KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
Karama : Ni zawadi anazotoa Mungu kwa watu au kipaji cha pekee kutoka kwa Mungu.
“Lakini kazi hizi zote huzitenda roho huyo mmoja yeye Yule, akimgaia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye” 1wakorotho12:11
Katika karama hizi kuna tofauti ya:
v Kuna tofauti ya huduma
v Kuna tofauti ya kutenda kazi
Bali Mungu ni yeye Yule azitendae kazi zote katika wote
“Bali pana tofauti za karama bali roho ni yeye Yule, tena pana tofauti za huduma na bwana ni yeye Yule, pana tofauti za kutendwa kazi pana tofauti za kutenda kazi bila Mungu ni yeye Yule azitendae kazi katika wote.”1Wakorithio 12:4-6
.kwenye huduma na kutenda kazi kila mtu anakuwa anapewa ufunuo ili kusaidiana.
“Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa roho kwa kufaidiana” 1Wakoritho 12:7
Kwa hiyo sasa baada ya kuokoka unatakiwa kumuomba Mungu akupe karama za rohoni ili mwili wa Yesu Kristo ujengwe kwa pamoja kwa umoja ndani ya kanisa
“Takeni sana karama zilizo kuu, hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora”.1wakoritho12:31
Kabla ya kuoka tulikuwa tunazifuata sanamu zisizo nena, yaani kuabudu miungu ya kishetani “Basi ndugu zangu kwa habari ya karama za roho, staki mkose kufahamu, mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa mataifa mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena kama mlivyoongozwa”1Wakolotho 12:1-2
AINA ZA KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
Kuna aina mbalimbali za karama za roho. Mwingine anaweza kupewa na Mungu karama zaidi ya moja:
“Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali kwa kadri ya nema mliopewa ikiwa ni unabii, ikiwa huduma katika huduma yetu, mwenye kuonya katika kuonya kwake, mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu kwa furaha” Warumi 12:6-8
1. Hekima: Ni hali bora ya mtu katika kutambua ukweli wa binadamu, vitu,matukio na mazingira mbalimbali hata kuchagua vizuri la kufanya au unaweza kusema ni maadili ya kitu na maadili ya ki mungu “Lakini hekima itakayo juu, kwanza ni safi tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya wato, imajua rehema na matunda mema haina fitina, haina unafiki” Yakobo 3:17
“Basi sasa nipe hekima na maarifa mjue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa kwa kuwa na nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi “2Nyakati 1:10
“Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako na kupambanua mema na mabaya maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako waliowengi” 1Wafalme 3:9.
“Maana mtu mmoja kwa roho apewa neno la hekima …. “1wakoritho 12:8
2. Maarifa: Ni ufahamu wa kuelewa kitu Fulani.
“--------- Mwingine neno la maarifa apewavyo roho yeye Yule “.1wakolitho 12:8(b)
“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa ----------“ Hosea 4:6 Kumbe ukikosa maarifa unaangamia na nguvu ya mtu siku zote ni kuwa na maarifa mengi(knowledge is power)
“Bali ajisifiyena ajisifu kwa sababu hii ya kwamba ananifahamu mimi na kunijua ya kuwa mimi ni bwana, nitendee wema na hukumu na haki katika nchi maana mimi napendezwa na mambo hayo asemaBwana,”.Yeremia 9:24.
“Ee mwanadamu yeye amekuonyesha yaliyo mema na Bwana anataka nini kwako ila kutenda haki na kupewa rehema na kwenda kwa unyenyekevu na mungu wako”. Mika 6:8.
“Na uzima wa milele ndio huu wanijua wewe mungu wa pekee wa kweli na yesu kristo aliyemtuma” Yohana 17:3
3.Imani: Ni kuwa na hakika ya mabo yatarajiwayo , ni bayana ya mabo yaliyo onekana
“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyo onekana” Waebrania 11:1
“mwingine imani katika roho yeye Yule …………1Wakoritho 12:9(a)
“maana twenenende kwa imani si kwa kuona” 2wakoritho 5:7
“Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani naye akisitasita roho yangu haina furaha naye lakini sisi hatumo miongoni mwao hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu. Waebrania 10:38-39.kwahiyo ukisoma katika hiki cha Waebrania sura ya 11yote utaona inazungumziwa imani kwa asilimia kubwa.
4)Kuponya: Ni kumfanya mtu ambaye amekuwa mgonjwa kimwili, kiakili au kiroho apate afya njema.
“----------- Mwenye karama za kuponya katika roho Yule mmoja” 1wakoritho 12:9(b)
“Pozeni wagonjwa, fufufeni watu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo, mmepata bure, toeni bure”.Mathayo 10:8.
“Akampeleka mfalme wa Israeli waraka ule kusema waraka huu utakapo kuwasilia tazama nimemtuma mtumishi wangu naamini kwako ili upate kuuponya ukoma wake” 2Wafalme 5:6
Naamini alikuwa jemedari wa jeshi la mfalme wa shamu lakini alikuwa na ukoma ambao ni ugonjwa hatari sana. Mfanya kazi wa ndani akitoa habari za mtumishi wa Mungu Elia kwamba anaweza kumponya.
“Lakini Petro akasema mimi sina fedha wala dhahabu lakini nilicho nacho ndicho nikipendacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa nazareti simama uende. A kamshika mkono wa kiume akamwinua mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu” Matendo 3:6-7
“Hata ikiwa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa na kuwaweka juu majamvi na magodoro ili petro akijagawa kimli chake kimwangukie mmoja wapo wao.Nayo makuja watu wa miji ilioko kandokando ya yerusalemu wakakutanika wakileta wagonjwa .
Nao walioingiliwa na pepo wachafu nao wote wakaponywa” matendo 5:15-16
“kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi walio pagawa nao, wakalia kwa sauti kuu na watu wengi walio pooza na viwete wakaponywa”matendo 8:7.
“Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea mtu huyo amelala kitandani miaka minane, maana alikuwa amepooza. Petro akamwambia Ainea Yesu Kristo akuponya, ondoka ujitandikie, mara akaondoka na watu wale waliokaa Lida na Sharoni wakamwona wakamgeukia bwana” matendo 9:33-35.
5)Matendo ya miujiza: Ni kutenda jambo kubwa lililo zaidi ya uwezo wako. Au ni jambo la ajabu ambalo hukutegemea kulipata au kutokea au umeweza kusema bila kuweza kulielezea.
“Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya,Yesu wa Nazareti mtu aliedhihirisha kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojuana” matendo 2:22.
“Na Stefano akijaa na neema na uwezo alikuwa akifanya maajabu na ashara kubwa katika watu. Matendo 6:8.
“Lakini walipomwamini Filipo akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu na jina lake Yesu Kristo wakabatizwa wanaume na wanawake na yeye Simon mwenyewe aliamini akabatizwa akashikamana na Filipo akashangaa alipo ziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka” Matendo 8:12-13
6) Unabii: Ni kitendo cha kutabili yaliyopo, yaliyopita na yanayokuja, Nabii ni mteuliwa wa Mungu aliyeitwa kupeleka ujumbe kwa watumwa.
“Mkijua neno hili kwanza ya kwamba hakuna unabii katika maadiko upatao kufasiliwa kama apendavyo mtu flani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu bali wanadamu walinena yaliyo toka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu”. 2Petro1:20-21
“Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi, naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake yohane alie lishuhudia neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani mambo yote aliyoyaona. Heri asomae na wao wajasikiapo maneno ya unabii huu na kuyashika yaliyo andikwa humo kwa maana wakati ukaribu”. Ufunuo1:1-3
“Basi uyaandike mambo hayo ulioyaona nayo yaliyopo na yale yatakayokuwa baada ya haya” Ufunuo1:19
Unabii utakao tolewa lazima utoke kwa Mungu ambao umebeba pumzi ya Mungu maneno au neno utakalo litoa linatakiwa liwe na mambo haya.
a. Lafaa kwa mafundisho
b. Lafaa kwa kuonya watu makosa yao
c. Lafaa kwa kuwaadilisha watu katika haki
d. Lafaa kwa kuwaongoza
“Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho na kwa kuwaonya watu makosa yao na kwa kuwaongoza na kwa kuwaadilisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” 2Timotheo 3:16-17
Lakini ifahamike kwamba kuna manabii wa kweli (Mungu) na kuna manabii wa uongo (shetani). Yesu kristo aliwatahadhalisha wanafunzi wake kuhusu manabii wa uongo. Akasema mtawatambua kwa matendo yao.
“Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajua wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali mtawatanbua kwa matendo yao. Je watu huchuma zabibu katika miiba au tini katika mibaruti vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwe motoni ndiposa kwa matunda yao nitawatambua” Mathayo 7:15-20
Yesu kristo anaposema mti hapa anamanisha mtu, tunapaswa kuzijaribu kila roho je, zinatokana na Mungu au lah.
“Wapenzi msiamini kila roho basi zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na mungu kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.katika hili Mwanijua roho kwa mungu kila ikiliyo kwamba yesu kristo amekuja katika mwili yatokana na mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga kristo ambayo mmesikia kwamba yaja na sasa imekwisha kwako duniani 1Yohana 4:1-3
7)Kupambanua roho: Ni kitendo cha kutambua kinachoendelea katika ulimwengu wa roho.
“Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku usiogope, bila nena wala usinyamaze. Kwa kuwa mimi ni pamoja nawe wala hapana mtu atakae kusababishia ili kukudhuru kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu. Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu” Matendo 18:9-11.
“Akamjibu usiogope mana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha akomba akasema ee bwana nakuishi mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yake mfumishi naye akaona na tazama kile kilima kilichokuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyo mzunguka Elisha pande zote” 2Wafalme 6:16-17.
8). Aina za lugha
Kikawaida kuna aina mbalimbali za lugha hapa duniani lakini pia kuna lugha ya mbinguni ambayo watu wake wanatumia (lugha za malaika)
“Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika kama sina upendo nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao”1wakoritho 13:1
“----------Mwingine aina za lugha “ 1wakoritho 12:10
Kwahiyo Mungu anawapa watu wake karama hii kwa kuelewa lugha mbalimbali kwa usemi.
9) Kutafsiri lugha
Mungu anapompa mtu karama hii lengo lake ni kufikisha ujumbe kwa wale watu ambao hawaifahamu lugha hiyo, kwa njia ya maombi au kwa njia ya kuhubiri.
“Kwasababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri”1wakoritho 14:13
“Yamkini ziko sauti za namna nyigi duniani wala hakuna moja isiyo na maana . Basi nisipo ijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye, naye anenaye atakuwa mjinga kwangu”1wakoritho 14:10-11
“Lakini katika napewa kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha” 1wakoritho 14:19.
1o)Kuhutubu (kuhubiri)
Ni kitendo cha kutoa ujumbe toka kwa Mungu kwa maneno ya kawaida yanayoeleweka kwa lugha.
“Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja ili wote wapate kujifunza na wote wafarijiwe” 1wakoritho 14:31
“Kwa ajili ya hiyo ndugu takeni sana kuhutubu wala msizuie kunena kwa lugha. Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu” 1wakoritho 14:39-40
“Ufuateni upendo na kutaka sana karama za rohoni lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu”1wakoritho14:1
“Bali yeye ahutubiye asema na watu maneno ya kuwajenga na kuwafariji na kuvuta moyo”1wakoritho14:3
Pamoja na karama hizo zipo za aina nyingi, Kulingana na neema ya Mungu alio mpa mwanadamu kama yeye atakayo roho..
Aina za Huduma ndani ya kanisa :
Huduma: Ni taasisi inayo simamia jambofulani kwa watu. Huduma ndani ya kanisa ni taasisi inayosimamia shughuli zote za kiroho kwa watu kimwili na kiroho lakini huduma hizi zinautofauti wa:
i. Kutenda kazi
ii. Kila mtu ufunuo wake
Ndani ya kanisa kuna huduma tofauti tofauti ambazo lengo lake ni kujenga mwili wa Yesu Kristo (kuukamilisha mwili wa Yesu Kristo)
HUDUMA TANO ZA MUNGU ( KANISA)
a. Mitume: Ni mtumwa wa dini anae unganisha watu na Mungu. Ni watu waliotumwa na Mungu na kupewa uwezo katika kufanya umisheni.
b. Manabii: ni wateuliwa Mungu aliewaita kupeleka ujumbe kwa watumwa.
c. Wainjilisti: Ni mkristo mwenye utume wa kuhubiri na kutoa elimu ya habari njema za Mungu
d. Wachungaji:Ni wahudumu ndani ya kanisa au mlezi wa wahumini mpaka amalize safari yake hapa duniani kwa kuwafikisha salama kuingia mbinguni .
e. Waalimu:Ni watu wanaotoa elimu au ufahamu na ujuzi kuhusu neno la Mungu (kufundisha )
“Naye alitoa wengine kuwa mitume na wengine kuwa manabii kuwa wachungaji na waalimu kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa kristo ujengwe” waefeso 14:11-12.
“Ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu, mwenye kufundisha katika kufundisha kwake:. Warumi 12:7.
No comments:
Post a Comment