UWEZA WA MAOMBI,
Uweza; Maana yake ni nguvu
Maombi; Maana yake ni mawasiliano au kuzungumza na Mungu.
-Ni mamlaka ya Mungu inayotenda kazi katika ulimwengu wa roho.
-Ni nguvu za Mungu zinazohusika kwa kujibu jambo Fulani.
AINA ZA MAOMBI
1. Maombi ya kawaida.
Mfano:- maombi ya kumbariki mtu
- Maombi ya toba na rehema
- Maombi ya kuombea chakula
- Maombi ya kuombea safari
- Maombi ya kumshukuru Mungu
- Maombi ya kuombea ndoa n.k
2. Maombi ya vita
Mfano- maombi ya mkesha.
-maombi ya mfungo
-maombi ya kuharibu falme na mamlaka za giza
- maombi ya kuombea wagonjwa.
- maombi ya kufunguliwa
- maombi ya ukombozi
- maombi ya urejesho (kurudisha) n.k.
Vilevile maombi ya muda mrefu na maombi ya muda mfupi yapo katika hizo aina za maombi.
MAMBO UNAYOPASWA KUYAJUA KUHUSU MAOMBI.
i). kupitia maombi Mungu anaweza kufanya mambo yote
‘lakini Yule malaika akamwambia, usiogope Zakaria maana dua yako imesikiwa na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanaume na jina lake utamwita Yohana ‘Luka 1;13
Siku hizo Hezekia akaugua akawa katika hatari ya kufa, Isaya nabii mwana wa Amozi akamjia akamwambia Bwana asema hili , tengeneza mambo ya nyumba yako maana utakufa wala hutapona Basi Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwambia Bwana ukumbuke sasa jinsi nilivyokwenda mbele yako katika kweli na moyo mkamilifu na kutenda yaliyomema machoni pako Hezekia akalia sana sana. Ikawa kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia kusema, Rudi ukamwambie Hezekia mkuu wa watu wangu Bwana Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, nimeyasikia maombi yako na kuyaona machozi yako, tazama nitakuponya siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana, Tena nitazidisha siku zako kiasi cha miaka kumi na mitano, name nitakuokoa wewe na mji huu na mkono wa mfalme wa Ashuru, name nitakulinda mji huu kwa ajili yangu na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, 2wafalme 1-6.
ii). Maombi kwa Mungu yanapaswa kuwa ni ya kuendelea kuwa sehemu ya maisha ya mkristo.
‘Akawaambia mfano ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tama Luka 18;1.
iii). Katika maombi tunatakiwa kupeleka haja zetu kwa Mungu.
‘Msijisumbue kwa neno lolote bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu.
iv). Tunatakiwa tuwe na imani.
‘Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima na oambe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yoyote maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililichukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku “ Yakobo 1;5-6.
“Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa Yule na Bwana atamwinua hata ikiwa amefanya dhambi atasamehewa Yakobo 5;15.
v). Tunatakiwa kuomba kwa jina la Yesu
“Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu hilo nitalifanya ili baba atukuzwe ndani ya mwana.
Yohana 14;13.
vi). Mungu anasikia maombi ya watu wote
“ katika shida yangu nalimwita Bwana na hekaluni mwake, kilio change kikaingia maskioni mwake , ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, misingi ya milima ikasuka-suka…. “Zaburi 18;6-7.
“kwa kuwa Bwana huwaakia wahitaji wala hawadharau wafungwa wake Zaburi 69;33.
Vii). Mungu anajibu maombi.
“ walilia naye Bwana akasikia , akawaponya na taabu zao zote, Zaburi 34;17.
Lakini panapo usiku wa manane Paulo na sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza ghafla kukatokea matetemeko kuu la nchi hata msisingi ya gereza ikatikisika na mara hiyo milango ikafunguka vifungo vya wote vikalegezwa. Matendo 16;25-26.
viii). Tunapaswa kuomba kwa bidii.
Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita, Akaomba tena mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake , Yakobo 5;17-18.
Maana ya kuomba kwa bidii,
-kuomba kwa kuweka akili zako zote kwenye jambo hilo
-kuomba kwa ujasiri
-kuomba kwa nia yako bila kukata tama.
-kuomba kwa nia moja.
-kuomba kila siku bila kuchoka.
-kuomba bila kuogopa
-kuomba kwa maarifa
-kuomba kwa mamlaka ya Mungu
Kumbuka sisi ni wana wa Mungu, hivyo tumepewa amri juu ya nguvu za giza kwamba tukitamka neno juu yao linakuwa vile vile kwa jina la Yesu- Amen.
Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za Yule adui wala hakuna kitu kitakacho wadhuru
Tumepewa amri ya kukanyaga nyoka na nge.
*kukanyaga tunguli
*vipembe
*mikoba
*kukanyaga nguvu za adui
*mapepo na majini
*kukanyaga silaha zote za kichawi.
Kila kitu kinatakiwa kukitakasa kwa Damu ya Yesu Kristo.
Kila sehemu tunayoingia tunatakiwa kupatakasa kwa Damu ya Yesu Kristo.
Hakuna kitakachowadhuru
FAIDA ZA MAOMBI
a) Hutusaidia kukua kiimani.
“Kisha akawaleta nje akasema Bwana zangu yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako, Matendo 16;30-31.
b) Mambo yako ya ndani yatafunguliwa
Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako “zaburi 119;18.
c) Maombi ni ulinzi
Basi akamfukuza huyo mtu akaweka makerubi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga wa moto uliogeuka huko na huko kulinda njia ya mji wa uzima “Mwanzo 3;24.
d) Maombi yanatufanya tumtafute Mungu,
Nanyi mtaniita mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza, Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa mioyo yenu yote.
Yeremia 29;12-13.
Ndipo Bwana akaniambia umeona vema kwa maana ninaliangalia neno langu ili nilitimize ‘Yermia 1;12’
Naliangalia neno langu ili nilitimize, hivyo Mungu hawezi kujipinga mwenyewe.
e) Utamruhusu Roho mtakatifu akutumie
“Kadharika Roho naye kutusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa “warumi 8;26.
‘Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja yeye Yule akiangamia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. “1wakoritho 12;11.
f) Utatumika vizuri kwa Mungu.
Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao wakawaacha waende zao, Matendo 13;2-3.
g) Utakuwa na nguvu za Mungu
“Tangu siku za Yohana mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu nao wenye nguvu wauteka, Mathayo 11;12
h) Maombi yanainua mtu
“Yesu akamwambia simama jituike godoro lako uende. Mara Yule mtu akawa mzima akajitwika godoro lake akaenda Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo, Yohana 5;8
Na kule kuoma kwa imani kutamwokoa mgonjwa Yule na Bwana atamwinua hata ikiwa amefanya dhambi atasamehewa ‘Yakobo 5;15
UMUHIMU WA KUFUNGA (mfungo).
Mfungo; Ni hali ya kukaa bila kula chakula au kinywaji ili kutekeleza masuala ya imani yako. Mfungo unatoa sauti inayopenya hadi kwenye kiti cha Mungu Baba na kuleta mabadiliko ya kudumu katika ulimwengu wa mwili, Hii ni kanuni ya ulimwengu wa Roho ili kufanya jambo lililokusudiwa litokee.
WALIOFUNGA KWENYE BIBLIA.
a) Yesu kristo,
Yesu kristo alifunga siku arobaini (40)
‘Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani ili ajaribiwe na ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa, Mathayo4;1-2.
b) Musa
Musa naye alifunga siku arobaini 40)ili asemezane na Mungu.
Nikaanguka nchi mbele za Bwana siku arobaini usiku na mchana kama pale kwanza sikula chakula wala kunywa maji kwasababu ya makosa yenu yote mliyokosa kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana kwa kumkasirisha, Torati 9;18.
Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake hakula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi “kutoka 34;28”
c) Daniel alifunga siku ishirini na moja(21)”Katika “siku zile mimi Daniel nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu” Danieli 10;13,”……. lakini mkuu wa ufalme alinipinga siku ishirini na moja” Daniel 10;2.
d) Esta; Esta na wayahudi alifunga siku tatu ili aingie kinyume cha sheria kwa mfalme.
“Uende ukakusanye wayahudi wote waliopo hapa shushani mkafunge kwa ajili yangu, msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku na mchana nami na wajakazi wangu tutafunga vilevile, kisha nitaingia kwa mfalme kinyume cha sheria, nami nikiangamia na niangamie “Esta 4;16.
e) Watu wa Ninawi.
Hawa walifunga wakimlilia Bwana awaepushe na hatari iliyokuwepo mbele yao.
“Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu, wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo, Yohana 3;5
f) Barnaba, Simion, Lukio Mkirene, Manaeni
Nao hawa walifunga ila Biblia haijaonyesha.
Walifunga siku ngapi
Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga.
Kwahiyo ni mifano michache tu kwa waliofanya kulikana na sababu Fulani Fulani kwao.
AINA ZA MIFUNGO (fasting)
1. Mfungo mwepesi.
Huu ni mfungo ambao mtu aliyefunga anaweza kunywa uji, maji na vitu vyepesi. Lengo la mfungo huu ni kujinyenyekeza mbele za Mungu au kutaka kumpa Mungu nafasi yake. Mfano. Mtu anasema nitafunga siku 3,21 au 40 nitakuwa nakunywa maji na jioni nafungulia.
2. Mfungo mkavu.
Huu ni mfungo wa kutaka kitu Fulani kwa Mungu ili ujibiwe haraka. Mfano Esta na wayahudi, walifunga siku tatu bila kula chochote na majibu yakaja bila kuchelewa.
SIFA ZA MFUNGO.
a) Kuongozwa na Roho ,takatifu
Mara Roho akamtoa aende nyikani, Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na shetani, naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu na malaika walikuwa wakimhudumia , Marko 1;12-13.
b) Mfungo ufanywe katika unyenyekevu,
ilikuwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia kutoka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao” 2zanyakati 7;14
c) Kuambatane na kuomba
“Ndipo mwakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao wakawaacha waende zao. “matendo 13;3
d) Mfungo ufanywe kwa furaha.
“Tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana, maana ujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga.Amini nawaambieni wamekwisha kupata thawabu yao” Mathayo 6;16.
e) Unapofunga watu wasikujue
Bali wewe ufungapo jipake mafuta kichwani unawe uso. Ili usionekane na watu kuwa unafunga ila na Baba yako aliyesirini na Baba yako aonaye sirini atakujazi, ‘Mathayo 6;17-18
NDANI YA MFUNGO KUNA VITU HIVI
Siku zote unapomuona kufunga mfungo wa aina yoyote ile tambua vitu hivi lazima vijitokeze au viwepo.
-Malaika watakuwepo wakikihudumia
-Shetani naye atakuwepo ili akujaribu.
-Utajisikia mchovu au kuishiwa nguvu
-Mwili utaisha (kupungua) lakini mtu wa ndani atakuwa na nguvu za rohoni.
-Utukufu wa Mungu utakufunika.
“Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama ngozi ya uso wake iling’aa nao wakaogopa kumkaribia “kutoka 34;30
FAIDA/ UMUHIMU WA MFUNGO
-Kuonyesha utii mbele za Mungu
“Lakini hata sasa anasema Bwana, nirudieni mimi, kwa miyo yenu yote na kwa kufunga na kwa kulia na kwa kuomboleza Yoeli 2;12
-Ili kujinyenyekeza mbele za Mungu
“Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe na kwa ajili ya watoto wetu na kwa mali yetu yote Ezra 8;21.
-Ili kupata msaada,
“Basi tukafunga tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo, naye akatutakabali, Ezra 8;23
-Ili katika udhaifu wetu nguvu za Mungu zionekana,
“Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta ‘Zaburi 109; 24
-Ili kuomba Rehema.
Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi na dua pamoja na kufunga na kuvaa nguo za magunia na majivu, Daniel 9;3
-Ili Hunao imani na kuongeza ujasiri.
“Uende ukawakusanye wayahudi wote waliopo hapa shushani mkafunge kwa ajili yangu’ Esta 4;16.
-Huongeza/ huleta nguvu ya maombi
‘Bali mimi walipougua wao, nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga, maombi yangu yakarejea kifuani mwangu “ Zaburi 35;13
-Kukuza kanisa na huduma ya Mungu isonge mbele.
“Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msipokee neema ya Mungu bure (kwa maana asema wakati uliokubalika na likusudia siku ya wokovu nalikusaidia, tazana wakati uliokubaliwa ndio sasa tazama siku ya wokovu ndiyo sasa)” 2wakoritho 6;1-2.
-Kuufanya ulimwengu wa Roho uwe wazi :”Maana ingawa tunaenda katika mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili.(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka kujiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii kristo ;2wakoritho 10;3-5
-Kuutiisha mwili,
‘Basi nasema enendeni katika Roho, wala hamtazitimiza kamwe tama za mwili, kwasababu mwili hutamani ukishindana na Roho na Roho kushindana na mwili, kwa maana hizi zinapingana hata hamwezi kufanya mnayotaka,Lakini mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria’ wagalatia 5;16-18.
No comments:
Post a Comment