BAADA YA KUOKOKA
KUOKOKA-:
Ni kitendo cha kutubu dhambi zako mbele ya Mungu na wanadamu. Kwa kukiri kwa kinywa chako mwenyewe kwamba umeacha dhambi zako na hautozirudia tena “namkataa shetani na mambo yake yote”. Kwahiyo tunapo okoka miili yetu inabaki vilevile lakini roho zetu zinakuwa mpya kwa kutakaswa na Damu ya Yesu Kristo.
“Kama vile Mungu Baba alivyo tangulia kuwajua katika kutakaswa na roho hata mkapata kutii na kunyunyizwa Damu ya Yesu kristo. Neema na amani na ziongozwe kwenu” 1petro1:2
Kuokoka: Ni mpango wa Mungu kwa wanadamu katika kuishinda dhambi.au ni kitendo cha kumkiri Yesu kwa kinywa chako na kuamini moyoni mwako kuwa ni Bwana na mwokozi wako.
“Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”. Warumi 10:9-10
Tunapokuwa tumeokoka tunakuwa tumezaliwa mara ya pili kiroho yaani mambo ya kale tunayaacha .
“Yesu akajibu akamwambia amini amini nakwambia mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuona ufalme wa Mungu”. Yohana 3:3
“Ahimidiwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa rehema zake nyingialituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu katika wafu tupate na urithi usioharibika usio na uchafu, usionyauka uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu”1petro 1:3-4
Hivyo basi baada ya kuokoka tunapata uzima wa milele ambao Yesu Kristo ametuandalia huko mbinguni, na tunakuwa tunalindwa na nguvu za Mungu hapa duniani kwa njia ya imani.
“Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu uliotayari kufunuliwa wakati wa mwisho “1Petro 1:5
WOKOVU
Wokovu ni mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu alie potea kupitia dini, Roho Mtakatifu na watumishi wake. Kwahiyo njia ya wokovu ni Yesu Kristo
“Yesu akamwambi mimi ni njia ya kweli na uzima mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi” Yohana 14:6.
Wokovu tulio nao ni wa muhimu sana tunatakiwa kuulinda kwa nguvu zetu zote maana ni kwa ajili ya roho zetu, inapaswa tumpende Yesu hata kama hatumuoni kimwili lakini kiroho yupo pamoja na sisi.
“Naye mwampenda ijapokuwa hamkuomwona ambaye ijapokuwa hamwoni sasa mnamwini na kufurahi sana kwa furaha isiyoneneka yenye utukufu katika kuupokea mwisho wa imani yenu yaani wokovu wa roho zenu”1Petro 1:8-9.
Tunapokuwa ndani ya wokovu hatutakiwi tena kujifananisha na tamaa zetu za kwanza za ujinga. Tunapaswa kuyashika na kuyatii yale anayotaka Yesu Kristo ndiyo tuishi nayo.
“Kama watoto wakutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu bali kama yeye alie waita alivyo mtakatifu ninyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote, kwa maana imeandikwa mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu “1Petro:14-16
Tuliokolewa si kwa vitu viharibikavyo, Yesu Kristo alikufa kwa ajili yetu kwa aibu ili sisi tupate thamani kubwa ya maisha yetu ya sasa na yabaadaye, maana alitutoa kwenye mwenendo usiofaa.
“Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo kwa fedha au dhahabu mpate kufika katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu bali kwa damu ya thamani kama ya mwanakondoo asiye na ila,asiye na waa yaani ya Kristo “1Petro 1:18-19
Tunapo okoka tunapaswa kuwa vielelezo kwa watu wengine (yaani ndugu,marafiki,majirani na jamii kwa ujumla ). Kama tukiwa na matendo mazuri mbele za watu, hata wewe mwenyewe binafsi, hapo Mungu anatukuzwa kupitia wewe ulieokoka, wewe ni alama ya Yesu Kristo hapa duniani.
“Wapenzi nawasihi kama wapitaji na wasafiri ziepukeni tamaa za mwili zipinganazo na roho mwe na mwenendo mzuri kati ya mataifa ili iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya wayatazamapo matendo yenu mazuri wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa “1Petro 2:11-12 hata nabii Isaya anasisitiza hilo.
“Jiosheni jitakaseni ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu, acheni kutenda mabaya” Isaya 1:16
Mungu siku zote anatuwazia mema na hataki mtu yeyote apotee kwenye Jehanamu ya moto, yeye ni mwenye huruma anataka tusogee mbele zake na tusemezane naye kuhusu dhambi zetu tulizo zitenda kwa kujua au kwakuto kujua tunazozifahamu na tusizozifahamu anatutaka tuwe watii kwenye kutubu dhambi zetu.
“Haya njooni tusezane asema BWANA, dhambi zenu zipojapokuwa nyekundu sana zitakuwa nyeupe kama theluji, zijapokuwa nyekundu kama bendera zinakuwa nyeupe kama sufu kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi, bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga, maana kinywa cha BWANA kimenena haya” Isaya 1;18-20
Tunapo tubu dhambi zetu mbele za Mungu kwanza anatusamehe maovu yetu, pili anatuponya magonjwa yetu, tatu anatukomboa uhai wetu na kaburi, nne anatuvika taji ya fadhili na rehema, tano aushihisha mema uzee wako na sita aurejesha ujana wako.
“Akusamehe maovu yako yote,akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kabuli akutia taji ya fadhili na rehema, aushibisha mema uzee wako, ujana wako ukarejezwa kama tai “Zaburi 103:3-5.
Hapo Mungu alikuwa na maana hii;
a) Akusamehe maovu yako yote
Kabla ya kuokoka ulikuwa unaishi maisha ya dhambi, ambayo yalikuwa hayampendezi Yesu anakuwa amekusamehe yale maovu yako yote uliyokuwa unayatenda, hivyo unakuwa mpya mbele za Mungu.
b) Akuponya magonjwa yako yote.
Mungu akisha kusamehe anaanza kushugulika na afya yako maana umefungua moyo wako kwake, na kama ulikuwa na magonjwa ataanza kukuponya.
c) Aukomboa uhai wako na kaburi.
Kama ulitakiwa kufa basi hapo Mungu anakomboa uhai wako, kutoka kwenye mauti na kukuingiza uzimani tena.
d) Akutia taji ya fadhili na rehema.
Hapa Yesu Kristo anakuangalia upya tena kwa huruma zake na kukuhurumia.
e) Aushibishe mema uzee wako.
Mungu kwa vile yeye ni mwema na mwaminifu uzee wako anaushibisha mema (yaani anakupa mambo mazuri wakati wa uzee wako)
f) Ujana wako ukarejezwa kama tai.
Yale mambo uliotakiwa yakupate mazuri wakati wa ujana wako na sasa yamepotea huna tena zile Baraka za ujana, Yesu Kristo anakwenda kukurejeshea tena kwa nguvu ya ukombozi kwa jina la Yesu halelujaah.
Yesu Kristo akishakusamehe dhambi zako hazikumbuki tena na anaziweka mbali nasi
“Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyoziweka mbali dhambi zetu mbali nasi” Zaburi 103:12
“Mimi naam mimi ndimi nifutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe wala sitazikumbuka dhambi zako” Isaya 43:25
“Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito na dhambi zako kama wingu unirudie maana nimekukomboa “ Isaya44:22
ALIZICHUKUA DHAMBI ZETU
Yesu Kristo alikuja hapa duniani kwa ajili ya kuja kuchukua maovu yetu ili atengeneze upatanishi kati ya wanadamu na Mungu Baba.
“Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi tuwe hai kwa mambo ya haki na kwa kupigwa kwake mliponywa. kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo lakini sa mmerudia mchungaji na mwangalizi wa roho zenu. 1Petro 2:24-25.
“Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu sababu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”. Isaya 53:5.
Yesu Kristo alijeruhiwa kwa ajili ya makosa yetu , maovu na adhabu zetu alizibeba yeye mwenyewe ili sisi tupone, ni jambo la thamani mno alilolifanya Yesu Kristo kwetu ili sisi tupone .
Yesu kristo alipigwa, alitemewa mate ili mimi na wewe tupone.
“Wengine wakaanza kumtemea mate wakamfunika uso na kumpiga mkonde na kumwambia tabiri hata watumishi nao wakampiga makofi.”Marko 14:65.
Yesu Kristo alivishwa taji la miiba kichwani.
“Wakamvika vazi la rangi ya zambarau wakasokota taji ya miiba wakamtia kichwani.” Marko 15:17.
Yote hayo aliyavumilia ili watu waokolewe kutoka kwenye dhambi.
Yesu Kristo alivuliwa nguo kwa ajili yetu.
“wakavua nguo wakamvika vazi jekundu”
Mathayo 27:28.
Yesu Kristo alidhihakiwa kwa ajili yetu .
“walipokwisha kumthihaki wakalivua lile vazi wakamvika mavazi yake wakamchukua kumsulubisha.” Mathayo 27:31
“Walipokwisha kumthihaki waligawa mavazi yake wakapiga kura ili litimie neno lililo nenwa na nabii waligawa nguo zangu kati yao na juu ya vazi langu walipiga kura” Mathayo 27:35
Yesu Kristo alipewa nyongo kwa ajili yetu.
“Wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa.”
Mathayo 27:34 “mara mmoja wao akaenda mbio akatoa sifongo akaijaza siki akaitia juu ya mwanzi akamnywesha” Mathayo 27:48.
Yesu Kristo alichomwa mkuki ubavuni kwa ajili yetu.
“lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki na mara ikatoka damu na maji” Yohana 19:3, damu na maji yaliyokuwa yakitoka ubavuni mwake, moja moyo wake ulikuwa umepasuka kwa sababu ya mkuki huo.
Hivyo Yesu Kristo aliteswa katika mwili wake na mateso yote aliofanyiwa ili sisi tuokolewe na dhambi ya moto tuliotakiwa, tuliostahili lakini yeye “aliyachukua maovu yetu” Kama yeye alifanya hivyo kwa ajili yetu basi nasi hatuna budi tuendelee kumtumkia yeye na kuziacha tamaa mbaya za dunia hii kama wafanyavyo mataifa, maadamu tumemkiri yeye tundelee kuwa naye siku zote za maisha yetu.
“Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ileile kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. Tangu sasa msiendelee kuishi katika tama za mwanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu wakati wetu wa kuaa hapa dunian. Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya mataifa kuenenda katika ufisadi na tama na ulevi na karamu za ulafi na vileo na idadi ya sanamu isiyo halali. Mambo ambayo wao huna kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi uleule usio na kiasi,
No comments:
Post a Comment