Friday, February 4, 2022

NDANI YA WOKOVU YAKUPASA KUELEWA HAYA.

 NDANI YA WOKOVU YAKUPASA KUELEWA HAYA.

-Ujue umesamehewa dhambi zako

-Dhambi zako hazikimbiwi tena

-Kuwa na imani kwa Yesu Kristo

-Una haki ya kumili

 

 

KUBADILISHWA JINA.

Kimsingi mtu anatambulika kutokana na jina lake. Lakini kabla ya kuokoka tulikuwa tunaitwa majina ya namna tofauti tofauti kulingana na ukoo au familia uliyozaliwa wapo walioitwa majina bila kujua maana zao au wengine wakijua maana zao, yamkini ni mazuri au mabaya. Mfano 1.Yabesi kwenye Biblia aliitwa jina hilo Yabesi yaani huzuni kwanini ni kwasababu alimzaa kwa huzuni (Alizaliwa kwa huzuni)

Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima  kuliko ndugu zake na mamaye akamuita jina lake Yabesi akisema ni kwasababu nalimzaa kwa huzuni. Huyo Yebesi

 

akamlingana Mungu wa Israel,akisema, Lau kwamba ungenibarikia kwelikweli na kunizidishia  hozi yangu na mkono wake ungekuwa pamoja nami nawe ungelishinda na uovu ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba 1Nyakati 4;9-10

         Kwahiyo tunajifunza mambo yafuatayo hapa

 

 

 

     a)Akamlingana Mungu

 

·        Akaanza kumtafuta Mungu

·        Akaanza kusoma neno la Mungu

·        Akaanza kufunga

·        Akaanza kwenda kanisani

·        Akaanza kuomba

·        Akaanza kwenda mikesha

·        Akaanza kumuabudu Mungu kwa nyimbo na tenzi za Rohoni

Lengo lake huyu Yabesi alishafahamu jina alilopewa siyo zuri bali ni baya hivyo akataka ajikomboe kutokana na nguvu ya jina alilopewa la huzuni (Yabesi)

 

b)Lau kwanza ungenibarikia kwelikweli hapa akawa anamuomba Mungu ambarikie kwelikweli alishaelewa ndani ya jina lake la Yabesi (huzuni) halina Baraka bali ni matatizo matupu tu kwake.

 

c)Kunizidishia kozi yangu

Alikuwa anamtaka Mungu amuongezee umiliki maana alishafahamu umiliki alionao ni mdogo kutokana na jina lake alitakaMungu

-Apanue mipaka yake kama ni kwenye kazi,mashamba, mifugo, fedha, biashara n.k.

 

-Apanue hema yake, maana yake nyumba ziongezeke, kama anayo moja ziongezeke zaidi kwa Jina Yesu. Amen.

 

d)Mkono wako ungekuwa pamoja nami

Alitaka mkono wa Mungu uwe pamoja naye kila mahali, alijua mkono wa Mungu.

 

·        Unanguvu ya kuokoa

·        Ni ulinzi

·        Ni afya njema

·        Ni wa huruma

·        Ni wa kuponya.

Alijua pasipo mkono wa Mungu kumuhatamia hakuna kitakachofanyika.

 

e)Nawe ungenilinda na uovu ili usiwe kwa huzuni yangu.

Alikuwa anatamka Mungu amlinde, ili ile laana ya jina isiwepo ndani yake, alielewa ndani ya jina hilo kuna;

 

·        Kuwaza mambo mabaya

·        Kukata tama.

·        Kuvunjika moyo.

·        Masikitiko.

·        Taabu

·        Laana.

·        Mikosi

·        Umasikini

·        Magonjwa  n.k

 

f)Naye Mungu akamjalia hayo aliyo yaomba.

Alijua maombi yanatufanya tumtafute Mungu “Nanyi mtanitafuta na kuniona mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” Yeremia 29:13

Alijua maombi yanainua mtu, Akawajibu yeyealiyemfanya mzima kuwa mzima ndiye aliyeniambia  jitwike godoro lako uende Yohana 5:11

Alijua maombi yankupa utajiri

“Maana nimejua Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa masikini kwaajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajirikwa umaskini wake 2Wakorintho 8;9

 

“Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya kristo Yesu. “Wafilipi 4;19”

 

Mfano 2. Ibrahimu (Baba yetu wa imani) na mke wake Sara.

Mungu alimuomba kwamba hawezi kumfanya baba wa mataifa mengi kama jina lake litabaki vile vile Abramu na hata mkewe ili awe mama wa uzao mwingi lazima jina libadilike asiitwe tena Sarai bali Sara.

 

“Mimi agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, wala jina lako hutoitwa tena Ibrahimu kwani ni mekuweka uwe baba wa mataifa mengi. Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana nami nitakufanya kuwa mataifa na wafalme watatoka kwako “ Mwanzo 17;4-6.

“Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo hutamwita jina lake Sarai kwakuwa jina lake litakuwa Sara. Nami nitambariki naye atakuwa mama wa mataifa na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake” Mwanzo 17;16.

 

Mfano 3. Yakobo

Yakobo alishindana na malaika wa Mungu, aking’ang’ania  Baraka. Lakini malaika alimuona Yakobo Baraka anazo ila kwasababu ya jina malaika akawa anaona ugumu kutoa Baraka mapaka akamuuliza jina lake naye akasema Yakobo hutaitwa tena Yakobo bali Israel.

“Yakobo akakaa peke yake na mtu mmoja akashindana naye mweleka hataalfajiri. Naye alipoona ya kuwa hamshindi alimgusa panapo uvungu  wa paja lake,

 

 ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. Akasema niache niende maana kunapambazuka. Akasema sikuachi usiponibariki, Akamuuliza jina lako nani, Akasema Yakobo. Akamwambia jinalako halitakuwa tena Yakobo bali Israel maana umeshindana na Mungu na watu nawe umeshinda. Yakobo akamuuliza akasema niambie tafadhali jina lako, Akasema kwanini waniuliza jina langu? Akambariki huko Yakobo akapata mahali pale Peneli maana alisema , nimeonana na Mungu uso kwa uso na nafsi yangu imeokoka” Mwanzo 32;24-30, Kwahiyo sasa baada ya kuokoka tumepewa majina mapya ,Majina yetu yamebadilishwa tunaitwa

 

a)Sisi sasa ni wana wa Mungu/watoto wa Mungu na baada tu ya kutubu dhambi zako (kuokoka) moja kwa moja ulimwengu war oho jina lina badilika.”Tazameni ni pendo la namna gani aliotupa Baba kwamba tuitwe wana wa Mungu na ndivyo tulivyo. Kwasbabu hii ulimwengu haututambui kwakuwa haukumtambua yeye 1Yohana 3;1” “Kwakuwa ninyi nyote  mmekuwa wana wa Mungu  kwa njia ya Imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo  mmemvaa Kristo” Wagalatia 3;26-27.

 

i)Majina yetu yameandikwa katika kitabu cha uzima.

Kwahiyo tunapookoka tunatakiwa kwendelea na wokovu ilimajina yetu yasifutwe.

“Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima name nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu na mbele ya malaika zake” Ufunuo 3;5

“Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandika katika kitabu cha uzima alitupwa katika lile ziwa la moto” Ufunuo 20;15

 

 

ii)Utaanza kuzijua siri za ufalme wa Mbinguni unapokuwa umeokoka unakuwa umejiunganisha na ufalme wa mbinguni yaani Mungu Baba anakujua , Mungu Mwana anakujua, Mungu Roho Mtakatifu anakujua na Malaika zake nao wanakujua. Hivyo utaanza kuzijua siri za ufalme wa Mungu, jinsi ya kuenenda na haki zako.

“Akajibu akawaambia ,Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakukaliwa” Mathayo 13;11.

 

iii)Tunapokea nguvu

Wakristo sisi nguvu yetu ni Roho mtakatifu aliye ndani yetu, hivyo baada ya kuokoka Roho mtakatifu aliye ndani yetu, hivyo baada ya kuokoka anakuwepo ndani sasa ni wewe kwa kumchochea ndani yake kwa kusoma neno la Mungu, kufunga na kuomba, kumsifu Mungu na kumuabudu n.k.

Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yelusalemu na uyahudi na somaria na hata mwisho wan chi” Matendo 1;8

 

Roho mtakatifu akianza kufanya kazi ndani yako mambo kadhaa yatabadilika;

i). Utakuwa jasiri

ii).Hutaogopa vitisho vya watu

iii)Hutaona aibu kushuhudia Neno la Mungu(utalisema neno la Mungu kwa ujasiri

iv)Utakuwa mtii kwa Mungu.

v)Atakubadilisha matendo yako mabaya

vi)Atakupa maarifa, kukuonya, kukwelekeza n.k

 

b)Unakuwa silaha ya bwana ya vita siku zote Mungu ni roho ili atende kazi katika mapambano atakutumia wewe kwenye maombi, Roho mtakatifu atatumia kinywa chako, mikono yako katika kupambana.

 

“Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi nay eye ampendaye na kwa wewe,nilivunja-vunja gari la vita nay eye achukuliwaye ndani yake, na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto na kwa wewe nitawavunja-vunja kijani mwanamume na kijana mwanamke na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake na kwa wewe nitavunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe na kwa wewe nitavunja-vunja maliwali na maakida. Nami nitamlipa babeli na wote wakaao ndani ya ukaldayo, mabaya yao yote waliyoyatenda katika sayuni mbele  ya macho yenu, asema BWANA” Yeremia 15;20-24.

c) Sisi si wa ulimwengu huu.

Kikawaida Yesu kristo yupo siku zote nasi haja ukamilifu wa dahali, Yeye yupo Rohoni lakini anatenda kazi kiroho na kimwili, kimwili tunaonekana jinsi tulivyo lakini kristo si waulimwengu huu. Yesu anasema katika maombi na Mungu Baba.

Mimi nimewapa neno lako na ulimwengu umewachukia kwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu, mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu.Uwatakase kwa ile kweli yako, neno lako ndiyo kweli.” Yohana 17;14-17

 

 

iv)Tunapewa uwezo na mamlaka na amri

Tunaposamehewa dhambi zetu, Yesu kristo anatupa mamlaka juu ya viumbe wote “Akawaita wale thenashara akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhiMathayo 9;1-2.

Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu wawatoe nakupooza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina”  Mathayo 10;1.

 

d)Wewe sasa ni mwali wa moto

Mungu anawapenda wana wake siku zote, katika maisha ya wokovu Mungu anatuwekea moto(miali ya moto) inakuwa ikitunzunguka pande zote. “Na kwa habari ya malaika asema, afanyaje malaika wake kuwa upepo na watumishi wake kuwa miali ya moto “Waebrania 1:7. Wewe ni mtumishi wa Mungu upo katika himaya yake (ndani ya ufalme wake).

Unapata ulinzi.

Unapo okoka unapata ulinzi toka kwa mungu kwa kuwatuma malaika zake wakulinde.  “Malaika wa bwana hufanya k…….akiwazungukia wamchao na kuwaokoa “. Zaburi 34:7

 

Sisi ni Nuru ya ulimwengu

Tunapo okoka tunafanyika kuwa kielelezo kwa wengine, kwa matendo yetu yanatakiwa kuwa mema ili wamtukuze baba yetu wa mbinguni.

Ninyi ni nuru ya ulimwengu mji hauwezi kusitirika ukwa juu yam lima –wala watu hawa washi taa na kiuweka chini ya pishi bali juu ya kiango nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu wapate kuyaona matendo yenu mema wamtukuze baba yenu aliye mbinguni

 

 

Mathayo 5:14-15

Sisi ni chumvi ya dunia

Unapompa Yesu Kristo maisha yako/ Mungu anakufananisha na chumvi, kwamba sisi ni msaada kwa wengine ambao hawamjui Mungu tunapokuwa sehemu hiyo lazima tuwabadilishe.

Ninyi ni chumvi ya dunia lakini chumvi ikiwa imeharibika itakuwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa ila kutupwa nje kukanyagwa na watu” Mathayo 5:13


 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


No comments:

Post a Comment