KUOMBA MAOMBI YA SHUKRANI.
Zaburi 92 : 1
Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu.
Yeremia 30:19
Humo zitatoka nyimbo za shukrani na sauti za wale wanaosherehekea. Nitawaongeza na wala hawatakuwa wachache; nitawafanya waheshimiwe wala hawatadharauliwa.
Yeremia 30:19
1. Mshukuru kwa ajili ya Pumzi ya Uhai na Afya.
2. Mshukuru Mungu kwa ajili ya Ulinzi na kukuepusha na Kila Uovu wa adui shetani na mabaya yote.
3. Mshukuru kwa ajili Ugavi na riziki kwa hatima yako, Family, huduma, Uzao nk.
4. Mshukuru Mungu kwa baraka zote za mwaka 2025 juu ya maisha yako, huduma, kanisa.
5. Mshukuru Mungu kwa ajili ya kukuvusha Salama toka 2024 kuingia 2025
6. Baba Asante kwa ajili ya Wokovu wa Nafsi na Injili kuhubiriwa kwa mwaka 2024
7. Baba Asante kwa Wate Uliowaleta kanisani na kuwafanya washirika na Wanafamilia.
8. Baba Asante kwa ajili ya Uwepo wako tuliofurahia kwenye Ibada zetu zote mwaka 2024
9. Baba Asante kwa ajili ya Neno la kutupatia Urithi wetu uliloliachilia kwenye Ibada zetu mwaka 2024.
10. Baba Asante kwa ajili ya Hekima na Neema ya kuwajibika uliyoiachilia juu ya viongozi wetu wa kanisa, Baba Askofu, Wachungaji, Watendakazi mbalimbali.
11. Baba, Asante kwa ajili ya Msaada wako, Neema yako na Mkono wako vilivyofanikisha Kanisa 2024.
12. Baba Asante kwa ajili ya Ustawi wa Mchungaji wetu, Pastor Baraka, mkewe na Watoto, asante kwa ajili ya Neema ya Utumishi na huduma juu yake.
13. Baba Asante kwa ajili ya Shuhuda Zote Ulizotubarikia kwa Mwaka 2024 kama kanisa na Mtu mmoja mmoja kwenye Ndoa, Uchumi, Ajira, masomo, Uzao na Kumiliki na Kuongezeka
KILA OMBI TUMIA WALAU DAKIKA 5 NA KUENDELEA,
HUSISHA KUOMBA KWA ROHO NA KUNENA KWA LUGHA.
USISAHAU KUABUDU KABLA HUJAANZA KUOMBA.
NOTE:
UKIWA KAZINI, OFISINI, TUMIA HEKIMA YA KUTOKUATHIRI KAZI, WAWEZA KUOMBA KIMOYOMOYO HUKU UKIENDELEA NA KAZI YA KUHUDUMIA, Lakini mda wa breki au Lunch jifungie mahali na Uombe.
No comments:
Post a Comment