Wednesday, May 20, 2020

MAHUBIRI


SOMO:KUTIMIZA KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO
MUHUBIRI:MINISTRY PASTOR(MP):DAVIS MAKENGA
Kusudi:Ni wazo au lengo lililowekwa ndani ya moyo wako ili liweze kutimiza lile ambalo Mungu ameweka katika maisha yako.
-watu wengi wamekua wakiishi
 katika maisha yao bila kujua kusudi alilo nalo
-Watu wanaishi maisha feki
1Yohana 3:8, Malaki 4:5-6,Luka 1:13, Yeremia 1:4
Kabla sijakuumba nalikujua.Maana yake Mungu anajaribu kumuambia Yeremia kwamba natambua kabisa nilichokuwa nafanya pindi nilipokuumba
-Nimekuweka juu ya mataifa na juu ya Falme; Maana yake kamuumba kwa kusudi lake ndani yake
.Kuwa Nabii wa mataifa
.Kuwa juu ya mataifa
.Kuwa juu ya falme
Akampa na kazi ya kufanya; kung’oa,kubomoa, kuharibu ,kuangamiza,kujenga na kupanda.
Kuwepo kwako ni kwa ajili ya kusudi la Mungu ndani yako.Ndani ya kusudi lako upo uwezo na mamlaka ya kuamuru na kubadilisha mazingira pinzani ndani yako.Utakutana na falme na ngome za maadui,vita,mapepo,wachawi utapambana navyo.
JINSI YA KUTAMBUA KUSUDI LAKO
Kutambua kusudi ulilo nalo ni kazi sana mfano mtu anafanya biashara hii au anafanya kazi ile au anajaribu kufuga kuku,kulima lakini mtu anaona bado kuna kitu kinadaiwa anataka akifanye.
Ili uweze kujua upo ndani ya kusudi la Mungu ni lazima kiwango cha amani yako kiendane na kiwango cha kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako
Lipo jambo umewahi kulifikiria kulifanya au tayari umekwisha lifanya na ukasikia amani ndani ya moyo wako hata kama ni dogo ,tambua kua hilo ndilo kusudi la Mungu kwako



SOMO:KUVUNJA NDOA ZA KISHETANI
MUHUBIRI: MINISTRY PASTOR(MP):DAVIS MAKENGA
Ndoa:Ni muunganiko kati ya mwanamke na mwanaume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao.
Kiingereza:Is a formal legal bond relationship between husband and wife
Aina za ndoa
.Ndoa za ukubwani
.Ndoa za utotoni
Kisheria(Ndoa zinazotambulika)
+Ndoa za kimila
+Ndoa za kiserikali
+Ndoa za kidini
-Za Kikristo
-Za kiislam
Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.Kimsingi Mungu ndiye akiyeanzisha ndoa(Taasisi ya kwanza duniani ni ndoa).Moja ya maagano ambayo Mungu ameweka ni ndoa
Mwanzo 2:24
Shetani anajua mtu huyu anaomba,anachokifanya anakutengenezea mke/mume wa kiroho.Unaweza kufunga ndoa/kufungishwa ndoa na mapepo katika ulimwengu war oho.Unaota ndoto unakutana na mtu Fulani unayemfahamu au usiyemfahamu, unaanza kufanya nae mapenzi maana yake unashiriki naye kwenye ulimwengu wa r oho.Kama umeoa/umeolewa utapata upinzani sana kwenye suala la kuoa/kuolewa.Mkataba wa maandishi,maneno,cheti,pete,mavazi,vyakula n.k
Torati 7:2-4, Kutoka 34:15-16,Walawi 17:7





SOMO:ROHO YA BWANA INIJILIE
MUHUBIRI: MINISTRY PASTOR(MP):DAVIS MAKENGA
Roho ya BWANA:Mungu mwenyewe,nguvu za Mungu,Uweza wa Mungu
2Wakorintho 3:17, 1Wakorintho 12:4-11, Waamuzi 14:6



CHRISTOFER UNITETEE

Davis Makenga 3