Thursday, May 1, 2025

KUZIKOMBOA SEHEMU ZA MTU

 

KUZIKOMBOA SEHEMU ZA MTU

-Roho

-Nafsi

Mwili

Kikawaida ili mtu aweze kuharibikiwa au asifanikiwe,shetani huwa anashughulika na sehemu hizo,ili kuleta uharibifu

1.     Mji wa Mafanikio

Hapa tunazungumzia mali,fedha,uchumi mzuri,utajiri,maisha mazuri n.k

Torati 28:1-13

Hapa ni sawa na kusema password za maisha

2.     Mji wa Afya

Hapa tunazungumzia afya njema,uhai,kuishi

3Yohana 1:2,Mithali 3:7-8,Isaya 58:8,Yeremia 30:17,33:6.

Shetani akipachezea ndiyo mtu anakuwa mgonjwa,mauti,kifo,maumivu n.k

3.     Mji wa Mahusiano

Hapa tunazungumzia Mungu,urafiki,undugu,upendo.Shetani akipachezea hapa,chuki itatengenezwa hapa,unaweza kumuona mke/mumeo kawaida tu.1Samweli 18:1-5,Waamuzi 19:3,Yohana 15:13

4.     Mji wa Kumbukumbu

Hapa hunazungumzia akili,ufahamu,maarifa,kuelewa,kuyashika unayofundishwa.Hapa pakichezewa utaona mtu amejiua,amechanganyikiwa,kusahausahau n.k

5.     Mji wa Sheria

Hapa tunazungumzia kanuni,taratibu,hiyali ya mtu,amri,hekima,adabu,heshima,maadiki.Mithali 3:1

Hapa wizi ndio unapoanza kwa mtu kama pakiharibiwa

6.     Mji wa Ndoto

Hapa tunazungumzia uwezo wa kutafsiri ndoto,kuota,macho ya rohoni-kufunguka jicho la tatu.Danieli 5:12

7.     Mji wa Vita

Hapa tunazungumzia ulinzi,vita vya rohoni,maombi,mashambulizi,nguvu za kiroho

Hapa ndiyo kituo cha pepoau jinni Torati 20:19-20,Hesabu 21:14,waefeso 6:10-12

No comments:

Post a Comment