UNABII KWA MWAKA 2025
1. 2025 NI MWAKA WENYE NURU KILA ENEO LA MAISHA. Iwe biashara na Uwekezaji, Siasa na Uongozi ata Taaluma, Ndoa na Familia, Tutafufurahia Nuru ya Kiungu na hakuna kubahatisha wala kupapasa ktk Jina Yesu. π“Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.
— Zaburi 119:105 (Biblia Takatifu)
2. 2025 NI MWAKA WA KUCHUKUA HATUA ZA UHAKIKA KILA ENEO LA MAISHA. HAKIKISHA UNACHUKUA HATUA KTK ENEO LAKO LA HATIMA NA HAKIKA UTAFANIKIWA KTK JINA LA YESU. π“Uendapo, hatua zako hazitadhiikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa.
— Mithali 4:12 (Biblia Takatifu)
π“Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake. Hatua zake hazitelezi.
— Zaburi 37:31 (Biblia Takatifu)
3. 2025 KILA MWANA WA MUNGU ANAGEUZWA KUWA MWOKOZI KWA JAMII YAKE KWENYE ENEO LAKE, kupitia Biashara, huduma ata siasa na Uongozi. πObadia 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁷ Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.
²¹ Tena waokozi watakwea juu ya mlima Sayuni ili kuuhukumu mlima wa Esau; na huo ufalme utakuwa ni mali ya Bwana.
4. 2025 NI MWAKA WA KUFURAHIA KIBALI CHA KIUNGU KILA MAHALI UTAKAPOBISHA HODI NA KUCHUKUA HATUA. Iwe huduma, biashara na kila eneo KTK Jina La Yesu. π“Basi Mungu alimjalia Danielii kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi.
”
— Danieli 1:9 (Biblia Takatifu)
5. 2025 NI MWAKA WA KUFURAHIA SHUHUDA NYINGI MPYA NA ZA KUONEKANA KWA WANA WA MUNGU WATAKAO TUMIA IMANI KUTHUBUTU NA KUCHUKUA HATUA. π“Nimeambatana na shuhuda zako, Ee Bwana, usiniaibishe.
”
— Zaburi 119:31 (Biblia Takatifu)
6. 2025 KILA MWANA WA MUNGU ATAFURAHIA KUSAIDIWA NA MKONO WA BWANA KULITIMIZA KUSUDI LA KUISHI KWAKE NA KUSUDI LA HATIMA YAKE. π“Kisha Bwana akawapa raha pande zote, sawasawa na hayo yote aliyokuwa amewaapia baba zao; wala katika adui zao wote hakusimama hata mtu mmoja miongoni mwao mbele zao; yeye Bwana akawatia adui zao wote mikononi mwao.
”
— Yoshua 21:44 (Biblia Takatifu)
7. 2025 KILA MWANA WA MUNGU AMEPEWA KUMILIKI MARADUFU NA KUONGEZEKA KILA ENEO NA KUWA NA UTAWALA. “maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele.
— Mwanzo 13:15 (Biblia Takatifu)
8. 2025 NI MWAKA WA KUFURAHIA AFYA YA KIUNGU KWA KILA MWANA WA MUNGU, KULINDWA NA KUEPUSHWA NA KILA UOVU KTK JINA LA YESU. Kumbukumbu la Torati 11 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹¹ lakini nchi mwivukiayo kuimiliki ni nchi ya vilima na mabonde, nayo hunyweshwa maji ya mvua ya mbinguni;
¹² nayo ni nchi itunzwayo na Bwana, Mungu wako; macho ya Bwana Mungu wako, ya juu yake, tangu mwanzo wa mwaka hata mwisho wa mwaka.
9. 2025 NI MWAKA WA KUFURAHIA KASI YA KIMUNGU KWENYE KULITIMIZA KUSUDI NAHAKUNA KUCHELEWESHWA KTK JINA LA YESU. π“Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Maneno yangu hayatakawilishwa tena hata moja, bali neno nitakalolinena litatimizwa, asema Bwana MUNGU.
— Ezekieli 12:28 (Biblia Takatifu)
10. KILA MWANA WA MUNGU ATAFURAHIA NEEMA YA KUSTAWISHWA PANDE ZOTE, KUSTAWISHWA NA KUSTAREHESHWA KILA ENEO LA MAISHA NA KUSUDI LA KUISHI. Tutafurahia kuvuka vizuizi na kushinda Upinzani, tutavuka mipaka ya kiroho na kiuchumi. Kupanda Kiwango mwaka huu ni urithi wa kila mwana wa Mungu. Ni pamoja na kurejeshewa kila chema alichotuibia adui ktk Jina La Yesu.
π“Na Yuda wote wakakifurahia kile kiapo; kwani wameapa ............ ; naye Bwana akawastarehesha pande zote.
”
— 2 Mambo ya Nyakati 15:15 (Biblia Takatifu).
NA HAKIKA NDIVYO ITAKAVYOVYOKUWA KTK JINA LA YESU,
No comments:
Post a Comment