📖DAY 5: MFUNGO WA MAOMBI YA SIKU 21, TAREHE 10/JANUARI/2025.
MAOMBI YA KUOMBEA UFALME:
Mathayo 6:33
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Ayubu 42:10
Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.
KUOMBEA UFALME NI KUWA NA MOYO WA KUPENDA KUONA WENGINE WAKISTAWI KWENYE NDOA, BIASHARA, UONGOZI NA SIASA NK.
KUOMBEA UFALME KUNATOKANA NA KUTOKUFURAHIA KUONA WENGINE WAKIHARIBIK I
MAHITAJI KWA AJILI YA KUOMBEA UFALME NA MASILAHI YA UFALME WA MUNGU:
1. MOYO SAFI, Moyo unaoshuka na kunyenyekea na kujawa na Toba na Rehema.
MAOMBI: BABA, KTK JINA LA YESU, NAOMBA UPONYE MOYO WANGU, UPONYE MAJERAHA YOTE NA MAKWAZO YOTE, UTEKETEZE KILA UCHAFU MOYONI MWANGU KWA MOTO WA ROHO MTAKATIFU (Nena kwa Lugha, Omba kwa Roho na Uruhusu Roho Mtakatifu moyoni mwako)
BABA KTK JINA LA YESU, NINAOMBA UNISAMEHE KWA JINSI NILIVYOKUWA MCHOYO NA MBINAFSI NA HIVYO KUTOKUWAJIBIKA KWA MAHITAJI YA UFALME IPASAVYO.
Baba, Ninaomba Uniumbie kwa Upya, Moyo wa Upendo, Moyo wa Nyama, Moyo wa kufurahia kuona wengine wakistawi, Moyo wa Unyenyekevu na Toba, Moyo wa kufurahia Mafanikio ya Ufalme na Wana wa Mungu.
BAADA YA KUOMBA MAOMBI HAYA YA UFALME HAKIKISHA UNAFURAHIA KUONA WENGINE WANAINUKA NA KUINULIWA. (Usifurahie kuona Wana wa Mungu Wanaharibikiwa, Wanakwama nk)
Mfano: Ukisikia Ndugu/Rafiki Ameteuliwa na Raisi kushika Cheo Fulani, Usione wivu,
Ukisikia Ndugu/Rafiki amepata Tenda ya kazi ya Mabilioni Usiumie Moyo, Sherekea kuwa Mungu anawastawisha Watoto wake kwa Namna Tofauti na kwa majira totofauti
KUOMBEA NDOA NA FAMILIA:
1. Baba, ninaomba ustawishe Kiungu NDOA na Familia za Wana wa Mungu ktk Jina La Yesu.
2. Baba, Ninamuombea kila Binti na Kijana Anayehitaji Ndoa , Umbariki na Ndoa Nzuri mwaka huu katika Jina La Yesu.
3. Baba, Ninaombea kila Ndoa Inayopitia Changamoto ya Migogoro, Uitulize na kuihuisha katika Jina La Yesu.
MAOMBI YA KUOMBEA UCHUMI, BIASHARA NA UWEKEZAJI
BABA, KTK JINA LA YESU, NINAOMBA UMSTAWISHE KIUNGU KILA MWANA WA MUNGU KWENYE UCHUMI, BIASHARA NA UWEKEZAJI WAKE KTK JINA LA YESU.
BABA, NINAOMBEA KILA MWANA WA MUNGU MWENYE KITEGA UCHUMI, KAMPUNI, KIWANDA, DUKA, SHAMBA NA MRADI WOWOTE, MWAKA HUU, UMFANYIE MIPENYO YA FAIDA MARADUFU KTK JINA LA YESU.
BABA, NINAMUOMBEA KILA MWANA WA MUNGU ANAYETESWA NA MADENI KWENYE BIASHARA ZAKE NA UWEKEZAJI, BWANA UMFANYIE MUUJIZA UTAKAOMTOA KWENYE MADENI MILELE KTK JINA LA YESU.
Baba, ninamuombea kila Mwana wa Mwenye Malengo ya kuanzisha Biashara Mpya, Kufungua Kampuni, kujenga Kiwanda, kuanzisha miradi ya Biashara yoyote mwaka huu, Bwana Umfanyie Muujiza wa Mipenyo ya kupata Mtaji ktk Jina La Yesu.
Baba, Ninamuombea kila Mwana wa Mungu, Kujenga Nidhamu na Mwenendo utakaomwezesha kukua kiuchumi na kudumu kustawi bila kushuka hasa kwa Uaminifu wa kulipa Fungu la kumi na kutoa Dhabihu mbalimbali za kuinua Ufalme ktk Jina La Yesu.
BABA, NINAOMBA UMWEZESHE KILA MWANA WA MUNGU KUJIHUSISHA KIKAMILIFU KWA MAMBO YA UFALME NA KUTOA DHABIHU NA RASILIMALI ZA KUINUA UFALME KTK JINA LA YESU
ENEO LA SIASA NA UONGOZI. (OMBEA USTAWI WA KITAIFA)
1. Baba, ktk Jina La Yesu Tunaombea haki na Amani kutawala Taifa letu.
2. Baba, Tunaomba Ulivushe salama Taifa letu kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu ktk Jina La Yesu.
3. Baba, Naomba Kiinuke kizazi cha Wana wa Mungu kitakachochukua Nafasi mbalimbali za Uongozi na Utawala kwenye Taifa letu ( Wana wa Mungu Wainuke sasa nal kugombea nafasi za Udiwani, Ubunge na Uraisi ktk Jina La Yesu) Wana wa Mungu Wakalishwe kwenye nafasi mbalimbali za Utawalal na Uongozi.
4. Baba, ninaomba ninaomba Waamshwe Usingizini Wana wa Mungu wpanaPaswa kuwa Waokozi wa Taifa letu, Waanze kukaa kwenye viti na Meza za maamuzi ya Utawala na Uongozi wa Nchi yetu ktk Jina La Yesu.
5. Baba, NinaAmuru kuwa Washirikina Watu wa Giza Walio kwenye Utawala na Uongozi, sasa Muhula wao na Ukomeshwe ktk Jina La Yesu, Ninaamuru wasirudi tena kwenye Uongozi na Utawala wa Taifa hili ktk Jina La Yesu.
BABA, NINAOMBA UINUE KIZAZI CHA WAOKOZI KWENYE TAIFA LETU KWENYE KILA ENEO IWE BIASHARA NA UWEKEZAJI, TAALUMA, SIASA NA UONGOZI NA IVYO KUKOMESHA KABISHA UTAWALA WA WAOVU NA WASHIRIKINA KTK JINA LA YESU. Baba, Ninaomba Ukomeshe Utawala wa dhuluma, Rushwa na Wizi wa Mali za Taifa letu kwenye Mwaka huu wa Uchaguzi ktk Jina La Yesu.
Omba kwa Imani
Omba kwa Roho
Omba ukiwa na Matarajio ya kuona Ulichokiomba kikiwa Ushuhuda machoni pako.
No comments:
Post a Comment