Friday, February 4, 2022

UPENDO WA MUNGU

 UPENDO WA MUNGU

Upendo: Ni hisia kali alizonazo mtu kwa mtu, kitu na namna mbalimbali zinazomuhasiri mtu.

Aina za upendo.

                                 i.            Upendo wa mzazi na mtoto

                               ii.            Upendo wa mume na mke

                            iii.            Upendo wa kitu

                            iv.            Upendo wa Mungu(Agape love)

                               v.            Upendo wa ndugu

Upendo wa Mungu (Agape love) kimsingi hakuna jambo la muhimu na la maana sana zaidi ya upendo, maana Mungu mwenyewe ni pendo.

“Nasi tumefahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi na kuliamini. Mungu ni pendo naye akaye katika pendo , hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake”.1Yohana 4:16

Mungu mwenyewe aliupenda ulimwengu alijua ndani ya ulimwengu amewaweka watu na watu hao lazima waokolewe ndiyo maana akamtuma mwana wake wa pekee ili kila amwaminie asipotee bali wote wawe na uzima wa milele, huo ni upendo wa Mungu kwetu sisi.

“kwa maana jinsi Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele” Yohana 3:16

 

Ukifuatilia huduma nyingi au makanisa mengi upendo wa Mungu haupo, kwa nini? Watu wanajifikilia wenyewe tu na hawana habari na watu wengine lakini. Biblia inasema kama sina upendo      ( kwa watu) nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao( shaba isiyo na kitu ndani yake)

 


“Nijaposema kwa lugha za wanadamu na malaika kama sina upendo nimekuwa kama shaba iliyo na upatu uvumao” 1wakoritho 13;1

 

Hata kama nitakuwa nimefahamu mambo mengi ya kiroho na kimwili kama sina upendo si kitu mimi. Hata kama wewe si kitu.

a.     Nijapokuwa na unabii .

b.     Kujua siri zote na maarifa yote

c.      Nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima. Kama sina upendo si kitu mimi.

d.     Hata nikitoa mali zangu zote kuwapa maskini.

e.      Hata nikijitoa mwili wangu niunguwe moto, kama sina upendo haisaidii kitu.

“Tena nijapokuwa na unabii na kujua siri zote na maarifa yote . nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo si kitu mimi. Tena nikijitoa mwili wangu niunguwe moto, kama sina upendo hainifani kitu” 1wakoritho 13:2-3

                   NGUVU YA UPENDO:

Upendo huvumilia:panapokuwa na upendo ndani ya kanisa, kwenye biashara, kazini, nyumbani kwenye jamii na sehemu zingine upendo huvumilia yote hata kama mtu amekutendea mabaya au akakusemea vibaya utavumilia kwa sababu ya upendo.

 

Upendo hufadhili: Kwa sababu ya upendo unaweza ukapata msaada kutoka kwa watu, mtu anaweza akakuonea huruma, akakusaidia kukulipia ada, kukupa chakula n.k.

 


Upendo hauhusudu: Kwenye upendo wivu usiokuwa na maana utaondoka, bali kutakuwa na wivu wa maendeleo.

 

Upendo hautakabari: Upendo unapokuwepo basi ujeuri utaondoka, kwa kila mmoja hamtafanyiana kiburi.

 

Upendo haujivuni: Panapo kuwa na upendo hakuna majivuno kujiona wewe ni bora kuliko mwingine jambo hilo linakuwa halina nafasi yake.

 

Upendo haukosi kuwa na adabu: Penye upendo lazima adabu itakuwepo, kuheshimiana.

 

Upendo hautafuti mambo yake:Upendo ukiwepo hauwezi kuanza kutafuta madhaifu ya mtu jinsi alivyo muumba Mungu ataendelea kupenda tu.

 

Upendo hauoni uchungu: upendo ukiwepo uchungu ya kuanza  kumjutia mtu na kuya weka ndani / kuyatunza ndani ya moyo wako kwa kuanza kumuachukia, kumsema vibaya utamuachilia na kuendelea  kumpenda (kupenda)

 

 

Upendo hauhesabu mabaya: upendo hauhesabu mabaya uliyotendewa.

 

Upendo haufurahii udhalimu: kama unampenda ndugu yako, au ameharibikiwa anatenda mabaya ni mrevi, kama unaupendo utamwombea  kwa Mungu amrehemu na atokane na hayo. Vile vile utamuonya kwa njia anayoenenda nayo kwamba sio nzuri.

 

 

Upendo hufurahi pamoja na kweli: mahali penye upendo panatakiwa kuwa na ukweli na uwazi ili zile taarifa  anazozipata mtu au alizo pata mtu ni vyema ukweli ukawepo ili mfurahi kwa pamoja.

 

Upendo huamini yote: kwenye upendo lazima tumaini liwepo, ili yule uliye au sehemu uliyopo uaminike.

 

 Upendo hutumaini yote: kwenye upendo lazima tumaini liwepo la kuona matumaini ya mbele au yatalajiwayo.

 

Upendo hustahimili yote :kwenye upendo kuna uimara, kusimama imara bila kusurubishwa.

 

Upendo haupungui neno wakati wowote:  Upendo ukiwepo utapewa kuyafuata maneno au neno zuri ili kuboresha mahusiano yaliyopo.  “Upendo huvumilia, hufadhili, upendo huwahusudu, upendo hautakabiri, haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake,haoni uchungu, hauhesabu mabaya, haufurahi udhalimu balihufurahi pamoja na kweli, huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote, upendo haupungui neno wakati wowote, bali ukiwepo unabii utabatilika, zikiwepo lugha zitakoma, yakiwepo maarifa yatabatilika “. 1wakolitho13:4-8

Upendo haunahofu: kwenye upendo hofu itakuwa haina nguvu bali mtu atakuwa jasiri, asiyeogopa chochote, na ambaye mwenye hofu hajakamilishwa na upemdo bado.

 

“Katika pendo hamna hofu, lakini  pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo”.1Yohana 4:18

 


Kanisa linapokuwa na upendo hapo Mungu anafurahi sana kwasababu  linamuakilisha yeye hapa duniani.

 

Alama za upendo:

                                           i.            Upendo umetoka kwa Mungu

                                         ii.            Kila apendaye amezaliwa na Mungu

                                      iii.            Anamjua Mungu

                                      iv.            Mungu amemtuma mwanawe wa pekee ulimwenguni(Yesu Kristo) ili tupate uzima wa milele.

 

“Wapenzi na mpendane kwa kuwa pendo latokea kwa Mungu na kila apendaye amezaliwa na Mungu. Yeye asiye penda hakumjua Mungu kwa maana Mungu ni upendo  katika hili pendo Mungu lilionekana kwetu kwamba Mungu amemtuma mwanae pekee ulimwenguni ili tupate uzima kwa yeye”1Yohana 4:7-9

v. Tumepatanishwa na Mungu baba

vi. Mungu hukaa ndani yetu

vii. Upendo wake umekamilika ndani yetu

viii. Ametushirikisha roho wake

 

“Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo,haya matatu na katika haya lililo kuu ni upendo” 1wakoritho13:13.

 

Kwahiyo tunaona hapo lililo  kuu ni upendo. Watu wengi kwenye jamii upendo umepoa , akienda kazini upendo haupo, mtaani upendo haupo, nyumbani upendo haupo, sasa basi kanisa ndilo linatakiwa kuwa tibia watu waliokosa upendo  ndani yao kwa jina la Yesu Kristo.Ameni

Kama tukisema kanisa tunampenda Mungu huku tunawachukia ndugu zetu ni waongo.

“Mtu akisema nampenda Mungu naye anamchukia ndugu yake ni mwongo kwa maana asiempenda ndugu yake ambaye amemuona hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumuona” 1Yohana 4:;20

“Upendano wa ndugu na udumu msisahau kuwafundisha wageni, maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua” Waebrania 13:1-2

 

Vitu vinavyo haribu upendo:

Moja ya vifungo kinacho sumbua watu ni kifungo cha tabia iwe ni kwenye:

Þ   Urafiki au mahusiano

Þ   Kwenye kazi au ofisini

Þ   Kwenye biashara na taasisi

Ili uweze kuendelea unatakiwa uwe na tabia nzuri.

“Hekima hiyo siyo ile ishikayo kutoka juu bali ni  ya dunia ya tabia ya kibinadamu na shetani. Yakobo 3;15.

 

Tabia;  ni hali au sifa za nafsi alizonazo mtu. Kwahiyo hapa utaona matendo, miitikio au mienendo itakayoweza kuonekana  wazi. Mfano; kunatabia za miti, wanyama, binadamu n.k, wapo wanaosema mazoea ujenga tabia.

 

Aina za tabia

Kunatabia ambazo mtu anakuwa

i)Amezaliwa nazo (kiasili)

ii).  Ameiga tabia kutokana na mazingira aliyokulia au kulelewa.

 

-Kuna wapo waliolelewa na mama peke yake

      -Kunawapo walio lelewa na baba peke yake

      -Kunawapo waliolelewa na mama na baba

      -Kuna wapo waliolelewa na ndugu

  -Kunawapo waliojilea wenyewe

Kwahiyo kwa namna zote hizo lazima mtu huyo hawezi kufanana na mtu mwingine kwasababu ya namna na mazingira aliyokulia au kulelewa lazima yatakuwa tofauti.

 

Tabia za kibinadamu

A.   Kuna msondani (introvert)

Mtu huyu ni Yule ambaye yeye sio mwongeaji sana, ni mkimya.

   Aina zake

                             I.            melancholy(melancolim)

-wapole na wasio na maneno mengi
-wanahisia kali za upendo( upendo wa dhati)

-wanajali wenzao

-wanamaombi mazuri kiimani

-wanahuruma

-wanabusara na hekima

 

                         II.            phlegmatic (pragmatic)

-ni mabingwa wa kuhairisha mambo

-wanapenda kupuuzia mambo

-watafiti na kufuatilia mambo

 

B.   Kuna msonje (extrovert)

Mtu huyu ni Yule ambaye ni muongeaji sana na anayeweza kujielezea kwa namna mbalimbali.

Aina zake

i). Sanguine

-ni wacheshi sana

-watu wenye maneno mengi wasio pumzika kuongea

-wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wanaongea.

-wana karama ya kuhubiri

-wanapenda kujaribu kila kitu..mfano petro.

 


ii). Choleric

-ni wakali

-wasiopenda kudharauliwa au kuonewa

-ni viongozi wa asili ya kuzaliwa

-wanajiamini

-hawaongei wala kucheka hovyo.

 

TABIA MBAYA AMBAZO MUNGU HAZIPENDI

i). Uzushi

ii). Umbea

iii). Usingiziaji

iv). Uongo

v).Uzinzi

vi).Ufitini

vii). Uasherati

viii).Ugomvi

ix). Kiburi

x). Jeuri

xi). Husuda

xii). Kijicho

xiii). Na mambo yote yanayofanana na hayo.

 

KUNAVITU ILI MTU AWEZE KUFANIKIWA

Ili mtu afanikiwe kunahitaji mambo mawili,

a)Kipawa / Karama.

Kipawa kinaweza kumfikisha mtu mbele za watu wakubwa na kujulikana.

“Zawadi ya mtu humpatia nafasi, humleta mbele ya watu wakuu” Mithali. 18;16

Mtu anaweza kuwa na kipawa  Fulani lakini tabia yako mbaya hakuna atakaye tamani kuwa karibu nawe.

 

b) Tabia ya mtu

Ili Mungu akutumie kwa kiwango cha juu ni muhimu kuanza kwa kubadili tabia yako mbaya na kuwa na tabia nzuri mbele ya Mungu na wandamu.

“kwa maana ndugu mnapendwa  na Mungu twajua uteule wenu ya kwamba injili yetu haikuwafililia katika maneno tu bali na katika nguvu na katika Roho Mtakatifu na zilivyokuwa tabia zetu kwenu kwa ajili yenu” 1wathesolenike 1;4-5.

“Lakini ndugu zangu mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo, 1wakorintho 3;1.

 

 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment