Baada ya kuandaa blog yako vizuri,hatua inayofuata
ni kutafuta kampuni zinazoweza kulipia Sponsored Posts.Watu wengi hufikiri
kwamba kampuni zitawatafuta zenyewe, lakini kwa blog mpya mara nyingi unahitaji
kuwa na juhudi za kuzitafuta na kujitambulisha.
Kadri blog yako inavyokuwa
na maudhui bora na wasomaji waaminifu, ndivyo nafasi ya kampuni kukufuata
yenyewe inavyoongezeka. Hata hivyo, usisubiri hilo pekee. Unaweza kuanza
kutafuta fursa mapema.
Kwa Nini Kampuni Zinalipa Sponsored Posts?
Lengo kuu la kampuni ni
kuwafikia wateja wapya na kuongeza mauzo. Badala ya kutumia matangazo ya
kawaida pekee, kampuni nyingi hupendelea kushirikiana na waandishi wa blog kwa
sababu makala hujenga uaminifu na zinaweza kuendelea kuonekana kwenye injini za
utafutaji kwa muda mrefu.
Makala nzuri inaweza
kuendelea kuleta wageni kwa miezi au hata miaka, jambo linaloifanya Sponsored
Post kuwa uwekezaji mzuri kwa kampuni.
Kampuni Zinazoweza Kuvutiwa na Blog
Karibu kila sekta inaweza
kutumia Sponsored Posts, kwa mfano:
i.
Kampuni za teknolojia
ii.
Kampuni za simu
iii.
Benki na taasisi za fedha
iv.
Kampuni za blockchain na
cryptocurrency
v.
Shule na vyuo
vi.
Hospitali na vituo vya
afya
vii.
Makampuni ya usafiri
viii.
Maduka ya mtandaoni
ix.
Kampuni za bima
x.
Watoa huduma za intaneti
xi.
Hoteli na kampuni za
utalii
xii.
Wauzaji wa vitabu
xiii.
Mashirika yasiyo ya
kiserikali
Kama blog yako inaandika
kuhusu mada maalumu,tafuta kampuni zinazohusiana na mada hiyo.
Jinsi ya Kutafuta Kampuni
Njia mojawapo ni kutafuta
kampuni kupitia Google kwa kutumia maneno yanayohusiana na niche yako.
Unaweza pia kufuatilia:
·
LinkedIn
·
Facebook
·
Instagram
·
X (Twitter)
Makampuni mengi hutangaza
bidhaa mpya kupitia mitandao hii.Hii inaweza kuwa nafasi ya kuwapa pendekezo la
kuandika makala ya udhamini.
Wasiliana kwa Njia ya Kitaalamu
Unapowasiliana na kampuni:
·
Jitambulishe kwa kifupi.
·
Eleza blog yako inahusu
nini.
·
Taja aina ya wasomaji
ulionao.
·
Eleza jinsi Sponsored Post
inaweza kuwasaidia.
·
Toa mawasiliano yako.
Usitume ujumbe mfupi
usioeleweka.Barua pepe au ujumbe wako uwe wa heshima na wa kitaalamu.
Tengeneza Media Kit
Media Kit ni faili
linaloelezea blog yako kwa ufupi.
Linaweza kujumuisha:
·
Jina la blog.
·
Historia fupi.
·
Mada unazoandika.
·
Idadi ya wasomaji kwa
mwezi.
·
Nchi wanazotoka wasomaji.
·
Mitandao ya kijamii.
·
Huduma unazotoa.
- Bei za Sponsored Posts (ikiwa umeamua kuziweka).
Media Kit huwapa wadhamini
picha ya haraka kuhusu thamani ya blog yako.
Tengeneza Ukurasa wa “Advertise With Us”
Wadhamini wengi hutembelea
blog kabla ya kuwasiliana nawe.
Tengeneza ukurasa maalumu
unaoeleza:
·
Unapokea Sponsored Posts.
·
Aina ya matangazo
unayokubali.
·
Jinsi ya kuwasiliana nawe.
·
Muda wa kuchapisha makala.
·
Masharti yako.
Hii inaonyesha kuwa uko
tayari kushirikiana na biashara mbalimbali katika kufanya nao kazi .
Jenga Mahusiano ya Muda Mrefu
Usifikirie Sponsored Post
kama kazi ya mara moja. Ukifanya kazi vizuri, kampuni inaweza kurudi tena na
tena.
Kwa hiyo:
·
Heshimu makubaliano.
·
Chapisha kwa wakati.
·
Wasiliana vizuri.
·
Toa ripoti ikiwa
mmeafikiana.
Mahusiano mazuri yanaweza
kukuletea mapato ya kudumu katika maisha yako.
Jinsi ya Kujua Kampuni Inayoaminika
Kabla ya kukubali kazi:
·
Tembelea tovuti yao.
·
Soma kuhusu kampuni.
·
Hakikisha bidhaa au huduma
zao ni halali.
·
Epuka kampuni zinazotaka
matangazo ya udanganyifu au zinazodai ahadi zisizo na msingi.
Sifa yako kama mmiliki wa
blog ni muhimu kuliko malipo ya haraka.
Makosa ya Kuepuka
Epuka:
·
Kukubali kutangaza bidhaa
usizozielewa.
·
Kupandisha bei kupita
kiasi bila sababu.
·
Kuandika makala yenye
taarifa za kupotosha.
·
Kupuuza maswali ya
wadhamini.
·
Kutokuweka wazi masharti
ya ushirikiano.
Hitimisho
Kupata kampuni za Sponsored
Posts kunahitaji utafiti,mawasiliano mazuri na kujenga uaminifu.Kadri blog yako
inavyokua na kuwa na maudhui bora, ndivyo fursa za ushirikiano zinavyoongezeka.Kumbuka
kuwa kampuni nyingi zinatafuta blog zinazoweza kuwafikia wasomaji halisi,si
idadi kubwa pekee.Katika sehemu inayofuata tutajifunza jinsi ya kuandika
Sponsored Post yenye ubora wa hali ya juu,jinsi ya kupanga bei ya huduma zako
na mbinu za kuhakikisha kampuni zinataka kuendelea kufanya kazi na wewe.
No comments:
Post a Comment