AHADI ZA MUNGU KWETU.
Ahadi. Ninamna Fulani ya kusubilia au
kutarajia kile unachokihitaji , mfano, ninakuahidi ile fedha nitakupa wiki
ijayo. Kwa hiyo ahadi kwa namna nyingine ni kama kiapo, Hivyo tunafahamu Neno
la Mungu limehakikishwa na Mungu mwenyewe ni hai tena linanguvu, kuna umuhimu
wa kulitumia Neno la Mungu na ahadi zake wakati wa maombi Na Mungu huwa
analiangalia Neno lake ili alitimize.
Na wewe kama
mwombaji unatakiwa kuzijua na kuzitumia ahadi kwa kumkumbusha Mungu anachosema
katika Neno lake ili kusababisha mabadiliko mazuri yatokee katika ulimwengu wa
mwili kama tunavyoomba,
‘Unikumbushe na
tuhojiane eleza mambo yako, upate kupewa haki yako ‘Isaya 43;26.
AHADI ZA MUNGU JUU YETU.
Kuna ahadi za
Mungu juu yetu zaidi ya elfu thelasini na sita (36,000) Lakini zifuatazo hizi
ni baadhi tu.
i)Ahadi za Mungu kuhusu mamlaka aliyotupa sisi.
“Tazama nimewapa
amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za Yule adui” Luka 10;19
ii) Ahadi
za Mungu za kumshinda shetani na nguvu za giza
“Utawakanyaga
simba na nyoka, Mwana- simba na joka utawaseta kwa miguu “Zaburi 91;13
iii)Ahadi za Mungu kuhusu uponyaji wa magonjwa.
Ili litimie lile
neno lililonenwa na nabii Isaya akisema, mwenyewe alimtwaa udhaifu wetu, na
kuyachukua magonjwa yetu. ‘Mathayo 8;17.
i)
Ahadi za Mungu
kuhusu ulinzi na usalama
‘Bwana ndiye mlinzi wako ,Bwana ni uvuli ,mkono wako
wa kuume, Zaburi 91;5.
ii)
Ahadi za Mungu
kuhusu akili njema,
maarifa ‘Yafahamu sana hayo nisemayo kwa maana Bwana
atakupa akili katika mambo yote. 2timotheo 2;7.
iii)
Ahadi za Mungu kuhusu utajiri na mafanikio
Mpenzi naomba
ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile Roho yako
ifanikiwavyo 3Yohana 1;2
Kwa maana hakuna
tofauti ya myahudi, maana yeye Yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote
wamwitao,warumi 10;12.
iv)
Ahadi za Mungu
kuhusu watoto na familia,
‘Na watoto wako
wote watafundishwa na Bwana na amani ya watoto itakuwa nyingi, Isaya 54;13.
MAMLAKA YA KUTAWALA, KUTIISHA NA KUMILIKI.
Mamlaka ; Ni nguvu aliyonayo mtu kutokana na
(kuhusiana) na jambo Fulani.
‘Mungu akasema
na tumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura
yetu wakatawale samaki wa bahari na ndege wa angani na wanyama na nchi yote pia
na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano
wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanake aliwaumba. Mungu
akawabarikia, Mungu akawambia zaeni mkaongezeke, mkazazike, mkaijaze nchi na
kuitiisha, mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na kila kiumbe
chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mwanzo 1;26-28.
*Akawabariki.
Hapa Mungu
aliachilia nguvu ndani yao na juu yao ya kuzipata hizo Baraka,
*Zaeni
mkaongezeke,
Maana yake ndani
ya mtu Mungu ameweka mbegu za Baraka na za uzao.
Lengo la Mungu
kumuumba mtu ili aweze kutawala, kumiliki na kutiisha vyote ambavyo ni dhana ya
ufalme.
“Msiogope enyi kundi dogo kwa kuwa Baba yenu
ameona vema kuwapa ule ufalme”,Luka 12;32
Nami nawawekea
ninyi ufalme kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi, Luka 22;29.
Mfalme
anawatawala kwa kutumia neno / amri
‘Kwa kuwa neno
la mfalme lina nguvu naye ni nani awezaye kumwambia huyo, wafanya nini? Mhubiri
8;4.
‘Na mbarikiwe
ninyi na Bwana aliyezifanya mbingu na nchi, Zaburi 115;15-16
Na mfumo ambao
Mungu ameuweka wa mtu kumiliki juu ya nchi ni kwa njia ya ufalme na ukuhani.
Ukuhani; Unafanya kazi ya utakaso na toba ili
kuweza kuunganisha mbingu na nchi.
Na kutufanya
kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu naye ni Baba yake, utukufu na ukuu una yeye
hata milele na milele.Amina. Ufunuo 1;6.
Kila mahali
zitakapokanyaga nyayo zangu nimemiliki sasa mbona shida, taabu, matatizo,
mikosi,n.k, suala hapa unakanyagaje?Lazima ukanyage kikuhani na mkanyago wa
kifalme kwa kusema neno la Mungu juu ya mahali hapo ulipo (Ardhi)
‘Katika siku zile mimi Daniel nalikuwa
nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili” Daniel 10;2.
Fahamu ardhi ya
eneo linapomilikiwa na adui kunakuwa na kukatika kwa mawasiliano kati ya mbingu
na ardhi. Baraka za Mungu zinakuwa ngumu sana kukifikia kwasababu ya mkuu wa
anga (pepo) atakuwa anazuia kila jema kutoka mbinguni.
Kwahiyo wewe
lazima ujitambue kwamba wewe upo ndani ya ufalme wa Mungu. Na unapozungumzia
ufalme lazima mfalme awepo.
Ufalme. Ni mfumo wa utawala (ni serikali)
Mfalme. Ni mtawala aliyepata nguvu za utawala
kwa njia ya urithi au uwezo Fulani.
Na alipoulizwa
na mafarisayo Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia ufalme wa
Mungu hauji kwa kuuchunguza, wala hawakusema tazama upo huku au kule kwa
maana,tazama ufalme wa Mungu umo ndani yenu Luka 17;20-21
Yesu
akajibu ufalme wangu sio wa ulimwengu
huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangenipigania
nisije nikatiwa mikononi mwa wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa, Basi
pilato akamwambia, wewe u mfalme basi?
Yesu akajibu wewe wasema kuwa mimi ni mfalme ,mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya
na kwa ajili ya haya mimi nakuja ulimwenguni ili nishuhudie kweli. kila aliye
wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu, Yohana 18;36-37.
Unapouzungumzia
ufalme unazungumzia,
*mamlaka
*uwezo
*kumiliki
*kutiisha
*utawala
MUUNGANIKO WA MTU NA MBINGUNI.
Baada ya kuokoka, kutubu dhambi zako. Sasa Mungu amekuunganisha
kwenye ufalme wake na una haki zote za msingi kuzungumza na Mungu au kumdai,
ahadi zake kwako.
Muunganiko, Ni uhusiano uliopo kati ya mmoja na mwingine
au ni muunganiko wa mtu na kitu au vitu.
Mbinguni, Ni makao makuu ya Mungu na malaika
zake watakatifu, maana yake hapa tunazungumzia
a)Mungu Baba.
b)Mungu Mwana.
c)Mungu Roho Mtakatifu
d)Malaika wake
(malaika wa Mungu).
“Baada ya hayo
naliona na tazama mlango ukafunguka mbinguni na sauti ile ya kwanza ukafunguka
kama sauti ya baragumu ikinena nami ikisema panda hata huku nami nitakuonyesha mambo magumu
ambayo huyana budi kuwako baada ya hayo. Na mara nalikuwa katika Roho na tazama kiti cha enzi kimewekwa
mbinguni na mmoja ameketi juu ya jiwe la yaspi na akiki na upande wa mvua
ulikizunguka kile kiti cha enzi ukionekana mithili ya Zumaridi. Ufunuo 4;1-11.
Ukiendelea
kusoma mpaka mstari wa kumi na moja uatona kuna wazee ishirini na wanne, kiti
cha enzi, taa saba za moto. (Roho saba za Mungu)
1.
Kiti
cha enzi; Hiki ni kiti cha Mungu Baba aliyeziumba mbingu na nchi.
2.
Wazee
ishirini na nne, Hawa ni viongozi wa kiroho kanisani.
3.
Taa
saba za moto (Roho saba za Mungu)
*Roho ya ushauri
*Uweza
*Kumcha Bwana
*Maarifa
*Hekima
*Ufahamu
*Kuonya
4. Wenye uhai wanne
a). Mfano
wa simba; maana yake ni roho ya
mapambano
b)Mfano wa ndama; maana yake ni roho ya
utayari kwenye kazi ya Mungu
c)mfano wa mwanadamu; maana yake ni roho ya upole na huruma.
d) Mfano wa tai arukae; maana yake ni
macho ya kinabii (kuona mbali) (prophetic eyes)
5. Maneno (sauti)
*mtakatifu,
mtakatifu, mtakatifu Bwana Mungu mwenyezi.
*Umestahili wewe
bwana wetu na Mungu wetu.
*Kuupokea utukukufu
na heshima na uweza.
*Wewe ndiwe
uliyeviumba vitu vyote,
*Kwa sababu ya
mapenzi yako vilikuwako navyo vikaumbwa.
6. Matendo
waliyokuwa wanayafanya.
*Wanatoa utukufu
na heshima na shukrani
*Walikuwa
wakipiga magoti.
*Wakimsujudia
yeye aliye hai.
Kwa hiyo
tunakuwa tumeunganishwa au tunamuunganiko na mbinguni.
“Hata petro
alipopata fahamu akasema, sasa nimejua ya kini ya kuwa Bwana amempeleka malaika
wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la
wayahudi. Matendo 12;11.
Vilevile sisi tuliookoka na kumtumainia Mungu
tunapaswa kuelewa ziara za malaika kwamba wanapanda na kushuka wakati gani.
Akaota ndoto na
tazama ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni na kushika
juu yake, Mwanzo 28;12.
Tunaona Yakobo alikuwa amelala usingizi akaota
ndoto hiyo na hapo jua lilikuwa limezama (sura ya 28;11). Hivyo basi kumbe
tunapoomba usiku ndiyo ratiba za malaika wanakuwa wanapanda na kushuka, kwa
ajili ya kuchukua maombi yetu na kuyapeleka mbinguni kwa Baba, (sio kwamba
mchana hawapo , wapo pia.)
Sisi ni watoto
wa Yesu Kristo na tunahitaji nguvu za Yesu zijizihirishe kwetu kwa kumshinda
shetani na malaika zake tunapaswa kuomba usiku wa manane. Kanisa letu la Tanzania Power of Jesus Christ, tunatakiwa tuwe na
nguvu za Rohoni. Kwasababu mchana tunashughuli nyingi ni vema tukautumia muda
huo wa usiku kuanzia saa 6 na saa 11 alfajiri hapo utazipata nguvu za Yesu Kristo,
Halelluya!!.
BARAKA ZA TOKA ULIMWENGU WA ROHO.
Baraka; Ni mafanikio ya mtu aliyonayo kiroho
au kimwili. Lakini kwenye ulimwengu wa roho wa Mungu Baba, Baraka zipo nyingi
sana ila tunashindwa kuzitoa huko na kuja kwetu kwenye ulimwengu wa mwili,
kwahiyo Baraka zozote iwe ni fedha, huduma, mashamba, magari, nyumba,
chakula, kazi, ndoa, biashara, elimu,
watoto n.k zote hizo zipo kwenye ulimwengu wa roho.
“Atukuzwe Mungu
Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni katika
ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo. Waefeso 1;3.
Mfano; Unataka kupata Picha au sauti (taarifa ya
habari) lazima uwe na vitu vifuatavyo.
a) Tv (runinga)
Maana yake hapa,
unatakiwa uwe na Yesu ndani ya moyo wako (umeokoka)
b) King’amuzi.
Hapa hitaji lako
ni nini kwa Mungu Baba unalolihitaji, je
ni fedha, kazi, ndoa n.k.
c) Umeme
Hapa unatakiwa
kuwa na nguvu za Roho Mtakatifu.
d) Muunganiko (connection)
Hapa unahitajika
kuwa na Neno la Mungu ndani yako.
e) Sigino (signal)
Hapa unatakuwa
upate sehemu sahihi ya kumuabudu Mungu Baba ili baraka zako uzione na kuzipata.
f) Remote.
Hapa ni Yule anayekuongoza
(baba yako wa kiroho) anatakiwa kuwa na nguvu za kiroho ili atakapokubariki
baraka ikufuate na sio kukutamkia laana.
Mungu yeye siku
zote anatenda mambo ya ajabu mno kuliko yote,
*Tuyaombayo
*Tuyawazayo
*kwa kadri ya
nguvu itendayo kazi ndani yetu (yako).
“Basi atukuzwe
yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo
kwa kadri ya nguvu itengayo kazi ndani yetu .Waefeso 3;20.
BIBLIA INAFUNDISHA.
1. Ufalme wa Mungu.
Naye alituokoa
katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa
pendo lake, ambaye katika yeye tunaukombozi yaani masamaha wa dhambi, Wakolosai
1;73.
2. Katiba ya ufalme wa Mungu.
Hata alipokitwaa
kile kitabu, hao wenye uhai wane na wale wazee ishirini na wane wakaanguka
mbele za mwana – kondoo, kila mmoja wao anaa kinubi na vitasa vya dhahabu
vilivyojaa manukato ambayo ni maombi ya watakatifu, Ufunuo 5;8.
3. Sheria ya ufalme
Mwanangu
usiisahau sheria yangu, bali moyo wako uzishike amri zangu. Maana zitakuongezea
wingi wa siku. Na miaka ya uzima na amani , Mithali 3;1-2
4. Uchumi wa ufalme wa Mungu.
Nchi na vyote
vilivyomo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake, Zaburi 24;1.
Fedha ni mali
yangu na dhahabu ni mali yangu, asema Bwanawa majeshi, Hagai 1;8,
5. Familia ya ufalme wa Mungu.
Mwili mmoja na
Roho moja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja ,
imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja naye Baba wa wote aliye juu ya yote na
katika yote na ndani ya yote “waefeso 4;4-6.
Nami nikaanguka
mbele ya miguu yake ili nimsujudie akaniambia angalia usifanye hivi mimi ni
mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushindi wa Yesu, Msujudie Mungu kwa maana
ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii,
Ufunuo 19;10,
6. Jeshi la ufalme wa Mungu
Yakobo akashika
njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye, Naye Yakobo alipowaona alisema,
Hili ni jeshi la Mungu, Akapaita mahali pale mahanaimu, Mwanzo 32;1-2
KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO.
Kusudi; Ni wazo au lengo lililowekwa ndani ya
moyo wako ili liweze kutimiza lile ambalo Mungu ameweka katika maisha yako,
watu wengi wamekuwa wakiishi katika maisha yao bila kujua kusudi alilonalo watu
wanishi maisha feki
Atendaye dhambi
ni wa ibilisi, kwa kuwa ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili mwana
wa Mungu alidhihirisha ili azivunje kazi za ibilisi, 1Yohana 3;8.
Angalieni
nitawapeleka Eliya nabii , kabla haijaja
siku ile ya Bwana iliyokuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao na mioyo ya
watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana, Malaki 4;5-6.
Kabla sijakuumba
katika tumbo nalikukujua na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa, nimekuweka
kuwa nabii wa mataifa “Yeremia 4;1.
=Kabla sijakuumba nalikujua.
Maana yake Mungu
anajaribu kumwambia Yeremia kwamba natambua kabisa nilichokuwa nafanya pindi
nilipokuumba.
=Nimekuweka juu
ya mataifa na juu ya mfalme.
Maana yake
kumuumba kwa kusudi lake ndani yake,
*kuwa nabii wa
mataifa
*kuwa juu ya
mataifa
*kuwa juu ya
falme.
=Akampa na kazi
ya kufanya.
*kung’oa
*kubomoa
*kuangamiza
*kuharibu
*kujenga na
kupanda
Angalia
nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa na kubomoa na
kuharibu na kuangamiza, ili kujenga na kupanda, Yeremia 1;10.
Kuwepo kwako leo ni kwaajili ya kusudi la
Mungu ndani yako. Ndani ya kusudi lako upo uwezo na mamlaka ya kuamuru na kubadilisha
mazingira pinzani juu yako utakutana na falme na ngome za maadui, vita, mapepo,
wachawi, utapambana navyo.
JINSI YA KUTAMBUA KUSUDI LAKO
Kutambua kusudi
ulilo nalo ni kazi sana
Mfano: mtu
anafanya biashara hii au anafanya kazi ile au anajaribu kufuga kuku, kulima
lakini mtu anaona bado kuna kitu kinadaiwa anataka akifanye.
a.
Mungu
kukuonyesha katika ndoto na maono kimsingi Mungu ndiye anayeweza kukuonyesha
au kusema na wewe, kwamba wewe nani? Kwa njia ya ndoto na maono.
“kwa
kuwa Mungu hunena mara moja naam hata mara ya pili ajapokuwa mtu hajali katika ndoto,
katika maono ya usiku, usingizi mzito uwajiliapo watu katika usingizi kitandani.
Ndipo huyatumia maskio ya watu na kuyatia mihuri mafundisho yao”. Ayubu
“Yusufu akaota ndoto akawapa ndugu zake
habari nao wakazidi kumchukia, akawambia tafadhali sikieni ndoto hii niliyoita tazama sisi tulikuwa tukifunga miganda
shambani kumbe mgawawangu ukaondoka ukasimama na tazama miganda yenu ikazunguka
ikainama mbele ya mganda wangu. Ndugu zake wakamwambia je kweli wewe
utatumiliki sisi nawe utatutawala sisi------------“. Mwanzo 37;5-8
“Akaota
tena ndoto nyingine akawambia ndugu zake, akasema angalieni nimeota ndoto
nyingine na tazama jua na mwezi na nyota kumi na moja zinaniinamia. Akamwambia
baba yake na ndugu zake baba yake akamkemea akamwambia, ni ndoto gani hii
uliyoita? Je mimi na mama yakona ndugu
zakotutakuja tukusujudie hata nchi?”. Mwanzo
37:9-10
b.
Kiwango chako
cha imani kiendane na kusudi lako
(kuwa na imani nachokwa kile unachoelewa) ili uweze kujua upo ndani ya kusudi
lako amani ndani ya moyo wako itakuwepo utapenda kulifafanya bilakujali
mazingira yakoje. Mfano lipo jambo umewahi lifanya na tayari umekwisha
kulifanya na ukasikia amani ndani ya moyo wako hata kama ni dogo tambua kuwa
hilo ndilo kusudi la Mungu kwao.
“ Yusufu akamwambia Farao ndoto ya Farao ni moja. Mungu
amemwonyesha Farao atakayo yafanya hivi karibu”. Mwanzo 41:25
c.
Kupitia kwa
watumishi wa Mungu na watu wengine
“Ndipo samweli akaatwa pembe yenyemafuta
akamtia mafuta kati ya ndugu zake na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu taku siku ile---------“ 1Samweli 16:13
d.
Jinsi vile
unavyo onekana mbele za watu
“Akamwona Petro akikota moto akamkazia
macho akasema wewe nawe ulikuepo pamoja na Yule Mnazalet Yesu”. Marko 14:67
e.
Mungu kusema na
wewe waziwazi (malaika wa Mungu
kukutokea)
“haya basi nitakutuma kwa Farao ili
upate kuwatoa watu wangu hao wana wa Israeli katika Misri”. Kutoka 3:10
“ Malaika wa BWANA akamtokea katika mwali wa roho uliotoka katikati ya kile
kijiti akatazama na kumbe kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea”. Kutoka 3:2