DHABIHU ZA MUNGU NI ROHO ILIYOVUNJIKA; MOYO ULIOVUNJIKA NA KUPONDEKA, EE MUNGU, HUTAUDHARAU.. Zaburi 51:17. Ee Yehova El-Shadai, Mungu Muumba wetu, wewe Utabaki kuwa Mungu wa pekee milele kwetu Ee Baba yetu. Tazama umeiamuru ipambazuke asubuhi nyingine mpya, siku ya jumanne ya kwanza ya mwezi, tarehe sita May 2025 mbele yetu zikisalia siku 239 kabla ya kufikia mwisho wa mwaka huu wa 2025. Baba yetu, pokea shukurani zetu za dhati ya moyo wa ndani wewe peke yako, kwa matendo makuu uliyotufanyia usiku kucha, macho yako yakitutazama mpaka asubuhi hii ya sita ya mwezi May. Baba si kwa uwezo wetu, au stahili yetu, la hasha, bali ni kwa neema na rehema zako tu, kwani kuna wenzetu wengi tuliokuwa nao siku ya kwanza ya mwezi huu, leo hii hatunao tena, kwani wametoweka,tena wengine kwa vifo vya ghafla, na bila tumaini la uzima wa milele. Ee Yehova, twajikabidhi mikononi mwako tena leo, ili utuongoze tunapo kabili majukumu yetu pamoja na ibada za baadaye leo jioni. Baba yetu, tuondolee kiburi , na utujalie moyo wa kuvunjika na kupondeka kwa kunyenyekea kwako, na iliyo tayari kufuata maagizo yako. Pia uzidi kututetea na kutuponya na majanga mbali mbali nchini mwetu , zikiwemo ajali na magonjwa mengi ya milipuko. Zaidi sana Ee Mola wetu, tunakushukuru kwa ajili ya mvua ambazo zimenyesha kwa utulivu, na sasa tumeanza kuvuna. Na kwa wale wote wanao safiri leo kwa njia ya anga, ardhini na majini, twakusihi utuongoze kwa mkono wako hodari ili tufike salama kule tuendako . Kwa machache haya, hata yale ambayo sijayatamka, twakuomba ututendee yote kwa jina la Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu.
No comments:
Post a Comment