Monday, March 28, 2022

NGUVU YA KIONGOZI WA KIROHO

 Kiongozi wa kiroho anapaswa kuyatekeleza mambo yafuatayo

1.Kuwa na Nia ya kuwajili wengine

Unapokuwa kiongozi unapaswa kuwa na Nia nzuri kwa wale unaowaongoza.Nia NI idara ya fikra,hivyo kill unachofikilia au kukiwaza je,Nia yako NI kuwafanya watu wamjue Mungu,kuwasaidia na sio kuwanyonya au kuwalazimisha kutekeleza Jambo Fulani halafu wao hawana uwezo nalo,Nia yako siku zote yakupasa iwe njema

"Iweni na Nia iyo hiyo NDANI yenu ambayo ilikuwamo pia NDANI ya Kristo Yesu" Wafilipi 2:5

2.Kuwapatanisha watu na Mungu

Yohana 8:26-30

3.Kuwa na hekima

1Wafalme 10:1-4

4.Kuwa na uweza

5.Kuwa na maarifa

6.Kumcha Mungu

Isaya 

Saturday, March 5, 2022

MAONO YAKO YAMEENDA WAPI?

 MAONO NI fikra za kinjozi au mtu mwenye uwezo wa kuona mbali au NI ile Hali ya kitu au tukio lioneoanalo kwenye akili lakini kiuhalisia halipo,picha ambayo ipo kwenye akili zako,kwamba unataka kuwa Nani,unataka kufanya Nini? 

AINA ZA MAONO

1.Maono Binafsi 

NI Yale MAONO ambayo NI ya kwako wewe mwenyewe Binafsi,lazima ujue Nini unataka katika maisha YAKO na Kama unataka kuendelea kamwe usiogope watu watasema Nini kuhusu wewe 

2.Maono ya Familia 

Hapa NI pale  unavyovipa vipaumbele vyenu vya maisha yenu mapya ya ndoa 

3.Unamfanyia Nini Mungu 

Hapa NI vile au NI Yale mambo yanayomuhusu Mungu ambayo unapaswa kuyatenda 

MAONO Ndiyo dira ya Safari yako ya mafanikio.Pasipo MAONO watu huacha kujizuia (kuangamia) 

"Pasipo maono watu huacha kujizuia Bali Ana heri mtu yule aishikaye sheria".Mithali 29:18 

Kimsingi Mwanzo ulikuwa na mipango mingi  Sana (maono),kwamba nikiwa mkubwa nitafanya hivi na vile.Nikipata hell nitafanya hili na Lile la maendeleo,yaani unakuwa na mipango lukuki lakini ukizipata hizo hela hakuna kinachoendelea,nakuuliza maono yako yako WAPI? 

"BWANA akajibu akasema iandike njozi ukaifanye iwe wasi Sana katika vibao,ili aisomae apate kuisoma Kama maji.Maana njozi hii bado NI kwa wakati ulioamriwa,inafanya haraka I'll kuufikilia mwisho wake,Wala haitasema uongo.Ijapokawia,ingojee kwa kuwa Haina budi kuja,haitakawia".Habakuki 2:2-3 

"Nawe angalia ya kwamba uvifanye Kama mfano wake,uliooyeshwa mlimani".KUTOKA 25:40 

"Nawe utaisimamisha hiyo maskani sawasawa na mfano wake uliooyeshwa mlimani".KUTOKA 26:30 

Leo hii maono yako YAMEENDA WAPI? Nani kayachukua? Mbona hayajatimia? Hujue happy wajanja wameshafanya Yao.Leo amka na simama Anza kudai maono yako Sasa kwa jina la Yesu Kristo 

MAOMBI 

BABA MUNGU KATIKA JINA LA YESU.LEO NIMETAMBUA KWAMBA MAONO YANGU YA KUJENGA NYUMBA,KUSOMA,KUOA,KUOLEWA,NK,YAMEIBIWA,YAMECHUKULIWA.NASOGEA KWENYE KITI CHA ENZI CHA MBINGUNI KULETA HAJA YANGU HII,KATIKA JINA LA YESU KRISTO.KILA MADHABAHU ZA KISHETANI ZILIZOSHIKILIA MAONO YANGU LEO NAZIPASUA KWA JINA LA YESU.LEO NATAKA MAONO YANGU UYAACHIE KWA JINA LA YESU .KILA MWENYE NGUVU ALIYEYAIBA MAONO YANGU NAMSHAMBULIA.MAONO YA BIASHARA,KUZAA,HUDUMA,LEO NAYATAKA KWA JINA LA YESU.EWE MZIMU WA UKOO ULIYOKAMATA MAONO YANGU YA KUFANIKIWA NAKUTEKETEZA,EWE MCHAWI NA MGANGA WA KIENYEJI ULIYOYAZUIA MAONO YANGU TEKETEA,NAYATAKA LEO MAONO YANGU YA KUSOMA CHUO KIKUU,YALE MAONO YANGU YA TANGU UTOTONI MWANGU NAYATAKA LEO KWA JINA LA YESU.NINAFANYA VITA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO NA KILA MAMLAKA ZA GIZA ZILIZONICHUKULIA MAONO YANGU KWA DAMU YA YESU.KILA KITI CHA KISHETANI KILICHOSHIKILIA MAONO YANGU NA KUYAZUIA,LEO NAKIPASUA KWA JINA LA YESU.EWE MKUU WA BAHARI,ANGA,ARDHI ULIYE NA UNAYEMILIKI MAONO YANGU NAKULIPUA KWA MOTO WA ROHO MTAKATIFU.LEO MAONO YANGU YATIMIE KWA JINA LA YESU,MAONO YANGU YA HUDUMA YATIMIE,MAONO YANGU YA KUSOMA, YATIMIE,MAONO YANGU YAKUJENGA NYUMBA,NDOA,KUZAA,KUOA,KUOLEWA NK YATIMIE KWA JINA LA YESU.NASAMBAZA DAMU YA YESU IENDE KILA MADHABAHU ZA KISHETANI IKAHARIBU NGUVU ZAO KWA JINA LA YESU.NINAANGAMIZA KILA MIPANGO MIBAYA JUU YA MAONO YANGU KWA JINA LA YESU.NATEMBEZA MOTO KILA MAHALI PENYE MAONO YANGU YALIYOKAMATWA,KILA KUZIMU YOYOTE ILIYOKAMATA MAONO YANGU NALIPUA KWA JINA LA YESU.NAMSAMBALATISHA KILA MTAWALA WA MAONO YANGU ANAYE YAMILIKI KWA JINA LA YESU.AMEN

MUNGU AWABARIKI NINI NYOOTE

Wednesday, March 2, 2022

NDOA NA FAMILIA(KWA WATU WENYE MIAKA 18* TU)

 NDOA NA FAMILIA

Nini maana ya ndoa?

NDOA NI muunganiko Kati ya mwanaume na mwanamke kuishi pamoja Kama mume na mke muda wao wote wa maisha Yao(umri lazima uzingatiwe)

"Kwahiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe,nao watakuwa mwili mmoja".Mwanzo 2:24

Maana yake hapo,Yale majukumu uliyokuwa unayafanya kwa wazazi wako hayataendelea kwa asilimia zote Bali majukumu yote yatakuwa NI kwa mke wako na familia yako,mnaenda kuungana kimwili na huyo mke wako uliyemchagua.Kwa maana nyingine unaweza kusema NI kuwa na makazi yenu,kutiana Moto na kusaidiana,kujitegemea kwa mahitaji yenu ya KILA siku.Hiyo ndiyo maana ya utamwacha baba na mama yako

KWA MUJIBU WA SHERIA YA NDOA YA TANZANIA(Mwaka 1971 kifungu Cha 9)

KILA nchi inautaratibu wake kwenye masuala ya ndoa, lakini kwa MUJIBU wa sheria ya ndoa Tanzania inasema;

i.Wanandoa wawe wamekubariana pasipo kulazimishwa na mtu

ii.Ndoa NI ya mwanamke na mwanaume

iii.Ni ndoa ya kudumu maishani

"BWANA Mungu akasema si vema mtu HUYU awe peke yake,nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye". Mwanzo 2:18

Kwahiyo Mungu alimuumba mwanamke KUTOKA kwa mwanaume ili awe msaidizi wa mwanaume

"BWANA MUNGU akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala, Kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akaufunika nyama mahali make".Mwanzo 2:21

Hivyo mwanamke alitokana na mwanaume yaani mume anatakiwa amuone mke wake NI Kama NI moja ya sehemu yake ya MWILI (ubavu wake)

"Na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA MUNGU akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu".Mwanzo 2:22

KUPITIA ule ubavu wa mwanaume,Mungu akaamua Sasa aufanye kwa kuweka nyama ili aweze KUTOKA mtu ambaye NI mwanamke ambaye anafanana na Adamu kwa njinsi na jinsia tofauti

"Adamu akasema,Sasa hutu NI mfupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama yangu,Basi ataitwa mwanamke kwa maana ametwaliwa katika mwanaume".Mwanzo 2:23

Kumbe mke wako unatakuwa umuone Kama NI moja ya mifupa yako na nyama ya MWILI wako.Kama utamuona mke wako kwa namna hiyo hakika utampenda Sana na kumjari kwa thamani kubwa maana NI moja ya viungo vyako,mfano akilia,akiumia maana yake wewe hauwezi kunyamaza na kumpuuzia lazima utamuangalia Kama vile jicho lako likiingia mchanga huwezi kuliacha Bali utaliangalia.Ndivyo hivyo mke wako unatakuwa umuone hivyo

NDOA NI AGANO (Mkataba)

Tunapozungumzia agano tunamaanisha makubaliano ya wawili na NI lazima kuwepo na kiapo.Ndoa ilianzishwa na Mungu mwenyewe,tunaweza kusema NI Taasisi iliyoanzishwa pale kwenye bustani ya Edeni.Maana yake Kuna kanuni zake na sheria zake za kuenenda au kufuatwa.Biblia inasema ndoa na iheshimiwe na watu wote 

"NDOA na iheshimiwe na watu wote na makazi yawe Safi kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu".Waebrania 13:4 

I..Ndoa lazima iheshimiwe,maana yake mtu anapokuwa yupo NDANI ya ndoa NI heshima kwa watu wote,Basi na nyinyi wanandoa jiheshimuni

ii.Malazi yawe Safi,maana yake NDANI ya ndoa nyinyi wenyewe mnapaswa kuwa safi kwamba unamke wako,unamume wako huyo ndiye atakayemaliza hamu yako ya tendo la ndoa na siyo mwingine wa nje,kwenda kufanya uzinzi hapana,lazima tendo la ndoa lifanywe na wanandoa tu wenyewe wawili tu!!!

NDOA NI ZAWADI TOKA KWA MUNGU

MUNGU ametupa ZAWADI hii inabidi na sisi tuilinde,tuithamini,tuitunze,tuikubali,tuipende n.k.Haiwezekani upewe ZAWADI harafu uipuuze,hila Jambo linakuwa si la kiungwana hata kidogo.Basi tukitambua ndoa NI ZAWADI TOKA KWA MUNGU Basi tutaiheshimu

NDOA NI TAASISI TAKATIFU

KILA mwanandoa atimize wajibu wake,kupendana,mapenzi yawepo (msinyimane)kujitambua kwamba wewe NI mwanandoa,kuachana na ubinafsi,kuendelea kujifunza kuhusu masuala ya ndoa,mtendee mwenzako mambo mazuri,NI baraka ,NI umoja n.k 

MAMBO YA KUZINGATIA WEWE MWANANDOA 

Aliyeanzisha ndoa NI Mungu mwenyewe,kutaka kuoa au kuolewa NI wazo la Mungu kabisa,ndoa NI kuondoa upweke,ndoa NI furaha,mwanaume NI kichwa,mwanamke NI moyo-msiadizi,ndoa inahitaji muwe pamoja hata Kama mpo mbali lakini muwe pamoja kimawazo,ndoa lazima itunzwe 

FAMILIA NI NINI? 

Familia NI mahusiano ya undugu wa damu au usio wa damu,lakini Mimi hapa nazungumzia familia ya wanandoa katika maisha Yao,kwa maana wanaoanzisha familia hiyo na waliopo 

"Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wake Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke aliwaumba".Mwanzo 1:27 

Kwa mantiki hiyo Mungu ndiye yeye aliyemuunganisha mwanaume na mwanamke ili watengeneze familia Yao 

"Mungu akawabarikia,Mungu akawaambia zaeni mkaongezeke,mkaijaze nchi....".Mwanzo 1:28 

Kimsingi hapa Mungu alikuwa anawataka wakatengeneze familia kwa kuzaa WATOTO ili waijaze nchi.Ndiyo dhana yangu ya familia hapa.Nawewe ambaye hauna mtoto, ninaiamuru mamlaka za mbinguni zikupatie WATOTO katika jina la YESU Kristo,Seema Amina napokea 

FAMILIA INAHUSIKA NA VITU GANI? 

1.BABA NDIYE KICHWA CHA FAMILIA 

Maana yake,yeye ndiye msimamizi mkuu katika kutatua changamoto mbalimbali ZILIZOpo NDANI ya familia.Yeye ndiye kiongozi wa familia katika kuiendesha kwa kuwajibika kwake 

2.MAMA NDIYE MSAIDIZI(MOYO) WA FAMILIA 

Maana yake NI msaidizi wa baba(mume wake) kuhakikisha familia Yao ipo sehemu Fulani katika kuiongoza.Hivyo baba na mama ndio viongozi wa kuhakikisha familia inakaa vizuri 

3.WATOTO/MTOTO 

Katika familia WATOTO NI viongozi au NI watendaji wadogo katika familia ambao Hawa ndiyo kichocheo Cha wazazi kufanya bidii zote kuhakikisha wanakuwa nafuraha  pamoja na amani NDANI ya familia Yao 

4.NDUGU 

Hapa nazungumzia ndugu wa Aina yoyote awe baba,mama,Bibi,shangazi n.kwote hao NI ndugu,hivyo Kama mume na mke NI kuhakikisha familia yenu inakuwa salama 

5.MARAFIKI 

Hawa NI moja ya ndugu katika familia NI kutokana na namna mnavyoishi nao,hapa nazungumzia wafanyakazi wenzako,majirani n.k.Mume na mke mnapaswa kuenenda kwa akili si kila ushauri mnaopewa muufanyie kazi,hapana,kaaeni Kwanza utathimini na mchambue je,unafaa au laah! 

6.UPENDO

Upendo ndiyo kila kitu katika maisha ya ndoa na familia bila upendo hapo ndoa haipo itakuwa NI kivuli Cha ndoa,upendo ndiyo tunda la roho 

"Liking tunda la Roho NI upendo,furaha,amani,uvumilivu,utu wema,fadhili,uaminifu,upole,kiasi,juu ya mambo Kama hayo hakuna sheria".Wagalatia 5:22-23 

"Enyi waume wapendeni wake zenu Kama Kristo naye alivyolipenda kanisa,akajutoa kwa ajili yake".Waefeso 5:25,endelea kusoma mpaka mstari wa 33.Kumbe wanaume tunatakiwa kuwapenda wake ZETU,wanawake wao wanataka kupendwa 

7.UTII(KUTII) 

Katika familia utii ukiwepo Basi mambo yataenda vizuri Sana lakini si kila kitu utii tu hapana.Wanawake wao ni mnatakiwa kuwatii waume zenu,wanaume wao wanapenda utii KUTOKA kwa mke wake 

"Ninyi wake watiini waume zenu Kama ipendezavyo katika BWANA*Wakolosai 3:18 

"Ninyi WATOTO watiini wazazi wenu katika Mambo yote,maana Jambo hili lapendeza katika BWANA".Wakolosai 3:20 

"Ninyi watumwa watiini hao ambao kwa mwili NI bwana zenu.....".Wakolosai 3:22

KATIKA FAMILIA NYINGI UTAKUTA UTII HAUPO,WAKE HAWATII WAUME ZAO,WATOYO NAO HAWATII WAZAZI WAO,WATUMWA NAO HAWATII BWANA ZAO.FAMILIA IKIFIKIA KATIKA MAZINGIRA HAYA INAKUWA KATIKA HATARI KUVWA SANA YA SHETANI KUINGIA NA KULETA MAMBO YAKE.KUMBUKA SHETANI YUPO ANAZUNGUKA ZUNGUKA AKITAFUTA MTU AMMEZE,AMEZE NDOA.FAMILIA IKISHAINGIA KWENYE MIGOGORO HAPO KAMA MUME NA MKE HAWATAKUWA MAKINI KUJUA TATIZO NI NINI,FAMILIA INAWEZA IKAHARIBIKA KABISA 

BWANA YESU AKUSAIDIE KATIKA JINA LAKE LA THAMANI

Thursday, February 24, 2022

MIKATABA YA MOTO PART 2

 Baada ya kukirishwa maneno na kupokea kipigo ambacho hujawai pigwa,kumbuka Kuna MAJINA ya sehemu hiyo wao wameweka kinamba,Kuna namba 6,5,4,3,2 zote sehemu hizo unakula kipigo.Namba moja unapelekwa kunyooshwa then unapigwa usingizi mzito na kupelekwa namba 6 na kukurudisha nyumbani kwako na kutoa/kukutoa kumbukumbu zako yaani wanayachomoa matukio,ukiamka unasema nimeota ndoto za kutisha,Kama uliota ndoto za kutisha Tisha na hukumbuki, lengo la shetani NI usitafute msaada,unajisikia amani kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.Mambo ya Ki-Mungu huna habari nayo na unachoka,kuomba unashindwa kusoma Biblia usingizi mzito Sana hata mistari miwili umalizi yaani unachoka.Mfano ukaamua kuanza kumtafuta Mungu,yanatumwa mapepo na wanaacha kazi zao ili wakushughulikie na kuhakikisha unarudi au unakuwa upande wao.Mtu mwenye mkataba wa Moto akaombewa mfano kuacha ulevi,uzinzi,uasherati,wizi n.k anarudia Tena na Tena,hawezi kuacha atajitahidi siku mbili au wiki moja hata mwezi mtamkuta Tena anafanya yaleyale na yuko radhi kupewa Sala ya toba,ukikutana na mtu Kama huyo muombee kwa kuvunja mikataba ya Moto aliyounganishwa kwa kwa kujua au kutokujitambua

KWA MTU ALIYEOKOKA

Shetani atakuuliza unataka kumtumikia Yesu au shetani?ukisema nitamtumikia Yesu, unapelekwa kwa bwana Moto,atakupokea HUYU MWILI wake wore unawaka Moto au tuseme umejengwa kwa Moto,ukiingizwa huko anamchomoa mtu wako wa NDANI kwa kukupasua sehemu yako ya kifua na anamchomoa mtu wa NDANI na anaweka pepo NDANI yako na kukurudisha na hukumbuki unamkataba unakuwa na siku 7-10,KILA baada ya siku 7,8 ugonjwa unakusumbua,hapa wanakuwekea MWILI wa kuzimu kwa matarumbeta na unapelekwa zone namba 9.Hapa Kuna uzio wa kioo kwenda zone namba 10 yaani NI uwanda wa mateso.Sehemu hii ndiyo ya kwenda kwa Mungu au kwa shetani.Mpaka hapo utakuwa umenielewa,Cha kuongezeka je,utafanyaje Sasa mtu asiingie,asiingizwe huko maana watu wengi wameunganishwa bill was kujua au kutokujua,Sasa Cha kukusaidia omba Maombi haya

MAOMBI YA KUJITOA KWENYE MIKATABA YA MOTO

1.Omba msamaha mbele za Mungu,muambie akusamehe maovu yako yote

2.Wasamehe wore waliokukosea na uwaacholie,Biblia inasema msipo wasamehe watu makosa Yao hata Baba wa mbinguni hata wasamehe ninyi makosa yenu,achilieni nanyi mtaachiliwa

3.Jivue KILA MWILI wa kuzimu uliovishwa

4.Mkomboe mtu wako wa NDANI

5.Vunja mikataba yote ya Moto uliyounganishwa kwa kujua au kwa kutokujua

BWANA YESU awe pamoja nawe na akupe kibali Cha kuomba