BEELZEBURI (Mkuu wa mapepo)
Beel maana yake ni mkuu/bwana
Zeburi maana yake ni mapepo wachafu
Beelizeburi ni shetani anayesimamia mapepo yote
kwa kuyapa amri Marko 3:20-30,Mathayo 12:22-24,Luka11:24.Mapepo tabia zao ni
anataka kuishi sehemu ambapo hapana maji (makavu/pakavu) pasipo na maji maana
yake ni moyo mkavu-Roho Mtakatifu hayupo,na mapepo hayana makao maalumu
yanasubilia kualikwa/kuitwa Marko 16:9,nchi ya Wagerasi Marko 5
AMEFUNGWA KWENYE MTI
Mti
ulitumika kwenye Biblia kama sehemu ya mwisho ya hukumu kwa mtu.Mtu akifungwa
kwenye mti baada ya hapo ni kifo.wachawi wanaweza kuutumia mti kama gereza
kuyafunga maisha ya mtu au mafanikio ya mtu Yoshua 8:28-29,Esta 7:8-10,2:23,Danieli
4:13-14,Mathayo 27:38-40
Maombi
-kuwapiga
waliokufunga kwenye mti
-kushuka
kwenye mtu
KUONDOA VIZUIZI VYA KISHETANI
Vizuizi ni vikwazo
Adui wa
maisha ya kila mtu ni shetani,shetani ni roho hutenda kazi kupitia mawakala
wake ambao ni wachawi,wasoma nyota,waganga wa kienyeji n.k wanauwezo wa kukaa
kwenye masomo,elimu,ndoa,kazi,biashara,fedha,maendeleo 1Wathesalonike
2:18,Mathayo 8:23-28,Danieli 10:11-14
Maombi
-kuwapiga
wanaokuzuia
-kuondoa
vizuizi
SAA INAYORUDI NYUMA
Saa ni kifaa
kinachoonesha mudauliopo.Kuna saa za analogia na kuna saa za kidigitali.Kuna
saa za asubuhi,kuna saa za mchana,kuwa saa za jioni,kuna saa za usiku.Zamani
hata sasa walikuwa wanatumia jua,mwezi,sauti Marko 14:32-42,Mathayo
27:45-50,Mathayo 10:19-20,Mathayo 24:36,25:13.Shetani anaweza kuiona saa yako
badala ya kwenda mbele yeye anairudisha nyuma au anaisimamisha mfano
biashara,kazi,familia,elimu.Anakuwekea saa feki,
BADILI LUGHA YAKO
Maana ya
lugha.Kuna lugha ya mazungumzo,maandishi,vitendo,picha.Kila nchi ina lugha yake
ya taifa,lugha ndiyo chombo cha mawasiliano mfano mke na mume.Lugha ndiyo nguvu
ya mahusiano 1Wakorintho 13:1
Lugha za
wanadamu,za malaika,mashetani
Kunena kwa
lugha ndiyo lugha ya ufalme wa Mungu lakini unaponena kwa lugha inapaswa moyo
wako uwe safi unaweza ukawa unaongea vitu vingine kwa Mungu au shetani akatumia
kinywa chako,hapa unapaswa kuwa makina sana.Matendo 2:1-4,Warumi
8:26,1Wakorintho 14:2.Sema nabadilisha lugha ya
magonjwa,umasikini,shida,balaa,laana,mikosi,kushindwa n.k juu ya maisha yangu
kwa jina la Yesu Kristo