VITA VYA KIROHO
Vita; Maana yake ni mapambano au mapigano makali yanayohusisha silaha baina ya pande mbili au zaidi, vita ni kufa au kupona lazima mwingine ashinde na mwingine ashindwe. Vita yoyote ile ni lazima ihusishe silaha, wapiganaji(maaskari) na uwanja wa mapambano vita inaweza kuangamiza watu wengi, kuharibu miundo mbinu n.k.
VITA VYA KIROHO
Vita vya kiroho ni namna ile ile ya mapambano makali yanayohusisha silaha vile hii inapiganwa katika ulimwengu wa roho kwa kutumia silaha za kiroho maadui hawaonekani kwa macho ya mwili, wala darubini, wala haiwezekani kuwashambulia kwa silaha za kimwili kama vile bunduki, mizinga, ndege za kivita au wanajeshi
Hii ni vita vya wafuasi wa Yesu Kristo na wafuasi wa shetani. Uwanja wa vita ni ulimwengu wa roho. Hii ni vita yenye.
A) Ni vita yenye wanajeshi,
Maana yake.
-wanaujuzi
-wanamaarifa
-wanahekima (saikolojia ya kijeshi)
-wanamipango
-wanasilaha na vifaa vyote vya mapambano.
B) Hii ni vita ya malaika aliyeasi
-mwenye uwezo na nguvu za kimamlaka.
SERIKALI YA KISHETANI
1. SHETANI (ibilisi)
Hii ni serikali kuu ya shetani kwenye ulimwengu wa roho.
i) Mkuu wa anga(malaika wa mbingu)
Huyu ni shetani anayekaa kwenye anga kwa ajili ya kuzuia maombi.
“Akaniambia ee Daniel mtu upendwaye sana yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimama kiwima maana kwako nimetumiwa sana. Na aliponiambia neno hili nalisimama nikitetemeka,
ndipo akaniambia usiogope Daniel kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwaa nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa uajemi alimpinga siku ishirini na moja, bali tazama huyo Mikaeli mmoja wa hao wakuu wa mbele akaja kumsaidia nami nikawaacha huko pamoja na wafalme wa uajemi.”Daniel 10;11-13
ii) Mkuu wa ardhi
Huyu ni malaika wa kuzimu anayesimamia kuharibu ardhi.
“Na juu yaowanaye mfalme naye ni malaika wa kuzimu jina lake kwa kiebrania ni Abadoni na kwa kiyunani analojina lake Apolioni, ufunuo 9;11,
“Kisha nikaona mnyama mwingine akipanda juu katika nchi naye alikuwa na pembe mbili mfano wa mwana-kondoo akanena kama joka, ufunuo 13;11
iii) Mkuu wa bahari.
Huyu ni malikia wa bahari anayetawala maeneo yote yanayo husu maji na ndiye anayesimamia mitindo yote duniani.
“Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari mwe nye pembe kumi na vichwa saba juu ya pembe zake ana vilemba kumi na juu ya vichwaa vyake majina ya makufuru , ufunuo 13;1
2. Serikali ndogo ya kishetani.
Mkuu wa mapepo (beelizeburi)
Huyu ni mkuu wa mapepo yote au ni shetani anayesimamia mapepo yote kwa kuyatuma na kuyapa amri na ndiyo maana walimwambia Yesu anatoa mapepo kwa nguvu ya beelizeburi.
Lakini Yesu alikuwa anayatoa kwa kutumia nguvu za Mungu aliyemtuma hapa duniani kwa kufungua watu kuwatoa kwenye mateso yao.
“Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema ana Beelizabuli na kwa mkuu wa pepo hawatoa pepo. Akawaita akawaambia kwa mifano awezaye shetani kumtoa shetani na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama’ Marko 3.22-24.
Mashetani wa kitendo hiki ndiyo yanayosimamia vitengo mbalimbali ili kuwatesa watu.
Vitengo vya kishetani
-kitengo cha mateso
-kitengo cha kufunga mafanikio
-kitengo cha kifo na mauti
-kitengo cha umasikini na ufukara
-kitengo cha mafarakano na fitina
-kitengo cha laana na balaa
-kitengo cha taabu na shida
-kitengo cha kukataliwa-
-kitengo cha kuharibu mimba
-kitengo cha kutokuolewa na kutokuoa
-kitengo cha magonjwa na maradhi
-kitengo cha matatizo na uharibifu
-kitengo cha majanga
-kitengo cha ajali
-kitengo cha chuma ulete
-kitengo cha kuleta uchungu
-kitengo cha kafara na umwagaji damu
Vipo vitengo vingi vya kishetani lengo lake ni kuleta uharibifu kwenye maisha ya watu, kuna mapepo yanayo
-Tambaa (mapepo yanayotambaa)
-Tembea (mapepo yanayo tembea)
-Ruka (mapepo yanayoruka)
3. Falme za giza
Hizi ni mamlaka za giza zinazosimamia kwenye utawala wao, hapa utakuta kuna;
i). mamlaka za giza
ii). Wakuu wa giza
iii)majeshi ya pepo wabaya
“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili,juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” Waefeso 6;12.
4. Idara za giza
Hizi ni idara za kishetani kwenye serikali yake ili iweze kushughulikia mambo yao ya uhalibifu. Kuna idara’
i). idara ya giza ya mapepo
ii)idara ya giza ya mizimu
iii)idara ya giza ya miungu
iv). Idara ya giza ya majoka
v). idara ya giza ya kichawi
mfano; idara ya wachawi, Namna wanavyotenda kazi.
-uchawi wa kutumia dawa
-uchawi wa kutumia tunguli
-uchawi wa kutumia vitabu
Pamoja na yote hayo kuhusu selikali ya kishetani lakini tunashinda zaidi ya kushinda na tunapaswa kuwa na silaha za vita za kiroho ndipo tutaweza kumshinda kwa namna ya kiroho na hata kimwili kwa Jina la Yesu.
SILAHA ZA VITA ZA KIMUNGU.
Hizi ni silaha za vita vyetu. Ulimwengu wa roho kuna zana maalumu za maangamizi unazotakiwa kuzitumia kama askari wa Yesu kristo.
“Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake, vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani “waefeso 6;10-10.
Kuwa hodari katika Bwana.
Tunapaswa kuwa hodari katika Bwana na uwezo wa nguvu zake, kwamba tunaamini Yesu Kristo kwamba yeye ndiye muweza wa yote kwa kuwa hodari,
“Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa, usiogope wala usifadhaike kwa kuwa Bwana Mungu wako yu pamoja nawe kila uendako” Yoshua 1;9
Lakini uhodari huo tunaupata kwa njia ya kujilinda na kila mashambulizi yoyote ya kishetani yatakayofanyika juu yako.
i)Toba..(utakatifu)
Kabla ya kuingia kwenye ulimwengu wa roho kwa ajili ya vita, unapaswa uombe toba juu yako na watu wote wanaomzunguka. Ili kusiwepo na kizuizi chochote katika kurusha makombola, kuna dhambi umeitenda kwa kujua au kwakutojua.
Omba toba na rehema mbele za Mungu maana tunaingia vitani kwenye ulimwengu wa roho ili utakapo tamka tu moto uende moja kwa moja kwa adui
“lakini maovu yenu yamewafarikima ninyi na Mungu wenu na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone hata hataki kuskia kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu, midomo yenu imenena uongo na ndimi zenu zimenong’ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki wala hapana atetaye kwa kweli hutumainia ubatili hunena uongo, hupata mimba ya madhala na kuzaa uovu”Isaya 59:2-4
ii)Damu ya Yesu Kristo
Shetani anaigopa damu ya Yesu Kristo. Hii pia ni silaha nyingine, unapoomba jifunike kwa damu ya Yesu inanena mema siku zote na hii ni silaha ya kumshinda shetani.
“ Na Yesu mjumbe wa agano jipya na damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya habili” waebrania 12:24
“Nao wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo na kwa neno la ushuhuda wao-----------“Ufunuo12:11
(iii) Moto wa Roho Mtakatifu (Roho Mtakatifu)
Katika kuomba ni vizuri ukamualika Roho Mtakatifu akusaidie katika kuomba, maana yeye atawasha moto ndani yako.
“Hata ilipotimia siku ya pentekoste walikuwako wote mahali pamoja, kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukaenda kasi, ukajaza nyumba yote waliokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizo gawanyika na kama ndimi za moto ulio wakalia kila mmoja wao, wote wakajazwa Roho Mtakatifu wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama roho alivyowajalia kumka” Matendo2:1-4
“Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake, yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto”. Mathayo 3:11
(iv) Imani:
Katika kuomba lazima uwe na imani, kwamba kile uncho kiomba kinafanyika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili unatakiwa usiwe na shaka yoyote unapo sema nawakimbiza, nawashambulia ujue wanashambuliwa kweli
“Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gidieoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii, ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba” Waebrania 11:32-33
“Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya Yule mwovu” waefeso 6:16
(v) Maarifa:
Lazima uwe na maarifa katika kushambulia. Unapaswa kuelewa na muda gani wa kushambulia, ni mahali gani pa kushambulia ,je adui au maadui wapo hiyo sehemu au wameshaondoka? Je wapo kushoto,kulia, mbele,nyuma juu au chini? Ili utakapo fyatua iende. Maarifa haya ya kijeshi lazima uyajue vizuri ni silaha gani uitumie na wao wanasilaha zipi unapaswa uwasome vizuri.
Mfano: Wewe unasilaha ndogo kama vile bastora halafu mwenzako anatumia mzinga katika kukushambulia, lakini kwa vile tunazo silaha za bwana za vita.
“ Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa mimi name nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi, kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako------------“Hesabu4:6.
(vi) Wokovu:
Wokovu ulionao ndiokibali cha ruhusa cha kuingia ulimwenguni wa mapambano.
“Tena ipokeeni chapeo ya wokovu-----“Waefeso 6:17
(vii) Maombi
Tunapokuwa ndani ya ufalme wa Mungu tunapaswa kuomba bila kukoma(bila kuchoka ) siku zote za maisha yetu. Tukijiombea wenyewe na kuwaombea wengine. Maombi ni silaha zidi ya adui.
“ Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika roho mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote” waefeso 6:18
“Dumuni sana katika kuomba mkikesha katika kuomba huku na shukrani” wakolosai 4:2
“Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni roho radhi lakini mwili ni dhaifu “mathayo 26:41
“Ombeni bila kukoma” 1wathesalomike 5:17
(viii) Jina la Yesu:
Jina la Yesu katika ulimwengu wa roho ni kama bomu hatari na tunapaswa kuomba kwa jina la Yesu, maana ni jina lipatalo majina yote.
“Amini, amini nawaambieni yeye aniaminiye mimi kazi nizifanyazo mimi yeye naye atazifanya naam na kubwa kuliko hizo atafanya kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu hilo nitalifanya ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana,mkiomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya” Yohana 14:12-14
“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno akamkiri jina lile lipitalo kila jina”Wafilipi 2:9
“Juu sana kuliko ufalume wote na mamlaka na nguvu na usultani na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia”. Waefeso 1:21
xi) Neno la Mungu.
Neno la Mungu ni silaha nyingine zidi ya shetani na malaika zake unapolitumia neno la Mungu linakusaidia kwenye mambo kadha wa kadha.
Mfano;
a)Neno la Mungu ni chakula cha kiroho “Maneno yako yalionekana nami nikayala na maneno yako yaliyokuwa ni furaha kwangu na shangwe ya moyo wangu maana nimeitwa kwa jina lako EE Bwana Mungu wa majeshi “ Yeremia 15;16.
b) Neno la Mungu ni moto na nyundo “Je neno langu si kama moto? Asema Bwana na nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? Yeremia 23;29.
c)Neno la Mungu ni hai.
Maana Neno la Mungu li hai………waebrania 4;12
d)Neno la Mungu lina nguvu tena linanguvu….waebrania 4;12
e) Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga.
f)Neno la Mungu lachoma.
Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uuwao wote ukatao kuwili tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake tena li jepesi
Kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo” waebrania 4;12.
a) Neno la Mungu ni ngao
“Kila neno la Mungu limehakikishwa, yeye ni ngao yao wamwaminio” Mthali 30;5
h). Neno la Mungu ni silaha.
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi :Zaburi 119:9
i)Neno la Mungu ni taa.
Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu, Zaburi 119;105.
No comments:
Post a Comment