NDOA NA FAMILIA
Nini maana ya ndoa?
NDOA NI muunganiko Kati ya mwanaume na mwanamke kuishi pamoja Kama mume na mke muda wao wote wa maisha Yao(umri lazima uzingatiwe)
"Kwahiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe,nao watakuwa mwili mmoja".Mwanzo 2:24
Maana yake hapo,Yale majukumu uliyokuwa unayafanya kwa wazazi wako hayataendelea kwa asilimia zote Bali majukumu yote yatakuwa NI kwa mke wako na familia yako,mnaenda kuungana kimwili na huyo mke wako uliyemchagua.Kwa maana nyingine unaweza kusema NI kuwa na makazi yenu,kutiana Moto na kusaidiana,kujitegemea kwa mahitaji yenu ya KILA siku.Hiyo ndiyo maana ya utamwacha baba na mama yako
KWA MUJIBU WA SHERIA YA NDOA YA TANZANIA(Mwaka 1971 kifungu Cha 9)
KILA nchi inautaratibu wake kwenye masuala ya ndoa, lakini kwa MUJIBU wa sheria ya ndoa Tanzania inasema;
i.Wanandoa wawe wamekubariana pasipo kulazimishwa na mtu
ii.Ndoa NI ya mwanamke na mwanaume
iii.Ni ndoa ya kudumu maishani
"BWANA Mungu akasema si vema mtu HUYU awe peke yake,nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye". Mwanzo 2:18
Kwahiyo Mungu alimuumba mwanamke KUTOKA kwa mwanaume ili awe msaidizi wa mwanaume
"BWANA MUNGU akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala, Kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akaufunika nyama mahali make".Mwanzo 2:21
Hivyo mwanamke alitokana na mwanaume yaani mume anatakiwa amuone mke wake NI Kama NI moja ya sehemu yake ya MWILI (ubavu wake)
"Na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA MUNGU akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu".Mwanzo 2:22
KUPITIA ule ubavu wa mwanaume,Mungu akaamua Sasa aufanye kwa kuweka nyama ili aweze KUTOKA mtu ambaye NI mwanamke ambaye anafanana na Adamu kwa njinsi na jinsia tofauti
"Adamu akasema,Sasa hutu NI mfupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama yangu,Basi ataitwa mwanamke kwa maana ametwaliwa katika mwanaume".Mwanzo 2:23
Kumbe mke wako unatakuwa umuone Kama NI moja ya mifupa yako na nyama ya MWILI wako.Kama utamuona mke wako kwa namna hiyo hakika utampenda Sana na kumjari kwa thamani kubwa maana NI moja ya viungo vyako,mfano akilia,akiumia maana yake wewe hauwezi kunyamaza na kumpuuzia lazima utamuangalia Kama vile jicho lako likiingia mchanga huwezi kuliacha Bali utaliangalia.Ndivyo hivyo mke wako unatakuwa umuone hivyo
NDOA NI AGANO (Mkataba)
Tunapozungumzia agano tunamaanisha makubaliano ya wawili na NI lazima kuwepo na kiapo.Ndoa ilianzishwa na Mungu mwenyewe,tunaweza kusema NI Taasisi iliyoanzishwa pale kwenye bustani ya Edeni.Maana yake Kuna kanuni zake na sheria zake za kuenenda au kufuatwa.Biblia inasema ndoa na iheshimiwe na watu wote
"NDOA na iheshimiwe na watu wote na makazi yawe Safi kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu".Waebrania 13:4
I..Ndoa lazima iheshimiwe,maana yake mtu anapokuwa yupo NDANI ya ndoa NI heshima kwa watu wote,Basi na nyinyi wanandoa jiheshimuni
ii.Malazi yawe Safi,maana yake NDANI ya ndoa nyinyi wenyewe mnapaswa kuwa safi kwamba unamke wako,unamume wako huyo ndiye atakayemaliza hamu yako ya tendo la ndoa na siyo mwingine wa nje,kwenda kufanya uzinzi hapana,lazima tendo la ndoa lifanywe na wanandoa tu wenyewe wawili tu!!!
NDOA NI ZAWADI TOKA KWA MUNGU
MUNGU ametupa ZAWADI hii inabidi na sisi tuilinde,tuithamini,tuitunze,tuikubali,tuipende n.k.Haiwezekani upewe ZAWADI harafu uipuuze,hila Jambo linakuwa si la kiungwana hata kidogo.Basi tukitambua ndoa NI ZAWADI TOKA KWA MUNGU Basi tutaiheshimu
NDOA NI TAASISI TAKATIFU
KILA mwanandoa atimize wajibu wake,kupendana,mapenzi yawepo (msinyimane)kujitambua kwamba wewe NI mwanandoa,kuachana na ubinafsi,kuendelea kujifunza kuhusu masuala ya ndoa,mtendee mwenzako mambo mazuri,NI baraka ,NI umoja n.k
MAMBO YA KUZINGATIA WEWE MWANANDOA
Aliyeanzisha ndoa NI Mungu mwenyewe,kutaka kuoa au kuolewa NI wazo la Mungu kabisa,ndoa NI kuondoa upweke,ndoa NI furaha,mwanaume NI kichwa,mwanamke NI moyo-msiadizi,ndoa inahitaji muwe pamoja hata Kama mpo mbali lakini muwe pamoja kimawazo,ndoa lazima itunzwe
FAMILIA NI NINI?
Familia NI mahusiano ya undugu wa damu au usio wa damu,lakini Mimi hapa nazungumzia familia ya wanandoa katika maisha Yao,kwa maana wanaoanzisha familia hiyo na waliopo
"Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wake Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke aliwaumba".Mwanzo 1:27
Kwa mantiki hiyo Mungu ndiye yeye aliyemuunganisha mwanaume na mwanamke ili watengeneze familia Yao
"Mungu akawabarikia,Mungu akawaambia zaeni mkaongezeke,mkaijaze nchi....".Mwanzo 1:28
Kimsingi hapa Mungu alikuwa anawataka wakatengeneze familia kwa kuzaa WATOTO ili waijaze nchi.Ndiyo dhana yangu ya familia hapa.Nawewe ambaye hauna mtoto, ninaiamuru mamlaka za mbinguni zikupatie WATOTO katika jina la YESU Kristo,Seema Amina napokea
FAMILIA INAHUSIKA NA VITU GANI?
1.BABA NDIYE KICHWA CHA FAMILIA
Maana yake,yeye ndiye msimamizi mkuu katika kutatua changamoto mbalimbali ZILIZOpo NDANI ya familia.Yeye ndiye kiongozi wa familia katika kuiendesha kwa kuwajibika kwake
2.MAMA NDIYE MSAIDIZI(MOYO) WA FAMILIA
Maana yake NI msaidizi wa baba(mume wake) kuhakikisha familia Yao ipo sehemu Fulani katika kuiongoza.Hivyo baba na mama ndio viongozi wa kuhakikisha familia inakaa vizuri
3.WATOTO/MTOTO
Katika familia WATOTO NI viongozi au NI watendaji wadogo katika familia ambao Hawa ndiyo kichocheo Cha wazazi kufanya bidii zote kuhakikisha wanakuwa nafuraha pamoja na amani NDANI ya familia Yao
4.NDUGU
Hapa nazungumzia ndugu wa Aina yoyote awe baba,mama,Bibi,shangazi n.kwote hao NI ndugu,hivyo Kama mume na mke NI kuhakikisha familia yenu inakuwa salama
5.MARAFIKI
Hawa NI moja ya ndugu katika familia NI kutokana na namna mnavyoishi nao,hapa nazungumzia wafanyakazi wenzako,majirani n.k.Mume na mke mnapaswa kuenenda kwa akili si kila ushauri mnaopewa muufanyie kazi,hapana,kaaeni Kwanza utathimini na mchambue je,unafaa au laah!
6.UPENDO
Upendo ndiyo kila kitu katika maisha ya ndoa na familia bila upendo hapo ndoa haipo itakuwa NI kivuli Cha ndoa,upendo ndiyo tunda la roho
"Liking tunda la Roho NI upendo,furaha,amani,uvumilivu,utu wema,fadhili,uaminifu,upole,kiasi,juu ya mambo Kama hayo hakuna sheria".Wagalatia 5:22-23
"Enyi waume wapendeni wake zenu Kama Kristo naye alivyolipenda kanisa,akajutoa kwa ajili yake".Waefeso 5:25,endelea kusoma mpaka mstari wa 33.Kumbe wanaume tunatakiwa kuwapenda wake ZETU,wanawake wao wanataka kupendwa
7.UTII(KUTII)
Katika familia utii ukiwepo Basi mambo yataenda vizuri Sana lakini si kila kitu utii tu hapana.Wanawake wao ni mnatakiwa kuwatii waume zenu,wanaume wao wanapenda utii KUTOKA kwa mke wake
"Ninyi wake watiini waume zenu Kama ipendezavyo katika BWANA*Wakolosai 3:18
"Ninyi WATOTO watiini wazazi wenu katika Mambo yote,maana Jambo hili lapendeza katika BWANA".Wakolosai 3:20
"Ninyi watumwa watiini hao ambao kwa mwili NI bwana zenu.....".Wakolosai 3:22
KATIKA FAMILIA NYINGI UTAKUTA UTII HAUPO,WAKE HAWATII WAUME ZAO,WATOYO NAO HAWATII WAZAZI WAO,WATUMWA NAO HAWATII BWANA ZAO.FAMILIA IKIFIKIA KATIKA MAZINGIRA HAYA INAKUWA KATIKA HATARI KUVWA SANA YA SHETANI KUINGIA NA KULETA MAMBO YAKE.KUMBUKA SHETANI YUPO ANAZUNGUKA ZUNGUKA AKITAFUTA MTU AMMEZE,AMEZE NDOA.FAMILIA IKISHAINGIA KWENYE MIGOGORO HAPO KAMA MUME NA MKE HAWATAKUWA MAKINI KUJUA TATIZO NI NINI,FAMILIA INAWEZA IKAHARIBIKA KABISA
BWANA YESU AKUSAIDIE KATIKA JINA LAKE LA THAMANI