Friday, February 4, 2022

KUOKOKA KWA MTU KUNA MAANA SANA

 BAADA YA KUOKOKA

 

KUOKOKA-:

Ni kitendo cha kutubu dhambi zako mbele ya Mungu na wanadamu. Kwa kukiri kwa kinywa chako mwenyewe kwamba umeacha dhambi zako na hautozirudia tena   “namkataa shetani na mambo yake yote”. Kwahiyo tunapo okoka miili yetu  inabaki vilevile lakini roho zetu zinakuwa mpya kwa kutakaswa na Damu ya Yesu Kristo.

Kama vile Mungu Baba alivyo tangulia kuwajua katika kutakaswa na roho hata mkapata kutii na kunyunyizwa Damu ya Yesu kristo. Neema na amani na ziongozwe kwenu” 1petro1:2

 

Kuokoka: Ni mpango wa Mungu kwa wanadamu katika kuishinda dhambi.au ni kitendo cha kumkiri  Yesu kwa kinywa chako na kuamini moyoni mwako kuwa ni Bwana na mwokozi wako.

Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana na kuamini moyoni  mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka  kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”. Warumi 10:9-10

 

Tunapokuwa tumeokoka tunakuwa tumezaliwa mara ya pili kiroho yaani mambo ya kale tunayaacha .

Yesu akajibu akamwambia amini amini nakwambia mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuona ufalme wa Mungu”.  Yohana 3:3

 

Ahimidiwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa rehema zake nyingialituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu katika wafu tupate na urithi  usioharibika usio na uchafu, usionyauka uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu”1petro 1:3-4

Hivyo basi baada ya kuokoka tunapata uzima wa milele ambao Yesu Kristo ametuandalia huko mbinguni, na tunakuwa tunalindwa na nguvu za Mungu hapa duniani kwa njia ya imani.

Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu uliotayari kufunuliwa wakati wa mwisho “1Petro 1:5

 

WOKOVU

Wokovu ni mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu alie potea kupitia dini, Roho Mtakatifu na watumishi wake. Kwahiyo njia ya wokovu ni Yesu Kristo

“Yesu akamwambi mimi ni njia ya kweli na uzima mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi” Yohana 14:6.

Wokovu tulio nao ni wa muhimu sana tunatakiwa kuulinda kwa nguvu zetu zote maana ni kwa ajili ya roho zetu, inapaswa  tumpende Yesu hata kama hatumuoni kimwili lakini kiroho yupo pamoja na sisi.

Naye mwampenda ijapokuwa hamkuomwona ambaye ijapokuwa hamwoni sasa mnamwini na kufurahi sana kwa furaha isiyoneneka yenye utukufu katika kuupokea mwisho wa imani yenu yaani wokovu wa roho zenu”1Petro 1:8-9.

 

Tunapokuwa  ndani ya wokovu hatutakiwi tena kujifananisha na tamaa zetu za kwanza za ujinga. Tunapaswa kuyashika na kuyatii yale anayotaka Yesu Kristo ndiyo tuishi nayo.

Kama watoto wakutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu bali kama yeye alie waita alivyo mtakatifu ninyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote, kwa maana imeandikwa mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu “1Petro:14-16

 

Tuliokolewa si kwa vitu viharibikavyo, Yesu Kristo alikufa kwa ajili yetu kwa aibu ili sisi tupate thamani kubwa ya maisha yetu ya sasa na yabaadaye, maana alitutoa kwenye mwenendo usiofaa.

Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo kwa fedha au dhahabu mpate kufika katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu bali kwa damu ya thamani kama ya mwanakondoo asiye na ila,asiye na waa yaani ya Kristo “1Petro 1:18-19

Tunapo okoka tunapaswa kuwa vielelezo kwa watu wengine (yaani ndugu,marafiki,majirani na jamii kwa ujumla ). Kama tukiwa na matendo mazuri mbele za watu,  hata wewe mwenyewe binafsi, hapo Mungu anatukuzwa kupitia wewe ulieokoka, wewe ni alama ya Yesu Kristo hapa duniani.

 

Wapenzi nawasihi kama wapitaji na wasafiri ziepukeni tamaa za mwili zipinganazo na roho mwe na mwenendo mzuri kati ya mataifa ili iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya wayatazamapo matendo yenu mazuri wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa “1Petro 2:11-12 hata nabii Isaya anasisitiza hilo.

“Jiosheni jitakaseni ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu, acheni kutenda mabaya” Isaya 1:16

Mungu siku zote anatuwazia mema na hataki mtu yeyote apotee kwenye Jehanamu ya moto, yeye ni mwenye huruma anataka tusogee mbele zake na tusemezane naye kuhusu dhambi zetu tulizo zitenda kwa kujua au kwakuto kujua tunazozifahamu na tusizozifahamu anatutaka tuwe watii kwenye kutubu dhambi zetu.

 

“Haya njooni tusezane asema BWANA, dhambi zenu zipojapokuwa nyekundu sana zitakuwa nyeupe kama theluji, zijapokuwa nyekundu kama bendera zinakuwa nyeupe kama sufu kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi, bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga, maana kinywa cha BWANA kimenena haya” Isaya 1;18-20

Tunapo tubu dhambi zetu mbele za Mungu kwanza anatusamehe maovu yetu, pili anatuponya  magonjwa yetu, tatu anatukomboa uhai wetu na kaburi, nne anatuvika taji ya fadhili na rehema, tano aushihisha mema uzee wako na sita aurejesha ujana wako.


 

“Akusamehe maovu yako yote,akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kabuli akutia taji ya fadhili na rehema, aushibisha mema uzee wako, ujana wako ukarejezwa kama tai “Zaburi 103:3-5.

 

Hapo Mungu alikuwa na maana hii;

a)     Akusamehe maovu  yako yote

Kabla ya kuokoka ulikuwa unaishi maisha ya dhambi, ambayo yalikuwa hayampendezi Yesu anakuwa amekusamehe yale maovu yako yote uliyokuwa unayatenda, hivyo unakuwa mpya mbele za Mungu.

b)    Akuponya magonjwa yako yote.

Mungu akisha kusamehe anaanza kushugulika na afya yako maana umefungua moyo wako kwake, na kama ulikuwa na magonjwa ataanza kukuponya.

c)     Aukomboa uhai wako na kaburi.

Kama ulitakiwa kufa basi hapo Mungu anakomboa uhai wako, kutoka kwenye mauti na kukuingiza uzimani tena.

d)    Akutia taji ya fadhili na rehema.

Hapa Yesu Kristo anakuangalia upya tena kwa huruma zake na kukuhurumia.

e)     Aushibishe mema uzee wako.

Mungu  kwa vile yeye ni mwema na mwaminifu uzee wako anaushibisha mema (yaani anakupa mambo mazuri wakati wa uzee wako)


 

f)      Ujana wako ukarejezwa kama tai.

Yale mambo uliotakiwa yakupate mazuri wakati wa ujana wako na sasa yamepotea huna tena zile Baraka za ujana, Yesu Kristo anakwenda kukurejeshea tena kwa nguvu ya ukombozi kwa jina la Yesu halelujaah.

Yesu Kristo akishakusamehe dhambi zako hazikumbuki tena na anaziweka mbali nasi

Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyoziweka mbali dhambi zetu mbali nasi” Zaburi 103:12

“Mimi naam mimi ndimi nifutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe wala sitazikumbuka dhambi zako” Isaya 43:25

“Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito na dhambi zako kama wingu unirudie maana nimekukomboa “ Isaya44:22

 

ALIZICHUKUA DHAMBI ZETU

Yesu Kristo alikuja hapa duniani kwa ajili ya kuja kuchukua maovu yetu ili atengeneze upatanishi kati ya wanadamu na Mungu Baba.

Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi tuwe hai kwa mambo ya haki na kwa kupigwa kwake mliponywakwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo lakini sa mmerudia mchungaji na mwangalizi wa roho zenu. 1Petro 2:24-25.

 

Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu sababu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”. Isaya 53:5.

Yesu Kristo alijeruhiwa kwa ajili ya makosa yetu , maovu na adhabu zetu alizibeba yeye mwenyewe ili sisi tupone, ni jambo la thamani mno alilolifanya Yesu Kristo kwetu ili sisi tupone .

 

Yesu kristo alipigwa, alitemewa mate ili mimi na wewe tupone.

“Wengine wakaanza kumtemea mate wakamfunika uso na kumpiga mkonde na kumwambia tabiri hata watumishi nao wakampiga makofi.”Marko 14:65.

Yesu Kristo alivishwa taji la miiba kichwani.

Wakamvika vazi la rangi ya zambarau wakasokota taji ya miiba wakamtia kichwani.” Marko 15:17.

Yote hayo aliyavumilia ili watu waokolewe  kutoka kwenye dhambi.

 

Yesu Kristo alivuliwa nguo kwa ajili yetu.

        “wakavua nguo wakamvika vazi jekundu

          Mathayo    27:28.

Yesu Kristo alidhihakiwa kwa ajili yetu .

walipokwisha kumthihaki wakalivua lile vazi wakamvika mavazi yake wakamchukua kumsulubisha.” Mathayo 27:31


Walipokwisha kumthihaki waligawa mavazi yake wakapiga kura ili litimie neno lililo nenwa na nabii waligawa nguo zangu kati yao na juu ya vazi langu walipiga kura” Mathayo 27:35

Yesu Kristo alipewa nyongo kwa ajili yetu.

“Wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa.”

 

Mathayo 27:34 “mara mmoja wao                                                                                                                                                                                                                                                                akaenda mbio akatoa sifongo akaijaza siki akaitia juu ya mwanzi akamnywesha”   Mathayo 27:48.

 

Yesu Kristo alichomwa mkuki ubavuni kwa ajili yetu.

 

lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki na mara ikatoka damu na maji” Yohana 19:3, damu na maji yaliyokuwa yakitoka ubavuni mwake, moja moyo wake ulikuwa umepasuka kwa sababu ya mkuki huo.

Hivyo Yesu Kristo aliteswa katika mwili wake na mateso yote aliofanyiwa ili sisi tuokolewe na dhambi ya moto tuliotakiwa, tuliostahili lakini yeye  “aliyachukua maovu yetu” Kama yeye alifanya hivyo kwa ajili yetu basi nasi hatuna budi tuendelee kumtumkia yeye na kuziacha tamaa mbaya za dunia hii kama wafanyavyo mataifa, maadamu tumemkiri yeye tundelee kuwa naye siku zote za maisha yetu.

  

“Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ileile kwa maana yeye aliyeteswa  katika mwili ameachana na dhambi. Tangu sasa msiendelee kuishi katika tama  za mwanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu wakati wetu wa kuaa hapa dunian. Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya mataifa kuenenda katika ufisadi na tama na ulevi na karamu za ulafi na vileo na idadi ya sanamu isiyo halali. Mambo ambayo wao huna kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi uleule usio na kiasi, 

KURUDISHA KILICHOIBIWA KIROHO

 KURUDISHA KILICHOIBIWA KIROHO

Kurudisha:Ni hali ya kurejesha kile ulichopoteza,inawezekana ulipoteza mwenyewe au mtu Fulani alikuchukulia au kukuibia na wewe haunacho tena.

Kimsingi Baraka zote zinaanzia katika ulimwengu war oho.Shetani anachokifanya ni kukuibia. Mungu anakuwa ameachilia Baraka zake kwako lakini yupo anayejitokeza anakuibia.

Isaya 42:6-7

Isaya 26:19

Isaya 42:22

 

ULICHOBEBA NDIYO VITA YAKO

Kuna watu wanafikiri kwasababu ya wazazi wao hawapo,hawana fedha,hawajasoma,hana mtaji,wagonjwa n.k ,hayo yote siyo ni kwasababu ya ulichokibeba ndani yako kutoka Mbinguni

Yeremia 1:4-

-Aliye gizani anaona sana kuliko wa nuruni mfano mama jusi Mathayo sura ya 2

Matendo 9:1-, Matendo 13:9,Zaburi 51:5

-Shetani anaangalia baadhi ya watu muhimu ili awatende mabaya

-Kuna matukio yanakupata wewe,simama nauseme sio hili mfano:Abrahamu,Yakobo aliwaita watoto wake

Gadi:Akamwambia jeshi litamsonga ila yeye atawasonga mpaka visigino Mwanzo 49:19 ,kuna watu wanasongwa kila mahali mfano:kwenye biashara,ndoa,kazini n.k.Yakobo aliona kwenye familia miaka ijayo atatokea mmoja atasongwa na jeshi lakini atalikanyaga mpaka visiginoni

Sifa za Wagadi

-Mashujaa

-Nyuso zao kama samba

-Walikuwa na uwezo wa kupigana vita

-Wepesi milimani

-Walikuwa viongozi wa jeshi

-Aliyekuwa mdogo analingana na watu 100

-Aliyekuwa mkuu (mkubwa) analingana na watu 1000

1Nyakati 12:8-

Shetani anakuona wewe ni mwepesi wa kufanikiwa,ukiachiwa upenyo tu umefanikiwa,ndiyo maana wanasema wakudhibiti na kukusonga lakini saa imefika uwasonge wao mpaka kisigino kwa jina la Yesu.Wana wa Gadi walimiliki ufalme wa Sihoni na familia ya Bashani,Wanefili na mali zao

 

KUWAFYEKA WATAABISHAJI WETU

Mtaabishaji:Ni mtu au mashetani yanayomzuia mtu asifanikiwe kimaisha.

1Wafalme 18:17

Zimri (Jemedari wa magari) alifanya fitina kwa mfalme (alimpiga),alitawala siku 7(Tirza).Wakaamua Omri Jemedari wajeshi awe mfalme.Alinusuru mji wa Tirza,kukatokea mabishano kati ya Tibni na Omri (alishinda)

Roho ya Yeroboamu alikuwa nayo.Omri alitawala miaka 12 Israel na miaka 6 Tirza alifanya mabaya akafa,akatawala Ahabu miaka 22 akafanya mabaya naye.

 

KUWAANGAMIZA MAKUHANI WA KISHETANI

Makuhani:Ni viongozi wanaotumika kwenye madhabahu.

Aina za Makuhani

a.Makuhani wa Mungu waefeso 4:11

b.Makuhani wa kishetani Torati 18:10-13 ,Isaya 47:12-15

Tunashindana na binadamu anayetumiwa na mashetani kuharibu maisha yetu

1Wafalme 18:15-40,19:15-27

Wachawi wameloga sana nchi mpaka imegawanyika.Eliya alimfunga lufifa,mashetani ,miungu ,majoka n.k

2Wafalme 10:18-27

 

MPAKA ILIYOHAMISHWA

Mpaka:Ni alama zinazoonesha eneo la umiliki wa mtu katika ardhi,anga,kwenye maji n.k au ni sehemu,mahali panapoonesha mwisho wa umiliki halali wa mtu.Kuna michoro yake na ramani zake,kuna mipaka ya wilaya,mkoa,nchi n.k.

Mungu baada ya kumuumba mwanadamualimuwekea mipaka yake ya utawala,kutiisha,kumiliki nchi,bahari na anga.Inawezekana kabla ya kuokoka ulikuwa baa mipaka yako ikaamishwa,wachawi wanaweza kuhamisha mipaka ya mtu mfano:kwenye biashara,afya,ndoa,kazi,elimu,fedha,mafanikio n.k Luka 4:1

Unaona hapa shetani hasemi kuwa vyote ni vyangu bali anasema vipo mikononi mwangu.akimaanisha vile alivyonavyo shetani alivipokonya kwa mmiliki wake (mwanadamu).Shetani ndivyo alivyohamisha mipaka.Endapi Mungu alikusudia wewe uishi miaka 120 wachawi hupenda kuipunguza ili usifike umri huo au kuwa waziri,mbuge ukiwa na miaka 40 ukikalibia wanafanya uganga  uugue ukose sauti ya kufanya kampeni au uwe Rais,mkurugenzi,daktari,mchungaji n.k lakini ukianza masomo ya kukufikisha huko unashindwa.

Mithali 23:10,Torati 27:17,Hesabu 5:10

Bwana Yesu anaweza kubadilisha tena Kutoka 34:24,Torati 11:24-25

Bwana Yesu anakwenda kuipanua mipaka yako iliyopindishwa kwa jina la Yesu

 

KUVUNJA ROHO YA  UMASIKINI

Umasikini:Ni hali ya kukosa mahitaji muhimu mfano chakula,maradhi,nguo.

Masikini:Ni mtu anayekosa mahitaji muhimu

Kuna umasikini ngazi ya Taifa na umasikini ngazi ya mtu binafsi

Mhubiri 9:14-16,10:19

Shetani anatumia kifungo hiki kuwafunga watu wa Mungu Ufunuo 2:8-9,Mathayo 6:24,Wafilipi 4:19

 

KUIKOMBOA MIGUU YANGU

Uumbaji wa Mungu,Mtu ni roho.Mtu anasehemu 3 .Shetani naye anawinda sana maeneo hayo

+ Ardhi kwa ajili ya kuujenga ufalme wa Mungu

+ Masikio kwa ajili ya kusikia. Zaburi 103:20

+ Miguu ni milango ya nafsi,ni ishara ya kumiliki eneo,ni kama silaha ya vita

Mithali 6:18,Luka 10:19,Torati 11:24-25,Zaburi 56:6,Ayubu 33:11,Zaburi 57:6

 

NIMEYASIKIA MAOMBI YAKO

Maombi:Ni mawasiliano kati ya mtu na Mungu kuhusiana na jambo Fulani ili ulipate.

Kiroho:Ni mawasiliano kati ya mtu na Mungu kuhusiana na jambo Fulani ili ulipate

2Wafalme 20:5-11, Matendo 10:30-31

 

ROHO YA UPATANISHI

Kupatanisha:Ni kitendo cha kuondoa migongano kati ya pande majo na pande nyingine Mathayo 5:9

Baada ya kufa Yoshua waamuzi waliojitokeza:Yuda,Othniel,Elihudi,Debora,Gideoni,Tola Yairi,Yeftha,Samson,Yesu

 

NGUVU YA NDOTO

Ndoto:Ni picha au matukio yanayotokea kwenye akili yako baada ya kulala Mfano:nimeota ndoto nimenunua gari,ni tumaini/wazo unalokuwa nalo la maisha yako mazuri ya baadae

Aina za ndoto

-Za KiMungu

-Za kishetani

-Za kawaida

Ndoto ina nguvu-nguvu yake ni pale inapotokea kwake.taarifa,maelekezo n.k

Ayubu 33:14,Habakuki 2:2-3

Mfano Yusufu ndoto zake zilitimia.soma Mwanzo sura ya 37

 

KIFUNGO CHA TANGU UTUTUNI

Kifungo:Ni gereza analofungiwa mtu au kitu kwa sababu za kweli au za uongo

Mhubiri 4:14

Marko 9:17-29

-mtoto wake anapepo bubu

-anampagawisha

-humbwaga chini

-hutuka povu

-kukonda

Walipompeleka kwa Yesu mambo  yakatokea

-alipomuona Yesu Yule pepo alimtia kifafa

-akaanguka chini

-akatokwa na povu

Yesu akamuuliza baba yake,amepatwa na haya tangu lini?

-tangu utoto

-mara nyingi amemtupa katika moto,katika maji

-amwangamize

 

AMEFUNGWA KWENYE MTI

Mti ulitumika kwenye Biblia kama sehemu ya mwisho ya hukumu kwa mtu.Mtu akifungwa kwenye mti baada ya hapo ni kifo,wachawi wanaweza kuutumia mti kama gereza kuyafunga maisha ya mtu au mafanikia ya mtu Yoshua 8:28-29,Esta 7:8-10,2:23,Daniel 4:13-14,Mathayo 27:38-40

 

KUONDOA VIZUIZI VYA KISHETANI

Vizuizi:Ni vikwazo

Adui wa maisha ya kila mtu ni shetani.shetani ni roho hutenda kazi kupitia mawakala wake ambao ni wachawi,wasoma nyota,waganga wa kienyeji n.k wanauwezo wa kukuua kwenye masomo,elimu,ndoa,kazi,biashara,fedha,maendeleo n.k

1Thesalonike 2:18,Mathayo 8:23-28,Daniel 10:11-14

 

KUTENGENEZA NJIA KATIKATI YA GIZA

Giza:Ni jambo Fulani lisilokuwa na nuru au lisilo la nuru

Mwanzo 1:1-5,Yohana 1:1-5,Isaya 9:2,Yohana 8:12,Luka 1:79

 

MWEZI HUU NAPATA NEEMA YA MUNGU

Neema:Ni upendeleo ambao mtu hakustahili kuupata

Luka 1:26

 

HATA SASA BWANA AMETUSAIDIA

Kusidia:Ni kitendo cha kutoa msaada vile usivyokuwa navyo kuhusiana na jambo Fulani

1Samwel 7:12-14, Mathayo 7:1-,Mathayo 28:1

 


UWEZA WA MAOMBI,

 UWEZA WA MAOMBI,

Uweza; Maana yake ni nguvu

Maombi; Maana yake ni mawasiliano au kuzungumza na Mungu.

-Ni mamlaka ya Mungu inayotenda kazi katika ulimwengu wa roho.

-Ni nguvu za Mungu zinazohusika kwa kujibu jambo Fulani.

 

AINA ZA MAOMBI

1.     Maombi ya kawaida.

Mfano:- maombi ya kumbariki mtu

-         Maombi ya toba na rehema

-         Maombi ya kuombea chakula

-         Maombi ya kuombea safari

-         Maombi ya kumshukuru Mungu

-         Maombi ya kuombea ndoa  n.k

2.     Maombi ya vita

Mfano- maombi ya mkesha.

-maombi ya mfungo

-maombi ya kuharibu falme na  mamlaka za giza

- maombi ya kuombea wagonjwa.

- maombi ya kufunguliwa

- maombi ya ukombozi

- maombi ya urejesho (kurudisha) n.k.

Vilevile maombi ya muda mrefu na maombi ya muda mfupi yapo katika hizo aina za maombi.


 

MAMBO UNAYOPASWA KUYAJUA KUHUSU MAOMBI.

i). kupitia maombi Mungu anaweza kufanya mambo yote

‘lakini Yule malaika akamwambia, usiogope Zakaria maana dua yako imesikiwa na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanaume na jina lake utamwita Yohana ‘Luka 1;13

 

Siku hizo Hezekia akaugua akawa katika hatari ya kufa, Isaya nabii mwana wa Amozi akamjia akamwambia Bwana asema hili , tengeneza mambo ya nyumba yako maana utakufa wala hutapona Basi Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwambia Bwana ukumbuke sasa jinsi nilivyokwenda mbele yako katika  kweli na moyo mkamilifu na kutenda  yaliyomema machoni pako Hezekia akalia sana sana. Ikawa kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia kusema, Rudi ukamwambie Hezekia mkuu wa watu wangu Bwana Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, nimeyasikia maombi yako na kuyaona machozi yako, tazama nitakuponya siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana, Tena nitazidisha siku zako kiasi cha miaka kumi na mitano, name nitakuokoa wewe na mji huu na mkono wa mfalme wa Ashuru, name nitakulinda mji huu kwa ajili yangu na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, 2wafalme 1-6.

 

ii). Maombi kwa Mungu yanapaswa kuwa ni ya kuendelea kuwa sehemu ya maisha ya mkristo.

‘Akawaambia mfano ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tama Luka 18;1.

 

iii). Katika maombi tunatakiwa kupeleka haja zetu kwa Mungu.

‘Msijisumbue kwa neno lolote bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu.

 

iv). Tunatakiwa tuwe na imani.

‘Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima na oambe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yoyote maana mwenye  shaka ni kama wimbi la bahari lililichukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku “ Yakobo 1;5-6.

“Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa Yule na Bwana atamwinua hata ikiwa amefanya dhambi atasamehewa Yakobo 5;15.

 

v). Tunatakiwa kuomba kwa jina la Yesu

“Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu hilo nitalifanya ili baba atukuzwe ndani ya mwana.

Yohana 14;13.

 

vi). Mungu anasikia maombi ya watu wote

“ katika shida yangu nalimwita Bwana na hekaluni mwake, kilio change kikaingia maskioni mwake , ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, misingi ya  milima ikasuka-suka…. “Zaburi 18;6-7.

 

“kwa kuwa Bwana huwaakia wahitaji wala hawadharau wafungwa wake Zaburi 69;33.

 

Vii). Mungu anajibu maombi.

“ walilia naye Bwana akasikia , akawaponya na taabu zao zote,  Zaburi 34;17.


Lakini panapo usiku wa manane Paulo na sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza ghafla kukatokea matetemeko kuu la nchi hata msisingi ya gereza ikatikisika na mara hiyo milango ikafunguka vifungo vya wote  vikalegezwa. Matendo 16;25-26.

 

viii). Tunapaswa kuomba kwa bidii.

Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita, Akaomba tena mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake , Yakobo 5;17-18.

 

Maana ya kuomba kwa bidii,

-kuomba kwa kuweka akili zako zote kwenye jambo hilo

-kuomba kwa ujasiri

-kuomba kwa nia yako bila kukata tama.

-kuomba kwa nia moja.

-kuomba kila siku bila kuchoka.

-kuomba bila kuogopa

-kuomba kwa maarifa

-kuomba kwa mamlaka ya Mungu

Kumbuka sisi ni wana wa Mungu, hivyo tumepewa amri juu ya nguvu za giza kwamba tukitamka neno juu yao linakuwa vile vile kwa jina la Yesu- Amen.

 

Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za Yule adui wala hakuna kitu kitakacho wadhuru


Tumepewa amri ya kukanyaga nyoka na nge.

*kukanyaga tunguli

*vipembe

*mikoba

*kukanyaga nguvu za adui

*mapepo na majini

*kukanyaga silaha zote za kichawi.

Kila kitu kinatakiwa kukitakasa kwa Damu ya Yesu Kristo.

Kila sehemu tunayoingia tunatakiwa kupatakasa kwa Damu ya Yesu Kristo.

Hakuna kitakachowadhuru

 

FAIDA ZA MAOMBI

a)    Hutusaidia kukua kiimani.

“Kisha akawaleta nje akasema Bwana zangu yanipasa nifanye nini nipate  kuokoka? Wakamwambia mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako, Matendo 16;30-31.

b)    Mambo yako ya ndani yatafunguliwa

Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako “zaburi 119;18.

 

c)     Maombi ni ulinzi

Basi akamfukuza huyo mtu akaweka makerubi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga  wa moto uliogeuka huko na huko kulinda njia ya mji wa uzima “Mwanzo 3;24.

 

d)    Maombi yanatufanya tumtafute Mungu,

Nanyi mtaniita mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza, Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa mioyo yenu yote.

 

 Yeremia 29;12-13.

Ndipo Bwana akaniambia umeona vema kwa maana ninaliangalia neno langu ili nilitimize ‘Yermia 1;12’

Naliangalia neno langu ili nilitimize, hivyo Mungu hawezi kujipinga mwenyewe.

e)     Utamruhusu Roho mtakatifu akutumie

“Kadharika Roho naye kutusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa “warumi 8;26.

‘Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja yeye Yule akiangamia kila  mtu peke yake kama apendavyo yeye. “1wakoritho 12;11.

 

f)      Utatumika vizuri kwa Mungu.

Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao wakawaacha waende zao, Matendo 13;2-3.

 

g)    Utakuwa na nguvu za Mungu

“Tangu siku za Yohana mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu nao wenye nguvu wauteka, Mathayo 11;12

 

h)    Maombi yanainua mtu

“Yesu akamwambia simama jituike godoro lako uende. Mara Yule mtu akawa mzima akajitwika godoro lake akaenda Nayo ilikuwa  ni sabato siku hiyo, Yohana 5;8

 

Na kule kuoma kwa imani kutamwokoa mgonjwa Yule na Bwana atamwinua hata ikiwa amefanya dhambi atasamehewa ‘Yakobo 5;15

 

 

UMUHIMU WA  KUFUNGA (mfungo).

Mfungo; Ni hali ya  kukaa bila kula chakula  au kinywaji ili kutekeleza masuala ya imani yako. Mfungo unatoa sauti inayopenya hadi kwenye kiti cha Mungu Baba na kuleta mabadiliko ya kudumu katika ulimwengu wa mwili, Hii ni kanuni ya ulimwengu wa Roho ili kufanya jambo lililokusudiwa litokee.

 

 

WALIOFUNGA KWENYE BIBLIA.

a)    Yesu kristo,

Yesu kristo alifunga siku arobaini (40)

‘Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani ili ajaribiwe na ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho  akaona njaa, Mathayo4;1-2.

 

b)    Musa

Musa naye alifunga siku arobaini 40)ili asemezane na Mungu.

Nikaanguka nchi mbele za Bwana siku arobaini usiku na mchana kama pale kwanza sikula chakula wala kunywa maji kwasababu ya makosa yenu yote mliyokosa kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana kwa kumkasirisha, Torati 9;18.

Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake hakula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi “kutoka 34;28”

c)     Daniel alifunga siku ishirini na moja(21)”Katika “siku zile mimi Daniel nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu” Danieli 10;13,”……. lakini mkuu wa ufalme alinipinga siku ishirini na moja” Daniel 10;2.

 

d)    Esta; Esta na wayahudi alifunga siku tatu ili aingie kinyume cha sheria kwa mfalme.

“Uende ukakusanye wayahudi wote  waliopo hapa shushani mkafunge kwa ajili yangu, msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku na mchana nami na wajakazi wangu tutafunga vilevile, kisha nitaingia kwa mfalme kinyume cha sheria, nami nikiangamia na niangamie “Esta 4;16.

e)     Watu wa Ninawi.

Hawa walifunga wakimlilia Bwana awaepushe na hatari iliyokuwepo mbele yao.

“Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu, wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo, Yohana 3;5

f)      Barnaba, Simion, Lukio Mkirene, Manaeni

Nao hawa walifunga ila Biblia haijaonyesha.

Walifunga siku ngapi

Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga.

Kwahiyo ni mifano michache tu kwa waliofanya kulikana na sababu Fulani Fulani kwao.

 

AINA ZA MIFUNGO (fasting)

1.     Mfungo mwepesi.

Huu ni mfungo ambao mtu aliyefunga anaweza kunywa uji, maji na vitu vyepesi. Lengo la mfungo huu ni kujinyenyekeza mbele za Mungu au kutaka kumpa Mungu nafasi yake. Mfano. Mtu anasema nitafunga siku 3,21 au 40 nitakuwa nakunywa maji na jioni nafungulia.

 

 

2.     Mfungo mkavu.

Huu ni mfungo wa kutaka kitu Fulani kwa Mungu ili ujibiwe haraka. Mfano Esta na wayahudi, walifunga siku tatu bila kula chochote na majibu yakaja bila kuchelewa.

 

SIFA ZA MFUNGO.

a)    Kuongozwa na Roho ,takatifu

Mara Roho akamtoa aende nyikani, Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na shetani, naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu na malaika walikuwa wakimhudumia , Marko 1;12-13.

 

b)    Mfungo ufanywe katika unyenyekevu,

 ilikuwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia kutoka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao” 2zanyakati 7;14

 

c)     Kuambatane na kuomba

“Ndipo mwakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao wakawaacha waende zao. “matendo 13;3

 

d)    Mfungo ufanywe kwa furaha.

“Tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana, maana ujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga.Amini nawaambieni wamekwisha kupata thawabu yao” Mathayo 6;16.

 

 

e)     Unapofunga watu wasikujue

Bali wewe ufungapo jipake mafuta kichwani unawe uso. Ili usionekane na watu kuwa unafunga ila na Baba yako aliyesirini na Baba yako aonaye sirini atakujazi, ‘Mathayo 6;17-18

 

NDANI YA MFUNGO KUNA VITU HIVI

Siku zote unapomuona kufunga mfungo wa aina yoyote ile tambua vitu hivi lazima vijitokeze au  viwepo.

-Malaika watakuwepo wakikihudumia

-Shetani naye atakuwepo ili akujaribu.

-Utajisikia mchovu au kuishiwa nguvu

-Mwili utaisha (kupungua) lakini mtu wa ndani atakuwa na nguvu za rohoni.

-Utukufu wa Mungu utakufunika.

“Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama ngozi ya uso wake iling’aa nao wakaogopa kumkaribia “kutoka 34;30

 

FAIDA/ UMUHIMU WA MFUNGO

-Kuonyesha utii mbele za Mungu

“Lakini  hata sasa anasema Bwana, nirudieni mimi, kwa miyo yenu yote na kwa kufunga na kwa kulia na kwa kuomboleza Yoeli 2;12

 

-Ili kujinyenyekeza mbele za Mungu

“Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe na kwa ajili ya watoto wetu na kwa mali yetu yote Ezra 8;21.


 

-Ili kupata msaada,

“Basi tukafunga tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo, naye akatutakabali, Ezra 8;23

 

-Ili katika udhaifu wetu nguvu za Mungu zionekana,

“Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta  ‘Zaburi 109; 24

 

-Ili kuomba Rehema.

Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi na dua pamoja na kufunga na kuvaa nguo za magunia na majivu, Daniel 9;3

 

-Ili Hunao imani na kuongeza ujasiri.

“Uende ukawakusanye wayahudi wote waliopo hapa shushani mkafunge kwa ajili yangu’ Esta 4;16.

 

-Huongeza/ huleta nguvu ya maombi

‘Bali mimi walipougua wao, nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga, maombi yangu yakarejea kifuani mwangu “ Zaburi 35;13

 

-Kukuza kanisa na huduma ya Mungu isonge mbele.

“Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msipokee neema ya Mungu bure (kwa maana asema wakati uliokubalika na likusudia siku ya wokovu nalikusaidia, tazana wakati uliokubaliwa ndio sasa tazama siku ya wokovu ndiyo sasa)” 2wakoritho 6;1-2.

 


-Kuufanya ulimwengu wa Roho uwe wazi  :”Maana ingawa tunaenda  katika  mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili.(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka kujiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii kristo ;2wakoritho 10;3-5

 

-Kuutiisha mwili,

‘Basi nasema enendeni katika Roho, wala hamtazitimiza kamwe tama za mwili, kwasababu mwili hutamani ukishindana na Roho na Roho kushindana na mwili, kwa maana hizi zinapingana hata hamwezi kufanya mnayotaka,Lakini mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria’ wagalatia 5;16-18.