Friday, February 4, 2022

VITA VYA KIROHO

 VITA VYA KIROHO

Vita;  Maana yake ni mapambano au mapigano makali yanayohusisha silaha baina ya pande mbili au zaidi, vita ni kufa au kupona lazima mwingine ashinde na mwingine ashindwe. Vita yoyote ile ni lazima ihusishe silaha, wapiganaji(maaskari) na uwanja wa mapambano vita inaweza kuangamiza watu wengi, kuharibu miundo mbinu n.k.

 

VITA VYA KIROHO

Vita vya kiroho ni namna ile ile ya mapambano makali yanayohusisha silaha vile hii inapiganwa katika ulimwengu wa roho kwa kutumia silaha za kiroho maadui hawaonekani kwa macho ya mwili, wala darubini, wala haiwezekani kuwashambulia kwa silaha za kimwili kama vile bunduki, mizinga, ndege za kivita au wanajeshi

 


Hii ni vita vya wafuasi wa Yesu  Kristo na wafuasi wa shetani. Uwanja wa vita ni ulimwengu wa roho. Hii ni vita yenye.

A)  Ni vita yenye wanajeshi,

Maana yake.

-wanaujuzi

-wanamaarifa

-wanahekima (saikolojia ya kijeshi)

-wanamipango

-wanasilaha na vifaa vyote vya mapambano.

 

B)   Hii ni vita ya malaika aliyeasi

-mwenye uwezo na nguvu za kimamlaka.

 

SERIKALI YA KISHETANI

1.     SHETANI (ibilisi)

Hii ni serikali kuu ya shetani kwenye ulimwengu wa    roho.

i)                   Mkuu wa anga(malaika wa mbingu)

Huyu ni shetani anayekaa kwenye anga kwa ajili ya kuzuia maombi.

“Akaniambia ee Daniel mtu upendwaye sana yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimama kiwima maana kwako nimetumiwa sana. Na aliponiambia neno hili nalisimama nikitetemeka,

ndipo akaniambia usiogope Daniel kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwaa nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini  mkuu wa ufalme wa uajemi alimpinga siku ishirini na moja, bali tazama huyo Mikaeli mmoja wa hao wakuu wa mbele akaja kumsaidia nami nikawaacha huko pamoja na wafalme wa uajemi.”Daniel 10;11-13


ii)                Mkuu wa ardhi

Huyu ni malaika wa kuzimu anayesimamia kuharibu ardhi.

 

“Na juu yaowanaye mfalme  naye ni malaika wa kuzimu jina lake kwa kiebrania ni Abadoni na kwa kiyunani analojina lake Apolioni, ufunuo 9;11,

 

“Kisha nikaona mnyama mwingine akipanda juu katika nchi naye alikuwa na pembe mbili mfano wa mwana-kondoo akanena kama joka, ufunuo 13;11

 

iii)              Mkuu wa bahari.

Huyu ni malikia wa bahari anayetawala maeneo yote yanayo husu maji na ndiye anayesimamia mitindo yote duniani.

“Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari mwe nye pembe kumi na vichwa saba juu ya pembe zake ana vilemba kumi na juu ya vichwaa vyake majina ya makufuru , ufunuo 13;1

 

2.     Serikali ndogo ya kishetani.

Mkuu wa mapepo (beelizeburi)

Huyu ni mkuu wa mapepo yote au ni shetani anayesimamia mapepo yote kwa kuyatuma na kuyapa amri na ndiyo maana walimwambia Yesu anatoa mapepo kwa nguvu ya beelizeburi.

Lakini Yesu alikuwa anayatoa kwa kutumia nguvu za Mungu aliyemtuma hapa duniani kwa kufungua watu kuwatoa kwenye mateso yao.

 

 

“Nao waandishi walioshuka  kutoka Yerusalemu wakasema ana Beelizabuli na kwa mkuu wa pepo hawatoa pepo. Akawaita akawaambia kwa  mifano awezaye shetani kumtoa shetani na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama’ Marko 3.22-24.

Mashetani wa kitendo hiki ndiyo yanayosimamia vitengo mbalimbali ili kuwatesa watu.

 

Vitengo vya kishetani

-kitengo cha mateso

-kitengo cha kufunga mafanikio

-kitengo cha kifo na mauti

-kitengo cha umasikini na ufukara

-kitengo cha mafarakano na fitina

-kitengo cha laana na balaa

-kitengo cha taabu na shida

-kitengo cha kukataliwa-

-kitengo cha kuharibu mimba

-kitengo cha kutokuolewa na kutokuoa

-kitengo cha magonjwa na maradhi

-kitengo cha matatizo na uharibifu

-kitengo cha majanga

-kitengo cha ajali

-kitengo cha chuma ulete

-kitengo cha kuleta uchungu

-kitengo cha kafara na umwagaji damu

Vipo vitengo vingi vya kishetani lengo lake ni kuleta uharibifu kwenye maisha ya watu, kuna mapepo yanayo

-Tambaa (mapepo yanayotambaa)

-Tembea (mapepo yanayo tembea)

-Ruka (mapepo yanayoruka)


 

3.     Falme za giza

Hizi ni mamlaka za giza zinazosimamia kwenye utawala wao, hapa utakuta kuna;

i). mamlaka za giza

ii). Wakuu wa giza

iii)majeshi ya pepo wabaya

 

“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili,juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” Waefeso 6;12.

 

4.     Idara za giza

Hizi ni idara za kishetani kwenye serikali yake ili iweze kushughulikia mambo yao ya uhalibifu. Kuna idara’

i). idara ya giza ya mapepo

ii)idara ya giza ya mizimu

iii)idara ya  giza ya miungu

iv). Idara ya giza ya majoka

v). idara ya giza ya kichawi

mfano; idara ya wachawi, Namna wanavyotenda kazi.

-uchawi wa kutumia dawa

-uchawi wa kutumia tunguli

-uchawi wa kutumia vitabu

 

Pamoja na yote hayo kuhusu selikali ya kishetani lakini tunashinda zaidi ya kushinda na tunapaswa kuwa na silaha za vita za kiroho ndipo tutaweza kumshinda kwa namna ya kiroho na hata kimwili kwa Jina la Yesu.

 

 

SILAHA ZA VITA ZA KIMUNGU.

Hizi ni silaha za vita vyetu. Ulimwengu wa roho kuna zana maalumu za maangamizi unazotakiwa kuzitumia kama askari wa Yesu kristo.

 

“Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake, vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani “waefeso 6;10-10.

 

Kuwa hodari katika Bwana.

Tunapaswa kuwa hodari katika Bwana na uwezo wa nguvu zake, kwamba tunaamini Yesu Kristo kwamba yeye ndiye muweza wa yote kwa kuwa hodari,

 

“Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa, usiogope wala usifadhaike  kwa kuwa Bwana Mungu wako yu pamoja nawe kila uendako” Yoshua 1;9

Lakini uhodari huo tunaupata kwa njia ya kujilinda na kila mashambulizi yoyote ya kishetani yatakayofanyika juu yako.

i)Toba..(utakatifu)

Kabla ya kuingia kwenye ulimwengu wa roho kwa ajili ya vita, unapaswa uombe toba juu yako na watu wote wanaomzunguka. Ili kusiwepo na kizuizi chochote katika kurusha makombola, kuna dhambi umeitenda kwa kujua au kwakutojua.

 

 Omba toba na rehema mbele za Mungu maana tunaingia vitani kwenye ulimwengu wa roho ili utakapo tamka tu moto uende moja kwa moja kwa adui

 

 

“lakini  maovu yenu yamewafarikima ninyi na Mungu wenu na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone hata hataki kuskia kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu, midomo yenu imenena uongo na ndimi zenu zimenong’ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki  wala hapana atetaye kwa kweli hutumainia ubatili hunena uongo, hupata mimba ya madhala na kuzaa uovu”Isaya 59:2-4

 

ii)Damu ya Yesu Kristo

Shetani anaigopa damu  ya Yesu Kristo. Hii pia ni silaha nyingine, unapoomba jifunike kwa damu ya Yesu inanena mema siku zote na hii ni silaha ya kumshinda shetani.

“ Na Yesu mjumbe wa agano jipya na damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya habili” waebrania 12:24

 

“Nao wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo na kwa neno la ushuhuda wao-----------“Ufunuo12:11

 

(iii) Moto wa Roho Mtakatifu (Roho Mtakatifu)

Katika kuomba ni vizuri ukamualika Roho Mtakatifu akusaidie katika kuomba, maana yeye atawasha moto ndani yako.

 

 

“Hata ilipotimia siku ya pentekoste walikuwako wote mahali pamoja, kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukaenda kasi, ukajaza nyumba yote waliokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizo gawanyika na kama ndimi za moto ulio wakalia kila mmoja wao, wote wakajazwa Roho Mtakatifu wakaanza kusema      kwa lugha nyingine, kama roho alivyowajalia kumka” Matendo2:1-4

 

“Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake, yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto”. Mathayo 3:11

 

(iv) Imani:

Katika kuomba lazima uwe na imani, kwamba kile uncho kiomba kinafanyika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili unatakiwa usiwe na shaka yoyote unapo sema nawakimbiza, nawashambulia ujue wanashambuliwa kweli

 

“Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gidieoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii, ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba” Waebrania 11:32-33

“Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani ambayo  kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya Yule mwovu” waefeso 6:16

(v) Maarifa:

Lazima uwe na maarifa katika kushambulia. Unapaswa kuelewa na muda gani wa kushambulia, ni mahali gani pa kushambulia ,je adui au maadui wapo hiyo sehemu au wameshaondoka? Je wapo kushoto,kulia, mbele,nyuma juu au chini? Ili utakapo fyatua iende. Maarifa haya ya kijeshi  lazima uyajue  vizuri ni silaha gani uitumie na wao wanasilaha zipi unapaswa uwasome vizuri.

 

Mfano: Wewe  unasilaha ndogo kama vile bastora halafu mwenzako anatumia mzinga katika kukushambulia, lakini kwa vile tunazo silaha za bwana za vita.

 

“ Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa mimi name nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi, kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako------------“Hesabu4:6.

 

(vi) Wokovu:

Wokovu ulionao ndiokibali cha ruhusa cha kuingia ulimwenguni wa mapambano.

“Tena ipokeeni chapeo ya wokovu-----“Waefeso 6:17

 

(vii) Maombi

Tunapokuwa ndani ya ufalme wa Mungu tunapaswa kuomba bila kukoma(bila kuchoka ) siku zote za maisha yetu. Tukijiombea wenyewe na kuwaombea wengine. Maombi ni silaha zidi ya adui.

 

        Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika roho mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote” waefeso 6:18

“Dumuni sana katika kuomba mkikesha katika kuomba huku na shukrani” wakolosai 4:2

 

“Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni roho radhi lakini mwili ni dhaifu “mathayo 26:41

“Ombeni bila kukoma” 1wathesalomike 5:17

 

(viii) Jina la Yesu:

Jina la Yesu katika ulimwengu wa roho ni kama bomu hatari na tunapaswa kuomba kwa jina la Yesu, maana ni jina lipatalo majina yote.

 

“Amini, amini nawaambieni yeye aniaminiye mimi kazi nizifanyazo mimi yeye naye atazifanya naam na kubwa kuliko hizo atafanya kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu hilo nitalifanya ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana,mkiomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya” Yohana 14:12-14

“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno akamkiri jina lile lipitalo kila jina”Wafilipi 2:9

“Juu sana kuliko ufalume wote na mamlaka na nguvu na usultani na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni     humu tu, bali katika ule ujao pia”. Waefeso 1:21

 

xi) Neno la Mungu.

Neno la Mungu ni silaha nyingine zidi ya shetani na malaika zake unapolitumia neno la Mungu linakusaidia kwenye mambo kadha wa kadha.

 

 

Mfano;

a)Neno la  Mungu ni chakula cha kiroho “Maneno yako yalionekana nami nikayala na maneno yako yaliyokuwa ni furaha kwangu na shangwe ya moyo wangu maana nimeitwa kwa jina lako EE Bwana Mungu wa majeshi “ Yeremia 15;16.

 

b) Neno la Mungu ni moto na nyundo “Je neno langu si kama moto? Asema Bwana na nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? Yeremia 23;29.

 

 

c)Neno la Mungu ni hai.

Maana Neno la Mungu li hai………waebrania 4;12

 

d)Neno la Mungu lina nguvu tena linanguvu….waebrania 4;12

 

e) Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga.

 

f)Neno la Mungu lachoma.

Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uuwao wote ukatao kuwili tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake tena li jepesi

Kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo” waebrania 4;12.

 

a)    Neno la Mungu ni ngao

Kila neno la Mungu limehakikishwa, yeye ni ngao yao wamwaminio” Mthali 30;5

 

h). Neno la Mungu ni silaha.

Moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi :Zaburi 119:9

 

i)Neno la Mungu ni taa.

Neno lako ni taa ya miguu  yangu na mwanga wa njia yangu, Zaburi 119;105.

 

 

 



 

UPENDO WA MUNGU

 UPENDO WA MUNGU

Upendo: Ni hisia kali alizonazo mtu kwa mtu, kitu na namna mbalimbali zinazomuhasiri mtu.

Aina za upendo.

                                 i.            Upendo wa mzazi na mtoto

                               ii.            Upendo wa mume na mke

                            iii.            Upendo wa kitu

                            iv.            Upendo wa Mungu(Agape love)

                               v.            Upendo wa ndugu

Upendo wa Mungu (Agape love) kimsingi hakuna jambo la muhimu na la maana sana zaidi ya upendo, maana Mungu mwenyewe ni pendo.

“Nasi tumefahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi na kuliamini. Mungu ni pendo naye akaye katika pendo , hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake”.1Yohana 4:16

Mungu mwenyewe aliupenda ulimwengu alijua ndani ya ulimwengu amewaweka watu na watu hao lazima waokolewe ndiyo maana akamtuma mwana wake wa pekee ili kila amwaminie asipotee bali wote wawe na uzima wa milele, huo ni upendo wa Mungu kwetu sisi.

“kwa maana jinsi Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele” Yohana 3:16

 

Ukifuatilia huduma nyingi au makanisa mengi upendo wa Mungu haupo, kwa nini? Watu wanajifikilia wenyewe tu na hawana habari na watu wengine lakini. Biblia inasema kama sina upendo      ( kwa watu) nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao( shaba isiyo na kitu ndani yake)

 


“Nijaposema kwa lugha za wanadamu na malaika kama sina upendo nimekuwa kama shaba iliyo na upatu uvumao” 1wakoritho 13;1

 

Hata kama nitakuwa nimefahamu mambo mengi ya kiroho na kimwili kama sina upendo si kitu mimi. Hata kama wewe si kitu.

a.     Nijapokuwa na unabii .

b.     Kujua siri zote na maarifa yote

c.      Nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima. Kama sina upendo si kitu mimi.

d.     Hata nikitoa mali zangu zote kuwapa maskini.

e.      Hata nikijitoa mwili wangu niunguwe moto, kama sina upendo haisaidii kitu.

“Tena nijapokuwa na unabii na kujua siri zote na maarifa yote . nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo si kitu mimi. Tena nikijitoa mwili wangu niunguwe moto, kama sina upendo hainifani kitu” 1wakoritho 13:2-3

                   NGUVU YA UPENDO:

Upendo huvumilia:panapokuwa na upendo ndani ya kanisa, kwenye biashara, kazini, nyumbani kwenye jamii na sehemu zingine upendo huvumilia yote hata kama mtu amekutendea mabaya au akakusemea vibaya utavumilia kwa sababu ya upendo.

 

Upendo hufadhili: Kwa sababu ya upendo unaweza ukapata msaada kutoka kwa watu, mtu anaweza akakuonea huruma, akakusaidia kukulipia ada, kukupa chakula n.k.

 


Upendo hauhusudu: Kwenye upendo wivu usiokuwa na maana utaondoka, bali kutakuwa na wivu wa maendeleo.

 

Upendo hautakabari: Upendo unapokuwepo basi ujeuri utaondoka, kwa kila mmoja hamtafanyiana kiburi.

 

Upendo haujivuni: Panapo kuwa na upendo hakuna majivuno kujiona wewe ni bora kuliko mwingine jambo hilo linakuwa halina nafasi yake.

 

Upendo haukosi kuwa na adabu: Penye upendo lazima adabu itakuwepo, kuheshimiana.

 

Upendo hautafuti mambo yake:Upendo ukiwepo hauwezi kuanza kutafuta madhaifu ya mtu jinsi alivyo muumba Mungu ataendelea kupenda tu.

 

Upendo hauoni uchungu: upendo ukiwepo uchungu ya kuanza  kumjutia mtu na kuya weka ndani / kuyatunza ndani ya moyo wako kwa kuanza kumuachukia, kumsema vibaya utamuachilia na kuendelea  kumpenda (kupenda)

 

 

Upendo hauhesabu mabaya: upendo hauhesabu mabaya uliyotendewa.

 

Upendo haufurahii udhalimu: kama unampenda ndugu yako, au ameharibikiwa anatenda mabaya ni mrevi, kama unaupendo utamwombea  kwa Mungu amrehemu na atokane na hayo. Vile vile utamuonya kwa njia anayoenenda nayo kwamba sio nzuri.

 

 

Upendo hufurahi pamoja na kweli: mahali penye upendo panatakiwa kuwa na ukweli na uwazi ili zile taarifa  anazozipata mtu au alizo pata mtu ni vyema ukweli ukawepo ili mfurahi kwa pamoja.

 

Upendo huamini yote: kwenye upendo lazima tumaini liwepo, ili yule uliye au sehemu uliyopo uaminike.

 

 Upendo hutumaini yote: kwenye upendo lazima tumaini liwepo la kuona matumaini ya mbele au yatalajiwayo.

 

Upendo hustahimili yote :kwenye upendo kuna uimara, kusimama imara bila kusurubishwa.

 

Upendo haupungui neno wakati wowote:  Upendo ukiwepo utapewa kuyafuata maneno au neno zuri ili kuboresha mahusiano yaliyopo.  “Upendo huvumilia, hufadhili, upendo huwahusudu, upendo hautakabiri, haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake,haoni uchungu, hauhesabu mabaya, haufurahi udhalimu balihufurahi pamoja na kweli, huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote, upendo haupungui neno wakati wowote, bali ukiwepo unabii utabatilika, zikiwepo lugha zitakoma, yakiwepo maarifa yatabatilika “. 1wakolitho13:4-8

Upendo haunahofu: kwenye upendo hofu itakuwa haina nguvu bali mtu atakuwa jasiri, asiyeogopa chochote, na ambaye mwenye hofu hajakamilishwa na upemdo bado.

 

“Katika pendo hamna hofu, lakini  pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo”.1Yohana 4:18

 


Kanisa linapokuwa na upendo hapo Mungu anafurahi sana kwasababu  linamuakilisha yeye hapa duniani.

 

Alama za upendo:

                                           i.            Upendo umetoka kwa Mungu

                                         ii.            Kila apendaye amezaliwa na Mungu

                                      iii.            Anamjua Mungu

                                      iv.            Mungu amemtuma mwanawe wa pekee ulimwenguni(Yesu Kristo) ili tupate uzima wa milele.

 

“Wapenzi na mpendane kwa kuwa pendo latokea kwa Mungu na kila apendaye amezaliwa na Mungu. Yeye asiye penda hakumjua Mungu kwa maana Mungu ni upendo  katika hili pendo Mungu lilionekana kwetu kwamba Mungu amemtuma mwanae pekee ulimwenguni ili tupate uzima kwa yeye”1Yohana 4:7-9

v. Tumepatanishwa na Mungu baba

vi. Mungu hukaa ndani yetu

vii. Upendo wake umekamilika ndani yetu

viii. Ametushirikisha roho wake

 

“Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo,haya matatu na katika haya lililo kuu ni upendo” 1wakoritho13:13.

 

Kwahiyo tunaona hapo lililo  kuu ni upendo. Watu wengi kwenye jamii upendo umepoa , akienda kazini upendo haupo, mtaani upendo haupo, nyumbani upendo haupo, sasa basi kanisa ndilo linatakiwa kuwa tibia watu waliokosa upendo  ndani yao kwa jina la Yesu Kristo.Ameni

Kama tukisema kanisa tunampenda Mungu huku tunawachukia ndugu zetu ni waongo.

“Mtu akisema nampenda Mungu naye anamchukia ndugu yake ni mwongo kwa maana asiempenda ndugu yake ambaye amemuona hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumuona” 1Yohana 4:;20

“Upendano wa ndugu na udumu msisahau kuwafundisha wageni, maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua” Waebrania 13:1-2

 

Vitu vinavyo haribu upendo:

Moja ya vifungo kinacho sumbua watu ni kifungo cha tabia iwe ni kwenye:

Þ   Urafiki au mahusiano

Þ   Kwenye kazi au ofisini

Þ   Kwenye biashara na taasisi

Ili uweze kuendelea unatakiwa uwe na tabia nzuri.

“Hekima hiyo siyo ile ishikayo kutoka juu bali ni  ya dunia ya tabia ya kibinadamu na shetani. Yakobo 3;15.

 

Tabia;  ni hali au sifa za nafsi alizonazo mtu. Kwahiyo hapa utaona matendo, miitikio au mienendo itakayoweza kuonekana  wazi. Mfano; kunatabia za miti, wanyama, binadamu n.k, wapo wanaosema mazoea ujenga tabia.

 

Aina za tabia

Kunatabia ambazo mtu anakuwa

i)Amezaliwa nazo (kiasili)

ii).  Ameiga tabia kutokana na mazingira aliyokulia au kulelewa.

 

-Kuna wapo waliolelewa na mama peke yake

      -Kunawapo walio lelewa na baba peke yake

      -Kunawapo waliolelewa na mama na baba

      -Kuna wapo waliolelewa na ndugu

  -Kunawapo waliojilea wenyewe

Kwahiyo kwa namna zote hizo lazima mtu huyo hawezi kufanana na mtu mwingine kwasababu ya namna na mazingira aliyokulia au kulelewa lazima yatakuwa tofauti.

 

Tabia za kibinadamu

A.   Kuna msondani (introvert)

Mtu huyu ni Yule ambaye yeye sio mwongeaji sana, ni mkimya.

   Aina zake

                             I.            melancholy(melancolim)

-wapole na wasio na maneno mengi
-wanahisia kali za upendo( upendo wa dhati)

-wanajali wenzao

-wanamaombi mazuri kiimani

-wanahuruma

-wanabusara na hekima

 

                         II.            phlegmatic (pragmatic)

-ni mabingwa wa kuhairisha mambo

-wanapenda kupuuzia mambo

-watafiti na kufuatilia mambo

 

B.   Kuna msonje (extrovert)

Mtu huyu ni Yule ambaye ni muongeaji sana na anayeweza kujielezea kwa namna mbalimbali.

Aina zake

i). Sanguine

-ni wacheshi sana

-watu wenye maneno mengi wasio pumzika kuongea

-wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wanaongea.

-wana karama ya kuhubiri

-wanapenda kujaribu kila kitu..mfano petro.

 


ii). Choleric

-ni wakali

-wasiopenda kudharauliwa au kuonewa

-ni viongozi wa asili ya kuzaliwa

-wanajiamini

-hawaongei wala kucheka hovyo.

 

TABIA MBAYA AMBAZO MUNGU HAZIPENDI

i). Uzushi

ii). Umbea

iii). Usingiziaji

iv). Uongo

v).Uzinzi

vi).Ufitini

vii). Uasherati

viii).Ugomvi

ix). Kiburi

x). Jeuri

xi). Husuda

xii). Kijicho

xiii). Na mambo yote yanayofanana na hayo.

 

KUNAVITU ILI MTU AWEZE KUFANIKIWA

Ili mtu afanikiwe kunahitaji mambo mawili,

a)Kipawa / Karama.

Kipawa kinaweza kumfikisha mtu mbele za watu wakubwa na kujulikana.

“Zawadi ya mtu humpatia nafasi, humleta mbele ya watu wakuu” Mithali. 18;16

Mtu anaweza kuwa na kipawa  Fulani lakini tabia yako mbaya hakuna atakaye tamani kuwa karibu nawe.

 

b) Tabia ya mtu

Ili Mungu akutumie kwa kiwango cha juu ni muhimu kuanza kwa kubadili tabia yako mbaya na kuwa na tabia nzuri mbele ya Mungu na wandamu.

“kwa maana ndugu mnapendwa  na Mungu twajua uteule wenu ya kwamba injili yetu haikuwafililia katika maneno tu bali na katika nguvu na katika Roho Mtakatifu na zilivyokuwa tabia zetu kwenu kwa ajili yenu” 1wathesolenike 1;4-5.

“Lakini ndugu zangu mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo, 1wakorintho 3;1.