KUEPUKA
UZINZI, NA UASHERATI NDANI YA WOKOVU.
Uzinzi: Ni kitendo cha
mume au mke kutoka nje ya ndoa yake na kuwa na mahusianoya kimapenzi na
mwanamke au mwanaume mwingine (kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa) Mungu
anatukataza kwamba tusizini .
“Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine
naam yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye na mwanamke hakika
watanawa”. Walawi 20:10
Usilale na mke wa
mwenzio ukajitia unajisi naye.Walawi 18 :20
Uasherati: Ni kitendo cha
watu wasio olewa au kuoa ambaye atafanya mapenzi kabla ya ndoa. Mungu anakataza
sana.
“mtu yeyote wa kwenu asimkaribie
mwenziwe alie wa jamaa yake wa karibu ili kumfunua utupu mimi ndimi BWANA”. Walawi 18:6
Kwa hiyo utaona ukisoma kitabu cha mambo ya walawi sura ya 18:1-23na 20:1-21 Mungu anavyokemea uzinzi na uasherati kwa nguvu zote, kwa kufafanua kwa uwazi. Ndani ya kanisa na nje ya kanisa tunatakiwa kuikimbia zinaa kwa nguvu zetu zote, maana sisi ni hekalu laMungu lazima mipaka (kujiwekea mipaka) kwa jinsia tofauti ili kuepuka uzinzi na uasherati kwetu. Kweli tumeokoka na tutaenda mbinguni.
Lakini kama hatutaitiisha miili yetu kwa
uzinzi na uasherati hatutaenda mbinguni. Kijana wa kiume na wakike mnatakiwa
kujilinda na kujichunga )sio vijana tu na watu wote) maana uzinzi na uasherati
hauchagui umri usiseme mimi ni mwombaji
sana na ninaupako sana lakini bila kuwa makini unaweza kuangukia huko.
MAMBO
YA KUFANYA KUEPUKA UZINZI NA UASHERATI
1.
Kuwa muombaji:
Unapokuwa muombaji mbele za Mungu
inasaidia kuepuka usiingie kwenye majaribu au jaribu la uzinzi.
“Kesheni mwombe msije mkaingia
majaribuni roho i radhi lakini mwili ni dhaifu” Mathayo.
2.
Kuepuka
mazingira hatarishi.
Ukishaona mazingira uliopo ni ya
hatarishi yananukia uzinzi au uasherati kimbia, Mfano:ukishaona mtu
anakuonyesha dalili hizo usiseme mtaomba cha kufanya kimbia.
“Ikimbieni zinaa kila dhambi aitendayo
mwanadamu ni nje ya mwili wake ili yeye afanyae zinaa hutenda dhambi juu ya
mwili wake mwenyewe”. 1 Wakoritho 6:18
3.
Jiepushe na
mavazi ya kikahaba:
Kimsingi shetani yupo na anatenda kazi
wewe mwanamke na mwanaume jiepusheni kuvaa mavazi yasio mpendeza Mungu(yasiyo
na utukufu wa Mungu). Mavazi hayo yanachochea uzinzi na uasherati kwa watu.
“Je humjui ya kuwa miili yenu ni viungo
vya kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha”
1Wakoritho 6:15
4.
Kuwa na hofu ya
Mungu:
Unapo kuwa na hofu ya Mungu, itakusaidia
sana utajua kama utatenda uzinzi au uasherati
utakuwa unamkosea Mungu aliekuokoa, maana sisi ni hekalu la Mungu(Roho Mtakatifu)
“ Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe
maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu” 1Wakoritho
6:19-20
5.
Kujiepusha na
vitendo vya ushawishi: kikawaida kuna vitendo ambavyo vinaweza kuwapelekea
au vikachochea uzinzi au uasherati. Mfano: kuchati muda mwingi na jinsia
tofauti kwa kuitana majina ambayo hukutakiwa kuyasema au kuwa na muda mwingi na
jinsia tofauti kutembeleana nyumbani peke yako ni hatari sana shetani anaweza
akawaingia mkafanya uovu. Ni vyema mkawa zaidi ya mmoja.
“Basi palitokea mashindano baina yao
hata wakatengana, Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda kipro, lakini Paulo
akamchukua sila, akaondoka akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana” Matendo
15:39-40
6.
Kufanya mazoezi
ya mwili:
Mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya afya
yako. Ni vema ukafanya mazoezi ili kuepuka zinaa.
“Je hamjui yakuwa wale washindanao kwa
kupiga mbio wote, lakini apokeae tuzo pigeni mbio namna hiyoili mpate”1wakoritho 9:24
7.
Kujiweka bize
Unapokuwa bise katika kumtafakari Mungu na
neno lake au ukuu wake itakusaidia sana. Mfano:Kama wewe ni mwanafunzi jiweke
bize katika kujisomea masomo yako.
“nimevipiga vitu vilivyo vizuri mwendo
nimeumaliza imani nimeilinda”.2timotheo 4:7
8.
Jitambue wewe ni
kielelezo kwa Mungu:
Unapo okoka unatakiwa uwe ni kielelezo
mbele za Mungu na mwanadamu. Kama utasema umeokoka na ujihusisha na maovu hapo
unakuwa unamtukanisha Mungu.
“Katika
mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema na katika
mafundisho yako ukionyesha usahili na usahivu”. Tito 2:7
MADHARA YA ZIINAA(
Uzinzi na uasherati)
Usisahau
dhambi ni kazi na ni lazima ulipwe (mshahara lazima ulipwe)
“kwa
maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu nai uzima wa milele
katika Kristo Yesu Bwana wetu” Warumi 6:23
i.
Zinaa
inaua utu wa ndani.
“Roho
ya mtu itastahimili udhaifu wake bali roho iliyovunjika nani awezaye
kuistahimili” Mithali 18:14
Zinaa
inajeruhi na kuumiza mtu wa ndani na kumuangamiza nafsi yake.
“Mtu
aziniye na mwanamke hana akili kabisa, afanya jambo litakalo mwangamiza nafsi
yake” Mithali 6:32
ii.
Humvunjia
mtu heshima na kupata fedheha.
“Atapata
jeraha na kuvunjiwa heshima wala fedheha yake haitafutika”Mithali 6:33
iii.
Inafuta
maono na ndoto zako(utamkosa Mungu ) Yusufu alijua kwamba amebeba maono ya Mungu
na ndiyo maana mke wa bosi wake alipotaka kufanya naye mapenzi alikimbia.
“Ikiwa
baada ya mambo hayo mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia lala nami.
lakini akakataa------------- Mwanzo 39:6-12
“Nifanyeje
ubaya huu mkubwa nimkosee Mungu?Mwanzo 6:9
iv.
Humwaondolea
mtu ujasiri wakukemea
dhambi.
Mtu
anakosa ujasiri mbele ya Mungu na wanadamu kwa sababu moyo wako unakuhukumu.
“Wapenzi
mioyo yetu isipotuhumu tunaujasiri kwa Mungu” 1Yohana 3:21
v.
Huleta
muunganiko wa mwili.
“Au
haujui yakuwa yeye aliyeungana na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema wale wawili
watakuwa mwili mmoja” 1wakoritho6:16
Kumbuka
hili ni agano(zinaa ni agano) au unaweza kusema ni kifungo unaunganisha,mwili,
nafsi na moyo (roho yako) ndiyo maana utakuta mtu kabla ya kuokoka alikuwa na
mtu wake (mpenzi)unakuta wameokoka wanaendelea na zinaa kama mwanzo.
vi.
Hukiingiza
kizazi chako kwenye vifungo
“Baba
zetu walitenda dhambi hata hawako na sisi tumeyachukua maovu yao” Maombolezo
5:7
vii.
Huambukiza
magonjwa.
Zinaa
inaweza kukuambukiza magonjwa ya namna mbalimbali.
viii.
Ni
mlango wa mapepo kwa wanadamu.
ix.
Inaua
kiroho na kimwili
“Ndipo
Bwana akanyosha juu ya sodoma na juu ya gomora kiberiti na moto toka mbinguni
kwa Bwana” Mwanzo 19:24.
x.
Inaweza
kukufanya usiurithi ufalme
wa Mungu (ukafutwa kwenye kitabu cha uzima)
“Bali
waoga na wasio amini na wachukizao na wauaji na wazinzi na wachawi na hao
waabuduo sanamu na waongo wote sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na
kiberit. Hii ndiyo mauti ya pili”
“Na
iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika
hilo ziwa la moto”Ufunuo 20:15
KAMA
HUJAOKOKA SEMA MANENO HAYA KWA KUYAKIRI NA KUYAAMINI MOYONI MWAKO.
Baba
Mungu katika jina la Yesu Kristo nakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi
ninaomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozitenda kwa kujua au kwakuto kujua
na ninazo zikumbuka na nisizo zikumbuka. Ninaomba unirehemu, ninaomba
unihurumie mimi mwenye dhambi, ninakuomba futa jina langu kwenye kitabu cha
hukumu na uandike jina langu kwenye kitabu cha uzima. Ninaomba uwe Bwana na
mwokozi wa maisha yangu, naomba unipe neema niwe mwaminifu mbele zako na hata
milele. Asante Yesu Kristo kwa kunisamehe dhambi zangu. Nimekuwa kiumbe kipya
mbele zako, katika jina la Yesu kristo. Ameni
Niseme kwamba Mungu amekusamehe dhambi
zako wala azikumbuki tena endelea kujifunza neno la Mungu ili neema uliyoipata
isipotee. Sasa wewe ni kiumbe kipya ndani ya Kristo Yesu yakale yamekwisha tazama
ni mapya ni katika jina la Yesu. Wokovu ulioupate ni wa thamani sana na hiyo
ndiyo tiketi ya kwenda mbinguni.
MUNGU AKUBARIKI.