Friday, February 4, 2022

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

  

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

Karama : Ni zawadi anazotoa Mungu kwa watu au kipaji cha pekee kutoka kwa Mungu.

Lakini kazi hizi zote huzitenda roho huyo mmoja yeye Yule, akimgaia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye” 1wakorotho12:11

Katika karama hizi kuna tofauti ya:

v Kuna tofauti ya huduma

v Kuna tofauti ya kutenda kazi

Bali Mungu ni yeye Yule azitendae kazi zote katika wote

“Bali pana tofauti za karama bali roho ni yeye Yule, tena pana tofauti za huduma na bwana ni yeye Yule, pana tofauti za kutendwa kazi pana tofauti za kutenda kazi bila Mungu ni yeye Yule azitendae kazi katika wote.”1Wakorithio 12:4-6

.kwenye huduma na kutenda kazi kila mtu anakuwa anapewa ufunuo ili kusaidiana.

“Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa  roho kwa kufaidiana” 1Wakoritho 12:7

Kwa hiyo sasa baada ya kuokoka unatakiwa kumuomba Mungu akupe karama za rohoni ili mwili wa Yesu Kristo ujengwe kwa pamoja kwa umoja ndani ya kanisa 

 

“Takeni sana karama zilizo kuu, hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora”.1wakoritho12:31

Kabla ya kuoka tulikuwa tunazifuata sanamu zisizo nena, yaani kuabudu miungu ya kishetani “Basi ndugu zangu kwa habari ya karama za roho, staki mkose kufahamu, mwajua  ya kuwa mlipokuwa watu wa mataifa mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena kama mlivyoongozwa”1Wakolotho 12:1-2

 

AINA ZA KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

Kuna aina mbalimbali za karama za roho. Mwingine anaweza kupewa na Mungu karama zaidi ya moja:

“Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali kwa kadri ya nema mliopewa   ikiwa ni unabii, ikiwa huduma katika huduma yetu, mwenye kuonya katika kuonya kwake, mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu kwa furaha” Warumi 12:6-8

 

1.     Hekima: Ni hali bora ya mtu katika kutambua ukweli wa binadamu, vitu,matukio na mazingira mbalimbali hata kuchagua vizuri la kufanya au unaweza kusema ni maadili ya kitu na maadili ya ki mungu “Lakini hekima itakayo juu, kwanza ni safi tena ni ya amani, ya upole, tayari  kusikiliza maneno ya wato, imajua rehema na matunda mema haina fitina, haina unafiki” Yakobo 3:17

“Basi sasa nipe hekima na maarifa mjue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa kwa kuwa na nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi “2Nyakati 1:10

“Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako na kupambanua mema na mabaya maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako waliowengi” 1Wafalme 3:9.

 

“Maana mtu mmoja kwa roho apewa neno la hekima …. “1wakoritho 12:8

 

        2. Maarifa:  Ni ufahamu wa kuelewa kitu Fulani.

“--------- Mwingine neno la maarifa apewavyo roho yeye Yule “.1wakolitho 12:8(b)

“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa ----------“ Hosea 4:6 Kumbe ukikosa maarifa unaangamia na nguvu ya mtu siku zote ni kuwa na maarifa mengi(knowledge is power)

 

“Bali ajisifiyena ajisifu kwa sababu hii ya kwamba ananifahamu mimi na kunijua ya kuwa mimi ni bwana, nitendee wema na hukumu na haki katika nchi maana mimi napendezwa na mambo hayo asemaBwana,”.Yeremia 9:24.

   Ee mwanadamu yeye amekuonyesha yaliyo mema na     Bwana anataka nini kwako ila kutenda haki na kupewa rehema na kwenda kwa unyenyekevu na mungu wako”. Mika 6:8.

Na uzima wa milele ndio huu wanijua wewe mungu wa pekee wa kweli na yesu kristo aliyemtuma” Yohana 17:3

 

3.Imani:    Ni kuwa na hakika ya  mabo yatarajiwayo , ni       bayana ya mabo yaliyo onekana

Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo ya mambo yatarajiwayo  ni bayana ya mambo yasiyo onekana” Waebrania 11:1

“mwingine imani katika roho yeye Yule …………1Wakoritho 12:9(a)

“maana twenenende kwa imani si kwa kuona” 2wakoritho 5:7

 

“Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani naye akisitasita roho yangu haina furaha naye lakini sisi hatumo miongoni mwao hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu. Waebrania 10:38-39.kwahiyo ukisoma katika hiki cha Waebrania sura ya 11yote utaona inazungumziwa imani kwa asilimia kubwa.

 

4)Kuponya: Ni kumfanya mtu ambaye amekuwa mgonjwa kimwili, kiakili au kiroho apate afya njema.

“----------- Mwenye karama za kuponya katika roho Yule mmoja” 1wakoritho 12:9(b)

“Pozeni wagonjwa, fufufeni watu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo, mmepata bure, toeni bure”.Mathayo 10:8.

“Akampeleka mfalme wa Israeli waraka ule kusema waraka huu utakapo kuwasilia tazama nimemtuma mtumishi wangu naamini kwako ili upate kuuponya ukoma wake” 2Wafalme 5:6

Naamini alikuwa jemedari wa jeshi la mfalme wa shamu lakini alikuwa na ukoma ambao ni ugonjwa hatari sana. Mfanya kazi wa ndani akitoa habari za mtumishi wa Mungu Elia kwamba anaweza kumponya.

“Lakini Petro akasema mimi sina fedha wala dhahabu lakini nilicho nacho ndicho nikipendacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa nazareti simama uende. A kamshika mkono wa kiume akamwinua mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu” Matendo 3:6-7

“Hata ikiwa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa na kuwaweka juu majamvi na magodoro ili petro akijagawa kimli chake kimwangukie mmoja wapo wao.Nayo makuja watu wa miji ilioko kandokando ya yerusalemu wakakutanika wakileta wagonjwa .


Nao walioingiliwa na pepo wachafu nao wote wakaponywa” matendo 5:15-16

“kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi walio pagawa nao, wakalia kwa sauti kuu na watu wengi walio pooza na viwete wakaponywa”matendo 8:7.

 

“Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea mtu huyo amelala kitandani miaka minane, maana alikuwa amepooza. Petro akamwambia Ainea Yesu Kristo akuponya, ondoka ujitandikie, mara akaondoka na watu wale waliokaa Lida na Sharoni wakamwona wakamgeukia bwana” matendo 9:33-35.

 

5)Matendo ya miujiza:  Ni kutenda jambo kubwa lililo zaidi ya uwezo wako. Au ni jambo la ajabu ambalo hukutegemea kulipata au kutokea au umeweza kusema bila kuweza kulielezea.

 

“Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya,Yesu wa Nazareti mtu aliedhihirisha kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara ambazo  Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojuana” matendo 2:22.

“Na Stefano akijaa na neema na uwezo alikuwa akifanya maajabu na ashara kubwa katika watu. Matendo 6:8.


 

“Lakini walipomwamini Filipo akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu na jina lake Yesu Kristo wakabatizwa wanaume na wanawake na yeye Simon mwenyewe aliamini akabatizwa akashikamana na Filipo akashangaa alipo ziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka” Matendo 8:12-13

 

6) Unabii: Ni kitendo cha kutabili yaliyopo, yaliyopita na yanayokuja, Nabii ni mteuliwa wa Mungu aliyeitwa kupeleka ujumbe kwa watumwa.

 

“Mkijua neno hili kwanza ya kwamba hakuna unabii katika maadiko upatao kufasiliwa kama apendavyo mtu flani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu bali wanadamu walinena yaliyo toka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu”. 2Petro1:20-21

 

“Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi, naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake yohane alie lishuhudia neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani mambo yote aliyoyaona. Heri asomae na wao wajasikiapo maneno ya unabii huu na kuyashika yaliyo andikwa humo kwa maana wakati ukaribu”. Ufunuo1:1-3

 

“Basi uyaandike mambo hayo ulioyaona nayo yaliyopo na yale yatakayokuwa baada ya haya” Ufunuo1:19

 

Unabii utakao tolewa lazima utoke kwa Mungu ambao umebeba pumzi ya Mungu maneno au neno utakalo litoa linatakiwa liwe na mambo haya.

a.     Lafaa kwa mafundisho

b.     Lafaa kwa kuonya watu makosa yao

c.      Lafaa kwa kuwaadilisha watu katika haki

d.     Lafaa kwa kuwaongoza

“Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho na kwa kuwaonya watu makosa yao na kwa kuwaongoza na kwa kuwaadilisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda  kila tendo jema” 2Timotheo 3:16-17

Lakini ifahamike kwamba kuna manabii wa kweli (Mungu) na kuna manabii wa uongo (shetani). Yesu kristo aliwatahadhalisha wanafunzi wake kuhusu manabii wa uongo. Akasema mtawatambua kwa matendo yao.

 

“Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajua wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali mtawatanbua kwa matendo yao. Je watu huchuma zabibu katika miiba au tini katika mibaruti  vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwe motoni ndiposa kwa matunda yao nitawatambua” Mathayo 7:15-20

Yesu kristo anaposema mti hapa anamanisha mtu, tunapaswa kuzijaribu kila roho je, zinatokana na Mungu au lah.

 

“Wapenzi msiamini kila roho basi zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na mungu kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.katika hili  Mwanijua  roho kwa mungu kila ikiliyo kwamba yesu kristo amekuja katika mwili yatokana na mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga kristo ambayo mmesikia kwamba yaja na sasa imekwisha kwako duniani 1Yohana 4:1-3

 

7)Kupambanua roho: Ni kitendo cha kutambua kinachoendelea  katika ulimwengu wa roho.

“Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku usiogope, bila nena wala usinyamaze. Kwa kuwa mimi ni pamoja nawe wala hapana mtu atakae kusababishia ili kukudhuru kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu. Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu”  Matendo 18:9-11.

“Akamjibu usiogope mana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha akomba akasema ee bwana nakuishi mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yake mfumishi naye akaona na tazama kile kilima kilichokuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyo mzunguka Elisha pande zote” 2Wafalme 6:16-17.

 

8). Aina za lugha

Kikawaida kuna aina mbalimbali za lugha hapa duniani lakini pia kuna lugha ya mbinguni ambayo watu wake wanatumia (lugha za malaika)

“Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika kama sina upendo nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao”1wakoritho 13:1

 

 

“----------Mwingine aina za lugha “ 1wakoritho 12:10

Kwahiyo Mungu anawapa watu wake  karama hii kwa kuelewa lugha mbalimbali kwa usemi.

 

9)  Kutafsiri lugha

Mungu anapompa mtu karama hii lengo lake ni kufikisha ujumbe kwa wale watu ambao hawaifahamu lugha hiyo, kwa njia ya maombi au kwa njia ya kuhubiri.

“Kwasababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri”1wakoritho 14:13

“Yamkini ziko sauti za namna nyigi duniani wala hakuna moja isiyo na maana . Basi nisipo ijua maana ya  ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye, naye anenaye atakuwa mjinga kwangu”1wakoritho 14:10-11

“Lakini katika napewa kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha” 1wakoritho 14:19.

 

1o)Kuhutubu (kuhubiri)

Ni kitendo cha kutoa ujumbe toka kwa Mungu kwa maneno ya kawaida yanayoeleweka kwa lugha.

“Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja ili wote wapate kujifunza na wote wafarijiwe” 1wakoritho 14:31

“Kwa ajili ya hiyo ndugu takeni sana kuhutubu wala msizuie kunena kwa lugha. Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu” 1wakoritho 14:39-40

 

“Ufuateni upendo na kutaka sana  karama za rohoni lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu”1wakoritho14:1

“Bali yeye ahutubiye asema na watu maneno ya kuwajenga na kuwafariji na kuvuta moyo”1wakoritho14:3

Pamoja na karama hizo zipo za aina nyingi, Kulingana na neema ya Mungu alio mpa mwanadamu kama yeye atakayo roho..

 

Aina za Huduma ndani ya kanisa :

Huduma: Ni taasisi inayo simamia jambofulani kwa watu. Huduma ndani ya kanisa ni taasisi inayosimamia shughuli zote za kiroho kwa watu kimwili na kiroho lakini huduma hizi zinautofauti wa:

                   i.            Kutenda kazi

                 ii.            Kila mtu ufunuo wake

Ndani ya kanisa kuna huduma tofauti tofauti ambazo lengo lake ni kujenga mwili wa Yesu Kristo (kuukamilisha mwili wa Yesu Kristo)

 

HUDUMA TANO ZA MUNGU ( KANISA)

a.     Mitume: Ni mtumwa wa dini anae unganisha watu na Mungu. Ni watu waliotumwa na Mungu na kupewa uwezo katika kufanya umisheni.

b.    Manabii: ni wateuliwa Mungu aliewaita kupeleka ujumbe kwa watumwa.

c.      Wainjilisti: Ni mkristo mwenye utume wa kuhubiri na kutoa elimu ya habari njema za Mungu

d.    Wachungaji:Ni wahudumu ndani ya kanisa au mlezi wa wahumini mpaka amalize safari yake hapa duniani  kwa kuwafikisha salama kuingia mbinguni .


 

e.      Waalimu:Ni watu wanaotoa elimu au ufahamu na ujuzi kuhusu neno la Mungu (kufundisha )

“Naye alitoa wengine kuwa mitume na wengine kuwa manabii kuwa wachungaji na waalimu kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa kristo ujengwe” waefeso 14:11-12.

“Ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu, mwenye kufundisha katika  kufundisha kwake:. Warumi 12:7.


 

 

 

 

 

 

 

 

NDANI YA WOKOVU YAKUPASA KUELEWA HAYA.

 NDANI YA WOKOVU YAKUPASA KUELEWA HAYA.

-Ujue umesamehewa dhambi zako

-Dhambi zako hazikimbiwi tena

-Kuwa na imani kwa Yesu Kristo

-Una haki ya kumili

 

 

KUBADILISHWA JINA.

Kimsingi mtu anatambulika kutokana na jina lake. Lakini kabla ya kuokoka tulikuwa tunaitwa majina ya namna tofauti tofauti kulingana na ukoo au familia uliyozaliwa wapo walioitwa majina bila kujua maana zao au wengine wakijua maana zao, yamkini ni mazuri au mabaya. Mfano 1.Yabesi kwenye Biblia aliitwa jina hilo Yabesi yaani huzuni kwanini ni kwasababu alimzaa kwa huzuni (Alizaliwa kwa huzuni)

Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima  kuliko ndugu zake na mamaye akamuita jina lake Yabesi akisema ni kwasababu nalimzaa kwa huzuni. Huyo Yebesi

 

akamlingana Mungu wa Israel,akisema, Lau kwamba ungenibarikia kwelikweli na kunizidishia  hozi yangu na mkono wake ungekuwa pamoja nami nawe ungelishinda na uovu ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba 1Nyakati 4;9-10

         Kwahiyo tunajifunza mambo yafuatayo hapa

 

 

 

     a)Akamlingana Mungu

 

·        Akaanza kumtafuta Mungu

·        Akaanza kusoma neno la Mungu

·        Akaanza kufunga

·        Akaanza kwenda kanisani

·        Akaanza kuomba

·        Akaanza kwenda mikesha

·        Akaanza kumuabudu Mungu kwa nyimbo na tenzi za Rohoni

Lengo lake huyu Yabesi alishafahamu jina alilopewa siyo zuri bali ni baya hivyo akataka ajikomboe kutokana na nguvu ya jina alilopewa la huzuni (Yabesi)

 

b)Lau kwanza ungenibarikia kwelikweli hapa akawa anamuomba Mungu ambarikie kwelikweli alishaelewa ndani ya jina lake la Yabesi (huzuni) halina Baraka bali ni matatizo matupu tu kwake.

 

c)Kunizidishia kozi yangu

Alikuwa anamtaka Mungu amuongezee umiliki maana alishafahamu umiliki alionao ni mdogo kutokana na jina lake alitakaMungu

-Apanue mipaka yake kama ni kwenye kazi,mashamba, mifugo, fedha, biashara n.k.

 

-Apanue hema yake, maana yake nyumba ziongezeke, kama anayo moja ziongezeke zaidi kwa Jina Yesu. Amen.

 

d)Mkono wako ungekuwa pamoja nami

Alitaka mkono wa Mungu uwe pamoja naye kila mahali, alijua mkono wa Mungu.

 

·        Unanguvu ya kuokoa

·        Ni ulinzi

·        Ni afya njema

·        Ni wa huruma

·        Ni wa kuponya.

Alijua pasipo mkono wa Mungu kumuhatamia hakuna kitakachofanyika.

 

e)Nawe ungenilinda na uovu ili usiwe kwa huzuni yangu.

Alikuwa anatamka Mungu amlinde, ili ile laana ya jina isiwepo ndani yake, alielewa ndani ya jina hilo kuna;

 

·        Kuwaza mambo mabaya

·        Kukata tama.

·        Kuvunjika moyo.

·        Masikitiko.

·        Taabu

·        Laana.

·        Mikosi

·        Umasikini

·        Magonjwa  n.k

 

f)Naye Mungu akamjalia hayo aliyo yaomba.

Alijua maombi yanatufanya tumtafute Mungu “Nanyi mtanitafuta na kuniona mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” Yeremia 29:13

Alijua maombi yanainua mtu, Akawajibu yeyealiyemfanya mzima kuwa mzima ndiye aliyeniambia  jitwike godoro lako uende Yohana 5:11

Alijua maombi yankupa utajiri

“Maana nimejua Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa masikini kwaajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajirikwa umaskini wake 2Wakorintho 8;9

 

“Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya kristo Yesu. “Wafilipi 4;19”

 

Mfano 2. Ibrahimu (Baba yetu wa imani) na mke wake Sara.

Mungu alimuomba kwamba hawezi kumfanya baba wa mataifa mengi kama jina lake litabaki vile vile Abramu na hata mkewe ili awe mama wa uzao mwingi lazima jina libadilike asiitwe tena Sarai bali Sara.

 

“Mimi agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, wala jina lako hutoitwa tena Ibrahimu kwani ni mekuweka uwe baba wa mataifa mengi. Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana nami nitakufanya kuwa mataifa na wafalme watatoka kwako “ Mwanzo 17;4-6.

“Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo hutamwita jina lake Sarai kwakuwa jina lake litakuwa Sara. Nami nitambariki naye atakuwa mama wa mataifa na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake” Mwanzo 17;16.

 

Mfano 3. Yakobo

Yakobo alishindana na malaika wa Mungu, aking’ang’ania  Baraka. Lakini malaika alimuona Yakobo Baraka anazo ila kwasababu ya jina malaika akawa anaona ugumu kutoa Baraka mapaka akamuuliza jina lake naye akasema Yakobo hutaitwa tena Yakobo bali Israel.

“Yakobo akakaa peke yake na mtu mmoja akashindana naye mweleka hataalfajiri. Naye alipoona ya kuwa hamshindi alimgusa panapo uvungu  wa paja lake,

 

 ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. Akasema niache niende maana kunapambazuka. Akasema sikuachi usiponibariki, Akamuuliza jina lako nani, Akasema Yakobo. Akamwambia jinalako halitakuwa tena Yakobo bali Israel maana umeshindana na Mungu na watu nawe umeshinda. Yakobo akamuuliza akasema niambie tafadhali jina lako, Akasema kwanini waniuliza jina langu? Akambariki huko Yakobo akapata mahali pale Peneli maana alisema , nimeonana na Mungu uso kwa uso na nafsi yangu imeokoka” Mwanzo 32;24-30, Kwahiyo sasa baada ya kuokoka tumepewa majina mapya ,Majina yetu yamebadilishwa tunaitwa

 

a)Sisi sasa ni wana wa Mungu/watoto wa Mungu na baada tu ya kutubu dhambi zako (kuokoka) moja kwa moja ulimwengu war oho jina lina badilika.”Tazameni ni pendo la namna gani aliotupa Baba kwamba tuitwe wana wa Mungu na ndivyo tulivyo. Kwasbabu hii ulimwengu haututambui kwakuwa haukumtambua yeye 1Yohana 3;1” “Kwakuwa ninyi nyote  mmekuwa wana wa Mungu  kwa njia ya Imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo  mmemvaa Kristo” Wagalatia 3;26-27.

 

i)Majina yetu yameandikwa katika kitabu cha uzima.

Kwahiyo tunapookoka tunatakiwa kwendelea na wokovu ilimajina yetu yasifutwe.

“Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima name nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu na mbele ya malaika zake” Ufunuo 3;5

“Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandika katika kitabu cha uzima alitupwa katika lile ziwa la moto” Ufunuo 20;15

 

 

ii)Utaanza kuzijua siri za ufalme wa Mbinguni unapokuwa umeokoka unakuwa umejiunganisha na ufalme wa mbinguni yaani Mungu Baba anakujua , Mungu Mwana anakujua, Mungu Roho Mtakatifu anakujua na Malaika zake nao wanakujua. Hivyo utaanza kuzijua siri za ufalme wa Mungu, jinsi ya kuenenda na haki zako.

“Akajibu akawaambia ,Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakukaliwa” Mathayo 13;11.

 

iii)Tunapokea nguvu

Wakristo sisi nguvu yetu ni Roho mtakatifu aliye ndani yetu, hivyo baada ya kuokoka Roho mtakatifu aliye ndani yetu, hivyo baada ya kuokoka anakuwepo ndani sasa ni wewe kwa kumchochea ndani yake kwa kusoma neno la Mungu, kufunga na kuomba, kumsifu Mungu na kumuabudu n.k.

Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yelusalemu na uyahudi na somaria na hata mwisho wan chi” Matendo 1;8

 

Roho mtakatifu akianza kufanya kazi ndani yako mambo kadhaa yatabadilika;

i). Utakuwa jasiri

ii).Hutaogopa vitisho vya watu

iii)Hutaona aibu kushuhudia Neno la Mungu(utalisema neno la Mungu kwa ujasiri

iv)Utakuwa mtii kwa Mungu.

v)Atakubadilisha matendo yako mabaya

vi)Atakupa maarifa, kukuonya, kukwelekeza n.k

 

b)Unakuwa silaha ya bwana ya vita siku zote Mungu ni roho ili atende kazi katika mapambano atakutumia wewe kwenye maombi, Roho mtakatifu atatumia kinywa chako, mikono yako katika kupambana.

 

“Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi nay eye ampendaye na kwa wewe,nilivunja-vunja gari la vita nay eye achukuliwaye ndani yake, na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto na kwa wewe nitawavunja-vunja kijani mwanamume na kijana mwanamke na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake na kwa wewe nitavunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe na kwa wewe nitavunja-vunja maliwali na maakida. Nami nitamlipa babeli na wote wakaao ndani ya ukaldayo, mabaya yao yote waliyoyatenda katika sayuni mbele  ya macho yenu, asema BWANA” Yeremia 15;20-24.

c) Sisi si wa ulimwengu huu.

Kikawaida Yesu kristo yupo siku zote nasi haja ukamilifu wa dahali, Yeye yupo Rohoni lakini anatenda kazi kiroho na kimwili, kimwili tunaonekana jinsi tulivyo lakini kristo si waulimwengu huu. Yesu anasema katika maombi na Mungu Baba.

Mimi nimewapa neno lako na ulimwengu umewachukia kwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu, mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu.Uwatakase kwa ile kweli yako, neno lako ndiyo kweli.” Yohana 17;14-17

 

 

iv)Tunapewa uwezo na mamlaka na amri

Tunaposamehewa dhambi zetu, Yesu kristo anatupa mamlaka juu ya viumbe wote “Akawaita wale thenashara akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhiMathayo 9;1-2.

Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu wawatoe nakupooza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina”  Mathayo 10;1.

 

d)Wewe sasa ni mwali wa moto

Mungu anawapenda wana wake siku zote, katika maisha ya wokovu Mungu anatuwekea moto(miali ya moto) inakuwa ikitunzunguka pande zote. “Na kwa habari ya malaika asema, afanyaje malaika wake kuwa upepo na watumishi wake kuwa miali ya moto “Waebrania 1:7. Wewe ni mtumishi wa Mungu upo katika himaya yake (ndani ya ufalme wake).

Unapata ulinzi.

Unapo okoka unapata ulinzi toka kwa mungu kwa kuwatuma malaika zake wakulinde.  “Malaika wa bwana hufanya k…….akiwazungukia wamchao na kuwaokoa “. Zaburi 34:7

 

Sisi ni Nuru ya ulimwengu

Tunapo okoka tunafanyika kuwa kielelezo kwa wengine, kwa matendo yetu yanatakiwa kuwa mema ili wamtukuze baba yetu wa mbinguni.

Ninyi ni nuru ya ulimwengu mji hauwezi kusitirika ukwa juu yam lima –wala watu hawa washi taa na kiuweka chini ya pishi bali juu ya kiango nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu wapate kuyaona matendo yenu mema wamtukuze baba yenu aliye mbinguni

 

 

Mathayo 5:14-15

Sisi ni chumvi ya dunia

Unapompa Yesu Kristo maisha yako/ Mungu anakufananisha na chumvi, kwamba sisi ni msaada kwa wengine ambao hawamjui Mungu tunapokuwa sehemu hiyo lazima tuwabadilishe.

Ninyi ni chumvi ya dunia lakini chumvi ikiwa imeharibika itakuwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa ila kutupwa nje kukanyagwa na watu” Mathayo 5:13


 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


BAADA YA KUOKOKA

  BAADA YA KUOKOKA

 

KUOKOKA-:

Ni kitendo cha kutubu dhambi zako mbele ya Mungu na wanadamu. Kwa kukiri kwa kinywa chako mwenyewe kwamba umeacha dhambi zako na hautozirudia tena   “namkataa shetani na mambo yake yote”. Kwahiyo tunapo okoka miili yetu  inabaki vilevile lakini roho zetu zinakuwa mpya kwa kutakaswa na Damu ya Yesu Kristo.

Kama vile Mungu Baba alivyo tangulia kuwajua katika kutakaswa na roho hata mkapata kutii na kunyunyizwa Damu ya Yesu kristo. Neema na amani na ziongozwe kwenu” 1petro1:2

 

Kuokoka: Ni mpango wa Mungu kwa wanadamu katika kuishinda dhambi.au ni kitendo cha kumkiri  Yesu kwa kinywa chako na kuamini moyoni mwako kuwa ni Bwana na mwokozi wako.

Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana na kuamini moyoni  mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka  kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”. Warumi 10:9-10

 

Tunapokuwa tumeokoka tunakuwa tumezaliwa mara ya pili kiroho yaani mambo ya kale tunayaacha .

Yesu akajibu akamwambia amini amini nakwambia mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuona ufalme wa Mungu”.  Yohana 3:3

 

Ahimidiwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa rehema zake nyingialituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu katika wafu tupate na urithi  usioharibika usio na uchafu, usionyauka uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu”1petro 1:3-4

Hivyo basi baada ya kuokoka tunapata uzima wa milele ambao Yesu Kristo ametuandalia huko mbinguni, na tunakuwa tunalindwa na nguvu za Mungu hapa duniani kwa njia ya imani.

Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu uliotayari kufunuliwa wakati wa mwisho “1Petro 1:5

 

WOKOVU

Wokovu ni mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu alie potea kupitia dini, Roho Mtakatifu na watumishi wake. Kwahiyo njia ya wokovu ni Yesu Kristo

“Yesu akamwambi mimi ni njia ya kweli na uzima mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi” Yohana 14:6.

Wokovu tulio nao ni wa muhimu sana tunatakiwa kuulinda kwa nguvu zetu zote maana ni kwa ajili ya roho zetu, inapaswa  tumpende Yesu hata kama hatumuoni kimwili lakini kiroho yupo pamoja na sisi.

Naye mwampenda ijapokuwa hamkuomwona ambaye ijapokuwa hamwoni sasa mnamwini na kufurahi sana kwa furaha isiyoneneka yenye utukufu katika kuupokea mwisho wa imani yenu yaani wokovu wa roho zenu”1Petro 1:8-9.

 

Tunapokuwa  ndani ya wokovu hatutakiwi tena kujifananisha na tamaa zetu za kwanza za ujinga. Tunapaswa kuyashika na kuyatii yale anayotaka Yesu Kristo ndiyo tuishi nayo.

Kama watoto wakutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu bali kama yeye alie waita alivyo mtakatifu ninyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote, kwa maana imeandikwa mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu “1Petro:14-16

 

Tuliokolewa si kwa vitu viharibikavyo, Yesu Kristo alikufa kwa ajili yetu kwa aibu ili sisi tupate thamani kubwa ya maisha yetu ya sasa na yabaadaye, maana alitutoa kwenye mwenendo usiofaa.

Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo kwa fedha au dhahabu mpate kufika katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu bali kwa damu ya thamani kama ya mwanakondoo asiye na ila,asiye na waa yaani ya Kristo “1Petro 1:18-19

Tunapo okoka tunapaswa kuwa vielelezo kwa watu wengine (yaani ndugu,marafiki,majirani na jamii kwa ujumla ). Kama tukiwa na matendo mazuri mbele za watu,  hata wewe mwenyewe binafsi, hapo Mungu anatukuzwa kupitia wewe ulieokoka, wewe ni alama ya Yesu Kristo hapa duniani.

 

Wapenzi nawasihi kama wapitaji na wasafiri ziepukeni tamaa za mwili zipinganazo na roho mwe na mwenendo mzuri kati ya mataifa ili iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya wayatazamapo matendo yenu mazuri wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa “1Petro 2:11-12 hata nabii Isaya anasisitiza hilo.

“Jiosheni jitakaseni ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu, acheni kutenda mabaya” Isaya 1:16

Mungu siku zote anatuwazia mema na hataki mtu yeyote apotee kwenye Jehanamu ya moto, yeye ni mwenye huruma anataka tusogee mbele zake na tusemezane naye kuhusu dhambi zetu tulizo zitenda kwa kujua au kwakuto kujua tunazozifahamu na tusizozifahamu anatutaka tuwe watii kwenye kutubu dhambi zetu.

 

“Haya njooni tusezane asema BWANA, dhambi zenu zipojapokuwa nyekundu sana zitakuwa nyeupe kama theluji, zijapokuwa nyekundu kama bendera zinakuwa nyeupe kama sufu kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi, bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga, maana kinywa cha BWANA kimenena haya” Isaya 1;18-20

Tunapo tubu dhambi zetu mbele za Mungu kwanza anatusamehe maovu yetu, pili anatuponya  magonjwa yetu, tatu anatukomboa uhai wetu na kaburi, nne anatuvika taji ya fadhili na rehema, tano aushihisha mema uzee wako na sita aurejesha ujana wako.


 

“Akusamehe maovu yako yote,akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kabuli akutia taji ya fadhili na rehema, aushibisha mema uzee wako, ujana wako ukarejezwa kama tai “Zaburi 103:3-5.

 

Hapo Mungu alikuwa na maana hii;

a)     Akusamehe maovu  yako yote

Kabla ya kuokoka ulikuwa unaishi maisha ya dhambi, ambayo yalikuwa hayampendezi Yesu anakuwa amekusamehe yale maovu yako yote uliyokuwa unayatenda, hivyo unakuwa mpya mbele za Mungu.

b)    Akuponya magonjwa yako yote.

Mungu akisha kusamehe anaanza kushugulika na afya yako maana umefungua moyo wako kwake, na kama ulikuwa na magonjwa ataanza kukuponya.

c)     Aukomboa uhai wako na kaburi.

Kama ulitakiwa kufa basi hapo Mungu anakomboa uhai wako, kutoka kwenye mauti na kukuingiza uzimani tena.

d)    Akutia taji ya fadhili na rehema.

Hapa Yesu Kristo anakuangalia upya tena kwa huruma zake na kukuhurumia.

e)     Aushibishe mema uzee wako.

Mungu  kwa vile yeye ni mwema na mwaminifu uzee wako anaushibisha mema (yaani anakupa mambo mazuri wakati wa uzee wako)


 

f)      Ujana wako ukarejezwa kama tai.

Yale mambo uliotakiwa yakupate mazuri wakati wa ujana wako na sasa yamepotea huna tena zile Baraka za ujana, Yesu Kristo anakwenda kukurejeshea tena kwa nguvu ya ukombozi kwa jina la Yesu halelujaah.

Yesu Kristo akishakusamehe dhambi zako hazikumbuki tena na anaziweka mbali nasi

Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyoziweka mbali dhambi zetu mbali nasi” Zaburi 103:12

“Mimi naam mimi ndimi nifutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe wala sitazikumbuka dhambi zako” Isaya 43:25

“Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito na dhambi zako kama wingu unirudie maana nimekukomboa “ Isaya44:22

 

ALIZICHUKUA DHAMBI ZETU

Yesu Kristo alikuja hapa duniani kwa ajili ya kuja kuchukua maovu yetu ili atengeneze upatanishi kati ya wanadamu na Mungu Baba.

Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi tuwe hai kwa mambo ya haki na kwa kupigwa kwake mliponywakwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo lakini sa mmerudia mchungaji na mwangalizi wa roho zenu. 1Petro 2:24-25.

 

Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu sababu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”. Isaya 53:5.

Yesu Kristo alijeruhiwa kwa ajili ya makosa yetu , maovu na adhabu zetu alizibeba yeye mwenyewe ili sisi tupone, ni jambo la thamani mno alilolifanya Yesu Kristo kwetu ili sisi tupone .

 

Yesu kristo alipigwa, alitemewa mate ili mimi na wewe tupone.

“Wengine wakaanza kumtemea mate wakamfunika uso na kumpiga mkonde na kumwambia tabiri hata watumishi nao wakampiga makofi.”Marko 14:65.

Yesu Kristo alivishwa taji la miiba kichwani.

Wakamvika vazi la rangi ya zambarau wakasokota taji ya miiba wakamtia kichwani.” Marko 15:17.

Yote hayo aliyavumilia ili watu waokolewe  kutoka kwenye dhambi.

 

Yesu Kristo alivuliwa nguo kwa ajili yetu.

        “wakavua nguo wakamvika vazi jekundu

          Mathayo    27:28.

Yesu Kristo alidhihakiwa kwa ajili yetu .

walipokwisha kumthihaki wakalivua lile vazi wakamvika mavazi yake wakamchukua kumsulubisha.” Mathayo 27:31


Walipokwisha kumthihaki waligawa mavazi yake wakapiga kura ili litimie neno lililo nenwa na nabii waligawa nguo zangu kati yao na juu ya vazi langu walipiga kura” Mathayo 27:35

Yesu Kristo alipewa nyongo kwa ajili yetu.

“Wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa.”

 

Mathayo 27:34 “mara mmoja wao                                                                                                                                                                                                                                                                akaenda mbio akatoa sifongo akaijaza siki akaitia juu ya mwanzi akamnywesha”   Mathayo 27:48.

 

Yesu Kristo alichomwa mkuki ubavuni kwa ajili yetu.

 

lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki na mara ikatoka damu na maji” Yohana 19:3, damu na maji yaliyokuwa yakitoka ubavuni mwake, moja moyo wake ulikuwa umepasuka kwa sababu ya mkuki huo.

Hivyo Yesu Kristo aliteswa katika mwili wake na mateso yote aliofanyiwa ili sisi tuokolewe na dhambi ya moto tuliotakiwa, tuliostahili lakini yeye  “aliyachukua maovu yetu” Kama yeye alifanya hivyo kwa ajili yetu basi nasi hatuna budi tuendelee kumtumkia yeye na kuziacha tamaa mbaya za dunia hii kama wafanyavyo mataifa, maadamu tumemkiri yeye tundelee kuwa naye siku zote za maisha yetu.

  

“Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ileile kwa maana yeye aliyeteswa  katika mwili ameachana na dhambi. Tangu sasa msiendelee kuishi katika tama  za mwanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu wakati wetu wa kuaa hapa dunian. Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya mataifa kuenenda katika ufisadi na tama na ulevi na karamu za ulafi na vileo na idadi ya sanamu isiyo halali. Mambo ambayo wao huna kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi uleule usio na kiasi, 

Thursday, February 3, 2022

BADILI MUONEKANO WA BLOG YAKO KWA KUWEKA TEMPLATE MPYA

 Kikawaida watu wengi wanaangaika Sana na hawajui JINSI ya kuweka Template lakini usiwe na wasi wasi leo jibu umelipata na moja kwa moja nitakufahamisha.lakini hapa sizungumzii Template za kawaida Bali nazungumzia zile ambazo umezidownload au kuzinunua na Sasa hapo unashindwa JINSI ya kuibadilisha ileile Kwanza na kuweka MPYA. 

Ifungue blog YAKO Kama siku zote unavyofanya yaani kwa kuisaini-email na password.Nenda upande wa kushoto wa blog YAKO utakutana na vimistari vitatu,bofya hapo.Tafuta sehemu iliyoandikwa Theme ukishaiona bonyeza hapo then tafuta neno lililoandikwa restore,bon bony happy.Tafuta neno lililoandikwa upload, bonyeza hapo.Tafuta file la Template uliyoidownload,bofya hapo ikimamalizika ku upload utakuwa umefanikisha zoezi Zima kwa urahisi kabisa

JINSI YA KUIFUFA BLOG YAKO

 Watu wengi wanajiuliza nitawezaje kuifuta blog yangu? Inawezekana kutokana na sababu mbalimbali ulizoziona wewe.Kuna vitu mbalimbali vilivyoousababishia mpaka kuitaka kuifuta blog YAKO, inawezekana ikisearch kwenye Google watu hawaioni,huioni.Nina maanisha haitokei na sababu nyinginezo.Sasa usiwe na wasi wasi jibu umelipata,na pia kumbuka unapotengeneza blog YAKO no vyema ukatafuta jina la pekee-unique,happy itakuwa rahisi kuonekana  mfano:Blo B yangu hii ya Dalusofa hakuna jina Kama hili duniani kote isipokuwa NI mimi nililolibuno.Kwahiyounapaswa kutulia kidogo na kuwa mbunifu,siku zote unapotengeneza blog YAKO ijalibu baada ya wiki moja.Je ,jina la blog YAKO linatokea? Kama hakuna badilisha jina Hilo.Naona mpaka happy umenielewa,Sasa nisipoteze muda naona unashauku Sana ya kujua JINSI ya kuifuta blog YAKO. 

1.Nenda kwenye Google search andika blogger.com 

2.Sign in,zile taarifa zako ulizofungua blog YAKO yaani email na password 

3.Ikifunguka blog YAKO ,nenda sehemu yenye vialama vitatu upa de wa kushoto,bonyeza happy,utakutana na create post,Sasa wewe itafute setting bonyeza hapo

4.Ikifunguka shuka pole pole  mpaka kwenye neno remove your blog bonyeza hapo  fuata maelekezo utakuwa umemaliza.Kama ujaelewa niulize kwenye email yangu-tuma ujumbe.Asante

Wednesday, February 2, 2022

MAOMBI YA KUJIKOMBOA ROHO YAKO

 Baba Mungu katika jina la Yesu.Naikomboa roho yangu mahala popote ilipo,kwa jina la Yesu.Ewe roho yangu mahali popote ulipo nakuita uje kwangu NDANI ya MWILI wangu kwa jina la Yesu.Roho yangu Kila sehemu iliposhikwa wakuachie kwa jina la Yes.Roho yangu ilipowekwa shimoni nakutoa, ilipowekwa kaburini nakutoa huko kwa jina la Yes.Roho yangu ilipowekwa baharini,kwenye mito,maziwa nakutoa leo kwa jina la Yes,ulipo ilipo kuzimu nakutoa, ilipowekwa kwenye msitu Leo ninaiamuru itoke huko kwa jina la Yesu.Ninaachilia Moto was Roho Mtakatifu uende kwenye Kila Kila chungu kilichoweka roho yangu,Kila pori lililoweka roho yangu nalicho.a Moto kwa jina la Yes.Kila njama zinazowinda roho yangu nazihalibu kwa jina la Yes,Kila mtaabishaji was Roho yangu teketea

MTU WA NDANI

 MTU night Nani?

MTU ni roho mwenye nafsi na inayokaa NDANI ya mwili.Ni roho anayekaa NDANI ya nyumba inayoitwa MWILI

"Mungu was amani mwenyewe awatakase kabisa,nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili bill lawama wakati was kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo".1Wathesalonike 5:23

Tunaona hapa Kuna mambo matatu

I.Roho(spirit)

I I.Nafsi(soul)

II.Mwili(body)

ROHO NI NINI?

ROHO NI I'll sehemu ya MTU yenye ufahamu was Mungu ambayo hufanywa hai na kupewa nguvu na Roho was Mungu,mfano MAOMBI,kumpokea Roho Mtakatifu,Vita vya kiroho,ndoto na mambo mengine.

"Roho ndiyo itiayo uzima,MWILI haufai kitu,maneno hayo niliyowaambia ni roho  tena ni uzima".Yohana 6:63

"Maana Kama vile MWILI pasipo roho umekufa,vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa".Yakobo 2:26

"Nayo mavumbi kuirudia nchi Kama yalivyokuwa nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa".Mhubiri 12:7