MUHIMU SANA KWA KILA MTUMISHI ALIYEONDOKA KATIKA HUDUMA FULANI.
Kwanza itambulike kuwa kutoka huduma moja kwenda huduma nyingine, sio dhambi wala tatizo,tatizo linaweza kutokea katika namna ya kuondoka.
Baadhi yetu wahudumu wa injili(nikiwemo mimi) tumetokea(tulikuzwa na kulelewa) katika huduma nyingine, na sasa tupo katika huduma nyingine. Hili sio tatizo, tatizo tuliondokaje kule?
Swali la muhimu la kujiuliza kila Mtumishi wa MUNGU aliyeondoka huduma fulani, "NILIONDOKAJE KWENYE HUDUMA ILE?" Je! Niliondoka kwa dhamira njema au mbaya? Nini kilipelekea kuondoka kwangu katika huduma ile? Na maswali mengine Kama hayo kila aliyeondoka katika huduma anapaswa kuwa na majibu yake.
NDUGU MTUMISHI WA MUNGU.
Ikiwa uliondoka katika huduma fulani na moyo wako unatambua kuwa ULIONDOKA VIBAYA, na Roho Mtakatifu amekuwa akisema na wewe kuwa ULIONDOKA VIBAYA KATIKA HUDUMA FULANI, fanya haya;
1:- RUDI MBELE ZA MUNGU KWA TOBA.
Mungu ni MUNGU anayerehemu kwa kila aliyejitambua kuwa anahitaji huruma zake. MUNGU si MUNGU wa machafuko, ikiwa umeondoka kwa namna ya ouvu/ubaya...hatatembea katika ule mtembeo wake dhidi ya utumishi na huduma uliyobeba.
Msingi wa huduma yenye matokeo ni kuwa na Ushirika usiotiliwa shaka na Mungu kwanza. Tutafuteni Ufalme wa MBINGUNI kwanza na haki yake, na hayo mengine tutazidishiwa..... mafanikio tunayoyataka kwenye huduma ni mengineyo.......msingi ni MUNGU KWANZA.
2:- RUDI KWA KIONGOZI WA HUDUMA ULIYOONDOKA, MUOMBE MSAMAHA ILI MOYO WAKE UKUBARIKI.
Ni tendo la baraka kupata baraka ya kihuduma/utumishi kutoka kwa kiongozi/Mtumishi wa MUNGU ambaye aliyewekeza Imani, gharama na muda wake.
Ni hatari kutumika huku aliyefanyika Baraka ya Utumishi wako kutambulika akiwa mwenye huzuni/uchungu moyoni dhidi ya utumishi wako(wangu).....kwa sababu ya kumlipa mabaya badala ya mema.
Wahenga walisema "Muungwana akikosea, huchutama". Tutafute kwa BIDII kuwa na Amani na watu wote ....Baraka nyingine zipo mikononi mwa watu.
KUMBUKA.
1:- Kujua kupangilia masomo/mahubiri haiwezi kuwa chanzo cha kufanikiwa kihuduma......mkono wa Bwana MUNGU unahitajika zaidi.
2:- Kuna ugumu Mtumishi wa MUNGU anaweza kukutana nao kwenye Utumishi wake kwa sababu ya msingi uliojenga huduma yake.
Fikiria......!
Mtumishi wa MUNGU ambaye alikataa maonyo katika huduma fulani na akaamua kuondoka....atawezaje yeye kusikilizwa katika kuonya kwake? Imeandikwa "Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho atakachovuna".
Kama mtu amekataa kuonywa...hana mamlaka ya kuonya wengine, na hata akiwaonya ....hatasikilizwa.
3:- Tunahitaji matamko ya viongozi wetu katika huduma ili tuweze kuvuka/kupata mpenyo zaidi.
Ni ukweli usiotiliwa shaka kuwa MUNGU ndiye huachilia mpenyo....lakini watumishi wake hiyo Neema ameichilia ndani yao. Wakitamka Neno huwa!
USIENDELEE KUPAMBANA KIHUDUMA, RUDI UKATENGENEZE ILI UENDELEE KATIKA BARAKA.
Ukiondoka mahali kwa ugomvi,vurugu na Mambo yote yasiyompendeza Bwana MUNGU.... shetani anapata uhalali wa kukushambulia. Wala usimpe nafasi ibilisi, rudi katengeneze.Katika kurudi kwako unapaswa kwanza umuulize Mungu maana wengine Ni hatari wanaweza wakakufanyia mabaya.Heshimu watu Ila usiamini watu.Wengi walipoteza maisha yao baada ya kuona Kama alikosea baadae hatari ilimpata.Ni vizuri zaidi ukatengeneza na Mungu Kama huyo mtumishi unajua alivyo.Kama anakuombea mabaya,anakuwazia mabaya na kutamka babaya juu yako mkwepe Sana,watumishi wa Mungu wengi wao Ni wivu unawasumbua na kumbuka wivu Ni uchawi.