Thursday, May 15, 2025

ROHO YA UFUKARA

 

ROHO YA UFUKARA

Ufukara ni hali ya kuishi zaidi ya umasikini.Ufukara ni roho inayoishi ndani ya nchi na familia,ukiangalia familia nyingi za Kiafrika na zile nchi zinazoendelea,roho hizi zinaendelea kizazi baada ya kizazi,kutoka ukoo au familia.Mambo waliyoyafanya huko nyuma na vitu hivi vinaenda mpaka kwenye damu,bila kuvunja na kujitenga huwa zinafuatilia.Yeremia 17:5-8

MALI ILIYOFICHWA

Mali ni Baraka.Isaya 45:3

KUFUTA RATIBA ZA KUZIMU

Ratiba ni mpangilio au utaratibu uliowekwa kwa makusudi ya jambo Fulani mfano ratibaza kanisani,ratiba za harusi,ratiba za mikutano,ratiba za nchi,ratiba binafsi

Nuru:Mungu alimwambia atengeneze safina maana ataachilia mvua siku 40 Mwanzo 7:11-12

Ratiba za kishetani/kuzimu ni ratiba anazotumia shetani kwa kutumia mawakala wake,ni namna gani wamuandalie mtu jambo baya,muda,mwezi,tarehe,mwaka,siku huwa wanazingatia vitu hivi.Waamuzi 16:15-17

KUFUTA DAMU ILIYOMWAGWA KWA AJILI YAKO

Damu ya Yesu ilimwagwa kwa ajili ya anguko la dhambi Mwanzo 26:28 na kwenye damu kuna uzima Yohana 6:54-56,Warumi 3:15,Torati 12:23,Zaburi 79:3

ARDHI IKUTAMBUE

Kuna siri kubwa kwenye ardhi (udongo) nchi.Maisha ya mtu yako kwenye ardhi. Mwanzo 2:7,Mwanzo 3:17.Tabu unayopitia inatokana kwenye ardhi Yeremia 22:29-30,Mfalme wa Yuda alionea mgeni,mjane,yatima Isaya 34:9,Ayubu 28:5-6,ufunuo 12:15-16

KUTAMBUA NYAKATI

Nyakati ni mabadiliko ya vipindi

Aina za nyakati Kibiblia

        i.            Wakati wa uumbaji (Adamu)

      ii.            Wakati wa sheria (Musa/Yoshua)

    iii.            Wakati wa Waamuzi (Deborah,Samsoni)

   iv.            Wakati wa Wafalme (Sauli,Daudi)

     v.            Wakati wa Manabii (Isaya,Yeremia)

   vi.            Wakati wa injili ya mbinguni (Yesu)

 vii.            Wakati wa nyakati za Mitume (Paulo,Petro,Mathayo n.k)

viii.            Wakati wa ufunuo na uumbaji Mpya

Mwanzo 1:1----

 

 

WIMBO MPYA

 

WIMBO MPYA

Tunapozungumzia wimbo kiroho ni neno la unabii

Aina za nyimbo kiroho

·        Wimbo wa Musa

·        Wimbo wa Mwanakondoo

·        Wimbo Mpya

1.     Wimbo wa Musa ni unabii wa Agano la kale

2.     Wimbo wa Mwanakondoo ni unabii wa Agano Jipya

3.     Wimbo Mpya ni injili ya milele (Neno lililofunuliwa)

Ufunuo 15:2-4,Ufunuo 14:6-7,Zaburi 119:54,172

MJUMBE WA MUNGU ALIYETUMWA KWAKO

Mjumbe ni mtu anayewakilisha watu wengine kwa shughuli Fulani Marko 1:1-3,Luka 3:4-6,Yeremia 49:14,Malaki 3:1-2,Waebrania 12:2 4 na Yesu mjumbe,Hagai 1:13

NIPE RUHUSA NIENDE

Ruhusa ni maombi au ombi linalofanywa na mtu kuhusiana na jambo Fulani mfano unaomba ruhusa kwenda sehemu Fulani na katika kuomba ruhusa kuna mambo mawili

         i.            Kukubaliwa

       ii.            Kukataliwa

Mwanzo 24:56

Mwanzo 30:25

Kutoka 4:18,Kutoka 7:14,Kutoka 8:1,Kutoka 14:3,Kutoka 14:13

BWANA AKUINULIE USO WAKE

Hesabu 6:22-27

         i.            BWANA akubarikie

       ii.            BWANA akulinde

     iii.            BWANA akuangazie nuru za uso wake

     iv.            BWANA akufadhili

       v.            BWANA akupe amani

KUFUKUA VISIMA VYA BARAKA

Mwanzo 26:25,Mwanzo 26:32,Mwanzo 21:22,Hesabu 21:17

KUFUTA AJALI ILIYOPANGWA JUU YAKO

Isaya 62:10-------

KUONDOA NIRA ZA KISHETANI

Nira ni kifaa ambacho huvikwa shingoni mwa mnyama.mfano ng’ombe,punda,farasi n.k kwa kusudi la kuvuta mzigo uliyo nyuma yake.Nira huwa na lijamu na hatamu ili kuweza kumuongoza mnyama njia ambayo mtu wake amekusudia kupita

Lijamu ni kifaa ambacho hufungwa mdomoni

Hatamu ni kamba ambazo zimefungwa kwenye lijamu ili kumwongoza mnyama kwa mwendo anaotaka Mathayo 11:27-30,Isaya 10:27

ATA WAKUZUIE VIPI UTAVUKA TU

 

ATA WAKUZUIE VIPI UTAVUKA TU

Katika maisha tunayoishi kuna mambo mengi,ambayo yanafanyika sirini juu ya mtu Fulani ili aharibikiwe.Na katika kukuharibia huko wanaana na kukuzuia kwamba usipenye,usivuke,uziende,usipite.Kutoka 14:15-16

Walivuka bahari ya shamu (Red sea-bahari nyekundu) Mathayo 14:22,Marko 4:35,Torati 9:1 ukivuka utamiliki, Matendo 16:9 Paulo aliona maono avuke akawasaidie watu

VITA YA KIUCHUMI

Uchumi ni jumla ya shughuli za watu zenye lengo la kutosheleza mahitaji mfano uzalishaji,matumizi ya bidhaa,usambazaji.

Uchumi ni rasilimali ni namna gani unaweza kuzitumia mfano ardhi,elimu,kipaji 2Wakoritho 8:9

Yesu alikuja ili awaokoe watu kiroho na kimwili kutoka kwenye umasikini Mwanzo 12:16,Mwanzo 13:2,Mwanzo 13:2,Mwanzo 26:12-14,Torati 8:17-20,8:1-16,Matendo 12:21-23,Ayubu 1:1-------,Ayubu 42:10-----

Kanuni ya uchumi

·        Kufanya kazi

·        Kuwa na maarifa

·        Kuwa na bidii

·        Kuweka akiba

·        Utoaji

·        Usishindane (usiige)

PINDUA MEZA

Pindua maana yake ni kuharibu.1Wakoritho 10:21,2Wakoritho 6:16,Waamuzi 1:6-7

MIKONO YA KUZIMU

Zaburi 49:15,Mithali 5:5,Isaya 28:15,Matendo 2:27

MUNGU ATIMIZE NENO LAKE

Neno la Mungu lina nguvu,mamlaka uweza,ni moto,nyundo,upanga Yeremia 1:11-12,Isaya 38:6-7

KUHESHIMISHWA NA MUNGU

Matendo 4:13,Yohana 12:26

BWANA YESU AIAMURU BARAKA IJE KWANGU

Torati 28:8,Hagai 2:8

BWANA NI NURU YANGU

Zaburi 27:1-5,Zaburi 27:10-14

MTAABISHAJI WA MAISHA YAKO

Mtaabishajilinatokana na neno taabika

FIMBO YA MUNGU

 

FIMBO YA MUNGU

Fimbo ni kifaa kinachotumika katika kutegemea mfano wapanda milima huwa wanatumia fimbo kama kitegemezi ambacho kinawarahisishia kupanda mlima vizuri.

Fimbo kiroho ni mtu aliye na neno la Mungu ambalo linaweza likamsaidia kwenye utegemezi.Kutoka 17:9---,Zaburi 2:8-9,Mithali 22:15,Mithali 23:13-14,Waebrania 1:7-8.Yesu Kristo ni fimbo tembelea

KUONDOA NGUVU YA KABURI YA KISHETANI

Hosea 13:14,Zaburi 49:15,Zaburi 6:5

KUWAANGAMIZA WATAABISHAJI WETU

Mtaabishaji linatokana na neno taabika.Mtaabishaji ni mtu anayeumiza,teas,haribu,anayekukosesha amani,raha n.k anataabisha kazi,ndoa,biashara,masomo na elimu,watoto,huduma n.k 1Wafalme 18:13-40.Omri alikuwa ni Jemedari wa jeshi alitawala Israeli,baada ya kufa akashikilia motto wake Ahabu ambaye alitawala miaka 22 wakati wa kipindi cha mfalme Asa.Baadaye alimuoa Yezebeli binti Ethbaali mfalme wa Sidoni.

Ahabu alifanya mabaya machoni pa Mungu alimjengea baali madhabahu na Ashera.1Wafalme 19:15-17,2Wafalme 10:18-28

Maombi

-kuwakusanya wataabishaji

-kuwapiga wataabishaji

KUONDOA ROHO ZA MAGONJWA

Kutoka 23:25,Kutoka 7:15,2Wafalme 1:2,Mathayo 4:23

UTAITWA MBARIKIWA

Mbarikiwa ni mtu aliye na Baraka/aliyepata Baraka (mafanikio) mfano fedha,ndoa,elimu,kazi,afya njema,mali,ustawi n.k Luka 1:42-48,Luka 1:49-50,Luka 1:26-41,Luka 3:3-6

SIRI YA MAOMBI

2Wafalme 20:3-9,Zaburi 54:2

KUMFUNGA MKUU WA KUZIMU

Ufunuo 20:1-10,Mathayo 16:19

KILA ULITENDALO LITAFANIKIWA

Zaburi 1:1-3,Isaya 55:11,Torati 6:3,Torati 6:18,Torati 12:28,Yoshua 1:7,1Wafalme 2:3,Ayubu 12:16,Zaburi 122:7

UTAPATA SHANGWE NA FURAHA

Isaya 51:11,Zaburi 126:5,Isaya 25:8

UPEPO WA UHARIBIFU

Upepo ni hali Fulani isiyoweza kuonekana wala kushikika.Yohana 3:8,Mhubiri 11:5,Marko 4:35-41

UZIMA NDANI YAKO

1Yohana 5:11-14,Mathayo 7:7----

YESU NI MWAMINIFU

1Wathesalonike 5:16----

NURU IMEWAANGAZA

Isaya 9:1-7

KUWA JUU YA FALME

Yeremia 1:4----

Maana yake Mungu amekuumba kwa makusudi,kuna kusudi juu yako ,atakupa na kazi ya kufanya.

NAIENDEA NCHI YENYE MAZIWA NA ASALI

Maana yake ni kumiliki mafanikio,Hesabu 13:25-33,Hesabu 14:1-9,Torati 1:21,Yoshua 1:3-9,Yoshua 2:24

UTUMISHI (MTUMISHI)

Utumishi ni uwezo wa kutumika kwa ajili yaw engine

Mtumishi ni mtu anayetumika kwa ajili yaw engine au kuwa mtumwa kwa wengine.Marko 10:42-45,Luka 22:24-27,Yohana 31:12-16,1Petro 5:2-6

Kanuni za utumishi (mtumishi)

·        Mnyenyekevu na mpole Mathayo 11:29

·        Mwenye heshima 1Petro 3:7

·        Mwenye Roho Mtakatifu Matendo 2:4

·        Anauwezo wa kufundisha na mvumilivu 2Timotheo 2:24-26

·        Mtii Waefeso 6:5

·        Mwaminifu na mwenye imani Luka 16:10,Waebrania 11:29

KUSAMBARATISHA UCHAWI NA UGANGA WA KIENYEJI

 

KUSAMBARATISHA UCHAWI NA UGANGA WA KIENYEJI

Uchawi:Ni nguvu zinazotumiwa na watu kwa nia ya uharibifu.Kuna uchawi mweupe na kuna uchawi mweusi

Uganga:Ni elimu ya kichawi inayohusiana na magonjwa

Ucawi na uganga ni kampuni moja ila sekta tofauti mfano jeshi.Uchawi na uganga lengo lao ni kuwatesa watu Isaya 47:12,Mika 5:12,Walawi 26:31,Torati 18:9-13,Kutoka 7:22,2Wafalme 21:6,2Nyakati 33:6

MOTO WA MADHABAHU

Madhabahu:Ni sehemu ambayo roho kwa roho hukutana au zinakutana.Ni mahakama ya kiroho ambapo kesi za kiroho zinaletwa na kutolewa hukumu Ufunuo 8:3-5,Ufunuo 5:8,Luka 12:49

 Chetezo ni mtu

Moto ni (neno,kuchoma) kufanya maombi

Moshi wa uvumba ni sauti ya maombi

Uvumba ni maombi

KUONDOA ROHO ZA ULEMAVU KATIKA MAISHA YETU

Ulemavu:Ni hali ya kutokuwa na nguvu au upungufu wa viungo au kutokuwa katika hali ya utimilifu

Aina za ulemavu

-kuna ulemavu wa kiroho

-kuna ulemavu wa kimwili

Matendo 3;1-2,Matendo 3:3-7,Matendo 3:8-10,Matendo 3:11-16

WANA NI URITHI

Zaburi 127:3,Torati 28:4,11

Wana ni watoto,kwa wanawake wao ndiyo wanaobeba watoto.Muunganiko anaoufanya Mungu ni wa ajabu sana,sisi binadamu tunatumika kama kiwanda cha uzalishaji (production)

NITAKUWA UKUTA WA MOTO

Ukuta ni kitu Fulani kinachojengwa ili kuzuia vitu Fulani visipite au kuingia kwa urahisi Zekaria 2:4-5,Isaya 4:5,Waebrania 1:7

KUFUTA KURASA MBAYA ZA ZAMANI

Kurasa ni sura za kwenye kitabu zikiwa na maana Fulani 2Wakorintho 5:17,2Wakoritho 5:18-19,2Wakorintho 5:20-21

KUKATAA SIKU ZA KUCHOKESHA

 

KUKATAA SIKU ZA KUCHOKESHA

Kuchokesha linatokana na neon kuchoka.Kuchoka maana yake ni kukata tama kwenye ndoa,kwenye kazi,kwenye biashara,kwenye huduma,kwenye maisha,kwenye mashamba n.k Ayubu 7:3-4,Ayubu 3:1-----Ayubu 42:1-----,Ayubu 42:16

KUHARIBU MAFURIKO YA MAUTI

Mauti:Ni roho inayoharibu jambo Fulani,roho hii inaweza kutembea,kukaa,kuishi sehemu mbalimbali. 2Samweli 22:5-8,Zaburi 9:13,Zaburi 78:50,Zaburi 23:4,2Wafalme 4:40

WALIOMPOKEA ALIWAPA UWEZO

Yohana 1:11-14,1Yohana 5:6-12

Washuhudiao Mbinguni

·        Mungu

·        Neon (Yesu)

·        Roho Mtakatifu

Washuhudiao duniani

·        Roho –mtu

·        Maji –ubatizo

·        Damu –ukombozi/utakaso

KUMILIKI MILANGO YA BARAKA ALIYOKUWA AMEISHIKILIA ADUI

Mlango:Ni kifaa kinachotumika kwa ajili ya kuingia na kutoka.Utabarikiwa uingiapo na utokapo Torati 28:6,Isaya 60:11,Mwanzo 22:17,Ufunuo 3:8 kumtoa aliyekuwa kwenye mlango wa Baraka.Nyumba ni kama ulimwengu,kiti ni kama Baraka yako.

PASAKA (PASSOVER)

Pita juu ya.Ni sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu.Kutoka 12:27,Mathayo 26:17,Luka 22:1, 1Wakorintho 5:7

UFALME WAKO UJE

Mathayo 6:9-13,Kutoka 19:5-6,Zaburi 103:19,Mhubiri 4:14,Matendo 8:12,Matendo 28:31,Mathayo 7:21,Luka 4:43

UWE NA MOYO WA USHUJAA

YOSHUA 1:5-9

YESU APELEKWA MBELE YA PILATO

Mathayo 27:1-2,Mathayo 27:11-18

BWANA MUNGU AKUONGOZE NJIA

Mwanzo 24:24

 

MAUTI ILIYOPANDWA

Ufunuo 6:8

BWANA NI MTU WA VITA

Kutoka 15:3-8,Kutoka 15:1-2,Yoshua 17:1

KUOMBA KWAKO KUMESIKIWA

Matendo 10:31

KUVUNJA ROHO YA KIUME KWA MWANAMKE NA ROHO YA KIKE KWA MWANAUME

Walawi 17:7

UNAPOINGIA KWENYE MAOMBI SAMEHE

Mathayo 6:14-15,Isaya 59:1-4

WALIOKUTENGENEZEA ULIE

Zaburi 69:1-3,Zaburi 69:6,Isaya 65:19,1Samweli 30:4,Waamuzi 21:2

TWENDE NG’AMBO

Marko 4:35-41,Marko 5:1----,Yoshua 9:1

KAZA MWANDO

Wafilipi 3:12-14

BIBLIA NI AGANO

 

BIBLIA NI AGANO

Maana ya Biblia:Ni agano kati ya Mungu na wanadamu

Muundo wa Biblia

·        Ina vitabu 66

·        Ina sura 1186

·        Ina mistari 31101

Mgawanyo wa Biblia

1.     Agano la kale lina vitabu 39,lina sura 929,lina mistari 23144,yaani kutoka kitabu cha Mwanzo hadi Malaki.Kiunganishi hapa alikuwa ni Musa

2.     Agano jipya lina vitabu 27,lina sura 260,lina mistari 7959,yaani kutoka kitabu cha Mthayo hadi Ufunuo na kiunganishi hapa ni Yeshu Kristo

Lengo la Agano

        i.            Ni kupata Baraka

      ii.            Ni kuwa mwaminifu

    iii.            Kutimiza ahadi yake

Kazi ya Mungu ni kuchagua wajibu wa mteule ni kutunza Agano

Mashariti ya Agano

        i.            Mlengwa

      ii.            Madhumuni/yaliyomo

    iii.            Muda

   iv.            Matokeo

Kwenye Agano kuna sheria

Kutoka 19:5-6,Kutoka 28:1-14(matokeo),Kutoka 20:1----,Waebrania 9:28,Mathayo 22:36-39,Yohana 1:11-14,Yohana 1:1-10

 

MCHORO WA UBAYA

 

Mchoro ni ramani inayowekwa kwa makusudi ya jambo Fulani.Michoro hiyo mibaya mara nyingi ni kuleta uharibifu.Wachawi wanatumia sna michoro kwa lengo la kuharibu maisha ya mtu/watu.Kitu chochote unachokiona mwilini kimeanzia kupangwa katika ulimwengu wa roho na likatokea ulimwengu wa mwili

Luka 6:45,mchoro huo uanzia moyoni,Mathayo 12:33,Warumi 12:21,1Samweli 17:28,Yohana 1:11,Zaburi 36:4,Ezekieli 33:19

 

ROHO YA UMASIKINI SI MALI YANGU

Umasikini:Ni uhitaji wa chakula,mavazi na malazi/ni hali ya kupungukiwa .Kuna umasikini wa mtu binafsi na umasikini wan chi.Torati 15:4-8,Mwanzo 13:2,Isaya 45:3,Mithali 19:17,Mithali 29:7,2Wakorintho 8:9,Wagalatia 2:10,Yakobo 1:27

Yesu alikuja kupindua mifumo na taratibu za dunia,unatakiwa uanze kujisemea bila kusema ni sawa na kutokuamini

FUNZA WA KIROHO

 

FUNZA WA KIROHO

Katika maisha kuna funza wapo wa kiroho ambao wanatesa maisha yako bila kujua,iwe kwenye uchumi,ndoa,familia,huduma,biashara,kazi n.k.anaweza kuingia na kuleta uharibifu katika maisha yako.

·        Anaweza akakuletea mateso na kila aina ya uharibifu,Isaya 14:11,Isaya 51:8,Marko 9:44

·        Ili adui atomize mpango wake anaandaa njama au mpango Danieli 6:3-4,Danieli 3:4-6,Danieli 3:28---- Shadraka,Meshaki na Abednego

 

ROHO WA MUNGU ATULIE JUU YAKO

Roho wa Mungu

Ø Nafsi ya Mungu

v Mungu Baba

v Mungu Mwana

v Mungu Roho Mtakatifu

1Yohana 5:7-9,Mwanzo 1:1--,Mwanzo 2:1-6,Zaburi 67:1---,Zaburi 65:9

 

CHACHU YA KIROHO

Chachu ni kitu kinachoweza kubadilisha kitu.

Maana kiroho:chachu ni mafundisho (maneno/neon) yanayoweza kubadilisha moyo na roho ya mtu, Mathayo 13:33

Ø Chachu-mafundisho

Ø Mwanamke-mchungaji

Ø Unga-moyo (mtu)

Mathayo 16:5-12

Aina za chachu

Ø Chachu ya Mungu yaani ya kweli

Ø Chachu ya shetani yaani uongo

Wagalatia 4:19 Kristo aumbike

1Wakorintho 5:6-8,Waefeso 4:21-24

 

BWANA AKUANGAZIE NURU ZA USO WAKE

Hesabu 6:22-27

Zaburi 4:6

Zaburi 31:16

Isaya 60:1-2

Isaya 58:8

 

KUFUTA RAMANI ZA UBAYA

Ramani ni mchoro unaoonyesha mfano wa kitu Fulani.Kuna wachoraji,kuna vipimo vyake,mipaka unapotaka kujenga nyumba lazima mchoro uwepo

Kila kitu unachokiona kiwe kizuri au kibaya kimeanzia rohoni Luka 6:45-49.Ubaya wowote unaopangwa unakuwa na ramani zake,ubaya unachorwa.Mathayo 12:33 wachawi wanakuchorea mchoro wa magonjwa,umasikini,matatizo,mauti, n.k

Ø Kuna mafundi wa ujenzi

Ø Kuna misingi na nguzo

Ø Wachora ramani

Ø Kuna wasimamizi wa ujenzi

Hapa namaanisha rohoni na kama vile katika ulimwengu wa kimwili na kiroho vile vile mambo haya yapo.

Hebu sasa anza kuchora/kujichorea michoro mizuri na kuifuta michoro mibaya

Chora michoro ya Baraka na mafanikio

 

MUNGU AKUZIDISHE NA KUKUONGEZA

Mwanzo 28:1-4,

Mwanzo 28:12----

Mwanzo 28:20-----

Mwanzo 32:24------

Torati 28:1-14

Saturday, May 10, 2025

NAWAPENDA WALE WANIPENDAO

 *🌲KAMA NINGALIWAZA MAOVU MOYONI MWANGU,BWANA ASINGESIKIA, HAKIKA MUNGU AMESIKIA; AMEISIKILIZA SAUTI YA MAOMBI YANGU. Zaburi 66:18-19🌲.Ee  Yehova Mungu Muumba wetu, Kwa mkono wako hodari, Umeiamuru tena ipambazuke asubuhi nyingine mpya siku  ya Ijumaa ya kwanza  ya  mwezi, tarehe mbili May 2025. Hii ikiwa ni weekend  ya kwanza ya mwezi May🌲🌲.Ee Baba yetu, tunazo sababu zote za kukurudishia wewe, shukurani, sifa na utukufu  kwa ulinzi ulio tupatia usiku kucha, hata asubuhi hii ya pili ya mwezi. Baba, kwa Roho wako Mtakatifu, utuongoze tena katika ibada zetu za maombi na maombezi ya ijumaa ya kwanza mbele yetu zikisalia siku 243 kabla  ya kuumaliza  mwaka huu wa 2025💫.Baba tupe kulitunza neno lako mioyoni mwetu ili tusipate kuwaza maovu ambayo huzuia usitusikie tukuombapo. Baba yetu, endelea kutuepusha na majanga mbali mbali nchini mwetu, zikiwemo ajali mbaya na nyingi zinazo tokea kila uchao. Pia uendelee  kutupatia  mvua za utulivu zenye neema ya chakula🌽🌾🌻🥔 . Mwisho kwa wale wote wanao safiri leo kwa njia mbalimbali, uwaongoze kwa Mkono wako hodari ili wafike salama kule waendako. Kwa machache haya na yale yote ambayo sijayatamka  twakuomba ututendee yote kwa  jina la Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu Aamin

*🌲NAWAPENDA WALE WANIPENDAO, NA WALE WANITAFUTAO KWA BIDII WATANIONA. Mithali 8:17🌲.Ee Yehova El-Shadai, Mungu wetu Muumba wa Mbingu na nchi uishiye milele. Umetupatia tena  siku mpya ya jumamosi ya pili  ya mwezi, tarehe kumi May 2025 🌲🌲.Ee Baba yetu , pokea shukurani zetu za dhati na adhama, Sifa na Utukufu wewe peke yako, kwa ulinzi uliotufanyia usiku kucha hata  tumeiona siku ya kumi ya mwezi . Ee Baba twakuomba kwa Roho wako Mtakatifu, utuongoze  tena weekend hii ya pili ya May tunapokabili majukumu yetu, pamoja na maandalio ya mioyo yetu kwa ajili ya ibada  za kesho siku ya jumapili ya  pili ya May, tutakapoingia ibadani ili kulihimidi jina  lako na kukuabudu kwa furaha, na kukutafuta uso wako kwa bidii ili ujifunue kwetu wewe pekee uliye kimbilio na nguvu na msaada uonekanao tele wakati wa mateso, mbele yetu zikiwa zimesalia siku 235 ili kuufikia mwisho wa mwaka huu wa 2025 💫. Baba yetu, endelea kutuepusha na majanga mbali mbali, kama ajali zinazo tokea mara kwa mara na kuchukua uhai wa ndugu zetu. Baba yetu, tunakushukuru sana pia kwa ajili ya mvua ambazo  zimenyesha vizuri sana, na sasa huku kwetu tayari tumeanza kuvuna 🌽🥔🌾🌻. Ee Baba yetu, tunawaleta kwako wale wote wanao safiri leo kwa njia mbalimbali, uwaongoze kwa Mkono wako hodari ili wafike salama kule waendako. Kwa machache haya, na yale yote ambayo sijayatamka,  twakuomba ututendee yote kwa  jina la Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu Aamin* 

NJIA NNE ZA MAPATO KWENYE SARAFU ZA KIDIGITALI

 NJIA NNE ZA MAPATO KWENYE SARAFU ZA KIDIGITALI.

1. MINING hii inahusisha kushiriki katika kujikusanyia sarafu wakati wa hatua za mwanzo, Mara nyingi Huwa ni kabla sarafu husika haijaenda sokoni. Mfano pi coin,Ai coin, cpen, delta, etc

2. TRADING.Hii inahusisha kununua sarafu sokoni Kwa bei ya chini na kuuza Kwa bei ya juu na kupata FAIDA. 

3. HOLDING. Hii inahusisha kununua sarafu na kukaa nazo Kwa muda mrefu kama miezi 6, MIAKA 2... Ambapo sarafu hiyo inakuwa imepanda bei sana na hapo watu hutajirika.

4. STAKING. Hii huhusisha kufungia sarafu kwenye block chain Kwa muda Fulani Ili kuongeza ulinzi kwenye Blockchain, aliyefungia pesa zake kwenye Blockchain hupata FAIDA iliyokubaliwa kila siku Kwa muda wa mkataba.

CRYPTEX imekuja kitofauti baada ya kuingia ubia na kampuni za bima na mabenki , Ili kumsaidia mtu kupewa mkopo mkubwa bila dhamana Ili FAIDA inayozalishwa kila siku iwe kubwa Kwa muda utakao chagua.

Baada ya MIAKA 3 unapata milioni 97. Na hii ndio nguvu ya kutumia pesa za watu wengine kutajirika.

Pi network future boom in the world

 Pi Network Yaingia Kati ya Programu 6 Zinazotrendi Zaidi nchini Finland

Katika dunia ambayo Instagram, TikTok na Facebook zinatawala kila skrini ya simu, jambo la kushangaza limetokea nchini Finland. Programu mpya iitwayo Pi Network imepanda hadi nafasi ya 6 katika orodha ya programu maarufu zaidi za kijamii (bila malipo). Na jambo la kushangaza zaidi ni kwamba, hii si programu ya kawaida ya mitandao ya kijamii.

Je, Pi Network ni nini – na kwa nini inazidi kuwa maarufu?

Yote Kuhusu Pi Network

Pi ni mradi unaoendeshwa na watu, si mashirika makubwa. Umejengwa juu ya wazo kuwa kila mtu, popote alipo na kazi yoyote aliyonayo, anapaswa kupata nafasi ya kushiriki katika uchumi mpya wa kidijitali.

Pi inawawezesha watumiaji kuchimba (mine) sarafu ya kidijitali kwa kutumia simu zao, kujenga jumuiya, na kushiriki katika mtandao wa kimataifa unaolenga ugatuaji wa mamlaka (decentralization) na umiliki wa kweli wa mali ya kidijitali.

Kwa programu ya blockchain kuweza kuvunja ukuta katika eneo linalotawaliwa na kampuni kubwa za teknolojia za mabilioni ya dola ni jambo kubwa. Lakini Pi Network si kama programu nyingine za mitandao ya kijamii zinazozingatia “likes” na “shares”—badala yake, inawapa watumiaji thamani halisi, yaani, Pi coins, kwa kuingia kila siku na kubonyeza kitufe cha “mine”.Nafasi ya Pi Network kwenye Chati ya Finland ni Zaidi ya Nambari.Kinachofanya wakati huu kuwa wa kipekee si umaarufu wa muda mfupi.

Kupanda kwa Pi Network nchini Finland si kuhusu tu idadi ya watu wanaopakua programu—bali inaonyesha mabadiliko ya namna watu wanavyoona zana za kidijitali. Watu wengi sasa wanaanza kuamini programu za blockchain—si kwa burudani tu—bali kwa fursa za kifedha za baadaye.

Kupaa kwa programu kwenye chati ni kiashiria cha hamasa halisi kutoka kwa watu halisi wa Finland. Maelfu wanapakua na kutumia programu ya Pi, si kwa ajili ya kuchat au kupakia picha, bali kuwa sehemu ya mtandao unaorudisha thamani kwa jamii yake.

Na hii ni mwanzo tu. Mafanikio ya programu hiyo nchini Finland yanaweza kuwa ishara ya kile kitakachotokea katika maeneo mengine duniani.Pi Network Tayari kwa Consensus 2025.Na sasa mambo yanazidi kusisimua.

Katika muda wa siku 4 tu zijazo, mkutano mkubwa wa blockchain wa Consensus 2025 utaanza Toronto, mojawapo ya matukio makubwa zaidi ya blockchain duniani. Wengi katika jumuiya ya Pi wanaamini kuwa tukio hili linaweza kuleta taarifa kubwa kutoka kwa timu ya msingi ya Pi.

Hii ni kwa sababu Dkt. Nicolas Kokkalis, mwanzilishi wa Pi Network, anatarajiwa kutoa hotuba katika mkutano huo. Kwa macho yote yakielekezwa kwake, watu wana matumaini kuwa atatangaza habari kubwa kuhusu mustakabali wa Pi, hasa uzinduzi rasmi wa mainnet ambao umekuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu.

Tuesday, May 6, 2025

DHABIHU ZA MUNGU BABA

 DHABIHU ZA MUNGU NI ROHO ILIYOVUNJIKA; MOYO ULIOVUNJIKA NA KUPONDEKA, EE MUNGU, HUTAUDHARAU.. Zaburi 51:17.  Ee Yehova El-Shadai, Mungu Muumba wetu, wewe Utabaki kuwa Mungu wa pekee milele kwetu Ee Baba yetu. Tazama umeiamuru ipambazuke asubuhi nyingine mpya, siku ya jumanne ya kwanza ya mwezi, tarehe  sita May 2025 mbele yetu zikisalia siku 239  kabla ya kufikia mwisho wa mwaka huu wa 2025. Baba yetu, pokea  shukurani zetu za dhati ya moyo wa ndani wewe peke yako, kwa matendo makuu uliyotufanyia usiku kucha, macho yako yakitutazama  mpaka asubuhi hii ya sita ya mwezi May. Baba si kwa uwezo wetu, au stahili yetu, la hasha, bali ni kwa neema na rehema zako tu, kwani kuna wenzetu wengi tuliokuwa nao siku ya kwanza ya mwezi huu, leo hii hatunao tena, kwani  wametoweka,tena wengine kwa vifo vya ghafla, na bila tumaini la uzima wa milele. Ee Yehova,  twajikabidhi  mikononi mwako tena leo, ili utuongoze  tunapo kabili majukumu yetu pamoja na ibada za baadaye leo jioni. Baba yetu, tuondolee kiburi , na utujalie moyo wa kuvunjika na kupondeka kwa kunyenyekea kwako, na iliyo tayari kufuata maagizo yako. Pia uzidi kututetea na kutuponya na majanga mbali mbali nchini mwetu , zikiwemo ajali na magonjwa mengi ya milipuko. Zaidi sana Ee Mola wetu, tunakushukuru  kwa ajili ya mvua ambazo zimenyesha kwa utulivu, na sasa tumeanza kuvuna. Na kwa wale wote wanao safiri leo kwa njia ya anga, ardhini na majini, twakusihi utuongoze kwa mkono wako hodari ili tufike salama kule tuendako . Kwa machache haya, hata yale ambayo sijayatamka, twakuomba ututendee yote  kwa jina la Yesu Kristo  Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu.


BARAKA ZA MWEZI WA TANO

 BARAKA ZA  MWEZI TANO

1. Mbingu zako ziwe wazi mwezi huu, Ufurahie baraka toka kwa Bwana kila Eneo la Maisha yako.

2. Malango ya kubarikiwa kwako mwezi huu yawe Wazi daima usiku na mchana.

3. Mwezi Mei na Uwe wa habari njema kwako, kwa Uwekezaji wako na Familia.

4. Na uwe mwezi wa hatua mpya na za utukufu kwenye projects zako na biashara .

5. Mwezi Mei ni mwezi wa Shuhuda Mpya na za Utukufu kwako. Naamuru Shuhuda Mpya zichipuke .

6. Mungu na akupe Amani mwezi huu, kwenye Ndoa na Ajira na Biashara

7. Kama kuna kitu chema kilikufa kwa hatima yako Mwezi kifufuke.

8. Na huu uwe mwezi wako wa Mipenyo na fursa mpya kwako, kwenye hatima yako kitaifa na kimataifa, MACHO YAKO YATIWE NURU UONE FURSA ZAKO MWEZI HUU.

9. Na huu uwe mwezi wa Amani, Furaha na kicheko kila Eneo. 

10. Mungu na AKUEPUSHE na hasara na kuharibiwa mwezi huu.  Na ulindwe na kuepushwa na maovu yote. 

11. Ninakuunganisha na masaa yako ya Mpenyo mwezi huu.

12. Ninakutuma Ukafanikiwe na Kustawi kila Eneo mwezi huu, Ninakutuma Ukamiliki na Kuongezeka mwezi huu kwa ajili ya Kristo Yesu .

NA HAKIKA HUU NI MWEZI WAKO WA VIWANGO VIPYA NA MIPENYO MIPYA,

KTK JINA LA YESU