Friday, October 10, 2025

MUNGU SIKU ZOTE ANATUPENDA SANA


 

UTOFAUTI WA KANISA LA TANZANIA NA MAKANISA YA NCHI ZINGINE

 KANISA LA TANZANIA NA KANISA LA NIGERIA TOFAUTI KATIKA WOKOVU, UAMSHO NA UTHUBUTU

Katika kulinganisha maendeleo ya kiroho kati ya kanisa la Tanzania na Nigeria, hoja kubwa imeibuka kwamba Tanzania bado ipo nyuma kwa kiwango kikubwa linapokuja suala la uamsho, uthubutu na mshikamano wa kanisa.

Nigeria: Historia ya Mababa Wenye Uthubutu

Nigeria imejipatia umaarufu mkubwa katika historia ya injili kutokana na watumishi waliolipa gharama kubwa kwa ajili ya wokovu.

Joseph Ayo Babalola (1930): Alitembea mji kwa mji akihubiri injili na kufufua zaidi ya watu 30.

Benson Idahosa: Anatajwa kufufua zaidi ya watu 24 na kufanikisha uamsho mkubwa unaoheshimiwa hadi leo.

Hadi sasa, majina makubwa kama Papa E.A. Adeboye (RCCG) – kanisa linalokusanya zaidi ya waumini milioni moja duniani, David Oyedepo (Winners Chapel) – ibada ikihusisha waumini 250,000 mara tatu kila Jumapili, na Paul Enenche (Dunamis International Gospel Centre) – anayekusanya zaidi ya waumini 100,000 kwa ibada moja, yanaendelea kushuhudiwa. Aidha, majenerali kama Chris Oyakilome, Ayo Oritsejafor, na Apostle Johnson Suleman wameendeleza mwendelezo wa nguvu za injili Nigeria.

Utafiti unaonyesha siri ya mafanikio yao ni umoja, mshikamano, na uthubutu wa watumishi waliotangulia, hali iliyosababisha kizazi cha vijana kurithi neema na kuendeleza huduma kwa urahisi zaidi.

Tanzania: Changamoto za Mgawanyiko na Ubinafsi

Tanzania pia imeshuhudia uamsho kupitia watumishi kama Mzee Moses Kulola, Mwalimu Christopher Mwakasege, Mchungaji Dustan Maboya, na Askofu Kakobe. Hata hivyo, tofauti kubwa iliyojitokeza ni mgawanyiko miongoni mwa watumishi wa injili.

Mara nyingi watumishi wapya walipoinuliwa, walipingwa na waliotangulia kwa kushutumiwa kuwa “pepo” au “shetani”.

Utamaduni huu wa kusemana na kugawanyika umeendelezwa hadi kizazi cha sasa, jambo linalodhoofisha umoja wa kanisa la Tanzania.

Aidha, historia ya uamsho nchini haijarekodiwa kwa kina, tofauti na Nigeria ambapo kumbukumbu za watumishi na matendo yao zimehifadhiwa na kuenziwa.

Swali linaloibuka ni kama Mungu ataikubalia Tanzania kufikia hata robo ya kile kinachoendelea Nigeria. Wengi wanaona bado anga la Tanzania halijashikiliwa kiroho kwa sababu ya roho ya ubinafsi, choyo na ukosefu wa mshikamano wa kanisa.

Wachambuzi wa kiroho wanasema, bila umoja na uthubutu wa kizazi kipya, ni vigumu kuona Tanzania ikipata ukombozi wa kweli wa kiroho, hata ukombozi wa kisiasa.

Nigeria imekuwa mfano wa taifa ambalo kanisa limeinuka na kushikilia anga za kiroho kwa uthubutu. Tanzania, licha ya kuwa na historia ya watumishi waliotumika kwa nguvu, bado inapambana na changamoto za mgawanyiko na ubinafsi.

Ipo haja ya mjadala wa dhati miongoni mwa Wakristo wa Tanzania, hususani vijana, ili kuamua kama wako tayari kulipa gharama na kupindua meza za mgawanyiko kwa ajili ya injili ya Kristo.

MAMBO YANAYOKUFANYA WADHALAULIKE WATUMISHI WA MUNGU

 MAMBO YATAKAYO FANYA HUDUMA YAKO KAMA KIJANA KUDHARAULIKA NA WATU AU WATUMISHI WENZAKO

01. KUMKOSA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO.

Ukimkosa Mungu , Umekosa Heshima , Ukimshika Mungu umebeba Heshima.

Katika Umri ambao Mungu hutengeneza watu wenye Heshima ni Ujana , Na Katika Umri ambao shetani huwaandaa Vijana wanao onekana watumishi lakini ni wa Hovyo na watazaa aibu Ni Ujanani.

Ikiwa kijana Mungu amekupa nafasi Ya Utumishi mwandame Katika kila siku mpya ili akuheshimishe , Imani yako na Upendo wako kwa Mungu uwe kielelezo kwa watu wote.

02. KUKOSA MAONO YALIYO WAZI KUHUSU NINI MUNGU ANATAKA KWENYE HUDUMA YAKO NA WAPI UNAELEKEA.

Maono ya Kijana Katika Huduma na namna anavyo yaishi maono yake Huleta Heshima , Bali kijana mtumishi asiye na maono kila kitu atataka kufanya , Kila mahali atataka kwenda , Na Kila mtu atataka kumuiga , Na Kila style ya maisha atataka kuishi kwa sababu Hana maono :

NB: Maono Kwa Kijana yanampa Nguvu ya Kufocus na Nguvu ya Kuzaa matokeo yenye Tija Yanayoshikika.

03. KUMFANYA KILA MTU MZAZI WAKO WA KIROHO NA MENTORS KILA MAHALI.

Moja ya Baa kubwa linaloleta dharau kwa vijana wengi ni Kutaka kila mtu maarufu awe baba yake wa kiroho , Kila mchungaji maarufu mtandaoni ni mentor wake na mlezi wake , 

Katika maisha ya kawaida tu mtoto anayekula kula kwa watu anaitwa mlafi na mwenye tamaa , Watumishi wengi vijana wanaonesha tabia ya tamaa kwa kufikiri kuwaita wachungaji maarufu ni mababa zake , Unatoka baba X kwenda Y , Kesho uko kwa Baba A , Tena unahama unaenda kwa baba H

NB: UTULIVU HULETA HESHIMA KUTANGA TANGA HULETA DHARAU 

04. KUDEKA DEKA KWA WATU ILI WAKUONEE HURUMA KAMA WEWE NI MTUMISHI WA MUNGU.

Watu watakuheshimu kwa kadiri unavyo onesha kumtegemea Mungu kupo kwa Namna Gani.

Tupo katika kizazi ambacho vijana wengi wapo kwenye Huduma na hawajui mipaka yao kwa washirika au watu , Unakuta mtumishi wa Mungu kijana amejaza inbox za watu akiomba omba fedha au anatembelea watu kueleza shida zake ili aonewe huruma , Huo ni Utoto wa kiroho acha haitakujenga.

05. KUOMBA OMBA WATU PESA INBOX, HASA PESA ZA MATUMIZI YAKO BINAFSI KAMA CHAKULA , KODI YA NYUMBA AU MAVAZI.

Ni fedheha mtumishi wa Mungu Kuomba Omba kwa watu chakula , Mavazi au kodi Ya Nyumba , NI BORA SANA KUMUOMBA MUNGU. Ni Mbaya sana kwa mtumishi wa Mungu kuwalemea watu katika kupata mahitaji yako Bonafsi.

2 Corinthians 11:9

“9.Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda.

06. KUKOSA UTARATIBU NDANI YA KANISA, IBADA  ISIYO NA UTARATIBU INALETA DHARAU KWA KIONGOZI WA KANISA.

1 Corinthians 14:40

Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.

07. KUWA NA WASAIDIZI WALIOKOSA AKILI AU MAARIFA YA HUDUMA [ WATU HAWA WANAWEZA KUKURUDISHA NYUMA KILA SIKU].

Kila msaidizi unayemuweka kwenye Huduma yako ni sura yako na maonyesho ya tabia zako, 

Msaidizi mwema kwenye Huduma atakuletea heshima bali msaidizi mbaya atakuletea Mavuno ya dharau kwenye Huduma yako, Chagua kwa hekima na Uongozi wa Roho Mtakatifu mtu anayeweza kukukaimu majukumu Yako au anayeweza kusimama na wewe Vema .

08. KUMDHARAU MUME AU MKE WAKO KUTAFANYA HUDUMA YAKO IDONDOKE KABISA.

Waebrania  13:4

4.Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

09. KUVAA VIBAYA NI NYAVU YA KUVUA DHARAU .

Moja ya mtego mdogo ila wenye kuvuna dharau nyingi ni Mavazi, Kuna watu walikuwa wanaheshimika vema kabisa ila mpaka walipovaa mavazi fulani, 

Mavazi yanaweza kuleta aibu au heshima, Mpangilio wa Uvaaji wako unaweza kuleta heshima au dharau ,

NB: Mavazi ni Jambo la Kiroho sana Usipuuze.

10. KUPOST MAMBO YASIYO FAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII NA KUENDANA NA UADILIFU WA HUDUMA HUONGEZA DHARAU.

Kila jambo ambalo unalifanya kupitia mitandao ya kijamii linaweza kukuweka kwenye kundi la watu watakao pokea heshima au wale watakao pokea dharau, 

Mitandao ya kijamii inaweza kuvuta watu heshima wakuheshimu au watu wenye dharau wakudharau.

11. KUAMBATANA NA WATUMISHI WASIO NA MAADILI NA WASIOTAKA KUBADILIKA HATA WAKIONYWA.

Mithali 13:20

“20.Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.”

12. KUKOPA WASHIRIKA WAKO FEDHA AU KUWALAZIMISHA WAKUPE FEDHA  , 

Mtumishi kijana anayekopa kopa washirika fedha Huishia kwenye fedheha na dharau kabosa ,

Fikiri kidogo , Mchungaji madhabahuni unahuburi halafu mshirika anakudai yuko kanisani anakusikiliza ukisema pokea fedha , Mshirika anawaza nikitoka hapa namdai , Na Mchungaji unachukua sadaka kila siku kulipa madeni ambayo ulipata kwa sababu ya matumizi binafsi. NI AIBU.

NB: EPUKA KUKOPA WASHIRIKA AU KUWALAZIMISHA WAKOPE ILI WAKUPE WEWE FEDHA 

WEWE NI KIJANA, UNA NDOTO ZA KUWA MTUMISHI WA MUNGU, HII NI FURSA YAKO.

MUNGU NI MWEMA SIKU ZOTE










 

AINA YA WASHIRIKA WASUMBUFU KANISANI

 AINA ZA WASHIRIKA WAKOROFI KWENYE MAKANISA YENYE WACHUNGAJI VIONGOZI VIJANA

01. WASHIRIKA WASIOTAKA MAOMBI WALA KUJIFUNZA NENO LAKINI WANATAKA UWAPE NAFASI YA KUFUNDISHA NA KUHUBIRI KILA MARA.

Washirika Hawa Hupenda sana kuonekana na Kujionyesha kuwa wanajua hata kama hawajui.

Washirika wa jinsi hutawakuta kwenye maombi , Madarasa ya neno au mikusanyiko ya vikundi kanisani ila wakija wanataka Uwapishe uwaachie madhabahu.

NB: Ukiwapa Nafasi washirika kama hawa kanisani Unatengeneza washirika wasiojali sauti ya Mchungaji wao, Na Wengi huangukia Mafunuo Batili Na Ujanja ujanja wa kidali katika Huduma.

02. WASHIRIKA WAPINGA UONGOZI , LOLOTE KIONGOZI ANALOSEMA WAO WAPO KINYUME NAO.

Aina hii ya washirika ni Hatari sana mfano wake ni Kora , Dathani na Abiramu , unaweza kusoma habari zao kutoka katika biblia kitabu cha Hesabu, Washirika wa jinsi HUTENGENEZA MIKUSANYIKO KINYUME NA MCHUNGAJI

Hesabu 16:1-3.

1. Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni;

2. nao, pamoja na watu kadha wa kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa;

3.nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, BWANA naye yu kati yao; n’nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa BWANA?

NB: Mchungaji wa kanisa la mahali pamoja Ukiona watu kama Kora usiwape hata nafasi ya kusimama mbele au Kuongea na washirika , Watu hawa lolote wanalofanya lengo lao mwishoni ni Kuiba na kuigeuza mioyo ya washirika kinyume cha mchungaji wao.

03. WASHIRIKA WANAOMCHUKULIA MCHUNGAJI KIONGOZI KAMA KIJANA WAO , HIVYO AKILETA MAONO WANAMWITA PEMBENI KUMKEMEA NA KUMWAMBIA UWE TARATIBU HAYO MAONO NI MAKUBWA.

Mara nyingi washirika wa jinsi Hii huwa wanahisi kwa sababu ni wakubwa kiumri basi wanatakiwa kumuongoza mchungaji na kumuamuru nini cha Kufanya , washirika kama hawa hupenda kuita makanisa yenye viongozi vijana kama makanisa ya watoto.

Kuna wakati Petro aliona kama Yesu anakosea mafundisho yake kwa kueleza kuwa kuna siku atakufa na kufufuka akamwita pembeni akamkemea kiongozi wake ,

Matthew 16:21-23

21.Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.

22.Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.

23.Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu. Msalaba na Kujikana

NB: Washirika Wa Jinsi Hii Wape nafasi ya kuwasikiliza na Kuyapima mashauri yao kama yatakupigisha hatua katika Huduma au La.

04. WASHIRIKA WANAOJUA KUTOA AHADI ZA MICHANGO TENA MIKUBWA WANAONGEZA MATUMAINI KWENYE MALENGO YA KIFEDHA KATIKA MIRADI YA KANISA LAKINI HAWATOI , LENGO LA HUWA NI KUPATA SIFA TU.

Ogopa sana ikiwa watu hawa wakatoa ahadi na wasizitimize wanakatisha tamaa wengine kutoa hata kama walikuwa wanatoa kidogo. 

MITHALI 20:25

“Ni mtego kwa mtu kutamka kwa haraka neno la nadhiri, kisha baadaye kufikiri juu yake.”

NB: Ukiwajua washirika wa Jinsi Hii Usiwape nafasi ya Kuahidi Tena kama hawaondoi nadhiri zao hii ni njia Ya Kuwalinda na Kuwapa nafasi ya Kujitathimini.

05. WASHIRIKA WANAOTONGOZA WAPENZI WAPYA KILA SIKU NA WANALETA KUTAMBULISHA KWA MCHUNGAJI LAKINI HAWAOI.

Washirika wa jinsi Hii huwa na mioyo myepesi katika kuanzisha mahusiano na kutoka mwishowe hutengeneza makovu kwa washirika yasiyopona. 

Katika kizazi cha sasa jambo hili si kwa vijana tu bali hata mabinti anaanza mahusiano na kijana akiona hana pesa anampiga chini anaanza mahusiano mengine mapya, Hakuna Uaminifu , KANISA LINAJAA WASHIRIKA WENYE MAGONJWA NA VIDONDA VYA MAHUSIANO.

06. WASHIRIKA WANAOJUA TAARIFA ZA WASHIRIKA WOTE KANISANI NA KAZI YAO KUBWA NI KUTOA MAELEKEZO KWA WASHIRIKA WAPYA KWA KUSEMA HABARI ZA NDUGU ZAKE.

Mithali  20:19 

19. Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.

“Mchongezi Hueneza Siri, basi usishirikiane naye azidishaye midomo yake.”

07. WASHIRIKA WAKOPAJI , KILA MTU KANISANI ANAKUWA ASHAKOPWA NA HALIPI.

Psalms 37:21

“21.Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.”

Hawa utawasikia wanasema Una Laki Hapo nitumie mara moja jioni kuna mchongo nausikilizia nakurudishia , Kwa sababu ni mpendwa Unampa Baada ya Hapo Harudishi, Hapokei simu , Hajibu sms , Akija kanisani anakuwa wa kwanza kuondoka asikutane na mtu.

Watu wa jinsi wakikutana na mshirika tajiri kanisani wanampiga kitu kizito mpaka mshirika anahama mpaka umegundua hilo tatizo ushapoteza washirika wapya wa maana.

NB: Usizoee kukopesha wapendwa ni Bora utoe kama sadaka ili kudumisha umoja 

08. WASHIRIKA WASIOJALI WANAVYO VAA WAKIDAI MUNGU ANAANGALIA ROHO TU :

Washirika hawa hupenda mavazi yanayowaonesha maungo yao , Na ukiwasema tu unaonekana mchungaji una changamoto , Washirika Hawa Huwa na nguvu sana ya kuwavuta vijana wajinga kwa tamaa,

1 Timothy 2:9

“9.Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi.”

NB: Unaweza Usijali Kuhusu mavazi kama mchungaji lakini Watu ambao tumeitwa kuwa nuru kwao Wanajali na wanalitambua kanisa kwa namna mnavyo vaa Pia.

09. WASHIRIKA WANAOLIGAWA KANISA , ENDAPO KUNA WAHUDUMU ZAIDI YA MMOJA.

Washirika kama Hawa hutengeneza makundi ndani ya kanisa , Utakuta wako wanaosema mimi simuelewi mchungaji namuelewa mzee fulani , Wengine wanasema mimi simuelewi Mtu fulani akiongoza sifa , [ WASHIRIKA HAWA HULIGAWA KANISA NA KUFANYA KANISA LISITAWALIKE]

1 Corinthians 1:12-13

“12.Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.

13.Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?”

Washirka hawa hutumia Fedha na mali katika kuimarisha makundi yao ndani ya kanisa, Mchungaji asipokuwa makini washirika hawa huweza kulipasua kanisa au kufanya kanisa lisitawalike kabisa na Huduma kuwa ngumu.

10. WASHIRIKA WANAOPENDA KUFUATILIWA SANA NA KUPEWA AHADI NYINGI ILI WAJE KANISANI.

Washirika wa jinsi wanapenda mchungaji uwapigie simu kila wakati , uwatumie message na uwape Ahadi nono kabla hawajaja kanisani na usipofanya hivyo Unakuta hawaji kabisa kanisani , Kabla ya siku ya ibada wanataka usiku uwapigie simu , wanachosha sana hawa.

Aina hii ya washirika wanapenda wakija kanisa uwape ahadi za chakula , Juice au nyama choma ili waje kwenye ibada au mikesha , 

NB: Mchungaji mzembe Huwazoesha washirika wa jinsi Hii Na Kutengeneza kanisa na washirika dhaifu wasioweza Kujisimamia .

Thursday, May 15, 2025

BEELZEBURI (Mkuu wa mapepo)

 

BEELZEBURI (Mkuu wa mapepo)

Beel maana yake ni mkuu/bwana

Zeburi maana yake ni mapepo wachafu

Beelizeburi ni shetani anayesimamia mapepo yote kwa kuyapa amri Marko 3:20-30,Mathayo 12:22-24,Luka11:24.Mapepo tabia zao ni anataka kuishi sehemu ambapo hapana maji (makavu/pakavu) pasipo na maji maana yake ni moyo mkavu-Roho Mtakatifu hayupo,na mapepo hayana makao maalumu yanasubilia kualikwa/kuitwa Marko 16:9,nchi ya Wagerasi Marko 5

AMEFUNGWA KWENYE MTI

Mti ulitumika kwenye Biblia kama sehemu ya mwisho ya hukumu kwa mtu.Mtu akifungwa kwenye mti baada ya hapo ni kifo.wachawi wanaweza kuutumia mti kama gereza kuyafunga maisha ya mtu au mafanikio ya mtu Yoshua 8:28-29,Esta 7:8-10,2:23,Danieli 4:13-14,Mathayo 27:38-40

Maombi

-kuwapiga waliokufunga kwenye mti

-kushuka kwenye mtu

KUONDOA VIZUIZI VYA KISHETANI

Vizuizi ni vikwazo

Adui wa maisha ya kila mtu ni shetani,shetani ni roho hutenda kazi kupitia mawakala wake ambao ni wachawi,wasoma nyota,waganga wa kienyeji n.k wanauwezo wa kukaa kwenye masomo,elimu,ndoa,kazi,biashara,fedha,maendeleo 1Wathesalonike 2:18,Mathayo 8:23-28,Danieli 10:11-14

Maombi

-kuwapiga wanaokuzuia

-kuondoa vizuizi

SAA INAYORUDI NYUMA

Saa ni kifaa kinachoonesha mudauliopo.Kuna saa za analogia na kuna saa za kidigitali.Kuna saa za asubuhi,kuna saa za mchana,kuwa saa za jioni,kuna saa za usiku.Zamani hata sasa walikuwa wanatumia jua,mwezi,sauti Marko 14:32-42,Mathayo 27:45-50,Mathayo 10:19-20,Mathayo 24:36,25:13.Shetani anaweza kuiona saa yako badala ya kwenda mbele yeye anairudisha nyuma au anaisimamisha mfano biashara,kazi,familia,elimu.Anakuwekea saa feki,

BADILI LUGHA YAKO

Maana ya lugha.Kuna lugha ya mazungumzo,maandishi,vitendo,picha.Kila nchi ina lugha yake ya taifa,lugha ndiyo chombo cha mawasiliano mfano mke na mume.Lugha ndiyo nguvu ya mahusiano 1Wakorintho 13:1

Lugha za wanadamu,za malaika,mashetani

Kunena kwa lugha ndiyo lugha ya ufalme wa Mungu lakini unaponena kwa lugha inapaswa moyo wako uwe safi unaweza ukawa unaongea vitu vingine kwa Mungu au shetani akatumia kinywa chako,hapa unapaswa kuwa makina sana.Matendo 2:1-4,Warumi 8:26,1Wakorintho 14:2.Sema nabadilisha lugha ya magonjwa,umasikini,shida,balaa,laana,mikosi,kushindwa n.k juu ya maisha yangu kwa jina la Yesu Kristo

KUONDOA ROHO ZA HASIRA

 

KUONDOA ROHO ZA HASIRA

Hasira ya mtu siku zote haitendi haki.Na hasira inaendana na vitu vitatu,moyo,akili na matendo.Hasira inaweza ikafanya maamuzi mabaya yaani haitendi haki hata mara moja.Siku zote ukiwa na hasira jaribu kujidhibiti,usifanye jambo baya au kufanya maamuzi mabaya na kamwe usiongee maneno mabaya siku zote Yakobo 1:20,Waefeso 4:26,Mhubiri 7:9,Mithali 19:11,Mithali 15:1,18,Mithali 14:17

MTAABISHAJI WA MAISHA YAKO

Mtaabishaji linatokana na neno taabika.Mtaabishaji ni mtu anayeumiza,teas,haribu,anayekukosesha amani,anayekukosesha raha n.k 1Wafalme 18:17-------

MTI WA KIROHO

Mathayo 13:31-32

Mti ni mtu

Ndege ni neno

Shamba ni moyo

Mungu anapanda mbegu kwa Yesu (amepanda ndani ya moyo wa Yesu).Yesu alikuwa mdogo sana kwa Wayahudi,Yesu akakua mpaka mtu mkubwa.Mbegu ni ndogo lakini inathamani kubwa sana Isaya 55:12

ROHO ZA URITHI

Urithi ni hali ya kumilikishwa kitu au vitu

Aina za urithi

·        Urithi wa Kimungu

·        Urithi wa kishetani

Urithi waKimungu

Yushua 19:49,Isaya 54:17---,Zaburi 127:3,Zaburi 16:6-8,Zaburi 33:12,Mithali 13:22,Mithali 19:14,Yeremia 3:19

Urithi wa kishetani

Yeremia 12:8-9,Mathayo 21:38-39

KUANGUSHA BABELI YA KIROHO

Babeli ni mji wa zamani ulikuwa umejengwa huko Mesopotamia mashariki ya kati 2Wafalme 24:11,Babeli ni gereza linalowashikilia watu.Isaya 21:9,Ufunuo 14:8,Ufunuo 17:1-18,Ufunuo 18:21

KUHARIBU ROHO ZA LAANA

Laana ni mkusanyiko wa mambo mabaya yanayompata mtu

Kuna laana ya ardhi na kuna laana ya mtu.Kinachobeba laana mpaka iwe na nguvu ni

·        Maneno Torati 29:19

·        Kafara 1Wafalme 2:8

·        Kiapo Zaburi 10:7,Warumi 3:14

LUCIFER DNA

Vinasaba vya shetani.Ni chembechembe ndogo ambazo hubeba taarifa zote za kibaiolojia kwa kila kiumbe(urithi) yaani uzao 1Yohana 3:10---,Mwanzo 6:1-4,Torati 2:20.Wanasayansi walishawai kugungua vinasaba vilivyochanganyikana na binadamu

KURA HUKOMESHA MASHINDANO

 

KURA HUKOMESHA MASHINDANO

Kura ni kuchagua mtu au kitu,Matendo 1:23-26,Mithali 18:18,Mithali 16:33

UNAONA NINI?

Katika maisha watu wengi wamefichwa macho ya rohoni.Ninapozungumzia macho,nazungumzia

·        Ufahamu,uzima,afya,uweza

·        Fikra,kumtafuta Yesu

·        Akili

·        Nguvu,maono yako

·        Hatua

·        Mafanikio

Yeremia 1:11-12,Yeremia alikuwa kuhani(mmoja wa makuhani)kwenye nchi ya Benyamini.Nenola BWANA lilimjia wakati wa kutawala kwake mfalme Yosia (Mfalme wa Yuda) Hesabu 13:33,Hesabu 14:6-10

MUNGU AKUKUMBUKE TENA

Kukumbukwa ni hali ya kuonekana kwa mtu/kitu(kutolewa/kukubaliwa) ulikuwa umesahaulika sasa umeonekana Mwanzo 8:1---.Mungu alimuambia Nuhu ajenge safina,urefu mikono 300

,upana mikono 50

,urefu kwenda juu mikono 30

.Tarehe 17/02/600 mvua ikaanza kunyesha mpaka

 tarehe 26/03/600 mvua iliacha.Maji yalitulia siku 150 (miezi 5),

tarehe 17/07/600 safina ikatua mlima Ararati (Uturuki ya leo)

,tarehe 01/10/600 maji yalipungua pungua

,tarehe 07/10/600 alimtoa kunguru na njiwa,

tarehe 14/10/600 alimtoa njiwa,

tarehe 01/01/601 nchi ilikuwa kavu

,Mungu akamwambia Nuhu toka kwenye safina

WAZAZI WETU WALITENDA MAOVU

Maombolezo 5:7,Yeremia 16,Mhubiri 3:1,Mhubiri 9:11

WAKATI NA BAHATI UWAPATA WOTE

Bahati ni kukipata kitu bila kutegemea au kuepuka kitu ambacho hukutegemea.Mhubiri 9:11,Mhubiri 11:5-6

BONDE LA MATESO

Mateso ni matatizo yaliyopo ndani au nje ya mtu Luka 3:1-6

JITAMKIE UNABII

Unabii ni kitendo cha kutabiri,yaliyopo,yaliyopita,yaliyopo na yanayokuja

Nabii ni mteule/mteuliwa wa Mungu aliyeitwa kupeleka ujumbe kwa watu.1Wakoritho 12:10,2Petro 1:20-21,Ufunuo 1:1-3,Ufunuo 1:19

KUFUTA PICHA ZILIZOKUWA KWENYE AKILI YAKO

Katika maisha kuna mambo yamesimama kama picha mbaya,inaweza ikawa ugonjwa,umasikini,taabu,mateso,balaa n.k 1Samweli 17:1-5

·        Goliath alikuwa na urefu futi 6

·        Chepeo ya shaba shekel elfu 5

·        Mabampa miguuni

·        Mkuki kwenye begani

1Samweli 17:42---,1Samweli 18:6,Hesabu 13:17,hesabu 14:1

 

UVUNJA ROHO ZA SODOMO NA GOMORA

 

KUVUNJA ROHO ZA SODOMO NA GOMORA

Sodoma na Gomora hii ilikuwa ni miji iliyokuwa ikitenda mambo mabaya mbele za Mungu,kwa wanaume kuwakiana tama na wanawake vile vile kuwakiana tama yaani kwenda kinyume na maumbile.Kutumia miili yao kinyume na asili ya viungo vya uzazi kwa matumizi yake.Mwanzo 13:13,Warumi 1:26-27,Warumi 1:24-25,Warumi1:28-32,Mwanzo 18:1-15,Mwanzo 19:4-11

HATA WAKUZUIE UTAVUKA

Torati 9:1-5,Torati 11:30-30,Marko 4:35-41,Marko 5:1---,Matendo 16:9-21

Kushukuru Zaburi 50:23,Wafilipi 4:4-7

-kusali –prayer

-kuomba- supplication

-kushukuru- thanksgiving

(humbly,begging,asking)

JIUNGANISHE NA MADHABAHU YAKO

Madhabahu (Altare,Alta) ni sehemu yoyote ile mtu anapokutana na roho inaweza kuwa ni roho ya Mungu au shetani

Ndani ya madhabahu kuna

·        Kutoa sifa-nyimbo

·        Kutoa sadaka

·        Kuomba (kupeleka mahitaji)

Ezra 3:1-6

Faida ya madhabahu

·        Ni upatanisho

·        Inafungua Baraka

·        Inatupa ulinzi wa Ki-Mungu Mwanzo 8:18-22

·        Madhabahu inasema mbele za Mungu

·        Inamdhihirisha Mungu unayemuabudu

 

KUVUNJA ROHO YA TALAKA

 KUVUNJA ROHO YA TALAKA

Talaka ni hati ya kiapo cha kuvunja ndoa

Aina za ndoa

        i.            Ndoa ya kidini yaani ya Kikristo na Kiislamu

      ii.            Ndoa ya kiserikali

    iii.            Ndoa ya kimila

Mwanzo 2:24

Ndoa na iheshimiwe Waebrania 13:4

Madhara ya talaka

·        Kuzuia hatima za watoto wenu zisitimie kwa wakati

·        Kuleta magonjwa

·        Familia kusambalatika

·        Heshima itapungua

·        Kuyumbisha watoto

·        Kuleta mauti

Marko 10:4-12,Malaki 2:16

Maagizo ya ndoa

 1Wakorintho 7:1-6,1Wakorintho 7:8-16,1Wakoritho 7:33-34,7:39

WAKUACHE UONEKANE

Ili mtu ufanikiwe kwenye jambo Fulani ni lazima aonekane,iwe kibiashara,kindoa,kikazi n.k Wafilipi 3:9-10,Mithali 17:8,Mhubiri 6:4

VINYAGO VYA BABAYE

Vinyago ni miungu inayoabudiwa au ni sanamu zinazoabudiwa kulingana na jamii husika,kuna miungu ngazi mbalimbali mfano kwenye familia,ukoo,kwenye wilaya,mkoa,kitaifa na kimataifa,inaabudiwa sehemu mbalimbali kama vile ofisini,nyumbani.Kutoka 20:1-6,Torati 6:14-15,Mwanzo 31:19,Mwanzo 35:2

HAKUNA ATAKAYESIMAMA MBELE YAKO

Yoshua 1:1-3,Yushua 1:-9,Ayubu 5:12,Zaburi 89:20-

MASHIMO YA KICHAWI (Kiroho)

 

MASHIMO YA KICHAWI (Kiroho)

Agano la kale mtu alipokuwa anafanya kosa au makosa alikuwa anahukumiwa kwa kutupwa kwenye mashimo marefu.

Mashimo yaliyokuwepo

        i.            Mashimo yenye wanyama mfano Danieli

      ii.            Shimo lenye moto mfano Shedraka,Meshaki na Abednego

    iii.            Shimo lenye maji mengi au matope mfano Yeremia 38:6

   iv.            Shimo lisilo na kitu

Sasa

Shetani naye vile vile naye ameyaweka mashimo yake haya kwa namna ya kiroho,hayaonekani kwa macho ya kawaida kwasababu shimo lenyewe ni roho kamili,lina akili,linaweza kukimbia na ukiingia ndani huwezi kutoka linageuka na kuwa giza.Zaburi 35:7,Ufunuo 9:1-2,Isaya 24:17,14:15,Isaya 38:18

Miji inaweza kuwa na mashimo ya rohoni na utakaposhughulika na shimo hilo unakuwa umeuteka mji.Kuna mashimo makubwa  yaani kuzimu ya angani,kuzimu ya baharini ,kuzimu ya nchi

Pia kuna vishimo vidogo mfano mtu anachukuliwa msukule na kuwekwa kabatini,kisimani,dukani,n.k Isaya 42:22

Kila mtu amewekewa Baraka zake sehemu Fulani mfano kwenye kinywa,tumbo,kumbukumbu,biashara,ndoa n.k

Familia,ukoo wanawekwa kwenye mashimo ya mauti,magonjwa,laana,mikosi,shida,balaa,utasa,umasikini n.k

Mambo unayotakiwa kuyafahamu kuhusu kuzimu

         i.            Malaika wa kuzimu ufunuo 9:11

       ii.            Makomeo ya kuzimu Ayubu 17:16

     iii.            Milango ya kuzimu Ayubu 38:17,Mathayo 16:18

     iv.            Kamba za kuzimu 2Samweli 22;6

       v.            Makao ya kuzimu Zaburi 89:88

     vi.            Shida za kuzimu Zaburi 116:3

   vii.            Kitanda cha kuzimu Zaburi 139:8

Maombi

-kuyashambulia mashimo yote ya kichawi

-kuwateketeza walinzi wa mashimo

-kutoka shimoni

ROHO YA MPINGA KRISTO

 

ROHO YA MPINGA KRISTO

Maana yake ni kwenda kinyume na Kristo au kugeuza ukweli wa Yesu Kristo kuwa uongo.1Yohana 2:18,1Yohana 2:22,1Yohana 4:1-3,2Yohana 1:7,2Wathesalonike 2:4,Mathayo 10:16

Dalili za roho ya mpinga Kristo zinazonyemelea mtu/watu

        i.            Kulizoea Neno la Mungu

      ii.            Kutokumuamini Yesu

    iii.            Kumkana Yesu Kristo

   iv.            Kuchukia mambo ya Mungu mfano maombi

     v.            Kuanza kuamini vitu ambavyo sio vitu vya Kimungu

   vi.            Kufanya uovu bila kuumia moyoni

 vii.            Kutokusamehe na kuachilia 1Yohana 4:20-21

viii.            Kutokuzifuata sheria na kanuni za Yesu Kristo

MTUMAINI BWANA

Tumaini maana yake kumtegemea Mungu Baba Mithali 3:5-10

·        Kwa moyo wako wote

·        Usizitegemee akili zako mwenyewe

·        Katika njia zako mkiri (mtaje Yesu/Mungu)

·        Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe

·        Utajiepusha na uovu

·        Mheshimu BWANA kwa mali zako

KUIPINGA ROHO YA UMASIKINI

Umasikini ni hali ya kupungukiwa .Kuna umasikini wa mtu binafsi na kuna umasikini wan chi,kata,tarafa,mtaa n.k Torati 15:4----,Torati 15:7,Mwanzo 13:2,Mithali 19:17,Yakobo 1:27

NIMEWEKA MLINZI

Ezekieli 3:17,Danieli 4:13,Zaburi 121:4-5,Zaburi 141:3

KUFUTA MASHIMO YA KIROHO

Zaburi 119:85,Yeremia 2:6,Waebrania 11:36

UNAJULIKANA MBINGUNI

Kujulikana ni hali ya kufahamika

·        Kufahamika na Mungu

·        Kufahamika na wanadamu

·        Kufahamika na mashetani

Yeremia 1:4-10

Faida za kujulikana na Mungu

·        Utapata msaada/watakusaidia

·        Utazawadiwa

·        Utapata kibali

·        Utapata neema

NABII WA MATAIFA

Nabii ni sauti ya Mungu duniani anayepewa ujumbe na Mungu kupeleka kwa wanadamu Yeremia 1:4-10,Hesabu 12:6,Torati 34:10,Waamuzi 4:4