahukumiwa kwa kutupwa
kwenye mashimo marefu.
Mashimo yaliyokuwepo
i.
Mashimo
yenye wanyama mfano Danieli
ii.
Shimo
lenye moto mfano Shedraka,Meshaki na Abednego
iii.
Shimo
lenye maji mengi au matope mfano Yeremia 38:6
iv.
Shimo
lisilo na kitu
Sasa
Shetani naye
vile vile naye ameyaweka mashimo yake haya kwa namna ya kiroho,hayaonekani kwa
macho ya kawaida kwasababu shimo lenyewe ni roho kamili,lina akili,linaweza
kukimbia na ukiingia ndani huwezi kutoka linageuka na kuwa giza.Zaburi
35:7,Ufunuo 9:1-2,Isaya 24:17,14:15,Isaya 38:18
Miji inaweza
kuwa na mashimo ya rohoni na utakaposhughulika na shimo hilo unakuwa umeuteka
mji.Kuna mashimo makubwa yaani kuzimu ya
angani,kuzimu ya baharini ,kuzimu ya nchi
Pia kuna
vishimo vidogo mfano mtu anachukuliwa msukule na kuwekwa
kabatini,kisimani,dukani,n.k Isaya 42:22
Kila mtu
amewekewa Baraka zake sehemu Fulani mfano kwenye
kinywa,tumbo,kumbukumbu,biashara,ndoa n.k
Familia,ukoo
wanawekwa kwenye mashimo ya
mauti,magonjwa,laana,mikosi,shida,balaa,utasa,umasikini n.k
Mambo unayotakiwa kuyafahamu kuhusu
kuzimu
i.
Malaika
wa kuzimu ufunuo 9:11
ii.
Makomeo
ya kuzimu Ayubu 17:16
iii.
Milango
ya kuzimu Ayubu 38:17,Mathayo 16:18
iv.
Kamba
za kuzimu 2Samweli 22;6
v.
Makao
ya kuzimu Zaburi 89:88
vi.
Shida
za kuzimu Zaburi 116:3
vii.
Kitanda
cha kuzimu Zaburi 139:8
Maombi
-kuyashambulia mashimo yote ya kichawi
-kuwateketeza walinzi wa mashimo
-kutoka shimoni
No comments:
Post a Comment