Friday, February 4, 2022

UWEZA WA MAOMBI,

 UWEZA WA MAOMBI,

Uweza; Maana yake ni nguvu

Maombi; Maana yake ni mawasiliano au kuzungumza na Mungu.

-Ni mamlaka ya Mungu inayotenda kazi katika ulimwengu wa roho.

-Ni nguvu za Mungu zinazohusika kwa kujibu jambo Fulani.

 

AINA ZA MAOMBI

1.     Maombi ya kawaida.

Mfano:- maombi ya kumbariki mtu

-         Maombi ya toba na rehema

-         Maombi ya kuombea chakula

-         Maombi ya kuombea safari

-         Maombi ya kumshukuru Mungu

-         Maombi ya kuombea ndoa  n.k

2.     Maombi ya vita

Mfano- maombi ya mkesha.

-maombi ya mfungo

-maombi ya kuharibu falme na  mamlaka za giza

- maombi ya kuombea wagonjwa.

- maombi ya kufunguliwa

- maombi ya ukombozi

- maombi ya urejesho (kurudisha) n.k.

Vilevile maombi ya muda mrefu na maombi ya muda mfupi yapo katika hizo aina za maombi.


 

MAMBO UNAYOPASWA KUYAJUA KUHUSU MAOMBI.

i). kupitia maombi Mungu anaweza kufanya mambo yote

‘lakini Yule malaika akamwambia, usiogope Zakaria maana dua yako imesikiwa na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanaume na jina lake utamwita Yohana ‘Luka 1;13

 

Siku hizo Hezekia akaugua akawa katika hatari ya kufa, Isaya nabii mwana wa Amozi akamjia akamwambia Bwana asema hili , tengeneza mambo ya nyumba yako maana utakufa wala hutapona Basi Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwambia Bwana ukumbuke sasa jinsi nilivyokwenda mbele yako katika  kweli na moyo mkamilifu na kutenda  yaliyomema machoni pako Hezekia akalia sana sana. Ikawa kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia kusema, Rudi ukamwambie Hezekia mkuu wa watu wangu Bwana Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, nimeyasikia maombi yako na kuyaona machozi yako, tazama nitakuponya siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana, Tena nitazidisha siku zako kiasi cha miaka kumi na mitano, name nitakuokoa wewe na mji huu na mkono wa mfalme wa Ashuru, name nitakulinda mji huu kwa ajili yangu na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, 2wafalme 1-6.

 

ii). Maombi kwa Mungu yanapaswa kuwa ni ya kuendelea kuwa sehemu ya maisha ya mkristo.

‘Akawaambia mfano ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tama Luka 18;1.

 

iii). Katika maombi tunatakiwa kupeleka haja zetu kwa Mungu.

‘Msijisumbue kwa neno lolote bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu.

 

iv). Tunatakiwa tuwe na imani.

‘Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima na oambe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yoyote maana mwenye  shaka ni kama wimbi la bahari lililichukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku “ Yakobo 1;5-6.

“Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa Yule na Bwana atamwinua hata ikiwa amefanya dhambi atasamehewa Yakobo 5;15.

 

v). Tunatakiwa kuomba kwa jina la Yesu

“Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu hilo nitalifanya ili baba atukuzwe ndani ya mwana.

Yohana 14;13.

 

vi). Mungu anasikia maombi ya watu wote

“ katika shida yangu nalimwita Bwana na hekaluni mwake, kilio change kikaingia maskioni mwake , ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, misingi ya  milima ikasuka-suka…. “Zaburi 18;6-7.

 

“kwa kuwa Bwana huwaakia wahitaji wala hawadharau wafungwa wake Zaburi 69;33.

 

Vii). Mungu anajibu maombi.

“ walilia naye Bwana akasikia , akawaponya na taabu zao zote,  Zaburi 34;17.


Lakini panapo usiku wa manane Paulo na sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza ghafla kukatokea matetemeko kuu la nchi hata msisingi ya gereza ikatikisika na mara hiyo milango ikafunguka vifungo vya wote  vikalegezwa. Matendo 16;25-26.

 

viii). Tunapaswa kuomba kwa bidii.

Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita, Akaomba tena mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake , Yakobo 5;17-18.

 

Maana ya kuomba kwa bidii,

-kuomba kwa kuweka akili zako zote kwenye jambo hilo

-kuomba kwa ujasiri

-kuomba kwa nia yako bila kukata tama.

-kuomba kwa nia moja.

-kuomba kila siku bila kuchoka.

-kuomba bila kuogopa

-kuomba kwa maarifa

-kuomba kwa mamlaka ya Mungu

Kumbuka sisi ni wana wa Mungu, hivyo tumepewa amri juu ya nguvu za giza kwamba tukitamka neno juu yao linakuwa vile vile kwa jina la Yesu- Amen.

 

Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za Yule adui wala hakuna kitu kitakacho wadhuru


Tumepewa amri ya kukanyaga nyoka na nge.

*kukanyaga tunguli

*vipembe

*mikoba

*kukanyaga nguvu za adui

*mapepo na majini

*kukanyaga silaha zote za kichawi.

Kila kitu kinatakiwa kukitakasa kwa Damu ya Yesu Kristo.

Kila sehemu tunayoingia tunatakiwa kupatakasa kwa Damu ya Yesu Kristo.

Hakuna kitakachowadhuru

 

FAIDA ZA MAOMBI

a)    Hutusaidia kukua kiimani.

“Kisha akawaleta nje akasema Bwana zangu yanipasa nifanye nini nipate  kuokoka? Wakamwambia mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako, Matendo 16;30-31.

b)    Mambo yako ya ndani yatafunguliwa

Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako “zaburi 119;18.

 

c)     Maombi ni ulinzi

Basi akamfukuza huyo mtu akaweka makerubi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga  wa moto uliogeuka huko na huko kulinda njia ya mji wa uzima “Mwanzo 3;24.

 

d)    Maombi yanatufanya tumtafute Mungu,

Nanyi mtaniita mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza, Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa mioyo yenu yote.

 

 Yeremia 29;12-13.

Ndipo Bwana akaniambia umeona vema kwa maana ninaliangalia neno langu ili nilitimize ‘Yermia 1;12’

Naliangalia neno langu ili nilitimize, hivyo Mungu hawezi kujipinga mwenyewe.

e)     Utamruhusu Roho mtakatifu akutumie

“Kadharika Roho naye kutusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa “warumi 8;26.

‘Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja yeye Yule akiangamia kila  mtu peke yake kama apendavyo yeye. “1wakoritho 12;11.

 

f)      Utatumika vizuri kwa Mungu.

Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao wakawaacha waende zao, Matendo 13;2-3.

 

g)    Utakuwa na nguvu za Mungu

“Tangu siku za Yohana mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu nao wenye nguvu wauteka, Mathayo 11;12

 

h)    Maombi yanainua mtu

“Yesu akamwambia simama jituike godoro lako uende. Mara Yule mtu akawa mzima akajitwika godoro lake akaenda Nayo ilikuwa  ni sabato siku hiyo, Yohana 5;8

 

Na kule kuoma kwa imani kutamwokoa mgonjwa Yule na Bwana atamwinua hata ikiwa amefanya dhambi atasamehewa ‘Yakobo 5;15

 

 

UMUHIMU WA  KUFUNGA (mfungo).

Mfungo; Ni hali ya  kukaa bila kula chakula  au kinywaji ili kutekeleza masuala ya imani yako. Mfungo unatoa sauti inayopenya hadi kwenye kiti cha Mungu Baba na kuleta mabadiliko ya kudumu katika ulimwengu wa mwili, Hii ni kanuni ya ulimwengu wa Roho ili kufanya jambo lililokusudiwa litokee.

 

 

WALIOFUNGA KWENYE BIBLIA.

a)    Yesu kristo,

Yesu kristo alifunga siku arobaini (40)

‘Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani ili ajaribiwe na ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho  akaona njaa, Mathayo4;1-2.

 

b)    Musa

Musa naye alifunga siku arobaini 40)ili asemezane na Mungu.

Nikaanguka nchi mbele za Bwana siku arobaini usiku na mchana kama pale kwanza sikula chakula wala kunywa maji kwasababu ya makosa yenu yote mliyokosa kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana kwa kumkasirisha, Torati 9;18.

Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake hakula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi “kutoka 34;28”

c)     Daniel alifunga siku ishirini na moja(21)”Katika “siku zile mimi Daniel nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu” Danieli 10;13,”……. lakini mkuu wa ufalme alinipinga siku ishirini na moja” Daniel 10;2.

 

d)    Esta; Esta na wayahudi alifunga siku tatu ili aingie kinyume cha sheria kwa mfalme.

“Uende ukakusanye wayahudi wote  waliopo hapa shushani mkafunge kwa ajili yangu, msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku na mchana nami na wajakazi wangu tutafunga vilevile, kisha nitaingia kwa mfalme kinyume cha sheria, nami nikiangamia na niangamie “Esta 4;16.

e)     Watu wa Ninawi.

Hawa walifunga wakimlilia Bwana awaepushe na hatari iliyokuwepo mbele yao.

“Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu, wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo, Yohana 3;5

f)      Barnaba, Simion, Lukio Mkirene, Manaeni

Nao hawa walifunga ila Biblia haijaonyesha.

Walifunga siku ngapi

Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga.

Kwahiyo ni mifano michache tu kwa waliofanya kulikana na sababu Fulani Fulani kwao.

 

AINA ZA MIFUNGO (fasting)

1.     Mfungo mwepesi.

Huu ni mfungo ambao mtu aliyefunga anaweza kunywa uji, maji na vitu vyepesi. Lengo la mfungo huu ni kujinyenyekeza mbele za Mungu au kutaka kumpa Mungu nafasi yake. Mfano. Mtu anasema nitafunga siku 3,21 au 40 nitakuwa nakunywa maji na jioni nafungulia.

 

 

2.     Mfungo mkavu.

Huu ni mfungo wa kutaka kitu Fulani kwa Mungu ili ujibiwe haraka. Mfano Esta na wayahudi, walifunga siku tatu bila kula chochote na majibu yakaja bila kuchelewa.

 

SIFA ZA MFUNGO.

a)    Kuongozwa na Roho ,takatifu

Mara Roho akamtoa aende nyikani, Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na shetani, naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu na malaika walikuwa wakimhudumia , Marko 1;12-13.

 

b)    Mfungo ufanywe katika unyenyekevu,

 ilikuwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia kutoka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao” 2zanyakati 7;14

 

c)     Kuambatane na kuomba

“Ndipo mwakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao wakawaacha waende zao. “matendo 13;3

 

d)    Mfungo ufanywe kwa furaha.

“Tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana, maana ujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga.Amini nawaambieni wamekwisha kupata thawabu yao” Mathayo 6;16.

 

 

e)     Unapofunga watu wasikujue

Bali wewe ufungapo jipake mafuta kichwani unawe uso. Ili usionekane na watu kuwa unafunga ila na Baba yako aliyesirini na Baba yako aonaye sirini atakujazi, ‘Mathayo 6;17-18

 

NDANI YA MFUNGO KUNA VITU HIVI

Siku zote unapomuona kufunga mfungo wa aina yoyote ile tambua vitu hivi lazima vijitokeze au  viwepo.

-Malaika watakuwepo wakikihudumia

-Shetani naye atakuwepo ili akujaribu.

-Utajisikia mchovu au kuishiwa nguvu

-Mwili utaisha (kupungua) lakini mtu wa ndani atakuwa na nguvu za rohoni.

-Utukufu wa Mungu utakufunika.

“Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama ngozi ya uso wake iling’aa nao wakaogopa kumkaribia “kutoka 34;30

 

FAIDA/ UMUHIMU WA MFUNGO

-Kuonyesha utii mbele za Mungu

“Lakini  hata sasa anasema Bwana, nirudieni mimi, kwa miyo yenu yote na kwa kufunga na kwa kulia na kwa kuomboleza Yoeli 2;12

 

-Ili kujinyenyekeza mbele za Mungu

“Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe na kwa ajili ya watoto wetu na kwa mali yetu yote Ezra 8;21.


 

-Ili kupata msaada,

“Basi tukafunga tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo, naye akatutakabali, Ezra 8;23

 

-Ili katika udhaifu wetu nguvu za Mungu zionekana,

“Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta  ‘Zaburi 109; 24

 

-Ili kuomba Rehema.

Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi na dua pamoja na kufunga na kuvaa nguo za magunia na majivu, Daniel 9;3

 

-Ili Hunao imani na kuongeza ujasiri.

“Uende ukawakusanye wayahudi wote waliopo hapa shushani mkafunge kwa ajili yangu’ Esta 4;16.

 

-Huongeza/ huleta nguvu ya maombi

‘Bali mimi walipougua wao, nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga, maombi yangu yakarejea kifuani mwangu “ Zaburi 35;13

 

-Kukuza kanisa na huduma ya Mungu isonge mbele.

“Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msipokee neema ya Mungu bure (kwa maana asema wakati uliokubalika na likusudia siku ya wokovu nalikusaidia, tazana wakati uliokubaliwa ndio sasa tazama siku ya wokovu ndiyo sasa)” 2wakoritho 6;1-2.

 


-Kuufanya ulimwengu wa Roho uwe wazi  :”Maana ingawa tunaenda  katika  mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili.(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka kujiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii kristo ;2wakoritho 10;3-5

 

-Kuutiisha mwili,

‘Basi nasema enendeni katika Roho, wala hamtazitimiza kamwe tama za mwili, kwasababu mwili hutamani ukishindana na Roho na Roho kushindana na mwili, kwa maana hizi zinapingana hata hamwezi kufanya mnayotaka,Lakini mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria’ wagalatia 5;16-18.

 

 

 

 


VITA VYA KIROHO

 VITA VYA KIROHO

Vita;  Maana yake ni mapambano au mapigano makali yanayohusisha silaha baina ya pande mbili au zaidi, vita ni kufa au kupona lazima mwingine ashinde na mwingine ashindwe. Vita yoyote ile ni lazima ihusishe silaha, wapiganaji(maaskari) na uwanja wa mapambano vita inaweza kuangamiza watu wengi, kuharibu miundo mbinu n.k.

 

VITA VYA KIROHO

Vita vya kiroho ni namna ile ile ya mapambano makali yanayohusisha silaha vile hii inapiganwa katika ulimwengu wa roho kwa kutumia silaha za kiroho maadui hawaonekani kwa macho ya mwili, wala darubini, wala haiwezekani kuwashambulia kwa silaha za kimwili kama vile bunduki, mizinga, ndege za kivita au wanajeshi

 


Hii ni vita vya wafuasi wa Yesu  Kristo na wafuasi wa shetani. Uwanja wa vita ni ulimwengu wa roho. Hii ni vita yenye.

A)  Ni vita yenye wanajeshi,

Maana yake.

-wanaujuzi

-wanamaarifa

-wanahekima (saikolojia ya kijeshi)

-wanamipango

-wanasilaha na vifaa vyote vya mapambano.

 

B)   Hii ni vita ya malaika aliyeasi

-mwenye uwezo na nguvu za kimamlaka.

 

SERIKALI YA KISHETANI

1.     SHETANI (ibilisi)

Hii ni serikali kuu ya shetani kwenye ulimwengu wa    roho.

i)                   Mkuu wa anga(malaika wa mbingu)

Huyu ni shetani anayekaa kwenye anga kwa ajili ya kuzuia maombi.

“Akaniambia ee Daniel mtu upendwaye sana yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimama kiwima maana kwako nimetumiwa sana. Na aliponiambia neno hili nalisimama nikitetemeka,

ndipo akaniambia usiogope Daniel kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwaa nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini  mkuu wa ufalme wa uajemi alimpinga siku ishirini na moja, bali tazama huyo Mikaeli mmoja wa hao wakuu wa mbele akaja kumsaidia nami nikawaacha huko pamoja na wafalme wa uajemi.”Daniel 10;11-13


ii)                Mkuu wa ardhi

Huyu ni malaika wa kuzimu anayesimamia kuharibu ardhi.

 

“Na juu yaowanaye mfalme  naye ni malaika wa kuzimu jina lake kwa kiebrania ni Abadoni na kwa kiyunani analojina lake Apolioni, ufunuo 9;11,

 

“Kisha nikaona mnyama mwingine akipanda juu katika nchi naye alikuwa na pembe mbili mfano wa mwana-kondoo akanena kama joka, ufunuo 13;11

 

iii)              Mkuu wa bahari.

Huyu ni malikia wa bahari anayetawala maeneo yote yanayo husu maji na ndiye anayesimamia mitindo yote duniani.

“Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari mwe nye pembe kumi na vichwa saba juu ya pembe zake ana vilemba kumi na juu ya vichwaa vyake majina ya makufuru , ufunuo 13;1

 

2.     Serikali ndogo ya kishetani.

Mkuu wa mapepo (beelizeburi)

Huyu ni mkuu wa mapepo yote au ni shetani anayesimamia mapepo yote kwa kuyatuma na kuyapa amri na ndiyo maana walimwambia Yesu anatoa mapepo kwa nguvu ya beelizeburi.

Lakini Yesu alikuwa anayatoa kwa kutumia nguvu za Mungu aliyemtuma hapa duniani kwa kufungua watu kuwatoa kwenye mateso yao.

 

 

“Nao waandishi walioshuka  kutoka Yerusalemu wakasema ana Beelizabuli na kwa mkuu wa pepo hawatoa pepo. Akawaita akawaambia kwa  mifano awezaye shetani kumtoa shetani na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama’ Marko 3.22-24.

Mashetani wa kitendo hiki ndiyo yanayosimamia vitengo mbalimbali ili kuwatesa watu.

 

Vitengo vya kishetani

-kitengo cha mateso

-kitengo cha kufunga mafanikio

-kitengo cha kifo na mauti

-kitengo cha umasikini na ufukara

-kitengo cha mafarakano na fitina

-kitengo cha laana na balaa

-kitengo cha taabu na shida

-kitengo cha kukataliwa-

-kitengo cha kuharibu mimba

-kitengo cha kutokuolewa na kutokuoa

-kitengo cha magonjwa na maradhi

-kitengo cha matatizo na uharibifu

-kitengo cha majanga

-kitengo cha ajali

-kitengo cha chuma ulete

-kitengo cha kuleta uchungu

-kitengo cha kafara na umwagaji damu

Vipo vitengo vingi vya kishetani lengo lake ni kuleta uharibifu kwenye maisha ya watu, kuna mapepo yanayo

-Tambaa (mapepo yanayotambaa)

-Tembea (mapepo yanayo tembea)

-Ruka (mapepo yanayoruka)


 

3.     Falme za giza

Hizi ni mamlaka za giza zinazosimamia kwenye utawala wao, hapa utakuta kuna;

i). mamlaka za giza

ii). Wakuu wa giza

iii)majeshi ya pepo wabaya

 

“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili,juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” Waefeso 6;12.

 

4.     Idara za giza

Hizi ni idara za kishetani kwenye serikali yake ili iweze kushughulikia mambo yao ya uhalibifu. Kuna idara’

i). idara ya giza ya mapepo

ii)idara ya giza ya mizimu

iii)idara ya  giza ya miungu

iv). Idara ya giza ya majoka

v). idara ya giza ya kichawi

mfano; idara ya wachawi, Namna wanavyotenda kazi.

-uchawi wa kutumia dawa

-uchawi wa kutumia tunguli

-uchawi wa kutumia vitabu

 

Pamoja na yote hayo kuhusu selikali ya kishetani lakini tunashinda zaidi ya kushinda na tunapaswa kuwa na silaha za vita za kiroho ndipo tutaweza kumshinda kwa namna ya kiroho na hata kimwili kwa Jina la Yesu.

 

 

SILAHA ZA VITA ZA KIMUNGU.

Hizi ni silaha za vita vyetu. Ulimwengu wa roho kuna zana maalumu za maangamizi unazotakiwa kuzitumia kama askari wa Yesu kristo.

 

“Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake, vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani “waefeso 6;10-10.

 

Kuwa hodari katika Bwana.

Tunapaswa kuwa hodari katika Bwana na uwezo wa nguvu zake, kwamba tunaamini Yesu Kristo kwamba yeye ndiye muweza wa yote kwa kuwa hodari,

 

“Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa, usiogope wala usifadhaike  kwa kuwa Bwana Mungu wako yu pamoja nawe kila uendako” Yoshua 1;9

Lakini uhodari huo tunaupata kwa njia ya kujilinda na kila mashambulizi yoyote ya kishetani yatakayofanyika juu yako.

i)Toba..(utakatifu)

Kabla ya kuingia kwenye ulimwengu wa roho kwa ajili ya vita, unapaswa uombe toba juu yako na watu wote wanaomzunguka. Ili kusiwepo na kizuizi chochote katika kurusha makombola, kuna dhambi umeitenda kwa kujua au kwakutojua.

 

 Omba toba na rehema mbele za Mungu maana tunaingia vitani kwenye ulimwengu wa roho ili utakapo tamka tu moto uende moja kwa moja kwa adui

 

 

“lakini  maovu yenu yamewafarikima ninyi na Mungu wenu na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone hata hataki kuskia kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu, midomo yenu imenena uongo na ndimi zenu zimenong’ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki  wala hapana atetaye kwa kweli hutumainia ubatili hunena uongo, hupata mimba ya madhala na kuzaa uovu”Isaya 59:2-4

 

ii)Damu ya Yesu Kristo

Shetani anaigopa damu  ya Yesu Kristo. Hii pia ni silaha nyingine, unapoomba jifunike kwa damu ya Yesu inanena mema siku zote na hii ni silaha ya kumshinda shetani.

“ Na Yesu mjumbe wa agano jipya na damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya habili” waebrania 12:24

 

“Nao wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo na kwa neno la ushuhuda wao-----------“Ufunuo12:11

 

(iii) Moto wa Roho Mtakatifu (Roho Mtakatifu)

Katika kuomba ni vizuri ukamualika Roho Mtakatifu akusaidie katika kuomba, maana yeye atawasha moto ndani yako.

 

 

“Hata ilipotimia siku ya pentekoste walikuwako wote mahali pamoja, kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukaenda kasi, ukajaza nyumba yote waliokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizo gawanyika na kama ndimi za moto ulio wakalia kila mmoja wao, wote wakajazwa Roho Mtakatifu wakaanza kusema      kwa lugha nyingine, kama roho alivyowajalia kumka” Matendo2:1-4

 

“Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake, yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto”. Mathayo 3:11

 

(iv) Imani:

Katika kuomba lazima uwe na imani, kwamba kile uncho kiomba kinafanyika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili unatakiwa usiwe na shaka yoyote unapo sema nawakimbiza, nawashambulia ujue wanashambuliwa kweli

 

“Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gidieoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii, ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba” Waebrania 11:32-33

“Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani ambayo  kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya Yule mwovu” waefeso 6:16

(v) Maarifa:

Lazima uwe na maarifa katika kushambulia. Unapaswa kuelewa na muda gani wa kushambulia, ni mahali gani pa kushambulia ,je adui au maadui wapo hiyo sehemu au wameshaondoka? Je wapo kushoto,kulia, mbele,nyuma juu au chini? Ili utakapo fyatua iende. Maarifa haya ya kijeshi  lazima uyajue  vizuri ni silaha gani uitumie na wao wanasilaha zipi unapaswa uwasome vizuri.

 

Mfano: Wewe  unasilaha ndogo kama vile bastora halafu mwenzako anatumia mzinga katika kukushambulia, lakini kwa vile tunazo silaha za bwana za vita.

 

“ Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa mimi name nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi, kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako------------“Hesabu4:6.

 

(vi) Wokovu:

Wokovu ulionao ndiokibali cha ruhusa cha kuingia ulimwenguni wa mapambano.

“Tena ipokeeni chapeo ya wokovu-----“Waefeso 6:17

 

(vii) Maombi

Tunapokuwa ndani ya ufalme wa Mungu tunapaswa kuomba bila kukoma(bila kuchoka ) siku zote za maisha yetu. Tukijiombea wenyewe na kuwaombea wengine. Maombi ni silaha zidi ya adui.

 

        Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika roho mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote” waefeso 6:18

“Dumuni sana katika kuomba mkikesha katika kuomba huku na shukrani” wakolosai 4:2

 

“Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni roho radhi lakini mwili ni dhaifu “mathayo 26:41

“Ombeni bila kukoma” 1wathesalomike 5:17

 

(viii) Jina la Yesu:

Jina la Yesu katika ulimwengu wa roho ni kama bomu hatari na tunapaswa kuomba kwa jina la Yesu, maana ni jina lipatalo majina yote.

 

“Amini, amini nawaambieni yeye aniaminiye mimi kazi nizifanyazo mimi yeye naye atazifanya naam na kubwa kuliko hizo atafanya kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu hilo nitalifanya ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana,mkiomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya” Yohana 14:12-14

“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno akamkiri jina lile lipitalo kila jina”Wafilipi 2:9

“Juu sana kuliko ufalume wote na mamlaka na nguvu na usultani na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni     humu tu, bali katika ule ujao pia”. Waefeso 1:21

 

xi) Neno la Mungu.

Neno la Mungu ni silaha nyingine zidi ya shetani na malaika zake unapolitumia neno la Mungu linakusaidia kwenye mambo kadha wa kadha.

 

 

Mfano;

a)Neno la  Mungu ni chakula cha kiroho “Maneno yako yalionekana nami nikayala na maneno yako yaliyokuwa ni furaha kwangu na shangwe ya moyo wangu maana nimeitwa kwa jina lako EE Bwana Mungu wa majeshi “ Yeremia 15;16.

 

b) Neno la Mungu ni moto na nyundo “Je neno langu si kama moto? Asema Bwana na nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? Yeremia 23;29.

 

 

c)Neno la Mungu ni hai.

Maana Neno la Mungu li hai………waebrania 4;12

 

d)Neno la Mungu lina nguvu tena linanguvu….waebrania 4;12

 

e) Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga.

 

f)Neno la Mungu lachoma.

Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uuwao wote ukatao kuwili tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake tena li jepesi

Kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo” waebrania 4;12.

 

a)    Neno la Mungu ni ngao

Kila neno la Mungu limehakikishwa, yeye ni ngao yao wamwaminio” Mthali 30;5

 

h). Neno la Mungu ni silaha.

Moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi :Zaburi 119:9

 

i)Neno la Mungu ni taa.

Neno lako ni taa ya miguu  yangu na mwanga wa njia yangu, Zaburi 119;105.