Tuesday, May 6, 2025

FUNDAMENTAL CRYPTO ANALYSIS

*FUNDAMENTAL ANALYSIS (FA)*

Fundamental Analysis ni mbinu ya kuchambua thamani halisi ya mali ya kifedha kwa kuchunguza mambo ya msingi yanayoathiri bei yake. Katika ulimwengu wa cryptocurrency, FA inalenga kuchambua vigezo kama:

*Utility ya Tokeni* – Je, tokeni ina matumizi halisi katika mfumo wake wa ikolojia?

*Team na Maendeleo* – Je, timu ya mradi ina uzoefu na uwezo wa kutekeleza maono yao?

*Tokenomics* – Ugavi wa tokeni, namna zinavyogawiwa, na mpango wa kuchoma (burning mechanism).

๐Ÿ‘‰ *Total Supply* 
Hii ni Jumla au idadi ya coin au Token zotee ambazo ziko kwenye Ecosystem.

๐Ÿ‘‰ *Circulating Supply*
Hi ni Jumla au idadi ya Coin au Token zote kwenye Ecosystem ambazo zinakuwa zimeshaingia kwenye mzunguko au sokon.

๐Ÿ‘‰ *Volume Supply*
Hii ni Jumla ya miamala yote ambayo imeshafanyika kwenye coin au Token Husika ndani ya masaa 24.

๐Ÿ‘‰ *Market cap*
Hii ni Jumla ya Mtaji wote ambao upo kwenye coin au Token ambazo ziko kwenye mzunguko.

NB:๐Ÿ‘‰Circulating supply ukiizidisha na Currency price ya Coin Husika ndiyo unapata Market cap.

*Community Strength* – Ushirikiano na ukuaji wa jamii inayounga mkono mradi.

*Partnerships & Integrations* – Je, mradi unaushirikiano gani wa kimkakati?

*Roadmap* – Mpango wa maendeleo wa mradi ukoje na je, wanafuata mipango yao?

*White paper* - White Paper ni hati rasmi ya kiufundi na kibiashara inayotoa maelezo ya kina kuhusu mradi wa sarafu ya kidijitali (cryptocurrency). Hati hii hutumika kueleza matatizo yanayolengwa kutatuliwa na mradi husika, suluhisho linalopendekezwa, teknolojia inayotumika, pamoja na maelezo ya kiuchumi kama vile tokenomics, usambazaji wa tokeni, na mpango wa maendeleo (roadmap).

*Umuhimu wa White Paper katika Mradi wa Cryptocurrency*

1. Kuaminika kwa Mradi:
White paper huonyesha uwazi na dhamira ya waandaaji wa mradi, hivyo kuongeza uaminifu kwa wawekezaji na jamii ya crypto.

2. Kutoa Maarifa kwa Wawekezaji:
Inawawezesha wawekezaji kuelewa thamani ya mradi, malengo, na nafasi yake katika soko kabla ya kuwekeza.

3. Mwongozo wa Maendeleo:
White paper ni dira ya kiufundi na kimkakati inayowaongoza watengenezaji wa mradi katika kutekeleza hatua kwa hatua kulingana na roadmap.

4. Kuvutia Ushirikiano na Rasilimali:
Wawekezaji wa taasisi, washirika wa kiteknolojia na jumuiya hupima ubora wa white paper kabla ya kujiunga au kuwekeza katika mradi.

5. Msingi wa Tokenomics:
Inafafanua kuhusu usambazaji wa tokeni, bei ya awali, matumizi ya fedha zilizokusanywa (fund allocation), na modeli ya uchumi wa tokeni.

Mfano:
Bitcoin white paper (iliyotolewa na Satoshi Nakamoto mwaka 2008) ndiyo msingi ulioanzisha mapinduzi ya fedha za kidijitali. Vivyo hivyo, kila mradi mpya unaotaka kuaminika lazima uandike na kuchapisha white paper yenye maudhui sahihi na ya kuvutia.

Hivyo Lengo kuu la Fundamental Analysis(FA):
Kupata picha halisi ya thamani ya tokeni kwa misingi ya kiuchumi, teknolojia, na mwenendo wa soko ili kusaidia wawekezaji kufanya maamuzi sahihi ya muda mrefu.

No comments:

Post a Comment