Baada ya kuanza kuelewa jinsi Sponsored Posts zinavyofanya kazi,hatua muhimu inayofuata ni kuongeza thamani ya blog yako.Kampuni hazilipi tu kwa sababu una blog,bali zinalipa kwa sababu blog yako inaweza kuwasaidia kufikia watu wanaoweza kuwa wateja wao.Thamani ya blog yako inategemea mambo mengi kama vile ubora wa maudhui,uaminifu wa wasomaji,idadi ya wageni wanaotembelea blog na uwezo wako wa kuwasilisha ujumbe wa kampuni kwa njia yenye kuvutia.
1. Jenga Chapa Binafsi (Personal Brand)
Mwandishi wa blog mwenye jina
linalojulikana huwa na nafasi kubwa ya kupata wadhamini kuliko mtu
asiyejulikana.
Chapa binafsi inamaanisha watu
wajue:
· Wewe ni nani.
· Unaandika kuhusu nini.
· Unasimamia maadili gani.
· Kwa nini wasomaji wakuamini.
Kwa mfano:kama blog yako inajulikana
kwa kutoa mafundisho ya kiroho,elimu ya maisha au taarifa za teknolojia, watu
wataanza kukuona kama mtu mwenye mamlaka katika eneo hilo.
2. Kuwa na Wasomaji Wanaoshiriki
Idadi ya wageni pekee haitoshi.Kampuni
zinapenda kuona kama wasomaji wako wanashiriki.
Mambo yanayoonyesha ushiriki
ni:
· Maoni kwenye makala.
· Kushirikishwa kwa makala kwenye mitandao
ya kijamii.
· Barua pepe kutoka kwa wasomaji.
· Muda ambao watu hutumia kusoma makala.
Blog yenye wasomaji 5,000
wanaoamini maudhui yako inaweza kuwa na thamani zaidi kuliko blog yenye wageni
wengi lakini wasiojali.
3. Tengeneza Orodha ya Wasomaji Kupitia Email
Email marketing ni moja ya mali
muhimu kwa blogger.
Unaweza kuwaomba wageni wako
waandike barua pepe zao ili wapokee:
· Makala mpya.
· Mafundisho.
· Habari muhimu.
· Matangazo maalumu.
Faida yake ni kwamba
hauitegemei kabisa mitandao ya kijamii au Google. Unaweza kuwafikia wasomaji
wako moja kwa moja.
4. Tumia Mitandao ya Kijamii Kuongeza Nguvu ya
Blog
Blog na mitandao ya kijamii
vinaweza kusaidiana.
Baada ya kuchapisha makala:
· Shiriki Facebook.
· Tuma kwenye WhatsApp.
· Tumia Telegram.
· Tumia X au LinkedIn kulingana na mada.
Kampuni zinapokuona una uwezo
wa kusambaza maudhui kwa watu wengi,thamani yako inaongezeka.
5. Tengeneza Portfolio ya Kazi Zako
Portfolio ni mkusanyiko wa kazi
zako bora.
Inaweza kuwa na:
· Viungo vya makala ulizoandika.
· Kampuni ulizowahi kushirikiana nazo.
· Takwimu za wasomaji.
· Ushuhuda kutoka kwa wateja.
Portfolio huwasaidia wadhamini
kuona uwezo wako kabla hawajakupa kazi.
6. Tafuta Wadhamini wa Kimataifa
Usijiwekee mipaka kwenye
kampuni za eneo lako pekee.Mtandao unakupa nafasi ya kufanya kazi na watu
kutoka nchi mbalimbali.
Unaweza kutafuta wadhamini
kutoka:
i.
Marekani.
ii.
Ulaya.
iii.
Asia.
iv.
Afrika
nyingine.
Blog yenye lugha ya Kiingereza
mara nyingi huwa na nafasi kubwa zaidi ya kufikia soko la kimataifa.
7. Andika Kwa Lugha Mbili Ikiwezekana
Kwa blogger wa Tanzania,kutumia
Kiswahili na Kiingereza kunaweza kuongeza nafasi.Kiswahili kinakufanya uwafikie
wasomaji wa Afrika Mashariki,wakati Kiingereza kinakufungulia soko la kimataifa,pia
ni vizuri ukaweka kipengere cha kutafsiri ili uweze kupata watu wa nchi tofauti
tofauti .Unaweza kuwa na:
i.
Makala
za Kiswahili kwa wasomaji wa ndani.
ii.
Makala
za Kiingereza kwa wasomaji wa kimataifa.
8. Kuwa Mtaalamu wa Eneo Fulani
Wadhamini wanapenda wataalamu.
Badala ya kuandika kila kitu
bila mwelekeo,chagua maeneo ambayo unaweza kujenga jina.
Mfano:
· Blockchain na teknolojia.
· Biashara mtandaoni.
· Maendeleo binafsi.
· Elimu.
· Huduma za kijamii.
· Mafundisho ya Kikristo.
Kadri unavyokuwa na utaalamu wa
kitu fulani kuhusu mada moja wapo hapo juu,ndivyo thamani yako inavyoongezeka.
9. Ongeza Huduma Nyingine Mbali na Sponsored
Posts
Unaweza kuongeza mapato kwa
kutoa huduma nyingine kama:
· Kuandika makala kwa watu wengine.
· Kutengeneza matangazo.
· Ushauri wa blog.
· Kutengeneza maudhui ya mitandao ya
kijamii.
· Kuuza vitabu vya kidijitali.
Blog inaweza kuwa kituo cha
biashara yako yote ya mtandaoni.
10. Linda Uaminifu wa Wasomaji
Usikubali kila tangazo kwa
sababu ya pesa.
Kabla ya kukubali Sponsored
Post jiulize:
i.
Je,bidhaa
hii inawasaidia wasomaji wangu?
ii.
Je,kampuni
hii inaaminika?
iii.
Je,nitakuwa
tayari kuitangaza mbele ya watu wanaoniamini?
Ukipoteza uaminifu wa wasomaji,unaweza
kupoteza thamani ya blog yako.
Hitimisho
Kujenga blog yenye thamani ni
mchakato wa muda mrefu.Wadhamini wakubwa hawataangalia tu idadi ya makala
ulizoandika,bali wataangalia ushawishi wako,uaminifu wako na uwezo wako wa
kufikia watu.Mmiliki wa blog anayejenga chapa binafsi,anayetengeneza maudhui
bora na anayeheshimu wasomaji wake anaweza kubadilisha blog kuwa chanzo kikubwa
cha kipato.Katika sehemu inayofuata tutajifunza makosa makubwa yanayowazuia bloggers
kupata Sponsored Posts,pamoja na mbinu za kuyarekebisha ili kuongeza nafasi ya
kupata mapato.
