Thursday, May 15, 2025

UVUNJA ROHO ZA SODOMO NA GOMORA

 

KUVUNJA ROHO ZA SODOMO NA GOMORA

Sodoma na Gomora hii ilikuwa ni miji iliyokuwa ikitenda mambo mabaya mbele za Mungu,kwa wanaume kuwakiana tama na wanawake vile vile kuwakiana tama yaani kwenda kinyume na maumbile.Kutumia miili yao kinyume na asili ya viungo vya uzazi kwa matumizi yake.Mwanzo 13:13,Warumi 1:26-27,Warumi 1:24-25,Warumi1:28-32,Mwanzo 18:1-15,Mwanzo 19:4-11

HATA WAKUZUIE UTAVUKA

Torati 9:1-5,Torati 11:30-30,Marko 4:35-41,Marko 5:1---,Matendo 16:9-21

Kushukuru Zaburi 50:23,Wafilipi 4:4-7

-kusali –prayer

-kuomba- supplication

-kushukuru- thanksgiving

(humbly,begging,asking)

JIUNGANISHE NA MADHABAHU YAKO

Madhabahu (Altare,Alta) ni sehemu yoyote ile mtu anapokutana na roho inaweza kuwa ni roho ya Mungu au shetani

Ndani ya madhabahu kuna

·        Kutoa sifa-nyimbo

·        Kutoa sadaka

·        Kuomba (kupeleka mahitaji)

Ezra 3:1-6

Faida ya madhabahu

·        Ni upatanisho

·        Inafungua Baraka

·        Inatupa ulinzi wa Ki-Mungu Mwanzo 8:18-22

·        Madhabahu inasema mbele za Mungu

·        Inamdhihirisha Mungu unayemuabudu

 

KUVUNJA ROHO YA TALAKA

 KUVUNJA ROHO YA TALAKA

Talaka ni hati ya kiapo cha kuvunja ndoa

Aina za ndoa

        i.            Ndoa ya kidini yaani ya Kikristo na Kiislamu

      ii.            Ndoa ya kiserikali

    iii.            Ndoa ya kimila

Mwanzo 2:24

Ndoa na iheshimiwe Waebrania 13:4

Madhara ya talaka

·        Kuzuia hatima za watoto wenu zisitimie kwa wakati

·        Kuleta magonjwa

·        Familia kusambalatika

·        Heshima itapungua

·        Kuyumbisha watoto

·        Kuleta mauti

Marko 10:4-12,Malaki 2:16

Maagizo ya ndoa

 1Wakorintho 7:1-6,1Wakorintho 7:8-16,1Wakoritho 7:33-34,7:39

WAKUACHE UONEKANE

Ili mtu ufanikiwe kwenye jambo Fulani ni lazima aonekane,iwe kibiashara,kindoa,kikazi n.k Wafilipi 3:9-10,Mithali 17:8,Mhubiri 6:4

VINYAGO VYA BABAYE

Vinyago ni miungu inayoabudiwa au ni sanamu zinazoabudiwa kulingana na jamii husika,kuna miungu ngazi mbalimbali mfano kwenye familia,ukoo,kwenye wilaya,mkoa,kitaifa na kimataifa,inaabudiwa sehemu mbalimbali kama vile ofisini,nyumbani.Kutoka 20:1-6,Torati 6:14-15,Mwanzo 31:19,Mwanzo 35:2

HAKUNA ATAKAYESIMAMA MBELE YAKO

Yoshua 1:1-3,Yushua 1:-9,Ayubu 5:12,Zaburi 89:20-

MASHIMO YA KICHAWI (Kiroho)

 

MASHIMO YA KICHAWI (Kiroho)

Agano la kale mtu alipokuwa anafanya kosa au makosa alikuwa anahukumiwa kwa kutupwa kwenye mashimo marefu.

Mashimo yaliyokuwepo

        i.            Mashimo yenye wanyama mfano Danieli

      ii.            Shimo lenye moto mfano Shedraka,Meshaki na Abednego

    iii.            Shimo lenye maji mengi au matope mfano Yeremia 38:6

   iv.            Shimo lisilo na kitu

Sasa

Shetani naye vile vile naye ameyaweka mashimo yake haya kwa namna ya kiroho,hayaonekani kwa macho ya kawaida kwasababu shimo lenyewe ni roho kamili,lina akili,linaweza kukimbia na ukiingia ndani huwezi kutoka linageuka na kuwa giza.Zaburi 35:7,Ufunuo 9:1-2,Isaya 24:17,14:15,Isaya 38:18

Miji inaweza kuwa na mashimo ya rohoni na utakaposhughulika na shimo hilo unakuwa umeuteka mji.Kuna mashimo makubwa  yaani kuzimu ya angani,kuzimu ya baharini ,kuzimu ya nchi

Pia kuna vishimo vidogo mfano mtu anachukuliwa msukule na kuwekwa kabatini,kisimani,dukani,n.k Isaya 42:22

Kila mtu amewekewa Baraka zake sehemu Fulani mfano kwenye kinywa,tumbo,kumbukumbu,biashara,ndoa n.k

Familia,ukoo wanawekwa kwenye mashimo ya mauti,magonjwa,laana,mikosi,shida,balaa,utasa,umasikini n.k

Mambo unayotakiwa kuyafahamu kuhusu kuzimu

         i.            Malaika wa kuzimu ufunuo 9:11

       ii.            Makomeo ya kuzimu Ayubu 17:16

     iii.            Milango ya kuzimu Ayubu 38:17,Mathayo 16:18

     iv.            Kamba za kuzimu 2Samweli 22;6

       v.            Makao ya kuzimu Zaburi 89:88

     vi.            Shida za kuzimu Zaburi 116:3

   vii.            Kitanda cha kuzimu Zaburi 139:8

Maombi

-kuyashambulia mashimo yote ya kichawi

-kuwateketeza walinzi wa mashimo

-kutoka shimoni

ROHO YA MPINGA KRISTO

 

ROHO YA MPINGA KRISTO

Maana yake ni kwenda kinyume na Kristo au kugeuza ukweli wa Yesu Kristo kuwa uongo.1Yohana 2:18,1Yohana 2:22,1Yohana 4:1-3,2Yohana 1:7,2Wathesalonike 2:4,Mathayo 10:16

Dalili za roho ya mpinga Kristo zinazonyemelea mtu/watu

        i.            Kulizoea Neno la Mungu

      ii.            Kutokumuamini Yesu

    iii.            Kumkana Yesu Kristo

   iv.            Kuchukia mambo ya Mungu mfano maombi

     v.            Kuanza kuamini vitu ambavyo sio vitu vya Kimungu

   vi.            Kufanya uovu bila kuumia moyoni

 vii.            Kutokusamehe na kuachilia 1Yohana 4:20-21

viii.            Kutokuzifuata sheria na kanuni za Yesu Kristo

MTUMAINI BWANA

Tumaini maana yake kumtegemea Mungu Baba Mithali 3:5-10

·        Kwa moyo wako wote

·        Usizitegemee akili zako mwenyewe

·        Katika njia zako mkiri (mtaje Yesu/Mungu)

·        Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe

·        Utajiepusha na uovu

·        Mheshimu BWANA kwa mali zako

KUIPINGA ROHO YA UMASIKINI

Umasikini ni hali ya kupungukiwa .Kuna umasikini wa mtu binafsi na kuna umasikini wan chi,kata,tarafa,mtaa n.k Torati 15:4----,Torati 15:7,Mwanzo 13:2,Mithali 19:17,Yakobo 1:27

NIMEWEKA MLINZI

Ezekieli 3:17,Danieli 4:13,Zaburi 121:4-5,Zaburi 141:3

KUFUTA MASHIMO YA KIROHO

Zaburi 119:85,Yeremia 2:6,Waebrania 11:36

UNAJULIKANA MBINGUNI

Kujulikana ni hali ya kufahamika

·        Kufahamika na Mungu

·        Kufahamika na wanadamu

·        Kufahamika na mashetani

Yeremia 1:4-10

Faida za kujulikana na Mungu

·        Utapata msaada/watakusaidia

·        Utazawadiwa

·        Utapata kibali

·        Utapata neema

NABII WA MATAIFA

Nabii ni sauti ya Mungu duniani anayepewa ujumbe na Mungu kupeleka kwa wanadamu Yeremia 1:4-10,Hesabu 12:6,Torati 34:10,Waamuzi 4:4

ROHO YA UFUKARA

 

ROHO YA UFUKARA

Ufukara ni hali ya kuishi zaidi ya umasikini.Ufukara ni roho inayoishi ndani ya nchi na familia,ukiangalia familia nyingi za Kiafrika na zile nchi zinazoendelea,roho hizi zinaendelea kizazi baada ya kizazi,kutoka ukoo au familia.Mambo waliyoyafanya huko nyuma na vitu hivi vinaenda mpaka kwenye damu,bila kuvunja na kujitenga huwa zinafuatilia.Yeremia 17:5-8

MALI ILIYOFICHWA

Mali ni Baraka.Isaya 45:3

KUFUTA RATIBA ZA KUZIMU

Ratiba ni mpangilio au utaratibu uliowekwa kwa makusudi ya jambo Fulani mfano ratibaza kanisani,ratiba za harusi,ratiba za mikutano,ratiba za nchi,ratiba binafsi

Nuru:Mungu alimwambia atengeneze safina maana ataachilia mvua siku 40 Mwanzo 7:11-12

Ratiba za kishetani/kuzimu ni ratiba anazotumia shetani kwa kutumia mawakala wake,ni namna gani wamuandalie mtu jambo baya,muda,mwezi,tarehe,mwaka,siku huwa wanazingatia vitu hivi.Waamuzi 16:15-17

KUFUTA DAMU ILIYOMWAGWA KWA AJILI YAKO

Damu ya Yesu ilimwagwa kwa ajili ya anguko la dhambi Mwanzo 26:28 na kwenye damu kuna uzima Yohana 6:54-56,Warumi 3:15,Torati 12:23,Zaburi 79:3

ARDHI IKUTAMBUE

Kuna siri kubwa kwenye ardhi (udongo) nchi.Maisha ya mtu yako kwenye ardhi. Mwanzo 2:7,Mwanzo 3:17.Tabu unayopitia inatokana kwenye ardhi Yeremia 22:29-30,Mfalme wa Yuda alionea mgeni,mjane,yatima Isaya 34:9,Ayubu 28:5-6,ufunuo 12:15-16

KUTAMBUA NYAKATI

Nyakati ni mabadiliko ya vipindi

Aina za nyakati Kibiblia

        i.            Wakati wa uumbaji (Adamu)

      ii.            Wakati wa sheria (Musa/Yoshua)

    iii.            Wakati wa Waamuzi (Deborah,Samsoni)

   iv.            Wakati wa Wafalme (Sauli,Daudi)

     v.            Wakati wa Manabii (Isaya,Yeremia)

   vi.            Wakati wa injili ya mbinguni (Yesu)

 vii.            Wakati wa nyakati za Mitume (Paulo,Petro,Mathayo n.k)

viii.            Wakati wa ufunuo na uumbaji Mpya

Mwanzo 1:1----

 

 

WIMBO MPYA

 

WIMBO MPYA

Tunapozungumzia wimbo kiroho ni neno la unabii

Aina za nyimbo kiroho

·        Wimbo wa Musa

·        Wimbo wa Mwanakondoo

·        Wimbo Mpya

1.     Wimbo wa Musa ni unabii wa Agano la kale

2.     Wimbo wa Mwanakondoo ni unabii wa Agano Jipya

3.     Wimbo Mpya ni injili ya milele (Neno lililofunuliwa)

Ufunuo 15:2-4,Ufunuo 14:6-7,Zaburi 119:54,172

MJUMBE WA MUNGU ALIYETUMWA KWAKO

Mjumbe ni mtu anayewakilisha watu wengine kwa shughuli Fulani Marko 1:1-3,Luka 3:4-6,Yeremia 49:14,Malaki 3:1-2,Waebrania 12:2 4 na Yesu mjumbe,Hagai 1:13

NIPE RUHUSA NIENDE

Ruhusa ni maombi au ombi linalofanywa na mtu kuhusiana na jambo Fulani mfano unaomba ruhusa kwenda sehemu Fulani na katika kuomba ruhusa kuna mambo mawili

         i.            Kukubaliwa

       ii.            Kukataliwa

Mwanzo 24:56

Mwanzo 30:25

Kutoka 4:18,Kutoka 7:14,Kutoka 8:1,Kutoka 14:3,Kutoka 14:13

BWANA AKUINULIE USO WAKE

Hesabu 6:22-27

         i.            BWANA akubarikie

       ii.            BWANA akulinde

     iii.            BWANA akuangazie nuru za uso wake

     iv.            BWANA akufadhili

       v.            BWANA akupe amani

KUFUKUA VISIMA VYA BARAKA

Mwanzo 26:25,Mwanzo 26:32,Mwanzo 21:22,Hesabu 21:17

KUFUTA AJALI ILIYOPANGWA JUU YAKO

Isaya 62:10-------

KUONDOA NIRA ZA KISHETANI

Nira ni kifaa ambacho huvikwa shingoni mwa mnyama.mfano ng’ombe,punda,farasi n.k kwa kusudi la kuvuta mzigo uliyo nyuma yake.Nira huwa na lijamu na hatamu ili kuweza kumuongoza mnyama njia ambayo mtu wake amekusudia kupita

Lijamu ni kifaa ambacho hufungwa mdomoni

Hatamu ni kamba ambazo zimefungwa kwenye lijamu ili kumwongoza mnyama kwa mwendo anaotaka Mathayo 11:27-30,Isaya 10:27

ATA WAKUZUIE VIPI UTAVUKA TU

 

ATA WAKUZUIE VIPI UTAVUKA TU

Katika maisha tunayoishi kuna mambo mengi,ambayo yanafanyika sirini juu ya mtu Fulani ili aharibikiwe.Na katika kukuharibia huko wanaana na kukuzuia kwamba usipenye,usivuke,uziende,usipite.Kutoka 14:15-16

Walivuka bahari ya shamu (Red sea-bahari nyekundu) Mathayo 14:22,Marko 4:35,Torati 9:1 ukivuka utamiliki, Matendo 16:9 Paulo aliona maono avuke akawasaidie watu

VITA YA KIUCHUMI

Uchumi ni jumla ya shughuli za watu zenye lengo la kutosheleza mahitaji mfano uzalishaji,matumizi ya bidhaa,usambazaji.

Uchumi ni rasilimali ni namna gani unaweza kuzitumia mfano ardhi,elimu,kipaji 2Wakoritho 8:9

Yesu alikuja ili awaokoe watu kiroho na kimwili kutoka kwenye umasikini Mwanzo 12:16,Mwanzo 13:2,Mwanzo 13:2,Mwanzo 26:12-14,Torati 8:17-20,8:1-16,Matendo 12:21-23,Ayubu 1:1-------,Ayubu 42:10-----

Kanuni ya uchumi

·        Kufanya kazi

·        Kuwa na maarifa

·        Kuwa na bidii

·        Kuweka akiba

·        Utoaji

·        Usishindane (usiige)

PINDUA MEZA

Pindua maana yake ni kuharibu.1Wakoritho 10:21,2Wakoritho 6:16,Waamuzi 1:6-7

MIKONO YA KUZIMU

Zaburi 49:15,Mithali 5:5,Isaya 28:15,Matendo 2:27

MUNGU ATIMIZE NENO LAKE

Neno la Mungu lina nguvu,mamlaka uweza,ni moto,nyundo,upanga Yeremia 1:11-12,Isaya 38:6-7

KUHESHIMISHWA NA MUNGU

Matendo 4:13,Yohana 12:26

BWANA YESU AIAMURU BARAKA IJE KWANGU

Torati 28:8,Hagai 2:8

BWANA NI NURU YANGU

Zaburi 27:1-5,Zaburi 27:10-14

MTAABISHAJI WA MAISHA YAKO

Mtaabishajilinatokana na neno taabika

FIMBO YA MUNGU

 

FIMBO YA MUNGU

Fimbo ni kifaa kinachotumika katika kutegemea mfano wapanda milima huwa wanatumia fimbo kama kitegemezi ambacho kinawarahisishia kupanda mlima vizuri.

Fimbo kiroho ni mtu aliye na neno la Mungu ambalo linaweza likamsaidia kwenye utegemezi.Kutoka 17:9---,Zaburi 2:8-9,Mithali 22:15,Mithali 23:13-14,Waebrania 1:7-8.Yesu Kristo ni fimbo tembelea

KUONDOA NGUVU YA KABURI YA KISHETANI

Hosea 13:14,Zaburi 49:15,Zaburi 6:5

KUWAANGAMIZA WATAABISHAJI WETU

Mtaabishaji linatokana na neno taabika.Mtaabishaji ni mtu anayeumiza,teas,haribu,anayekukosesha amani,raha n.k anataabisha kazi,ndoa,biashara,masomo na elimu,watoto,huduma n.k 1Wafalme 18:13-40.Omri alikuwa ni Jemedari wa jeshi alitawala Israeli,baada ya kufa akashikilia motto wake Ahabu ambaye alitawala miaka 22 wakati wa kipindi cha mfalme Asa.Baadaye alimuoa Yezebeli binti Ethbaali mfalme wa Sidoni.

Ahabu alifanya mabaya machoni pa Mungu alimjengea baali madhabahu na Ashera.1Wafalme 19:15-17,2Wafalme 10:18-28

Maombi

-kuwakusanya wataabishaji

-kuwapiga wataabishaji

KUONDOA ROHO ZA MAGONJWA

Kutoka 23:25,Kutoka 7:15,2Wafalme 1:2,Mathayo 4:23

UTAITWA MBARIKIWA

Mbarikiwa ni mtu aliye na Baraka/aliyepata Baraka (mafanikio) mfano fedha,ndoa,elimu,kazi,afya njema,mali,ustawi n.k Luka 1:42-48,Luka 1:49-50,Luka 1:26-41,Luka 3:3-6

SIRI YA MAOMBI

2Wafalme 20:3-9,Zaburi 54:2

KUMFUNGA MKUU WA KUZIMU

Ufunuo 20:1-10,Mathayo 16:19

KILA ULITENDALO LITAFANIKIWA

Zaburi 1:1-3,Isaya 55:11,Torati 6:3,Torati 6:18,Torati 12:28,Yoshua 1:7,1Wafalme 2:3,Ayubu 12:16,Zaburi 122:7

UTAPATA SHANGWE NA FURAHA

Isaya 51:11,Zaburi 126:5,Isaya 25:8

UPEPO WA UHARIBIFU

Upepo ni hali Fulani isiyoweza kuonekana wala kushikika.Yohana 3:8,Mhubiri 11:5,Marko 4:35-41

UZIMA NDANI YAKO

1Yohana 5:11-14,Mathayo 7:7----

YESU NI MWAMINIFU

1Wathesalonike 5:16----

NURU IMEWAANGAZA

Isaya 9:1-7

KUWA JUU YA FALME

Yeremia 1:4----

Maana yake Mungu amekuumba kwa makusudi,kuna kusudi juu yako ,atakupa na kazi ya kufanya.

NAIENDEA NCHI YENYE MAZIWA NA ASALI

Maana yake ni kumiliki mafanikio,Hesabu 13:25-33,Hesabu 14:1-9,Torati 1:21,Yoshua 1:3-9,Yoshua 2:24

UTUMISHI (MTUMISHI)

Utumishi ni uwezo wa kutumika kwa ajili yaw engine

Mtumishi ni mtu anayetumika kwa ajili yaw engine au kuwa mtumwa kwa wengine.Marko 10:42-45,Luka 22:24-27,Yohana 31:12-16,1Petro 5:2-6

Kanuni za utumishi (mtumishi)

·        Mnyenyekevu na mpole Mathayo 11:29

·        Mwenye heshima 1Petro 3:7

·        Mwenye Roho Mtakatifu Matendo 2:4

·        Anauwezo wa kufundisha na mvumilivu 2Timotheo 2:24-26

·        Mtii Waefeso 6:5

·        Mwaminifu na mwenye imani Luka 16:10,Waebrania 11:29

KUSAMBARATISHA UCHAWI NA UGANGA WA KIENYEJI

 

KUSAMBARATISHA UCHAWI NA UGANGA WA KIENYEJI

Uchawi:Ni nguvu zinazotumiwa na watu kwa nia ya uharibifu.Kuna uchawi mweupe na kuna uchawi mweusi

Uganga:Ni elimu ya kichawi inayohusiana na magonjwa

Ucawi na uganga ni kampuni moja ila sekta tofauti mfano jeshi.Uchawi na uganga lengo lao ni kuwatesa watu Isaya 47:12,Mika 5:12,Walawi 26:31,Torati 18:9-13,Kutoka 7:22,2Wafalme 21:6,2Nyakati 33:6

MOTO WA MADHABAHU

Madhabahu:Ni sehemu ambayo roho kwa roho hukutana au zinakutana.Ni mahakama ya kiroho ambapo kesi za kiroho zinaletwa na kutolewa hukumu Ufunuo 8:3-5,Ufunuo 5:8,Luka 12:49

 Chetezo ni mtu

Moto ni (neno,kuchoma) kufanya maombi

Moshi wa uvumba ni sauti ya maombi

Uvumba ni maombi

KUONDOA ROHO ZA ULEMAVU KATIKA MAISHA YETU

Ulemavu:Ni hali ya kutokuwa na nguvu au upungufu wa viungo au kutokuwa katika hali ya utimilifu

Aina za ulemavu

-kuna ulemavu wa kiroho

-kuna ulemavu wa kimwili

Matendo 3;1-2,Matendo 3:3-7,Matendo 3:8-10,Matendo 3:11-16

WANA NI URITHI

Zaburi 127:3,Torati 28:4,11

Wana ni watoto,kwa wanawake wao ndiyo wanaobeba watoto.Muunganiko anaoufanya Mungu ni wa ajabu sana,sisi binadamu tunatumika kama kiwanda cha uzalishaji (production)

NITAKUWA UKUTA WA MOTO

Ukuta ni kitu Fulani kinachojengwa ili kuzuia vitu Fulani visipite au kuingia kwa urahisi Zekaria 2:4-5,Isaya 4:5,Waebrania 1:7

KUFUTA KURASA MBAYA ZA ZAMANI

Kurasa ni sura za kwenye kitabu zikiwa na maana Fulani 2Wakorintho 5:17,2Wakoritho 5:18-19,2Wakorintho 5:20-21

KUKATAA SIKU ZA KUCHOKESHA

 

KUKATAA SIKU ZA KUCHOKESHA

Kuchokesha linatokana na neon kuchoka.Kuchoka maana yake ni kukata tama kwenye ndoa,kwenye kazi,kwenye biashara,kwenye huduma,kwenye maisha,kwenye mashamba n.k Ayubu 7:3-4,Ayubu 3:1-----Ayubu 42:1-----,Ayubu 42:16

KUHARIBU MAFURIKO YA MAUTI

Mauti:Ni roho inayoharibu jambo Fulani,roho hii inaweza kutembea,kukaa,kuishi sehemu mbalimbali. 2Samweli 22:5-8,Zaburi 9:13,Zaburi 78:50,Zaburi 23:4,2Wafalme 4:40

WALIOMPOKEA ALIWAPA UWEZO

Yohana 1:11-14,1Yohana 5:6-12

Washuhudiao Mbinguni

·        Mungu

·        Neon (Yesu)

·        Roho Mtakatifu

Washuhudiao duniani

·        Roho –mtu

·        Maji –ubatizo

·        Damu –ukombozi/utakaso

KUMILIKI MILANGO YA BARAKA ALIYOKUWA AMEISHIKILIA ADUI

Mlango:Ni kifaa kinachotumika kwa ajili ya kuingia na kutoka.Utabarikiwa uingiapo na utokapo Torati 28:6,Isaya 60:11,Mwanzo 22:17,Ufunuo 3:8 kumtoa aliyekuwa kwenye mlango wa Baraka.Nyumba ni kama ulimwengu,kiti ni kama Baraka yako.

PASAKA (PASSOVER)

Pita juu ya.Ni sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu.Kutoka 12:27,Mathayo 26:17,Luka 22:1, 1Wakorintho 5:7

UFALME WAKO UJE

Mathayo 6:9-13,Kutoka 19:5-6,Zaburi 103:19,Mhubiri 4:14,Matendo 8:12,Matendo 28:31,Mathayo 7:21,Luka 4:43

UWE NA MOYO WA USHUJAA

YOSHUA 1:5-9

YESU APELEKWA MBELE YA PILATO

Mathayo 27:1-2,Mathayo 27:11-18

BWANA MUNGU AKUONGOZE NJIA

Mwanzo 24:24

 

MAUTI ILIYOPANDWA

Ufunuo 6:8

BWANA NI MTU WA VITA

Kutoka 15:3-8,Kutoka 15:1-2,Yoshua 17:1

KUOMBA KWAKO KUMESIKIWA

Matendo 10:31

KUVUNJA ROHO YA KIUME KWA MWANAMKE NA ROHO YA KIKE KWA MWANAUME

Walawi 17:7

UNAPOINGIA KWENYE MAOMBI SAMEHE

Mathayo 6:14-15,Isaya 59:1-4

WALIOKUTENGENEZEA ULIE

Zaburi 69:1-3,Zaburi 69:6,Isaya 65:19,1Samweli 30:4,Waamuzi 21:2

TWENDE NG’AMBO

Marko 4:35-41,Marko 5:1----,Yoshua 9:1

KAZA MWANDO

Wafilipi 3:12-14

BIBLIA NI AGANO

 

BIBLIA NI AGANO

Maana ya Biblia:Ni agano kati ya Mungu na wanadamu

Muundo wa Biblia

·        Ina vitabu 66

·        Ina sura 1186

·        Ina mistari 31101

Mgawanyo wa Biblia

1.     Agano la kale lina vitabu 39,lina sura 929,lina mistari 23144,yaani kutoka kitabu cha Mwanzo hadi Malaki.Kiunganishi hapa alikuwa ni Musa

2.     Agano jipya lina vitabu 27,lina sura 260,lina mistari 7959,yaani kutoka kitabu cha Mthayo hadi Ufunuo na kiunganishi hapa ni Yeshu Kristo

Lengo la Agano

        i.            Ni kupata Baraka

      ii.            Ni kuwa mwaminifu

    iii.            Kutimiza ahadi yake

Kazi ya Mungu ni kuchagua wajibu wa mteule ni kutunza Agano

Mashariti ya Agano

        i.            Mlengwa

      ii.            Madhumuni/yaliyomo

    iii.            Muda

   iv.            Matokeo

Kwenye Agano kuna sheria

Kutoka 19:5-6,Kutoka 28:1-14(matokeo),Kutoka 20:1----,Waebrania 9:28,Mathayo 22:36-39,Yohana 1:11-14,Yohana 1:1-10

 

MCHORO WA UBAYA

 

Mchoro ni ramani inayowekwa kwa makusudi ya jambo Fulani.Michoro hiyo mibaya mara nyingi ni kuleta uharibifu.Wachawi wanatumia sna michoro kwa lengo la kuharibu maisha ya mtu/watu.Kitu chochote unachokiona mwilini kimeanzia kupangwa katika ulimwengu wa roho na likatokea ulimwengu wa mwili

Luka 6:45,mchoro huo uanzia moyoni,Mathayo 12:33,Warumi 12:21,1Samweli 17:28,Yohana 1:11,Zaburi 36:4,Ezekieli 33:19

 

ROHO YA UMASIKINI SI MALI YANGU

Umasikini:Ni uhitaji wa chakula,mavazi na malazi/ni hali ya kupungukiwa .Kuna umasikini wa mtu binafsi na umasikini wan chi.Torati 15:4-8,Mwanzo 13:2,Isaya 45:3,Mithali 19:17,Mithali 29:7,2Wakorintho 8:9,Wagalatia 2:10,Yakobo 1:27

Yesu alikuja kupindua mifumo na taratibu za dunia,unatakiwa uanze kujisemea bila kusema ni sawa na kutokuamini