Friday, January 28, 2022

KUEPUKA UZINZI, NA UASHERATI NDANI YA WOKOVU.

  

KUEPUKA UZINZI, NA UASHERATI NDANI YA WOKOVU.

 

Uzinzi: Ni kitendo cha mume au mke kutoka nje ya ndoa yake na kuwa na mahusianoya kimapenzi na mwanamke au mwanaume mwingine (kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa) Mungu anatukataza kwamba tusizini .

“Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine naam yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye na mwanamke hakika watanawa”. Walawi 20:10

 

Usilale na mke wa mwenzio ukajitia unajisi naye.Walawi 18 :20

 

Uasherati: Ni kitendo cha watu wasio olewa au kuoa ambaye atafanya mapenzi kabla ya ndoa. Mungu anakataza sana.

“mtu yeyote wa kwenu asimkaribie mwenziwe alie wa jamaa yake wa karibu ili kumfunua utupu mimi ndimi BWANA”. Walawi  18:6  

 

Kwa hiyo utaona ukisoma kitabu cha mambo ya walawi sura ya 18:1-23na 20:1-21 Mungu anavyokemea uzinzi na uasherati kwa nguvu zote, kwa kufafanua kwa uwazi. Ndani ya kanisa na nje ya kanisa tunatakiwa kuikimbia zinaa kwa nguvu zetu zote, maana sisi ni hekalu laMungu lazima mipaka (kujiwekea mipaka) kwa jinsia tofauti ili kuepuka uzinzi na uasherati kwetu. Kweli tumeokoka na tutaenda mbinguni.

Lakini kama hatutaitiisha miili yetu kwa uzinzi na uasherati hatutaenda mbinguni. Kijana wa kiume na wakike mnatakiwa kujilinda na kujichunga )sio vijana tu na watu wote) maana uzinzi na uasherati hauchagui umri  usiseme mimi ni mwombaji sana na ninaupako sana lakini bila kuwa makini unaweza kuangukia huko.

 

MAMBO YA KUFANYA KUEPUKA UZINZI NA UASHERATI

1.     Kuwa muombaji:

Unapokuwa muombaji mbele za Mungu inasaidia kuepuka usiingie kwenye majaribu au jaribu la uzinzi.

“Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni roho i radhi lakini mwili ni dhaifu” Mathayo.

2.     Kuepuka mazingira hatarishi.

Ukishaona mazingira uliopo ni ya hatarishi yananukia uzinzi au uasherati kimbia, Mfano:ukishaona mtu anakuonyesha dalili hizo usiseme mtaomba cha kufanya kimbia.

“Ikimbieni zinaa kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake ili yeye afanyae zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”. 1 Wakoritho 6:18

3.     Jiepushe na mavazi ya kikahaba:

Kimsingi shetani yupo na anatenda kazi wewe mwanamke na mwanaume jiepusheni kuvaa mavazi yasio mpendeza Mungu(yasiyo na utukufu wa Mungu). Mavazi hayo yanachochea uzinzi na uasherati kwa watu.

“Je humjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha” 1Wakoritho 6:15

 

 

4.     Kuwa na hofu ya Mungu:

Unapo kuwa na hofu ya Mungu, itakusaidia sana utajua kama utatenda uzinzi au uasherati  utakuwa unamkosea Mungu aliekuokoa, maana sisi ni hekalu la Mungu(Roho Mtakatifu)

“ Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu” 1Wakoritho 6:19-20

 

 

5.     Kujiepusha na vitendo vya ushawishi: kikawaida kuna vitendo ambavyo vinaweza kuwapelekea au vikachochea uzinzi au uasherati. Mfano: kuchati muda mwingi na jinsia tofauti kwa kuitana majina ambayo hukutakiwa kuyasema au kuwa na muda mwingi na jinsia tofauti kutembeleana nyumbani peke yako ni hatari sana shetani anaweza akawaingia mkafanya uovu. Ni vyema mkawa zaidi ya mmoja.

“Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana, Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda kipro, lakini Paulo akamchukua sila, akaondoka akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana” Matendo 15:39-40

 

6.     Kufanya mazoezi ya mwili:

Mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya afya yako. Ni vema ukafanya mazoezi ili kuepuka zinaa.

“Je hamjui yakuwa wale washindanao kwa kupiga mbio wote, lakini apokeae tuzo pigeni mbio  namna hiyoili mpate”1wakoritho 9:24

 

 

7.     Kujiweka bize

Unapokuwa bise katika kumtafakari Mungu na neno lake au ukuu wake itakusaidia sana. Mfano:Kama wewe ni mwanafunzi jiweke bize katika kujisomea masomo yako.

“nimevipiga vitu vilivyo vizuri mwendo nimeumaliza imani nimeilinda”.2timotheo 4:7

 

8.     Jitambue wewe ni kielelezo kwa Mungu:

Unapo okoka unatakiwa uwe ni kielelezo mbele za Mungu na mwanadamu. Kama utasema umeokoka na ujihusisha na maovu hapo unakuwa unamtukanisha Mungu.

“Katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema na katika mafundisho yako ukionyesha usahili na usahivu”. Tito 2:7

 

MADHARA YA ZIINAA( Uzinzi na uasherati)

Usisahau dhambi ni kazi na ni lazima ulipwe (mshahara lazima ulipwe)

“kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu nai uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” Warumi 6:23

                                             i.            Zinaa inaua utu wa ndani.

“Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili” Mithali 18:14

Zinaa inajeruhi na kuumiza mtu wa ndani na kumuangamiza nafsi yake.

 

“Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa, afanya jambo litakalo mwangamiza nafsi yake” Mithali 6:32

                                           ii.            Humvunjia mtu heshima na kupata fedheha.

“Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima wala fedheha yake haitafutika”Mithali 6:33

              iii.            Inafuta maono na ndoto zako(utamkosa Mungu ) Yusufu alijua kwamba amebeba maono ya Mungu na ndiyo maana mke wa bosi wake alipotaka kufanya naye mapenzi alikimbia.

“Ikiwa baada ya mambo hayo mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia lala nami. lakini akakataa------------- Mwanzo 39:6-12

“Nifanyeje ubaya huu mkubwa nimkosee Mungu?Mwanzo 6:9

              iv.            Humwaondolea mtu ujasiri wakukemea dhambi.

Mtu anakosa ujasiri mbele ya Mungu na wanadamu kwa sababu moyo wako unakuhukumu.

“Wapenzi mioyo yetu isipotuhumu tunaujasiri kwa Mungu” 1Yohana 3:21

                 v.            Huleta muunganiko wa mwili.

“Au haujui yakuwa yeye aliyeungana na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema wale wawili watakuwa mwili mmoja” 1wakoritho6:16

Kumbuka hili ni agano(zinaa ni agano) au unaweza kusema ni kifungo unaunganisha,mwili, nafsi na moyo (roho yako) ndiyo maana utakuta mtu kabla ya kuokoka alikuwa na mtu wake (mpenzi)unakuta wameokoka wanaendelea na zinaa kama mwanzo.


              vi.            Hukiingiza kizazi chako kwenye vifungo

“Baba zetu walitenda dhambi hata hawako na sisi tumeyachukua maovu yao” Maombolezo 5:7

 

            vii.            Huambukiza magonjwa.

Zinaa inaweza kukuambukiza magonjwa ya namna mbalimbali.

 

         viii.            Ni mlango wa mapepo kwa wanadamu.

 

              ix.             Inaua kiroho na kimwili

“Ndipo Bwana akanyosha juu ya sodoma na juu ya gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana” Mwanzo 19:24.

 

     x.            Inaweza kukufanya usiurithi ufalme wa Mungu (ukafutwa kwenye kitabu cha uzima)

“Bali waoga na wasio amini na wachukizao na wauaji na wazinzi na wachawi na hao waabuduo sanamu na waongo wote sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberit. Hii ndiyo mauti ya pili”

“Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika hilo ziwa la moto”Ufunuo 20:15

 


KAMA HUJAOKOKA SEMA MANENO HAYA KWA KUYAKIRI NA KUYAAMINI MOYONI MWAKO.

 

Baba Mungu katika jina la Yesu Kristo nakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi ninaomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozitenda kwa kujua au kwakuto kujua na ninazo zikumbuka na nisizo zikumbuka. Ninaomba unirehemu, ninaomba unihurumie mimi mwenye dhambi, ninakuomba futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uandike jina langu kwenye kitabu cha uzima. Ninaomba uwe Bwana na mwokozi wa maisha yangu, naomba unipe neema niwe mwaminifu mbele zako na hata milele. Asante Yesu Kristo kwa kunisamehe dhambi zangu. Nimekuwa kiumbe kipya mbele zako, katika jina la Yesu kristo. Ameni

 

Niseme kwamba Mungu amekusamehe dhambi zako wala azikumbuki tena endelea kujifunza neno la Mungu ili neema uliyoipata isipotee. Sasa wewe ni kiumbe kipya ndani ya Kristo Yesu yakale yamekwisha tazama ni mapya ni katika jina la Yesu. Wokovu ulioupate ni wa thamani sana na hiyo ndiyo tiketi ya kwenda mbinguni.

 


 

MUNGU AKUBARIKI.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment