SOMO:KUTIMIZA KUSUDI LA MUNGU NDANI
YAKO
MUHUBIRI:MINISTRY PASTOR(MP):DAVIS
MAKENGA
Kusudi:Ni
wazo au lengo lililowekwa ndani ya moyo wako ili liweze kutimiza lile ambalo
Mungu ameweka katika maisha yako.
-watu wengi
wamekua wakiishi
katika maisha yao bila kujua kusudi alilo nalo
-Watu
wanaishi maisha feki
1Yohana 3:8,
Malaki 4:5-6,Luka 1:13, Yeremia 1:4
Kabla
sijakuumba nalikujua.Maana yake Mungu anajaribu kumuambia Yeremia kwamba
natambua kabisa nilichokuwa nafanya pindi nilipokuumba
-Nimekuweka
juu ya mataifa na juu ya Falme; Maana yake kamuumba kwa kusudi lake ndani yake
.Kuwa Nabii
wa mataifa
.Kuwa juu ya
mataifa
.Kuwa juu ya
falme
Akampa na
kazi ya kufanya; kung’oa,kubomoa, kuharibu ,kuangamiza,kujenga na kupanda.
Kuwepo kwako
ni kwa ajili ya kusudi la Mungu ndani yako.Ndani ya kusudi lako upo uwezo na
mamlaka ya kuamuru na kubadilisha mazingira pinzani ndani yako.Utakutana na
falme na ngome za maadui,vita,mapepo,wachawi utapambana navyo.
JINSI YA
KUTAMBUA KUSUDI LAKO
Kutambua
kusudi ulilo nalo ni kazi sana mfano mtu anafanya biashara hii au anafanya kazi
ile au anajaribu kufuga kuku,kulima lakini mtu anaona bado kuna kitu kinadaiwa
anataka akifanye.
Ili uweze
kujua upo ndani ya kusudi la Mungu ni lazima kiwango cha amani yako kiendane na
kiwango cha kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako
Lipo jambo
umewahi kulifikiria kulifanya au tayari umekwisha lifanya na ukasikia amani
ndani ya moyo wako hata kama ni dogo ,tambua kua hilo ndilo kusudi la Mungu
kwako
SOMO:KUVUNJA
NDOA ZA KISHETANI
MUHUBIRI: MINISTRY PASTOR(MP):DAVIS MAKENGA
Ndoa:Ni muunganiko kati ya mwanamke
na mwanaume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao.
Kiingereza:Is a formal legal bond
relationship between husband and wife
Aina za ndoa
.Ndoa za ukubwani
.Ndoa za utotoni
Kisheria(Ndoa zinazotambulika)
+Ndoa za kimila
+Ndoa za kiserikali
+Ndoa za kidini
-Za Kikristo
-Za kiislam
Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo
kulazimishwa na mtu.Kimsingi Mungu ndiye akiyeanzisha ndoa(Taasisi ya kwanza
duniani ni ndoa).Moja ya maagano ambayo Mungu ameweka ni ndoa
Mwanzo 2:24
Shetani anajua mtu huyu
anaomba,anachokifanya anakutengenezea mke/mume wa kiroho.Unaweza kufunga
ndoa/kufungishwa ndoa na mapepo katika ulimwengu war oho.Unaota ndoto unakutana
na mtu Fulani unayemfahamu au usiyemfahamu, unaanza kufanya nae mapenzi maana
yake unashiriki naye kwenye ulimwengu wa r oho.Kama umeoa/umeolewa utapata
upinzani sana kwenye suala la kuoa/kuolewa.Mkataba wa
maandishi,maneno,cheti,pete,mavazi,vyakula n.k
Torati 7:2-4, Kutoka 34:15-16,Walawi
17:7
SOMO:ROHO YA BWANA INIJILIE
MUHUBIRI: MINISTRY PASTOR(MP):DAVIS MAKENGA
Roho ya BWANA:Mungu
mwenyewe,nguvu za Mungu,Uweza wa Mungu
2Wakorintho
3:17, 1Wakorintho 12:4-11, Waamuzi 14:6